Sunday, 10 July 2016

HATUA 5 ZA KUPATA MTOTO WA KIUME




Kupata mtoto wa kiume ni jambo linalohitaji ushirikiano wa pande zote mbili, yaani mke na mume na ni jambo linalohitaji hatua kwa hatua na kwa umakini, ingawa njia nitakayoeleza hapa haimaanishi kuwa inaweza kufanya kazi kwa asilimia 100.  Bali ni njia ambayo imekuwa ikitumika mara kwa mara na ndiyo njia rahisi na ukiifuata unaweza ukapata kwa asilimia 75.

Mwaka 1960 mwanasayansi Landrum Shettles aliandika kitabu kinachohusu uchaguzi wa jinsi ya mtoto.  Mwanasayansi huyo wa tiba ndiye aliyeileta nadharia yake iliyojikita zaidi katika vitu vilivyomo ndani ya seli, yaani malighafi za kijenetiki ziitwazo chromosomes ambayo ndiyo inayotumika na kama ikifuatwa vizuri basi huweza kuwa na mafanikio.

Sayansi ya kijenetiki inaeleza kuwa mwanamke huwa na mbegu ya XX na wa kiume huwa na XY, na pale yai la kike linaporutubishwa hutokea mgawanyiko wa seli na mbadilishano wa malighafi za kijenetiki hutokea.

Hivyo kiumbe kinachotungwa yaani mtoto, huwa na nusu ya malighafi za kijenetiki kutoka kwa mama na nusu nyingine kutoka kwa baba, na akipata mbegu XX huwa ni jinsi ya kike na akipata XY ni wa kiume.
Kiasilia mbegu Y huwa ni ndogo kimaumbo, zina mwendokasi mkubwa lakini hufa mapema ukilinganisha na za kike X ni kubwa, hazina kasi, lakini huishi kwa muda mrefu.  Kwa kutumia ufahamu huu ndipo mwanasayansi Shettels aliweka nadharia ambazo zinatumika katika uchaguzi wa jinsia.

Kuna hatua tano za kufuata kwa umakini ili uweze kufanikiwa, ingawa haimaanishi kuwa ni lazima ufanikiwe kwani hatua hizi huongeza nafasi zaidi ya kupata jinsi ya kiume na kwa yule atakayehitaji jinsi ya kike afanye kinyume cha hatua hizi.

Hatua ya kwanza
Hatua ya kwanza ni kugundua wakati wa ovulation, ama siku ambayo yai la kike linatoka.  Hiki ni kipindi ambacho yai la mwanamke lipo tayari kurutubishwa na mbegu ya kiume hivyo mimba huweza kutungishwa.

Ili kugundua kuwa upo katika ovulation, inabidi kufuatilia yafuatayo: Inabidi uwe na chati ya kuangalia na kufuatilia ute wa kizazi unaotoka ukeni, maana muda mfupi kabla ya ovulation ute huwa wa majimaji na wa kuvutika hufanana kama vile wa mayai ya kawaida, nikimaanisha ya kuku, ambayo yamezoeleka kwa wengi.

Ni vizuri kupanga chati hii kwa zaidi ya miezi mitatu ili kusudi uwe na uzoefu wa kugundua tofauti ya ute.  Vilevile inabidi uwe na chati ya kuweka rekodi ya joto la chini la mwili wakati ukiwa umepumzika, nikiwa na maana mara nyingi ukiwa umelala.

Joto la chini la mwili hupanda kwa nyuzi joto 0.5 sentigredi kipindi cha ovulation.  Ni vizuri chati hii iwe pamoja na ya ute wa kizazi, kusudi uweze kufuatilia mabadiliko haya kwa pamoja.

Kipimo cha kugundua ovulation ni kipimo ambacho huangalia wingi wa homoni aina ya Lutenizing ambayo hutolewa kwa wingi kipindi hiki.  Kipimo hiki ni vizuri kufanya mara mbili kwa siku, kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 9:00 mchana.  Vilevile kati ya saa 11:00 jioni na saa 4:00 usiku.

Hatua ya pili
Hii ni hatua ya kutegea wakati muafaka wa kufanya tendo la ndoa.  Ni vizuri kufanya tendo la ndoa kipindi cha saa 24 kabla ya ovulation na saa 12 baada ya ovulation.  Kwa sababu tindikali na utelezi katika ute wa kizazi hupungua na hivyo husaidia mbegu za mwanaume hasa aina ya Y kusafiri haraka na kulifikia yai la mwanamke na kulirutubisha.

