Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia uwepo wa hii somo hili ikiwa leo tunaendelea sehemu ya pili. Mada yetu inasomeka hapo juu linawatokea Zaidi wanawake pasipo wao kutambua tatizo karibu asilimia 30%-45% ya wanawake wote wana matatizo haya huwa wanafanya tu tendo la ndoa kuwaridhisha waume zao na wao kutokufurahia tendo hili la kipekee.
~tatizo hili hutokana na sababu tofauti mfano uwiano mbaya wa homoni nk
~Mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na mambo makuu mawili ambayo ni matatizo ya kimwili na matatizo ya kisaikolojia kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya somo hili.
UTAJIGUNDUAJE KAMA UNA TATIHili O HILI?
Hili tulilisema sehemu iliyopita, mojawapo ni kusikia maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa, kingine ni kwamba una uwezo wa kufanya tendo mara moja tu huhitaji tena maana mzunguko wa kwanza wenyewe hata haukufika mwisho, tutakuja kuona mbeleni kabisa madhara ya hali hii kwani hatari ni kubwa kuliko unavyofikiria wewe mpenzi msomaji wa makala hii.
JINSI YA KUJIKINGA NA MATIBABU YAKE
Matibabu yake Hospitali ni magumu kwani hakuna dawa maalumu na Zaidi hufanyika kupitia vipimo vya uchunguzi, historia ya mhusika pamoja na Dalili za magonjwa mbalimbali, pamoja na hayo tatizo hili unaweza kulidhibiti kwa kufanya yafuatayo
-EPUKA KUVUTA SIGARA NA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI
-ZINGATIA ULAJI ULIO SAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI
-ONDOA MAWAZO NA HUZUNI
-BADILISHA MFUMO WA MAISHA YAKO
-ONGEZA UPENDO KATIKA MAHUSIANO YAKO
-WEKA MAZINGIRA MAZURI NA MUDA WA KUFANYA TENDO LA NDOA
-BADILISHA ENEO LA KUFANYIA MAPENZI, SIYO KILA SIKU KITANDANI TU.
Kaa tayari kwa sehemu ya tatu ya somo hili ambapo tutajifunza MWANAUME UFANYE NINI KAMA MKEO/MPENZI WAKO HAFIKI KILELENI.
MASHA MASANJA
Whatsapp 0622925000
TAFADHALI USISAHAU KUSHARE, KU-COMENT, KU-LIKE NA KUWAALIKA WENZAKO KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK "Mimea Yenye Ufumbuzi Wa Matatizo Yako" KWANI KUNA MASOMO KIBAO YAPO PALE KWA AJILI YA AFYA YAKO.