Sunday, 28 June 2015

UVIMBE KWENYE KIZAZI(UTERINE FIBROIDS/MYOMA)

Kumekuwa na ongezeko kubwa la tatizo la akinamama kuwa na uvimbe kwenye kizazi. Suala hili ni gumu na hupelekea akinamama wengi kutozaa tena katika maisha yao japo hutegemeana na sehemu uvimbe ulipo.
Kwa leo tutaona ni jinsi gani ugonjwa huu tunavyoupata, dalili na matibabu yake yanavyokuwa. Tukumbuke kuwa mgonjwa wa uvimbe kwenye kizazi haendi hospitali kwa sababu ya ukubwa wa uvimbe bali anaenda Hospitali kutokana na dalili atakazokuwa anazipata. Wanawake wengi tu wanakuwa na tatizo hili lakini wanajikuta wanabeba hata mimba hadi wanajifungua salama. Hii ni kutokana kuwa bado hawajapata dalili za ugonjwa huu/yaani hawajaanza kusumbuliwa.

HIZI HAPA NDIYO DALILI ZA KUWA NA UVIMBE KWENYE KIZAZI
1. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
2. Kupata hedhi mara nyingi zaidi ya siku za kawaida
3. Kuumwa na tumbo la hedhi zaidi ya kawaida
4. Kutokwa na uchafu na majimaji yenye harufu kali sehemu za siri
5. Kukojoa mara kwa mara
6. Figo kujaa maji na kusababisha kiuno kuuma sana(uvimbe umekandamiza ureter moja)
HIZO NDIYO DALILI ZINAZOMFANYA MGONJWA KWENDA HOSPITALI NA SIYO UKUBWA WA UVIMBE.

Mgonjwa anapofika na dalili hizo hubidi kufanyiwa kipimo cha picha ya tumbo(ultrasound) lengo na madhumuni ya kipimo hicho ni kujua uvimbe upo wapi, kujua uvimbe uko mmoja au zaidi, kutambua kama uvimbe umeathiri sehemu zingine kama kuziba ureter kama upo nje ya kizazi. Kipimo hicho kitamsaidia Daktari kujua anamsaidiaje mgonjwa wake kimatibabu.
VISABABISHI VYA UVIMBE KWENYE KIZAZI
-Kisababishi kikuu ni kuharibika kwa uwiano wa vichocheo vya estrogen na kusababisha kiwango cha estrogen kuwa kikubwa.
-ulaji wa vyakula vya viwandani vilivyovundikwa au kuhifadhiwa kwa msaada wa kemikali
-unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi (added sugar), kionjo na rangi ambavyo ni industrial products
-unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara

WATU AMBAO WAPO HATARINI KUPATA UGONJWA HUU
~Wanawake wote ambao hawajawahi kupata mtoto
~wanawake wote ambao wapo katika umri wa kuweza kuzaa, maana yake wote kuanzia umri wa kubalehe hadi kikomo cha kuzaa ~wanawake wanene kupita kiasi n.k

MATIBABU
Matibabu yake yanaweza kuwa kama ifuatavyo kutegemeana sehemu uvimbe ulipo
=>kupewa vidonge vya kutuliza maumivu tu, vidonge hivyo ni ghali sana lakini pia mgonjwa hushauriwa kutumia kwa muda mfupi tu kwani vina madhara ya kuweza kumfanya mwanamke kuwa na muonekano wa kiume kana vile kuota ndevu n.k
=>kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe tu endapo uvimbe upo pembeni ya kizazi. Ukifanyiwa hiyo Huduma bado mwanamke unaweza kupata mimba na kuzaa.
=>kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kabisa kizazi endapo Uvimbe upo ndani ya kizazi. Hapa mwanamke akifanyiwa upasuaji huu hawezi kuzaa tena katika maisha yake yote
NB: KUMBUKA KUWA HATA KAMA UTAUONDOA UVIMBE HUO, HAIMAANISHI KUWA UVIMBE UMEISHA, TATIZO HUJIRUDIA TENA MAANA BADO UNAKUWA HUJATIBU VYANZO VYA TATIZO AMBAVYO NI PAMOJA NA UWIANO MBOVU WA HORMONES NA MENGINE.

Vipo vidonge vilivyotengenezwa kwa mimea na uyoga mwekundu unaopatikana katika nchi za China na Thailand vinatibu kabisa tatizo hilo la uvimbe kwenye kizazi kwa kusambaza, kukausha na hatimaye kuumaliza kabisa uvimbe huo. Vidonge hivyo vinapatikana sasa Tanzania na kama wewe una tatizo hilo au ndugu na rafiki zako wana tatizo hilo basi wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 uweze kujipatia vidonge hivyo