Hatua ya tatu
Pendelea mtindo au staili inayofanywa na wanyama kama mbuzi wakati wa tendo la ndoa, yaani mtindo wa mwenza wako kuinama.
Mtindo huu huwezesha mlango wa uzazi kuwa karibu na sehemu ya kiume pia kuingia umbali mrefu zaidi ndani ya uke, hivyo basi mbegu za kiume humwagwa karibu na shingo ya kizazi na kulifikia yai haraka zaidi.

Hatua ya nne
Ni muhimu mwanamke kufika kileleni kabla ya mwanaume; kufika kileleni kwa mwanamke husaidia kubadili mazingira katika uke kuwa ya ukakasi (alkaline) hivyo kusaidia mbegu za kiume “Y” kuwa imara zaidi.  Uke kuwa na tindikali huipunguza uimara wa mbegu ya kiume.

Hatua ya tano
Hii ni kwa upande wa mwanaume.  Ni vizuri kuvaa nguo zisizoweka joto kali na kubana.  Unapaswa kuvaa chupi au nguo ambazo hupwaya na zimetengenezwa kwa pamba.  Nguo za ndani zinazobana ambazo huongeza joto hupunguza idadi ya mbegu za kiume.  Joto pia hupunguza ubora na utengenezaji wa mbegu za kiume.

Vilevile inabidi kunywa vinywaji vyenye caffeine kabla ya tendo la ndoa.  Hii huongeza nguvu ya mbegu za kiume aina ya Y.

Mambo mengine ya kuzingatia ni mlo.  Hakikisha unakula vizuri wiki moja kabla na siku ya tendo.  Tafiti zinaonyesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye sukari huiwezesha mbegu ya Y kuimarika zaidi na kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume.  Vyakula hivi ni kama matunda matamu, vyakula vya wanga na vinywaji vyenye glukosi.

Vyakula vingine ni kama vile nyama nyekundu, mayai, maziwa, vyakula vya baharini kama vile samaki, kamba na pweza.

Kwa upande wa mwanamke, anapaswa kula zaidi vyakula visivyo na tindikali kama vile kuepuka kula matunda yenye uchachu na vyakula jamii ya kunde kupitia kiasi.

Mambo mengine ni kuzingatia mazingira ya tendo lenyewe, hakikisha upo vizuri kiafya, kimwili na kiakili.  Usiwe na msongo wa mawazo na sonona kwa sababu huleta mwingiliano na tendo, hivyo kulifanya kuwa dhaifu.


Ni vyema pia kutafuta mazingira mazuri ya kufanyika kwa tendo lenyewe.  Lengo ni kuwa na utulivu wa kimwili na kiakili pia.  Hii itakuepusha pia na usumbufu utakaoweza kuleta mwingiliano na tendo lenyewe

FAHAMU KUHUSU TATIZO SUGU LA CHUNUSI

chunusi ni nini? 
hivi ni vipele vinavyotokea usoni, kifuani na mgongoni sababu ya kubadilika kwa mfumo wa kutengeneza mafuta wa ngozi.

chanzo ni nini?
hii husababishwa na kuongezeka hormone za uzazi aina ya testosterone kwa jinsia zote hasa hasa kipindi cha kubalehe na kuvunja ungo kwa jinsia zote.

matibabu.
matibabu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo....matibabu kwa chakula, matibabu ya kimwili na matibabu ya dawa za hospitali.


matibabu ya chakula..

  •  ondoa chumvi kwenye chakula chako au kula chumvi kidogo sana.
  •  epuka ulaji wa sukari na vyakula vyote vya kukaanga kama chips, maandazi na chapati.           
  • pendelea kula vyakula vya asili kama wali, ugali, mchicha, maharage, njegere vikiwa vimeungwa mafuta kidogo sana  pia kula kwa wingi karoti mbichi kwa sababu zina vitamin A ambayo ni nzuri sana kwa ngozi
  • kunywa maji mengi ili kuondoa sumu zote mwilini na kulainisha ngozi.

matibabu ya  kimwili.

