Saturday, 24 October 2015

FAHAMU NJIA SALAMA YA KUTIBU MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI ( DISMENORRHEA)




Haya ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.

Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani lakin baadhi ya Wanawake hupata maumivu makali zaidi . Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka ktk mirija na kutelemka chini ya mirija hiyo wakati wakati wa Ovulation au kipindi cha uwezekano wa kupata mimba.

Maumivu haya yapo ya aina mbili:

1. Primary Dismenorrhea.
Haya ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za msingi kitiba. Ktk aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni na huanza siku 1 au 2 kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku 2 au 4.

2. Secondary Dismenorrhea
Haya ni maumivu makali zaidi na yanakuwa na sababu maalum za kitiba km vile matatizo ktk kizazi, Ugonjwa wa Nyonga (P.I.D) na matatizo ktk mirija ya uzazi.

Karibu nusu ya Wasichana wote hupata maumivu wakati wa hedhi, huku 15% kati yao wanasema kuwa hupata maumivu makali sn.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi:
🚫 kuwa na umri chini ya miaka 20
🚫 kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya hapo
🚫 kutoka damu nyingi wakati wa hedhi (suala hili linaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba)
🚫 Wanawake ambao hawajawahi kuzaa
🚫 Endometriosis - hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa kizazi huanza kuota nje ya fuko hilo au huota sehemu nyinginezo
🚫 Adenomyosis - huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe ( tumors) zinaota ktk mfuko wa uzazi
🚫 Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya zinaa ya kuambukiza
🚫 Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba inazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

SASA HEBU TUONE, TUMBO LA HEDHI HUUMAJE ( DALILI)

⚠ Maumivu mara nyingi si makali
⚠ Maumivu yanaweza kuja na kuondoka
⚠ Maumivu zaidi huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo
⚠ Maumivu yanaweza kuchanganyikana na maumivu ya chini ya mgongo ambayo husambaa hadi mapajani
⚠ Kujihisi kutapika/kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho
⚠ Kupata choo kilaini au kuharisha
⚠ Kufunga choo
⚠ Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu
⚠ Kuhisi maumivu ya kichwa
⚠ Kutojihisi vizur au uchovu

Inapaswa kujua kuwa, kiwango cha maumivu hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke au kutegemeana na dalili. Wanawake wengi huzitambua dalili hizo bila ht msaada wa Daktari.
Wanawake nawashauri mara mnapopata maumivu makali zaidi ni vyema mkamuone Daktari au Mshauri wa Afya ili ikiwezekana kufanya vipimo km vile Ultrasound, MRI na vinginevyo ili kufahamu iwapo kuna matatizo mengine ya kitiba yanayosababisha maumivu kuwa makali.

MATIBABU
Matibabu ya Maumivu ya tumbo la hedhi huweza kutibiwa kirahisi kwa kutumia Vidonge vya maumivu km Ibuprofen, Naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na STEROIDS (NSAIDS). Pia kuna wakati Madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba. Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.
Lakini pia ifahamike kuwa vidonge vyote hivyo havitibu tatizo hili moja kwa moja bali utatakiwa kuvitumia kila mwezi unapoingia hedhi.


Zipo tiba za moja kwa moja kwa kutumia vidonge vilivyotengenezwa kwa mimea na havina madhara mwilini km vidonge vya maumivu nilivyovitaja huko. Vidonge hivi vya mimea vinapatikana sehemu mbalimbali za Tanzania na tiba yake hufanyika kwa miezi miwili - mitatu na baada ya hapo mwanamke/msichana hautasikia tena maumivu ya hedhi maishani mwako.

Mawasiliano:
0767925000
0784925000
0622925000 (whatsapp)

posted from Bloggeroid