Sunday, 9 August 2015

Vyakula vinavyoimarisha Afya ya Ngozi



Ni matumaini yetu kuwa hamjambo na mnaendekea na shughuli za uzalishaji ili kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Karibuni tena wasomaji wa makala zetu za Afya. Leo tutaangalia aina ya vyakula vinavyoweza kuimarisha Afya ya Ngozi.

Bila shaka kula vyakula vyenye virutubisho ni jukumu la lazima kwa kila binadamu kama anahitaji kuwa na Afya njema. Dunia ina vyakula vya Asili ambavyo ndani yake kuna virutubisho muhimu vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa na pia kuimarisha Afya.
Vyakula hivyo si vingine bali ni vile vya kijani ambavyo vina uwezo mkubwa zaidi katika kuponya maradhi na kusaidia pia kukarabati, kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Ngozi ni sehemu muhimu ya mwili ambayo ina jukumu kubwa la kuukinga na kuufunika mwili na viungo mbalimbali na Afya yake ni jambo la kuzingatiwa.

Aina ya vyakula tunavyopendelea kula vinaweza kuchangia katika mwonekano wa ngozi zetu na kusaidia kupambana na matatizo ya ngozi, kupunguza mikunjo ya uso na suala zima la Afya na muonekano wa ngozi. Inawezekana kabisa kila mmoja anapenda kuonekana na ngozi nzuri isiyoonekana kuzeeka mapema lakini tatizo kubwa ni kutojua nini cha kufanya ili kudumisha Afya ya ngozi zetu na matokeo yake tunajikuta tunajiletea madhara yasiyoweza kutibika kirahisi kwa kupenda urembo wa njia mkato (vipodozi vyenye sumu kali). Pia inawezekana tukatumia pesa na muda mwingi katika kuhakikisha ngozi inakuwa nyororo, nzuri na ya kuvutia, lakini pengine ukawa hufahamu kuwa kuna aina za vyakula vinavyosaidia katika kutunza ngozi na tena bila gharama kubwa. Kwa kawaida kila aina ya chakula tunachokula huenda moja kwa moja kuwa sehemu ya mwili na pia matatizo mengi ya ngozi kama chunusi ya Eczema yanahusiana kwa kiasi kikubwa na Lishe. Kwa hiyo tunashauliwa kula vyakula ambavyo vina virutubisho vyote vya muhimu kwa kufuata kanuni za Afya ili kuufanya mwili uwe na Afya nzuri kwa kula chakula bora, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupumzika kwa muda mrefu. Vivyo hivyo ngozi nayo inatakiwa kutunzwa vyema kupitia lishe.

Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kuimarisha Afya ya ngozi:
1. ASALI=> Asali ambayo hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia ni chakula muhimu kwa ajili ya ngozi na pia Afya ya binadamu. Husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu  kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambavyo huzuia vijidudu wanaozaliana kwenye ngozi. Tunashauriwa kuwa ili tuweze kulinda ngozi, paka asali wakati wa kuoga, acha muda kiasi kisha ioshe. Kufanya hivyo husaidia sana kuimarisha na kunawirisha ngozi.

2. VYAKULA VYA BAHARINI=> Vyakula hivi huwa vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu sana kwa ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi. Zinc husaidia chunusi na harara katika ngozi kwa kuyeyusha homoni za testosterone. Pia husaidia kuzalishwa seli au chembe zilizokufa huku ikiifanya ngozi ing'ae na kuwa na mvuto.

3. MAYAI=> Kiini cha yai kina Vitamini A na B huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo ni muhimu sana kwa ngozi. Vitamini A husaidia kuondoa chunusi na mikunjo ya ngozi. Vitamini B pamoja na Protini ni muhimu kwa Afya ya ngozi/kucha na huifanya ngozi iwe nyororo na yenye kung'aa. Husaidia pia kuilinda ngozi na mionzi ya jua.


Mpenzi msomaji, matunda yenye vitamini C ambayo ni Machungwa, Malimao na mengineyo ni muhimu pia katika afya ya ngozi kwa sababu husaidia kutengeneza Collagen ambayo ni aina ya Protini unayotengeneza ngozi. Vitamini C inasaidia kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema.

Hivyo ni baadhi tu ya vyakula ambavyo ni muhimu kwa Afya ya ngozi. Pia tunatoa huduma za tiba kwa dawa ambazo hazina kemikali, dawa zetu zipo katika mfumo wa vidonge. Zinatibu magonjwa tabia yote (yasiyo ya kuambukizwa) kama vile Kisukari, Presha, Matatizo ya moyo, Vidonda vya tumbo, kukosa choo, matatizo ya hedhi, mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa, upungufu wa nguvu za kiume n.k.
Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000. Tunatoa huduma popote Tanzania kupitia kwa Mawakala wetu.
KARIBUNI SANA