  •  acha ngozi yako ipate jua la asubuhi na jioni kila siku.
  • weka sura yako kwenye mvuke wa maji ya moto kila siku. 
  • shiriki mazoezi ya aina yeyote hata kama ni kuruka kamba tu angalau utokwe jasho kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.                                                                                                                                          
 matibabu ya dawa

  • kuna dawa zinasaidia kuondoa chunusi i.e antibiotiki kama doxcycline, vidonge vya vitamini A na vidonge vya hormone kwa wanawake mfano oetrogen, persol tube na kadhalika. 

 mwisho:
 watu wengi hawaponi chunusi kwa sababu ya kupenda  kutumia njia moja tu ya matibabu {dawa}, ni vizuri kuchanganya njia zote hapo juu kwa matokeo mazuri na inaposhindikana ni vizuri kumuona daktari bingwa wa ngozi kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Uvimbe sehemu ya haja kubwa - bawasiri/bawasili (HAEMORRHOIDS)



Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
  • Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
  • Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
  • Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
  • Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
                 
Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;
  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayoongeza shinikizo katika tumbo.
  • Umri mkubwa
Dalili za bawasiri
  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri
  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids
Vipimo na uchunguzi
  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
Upasuaji;
  • Hemorrhoidectomy
  • Stapled hemorrhoidopexy
Njia za kuzuia Bawasiri
  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
Njia zingine za kuzuia Bawasiri
1. Jaribu kunywa maji ya kutosha na kula chakula chenye fiber nyingi ili uepuke kupata Choo kigumu.
2. Epuka kusimama muda mrefu au kukaa muda mrefu kama ulikuwa unafanya hivo awali
3. Fanya mazoezi ili kuongeza intenstine motility
4. Epuka kujikamua sana ukipatwa na haja kubwa
NB: Huu ugonjwa hauhusiani na matatizo ya uzazi
Baadhi ya sababu zinazopelekea hali hiyo ni

-kufunga choo ama kupata choo ngumu 
-ujauzito
-sababu za kiurithi-baadhi ya watu wanaweza kuwa na kuta dhaifu

Njia sahihi ya kupunguza Kitambi na Unene



Mtindo wa maisha, vyakula na shughuli za kila siku za mwanadamu ni baadhi ya vitu vinavyosababisha idadi kubwa ya wake kwa waume kuwa na uzito au unene kupita kiasi na wakati mwingine kuwa na vitambi.
Matatizo haya yamekuwa yakiwapata watu wa jinsia zote na kuwanyima raha wanawake wengi, ambao hufikia hatua ya kutumia mikanda maalumu ya kufunga tumbo au kuhangaika kupitia njia mbalimbali ili kupunguza kadhia hiyo kwao.

Kutokana na kuongezeka kwa tatizo hilo, kumezuka dawa nyingi zinazodaiwa kuwa na uwezo wa kupunguza vitambi na uzito mkubwa, lakini wataalamu wa afya wanaonya kuwa ni sumu.

Tafiti nyingi za kisayansi zinaonesha kuwa dawa hizi kwa kiasi kikubwa zina kemikali kama vile phentermine, sibutramine, phenolphthalein, caffein, hydroxycitric acid (HCA) na senna ambazo zina madhara makubwa kwa afya ya mwanadamu.
Dk. Phil McGraw anasema baadhi ya dawa hizo huathiri sehemu ya ubongo inayohusika na hamu ya chakula.  "Hamu ya chakula ni muhimu kwa ajili ya ubora wa afya na maisha.  Dawa yoyote inayoharibu hamu ya chakula kwa kipindi kirefu, inaweza kusababisha madhara ya kiafya", anasema Dk. Phil.
Mama mwenye uzito wa kilo 108, Doreen Shayo anasema amewahi kujaribu dawa za kupunguza mwili, lakini akapatwa na homa kali iliyohatarisha maisha yake baada ya wiki moja, hivyo alishindwa kuendelea na dozi hiyo.

"Nilishawishiwa kununua dawa hiyo ya kupunguza uzito na nilishauriwa kula mbogamboga, matunda na maji kwa wingi wakati wa dozi, sikuwa nakula wanga wala chakula kamili.  Nilipata homa ya ghafla madaktari wakanishauri kwamba dawa zile hazikuwa nzuri kwangu hivyo niachane nazo, wakati huo nilikuwa na kilo 120 lakini nilipungua kutokana na maelekezo ya madaktari", anasema Doreen.
Baadhi ya madaktari bingwa wa afya ya binadamu wanasema msukumo wa dawa hizo unaowafanya wahusika kuharisha mafuta mengi kwa wakati mmoja, ni njia isiyo sahihi ambayo pia huathiri baadhi ya viungo ndani ya tumbo, huku madhara yake yakijitokeza miaka kadhaa mbeleni.

