Friday, 17 July 2015

UFAHAMU UGONJWA WA ASTHMA (PUMU)

 Ugonjwa wa Pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa  katika mapafu. Mtu akipata ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu na kuvimba. Maumivu katika njia za hewa huzifanya njia hizo kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda katika mapafu. Hali hii hufanya muathirika kutoa mlio kama filimbi au mluzi wakati wa kupumua.

VYANZO VYA PUMU
Baadhi ya allergy au vizio vifuatavyo huweza kusababisha Pumu:
-Vumbi
-Mende
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k
-Moshi wa sigara
-Harufu kali kutoka kwenye rangi au chakula
-Msongo wa mawazo
-Uchafuzi wa hewa

Vingine ni kama:
-Dawa kama Aspirin
-Ugonjwa wa kucheua
-Kuwashwa mwili au vizio vitokanavyo na kemikali
-Magonjwa ya njia za hewa

DALILI ZA PUMU
Ugonjwa wa Pumu unaweza kuendana na dalili zifuatazo;
-Kikohozi kikali hasa nyakati za usiku na alfajiri, hali hii humfanya mgonjwa kutolala
-Kutoa mlio kama vile mtu anapiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua
-Kifua kubana. Mgonjwa husikia kama vile kuna kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine kujisikia kama vile kuna mtu amemkalia kifuani.
-Uwezo wa kupumua kupungua au mgonjwa anapumua kwa shida. Hali huu husababishwa na kukosekana kwa hewa inayoingia na kutoka kwenye mapafu.
-Kupumua haraka haraka.


Ikumbukwe kuwa si watu wote wanaokuwa na dalili hizo kuwa watakuwa na Asthma, japo hali hiyo yote huashiria uwepo wa matatizo katika njia za upumuaji. Ni vyema kutembelea kituo cha huduma za Afya kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Pumu ni ugonjwa sugu, hivyo matibabu yake ni ya muda mrefu. Vipimo mbalimbali vinaweza kufanyika vikiwemo X-ray ya kifua, Skin allergy test, kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oxygen kilichopo kwenye damu ya mgonjwa (oximetry) n.k.

Matibabu ya Pumu ni pamoja na kuepuka vyanzo vya ugonjwa huo. Wanaopata ugonjwa huu kutokana na msongo wa mawazo hupewa ushauri maalumu. Kuna matibabu ya aina mbalimbali ya ugonjwa huu yakiwemo ya kawaida na yale ya dharura endapo mgonjwa kapatwa na shambulio la ghafla (asthmatic attack). Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na zile za expectorants, bronchodilators, drip ya cortisone au nebulizer, antihistamine, steroids drugs, intravenous muscles relaxants n.k.

Pamoja na hayo, tiba hizo mara nyingi hutuliza dalili tu au muonekano wa namna ambavyo mgonjwa anajisikia kwa muda huo. Tunazo dawa zilizotengenezwa kwa mimea ya militaris, biloba na uyoga mwekundu ambazo zina jumla ya vidonge 60 kila moja, mgonjwa atazitumia kwa muda wa miezi mitatu na atapona kabisa.
Kazi ya uyoga mwekundu katika mwili ni kuongeza uwezo wa mwili kupambana na magonjwa, huufanya mwili uwe imara, kwa kushirikiana na militaris na biloba hutibu kabisa matatizo yote ya mfumo wa upumuaji na kuondoa matatizo yote yanayohusiana na upumuaji. Dawa zote hizo zipo katika mfumo wa vidonge.
NB: MGONJWA ATUMIE DAWA HIZI KWA MIEZI MITATU PASIPO KUKATIZA DOZI 

WASILIANA NASI KWA NAMBA 0767925000 AU WHATSAPP  0622925000 KWA MAELEZO ZAIDI. PIA like page yetu ya facebook 'Masha Health Products" UTAJIFUNZA MENGI KWA AFYA YAKO