Tabibu mmoja wa tiba mbadala anasema asilimia kubwa ya dawa za kupunguza kitambi na mwili kwa uharaka ni sumu.
"Mtu anapewa dawa anaharisha sana, swali la kujiuliza nini dawa inafanya tumboni na kusababisha kupata choo laini au kuyeyusha mafuta kwa muda mfupi?  Lazima tujue kwamba zina madhara baada ya muda, wengi wanauziwa vitu vibaya na mbegu fulani ambazo ni sumu halafu mwili unabadilika anaharisha sana, anaambiwa dawa ndio inafanya kazi yanatoka mafuta mengi, si njia sahihi ya kupunguza uzito wa mwili au kitambi."

Dk. Samuel Shita kutoka Hospitali ya Mwananyamala anasema kwa kawaida kuharisha humfanya mtu kupunguza maji mengi na chumvichumvi mwilini na hivyo huathiri kazi ya seli na mfumo wa fahamu.

"Dawa hizo nyingi hazijaruhusiwa kutumika na Wizara ya Afya na wala hazijathibitika kwamba ni sahihi kwa matumizi ya binadamu, lakini wanazitumia na madhara yake yanaanza kujitokeza baada ya kutumia mtu anaharisha sana na yeye anadhani ana mafuta lakini ule ni uteute unaokaa tumboni unaosaidia tumbo kufanya kazi.

"Utafiti unaonesha kuwa watu wanaopendelea kula katika migahawa mikubwa ndio wanaoongoza kuwa na miili mikubwa, teknolojia zipo na dawa zitumikazo lazima ziwe zimefanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 10.  Kuna madhara mengi yanayoweza kuwakuta watu ikiwamo ya figo, moyo, ini na mishipa ya damu."


Dk Shita anasema kuna njia sahihi za kupunguza tumbo ambazo pia ni salama.  "Mtu anatakiwa kufanya mazoezi mepesi na matumizi sahihi ya vyakula, tunatakiwa kupunguza vyakula vya wanga kupita kiasi, sukari na mafuta.
Anasema soda, pipi na chocolate ni vyakula ambavyo havitakiwi kutumika kupita kiasi.

Tabibu wa tiba mbadala anazitaja hatua sahihi za kupunguza kitambi na kuondoa sumu mwilini akisema: "Kutumia juisi za matango na nyanya kila siku kwa muda wa mwezi mmoja sumu zote zinaondoka."
Hata hivyo, Mwaka anasema mtu anapokula chakula ni lazima kiishe tumboni kabla ya kuingiza kingine, vinginevyo anakuwa ametunza sumu mwilini kutokana na kuwa na mabaki mengi ya chakula cha takriban hata mwaka mmoja.

"Mfuko wa chakula una uwezo wa kutunza chakula kwa muda mrefu, ndiyo maana binadamu hufa akikosa chakula kwa siku nyingi.  Miongoni mwa vitu vinavyofanya uondoe sumu mwilini ni kufuata sheria za ulaji na njia za asili za kuondoa sumu hiyo na si njia za haraka kwani zina madhara," alisema.
Wataalamu wa masuala ya dawa Deborah Mitchel na David Dadson, katika kitabu chao kilichochapishwa mwaka 2002 cha "The Diet Pill Guide: The Consumer's Book of Over-the-Counter and Prescription Weight -Loss Pills and Supplements," wanasema:

"Ingawa ushahidi wa dawa hizi unazidi kuongezeka, bado watu wengi wanaaminishwa kwa uongo kuwa zina manufaa.  Hata hivyo, pia watu wanaendelea kuamini kuwa dawa hizi zinazotokana na mimea na ni dawa salama za asili zinazofanyiwa utafiti wa kina na kuthibitishwa na mamlaka za udhibiti na usalama wa dawa kama nyingine za hospitalini."

Namna ya kupunguza kitambi


Maji ya moto yakitumiwa kwa umakini yana uwezo wa kupunguza kitambi, tumbo au uzito mkubwa wa mwili kwa asilimia 60.
"Maji ya moto yana uwezo wa kupunguza tumbo kwa zaidi ya asilimia 60, unachotakiwa kufanya ni kuyachemsha yawe ya vuguvugu kiasi kunywa kati ya glasi nne mpaka sita na iwe ni katikati ya mlo mpaka mlo ndiyo maana kuna watu wanashauri unywe asubuhi au iwe katikati ya mlo wa jana usiku na ule utakaokwenda kuula baadaye.

"Lakini pagumu zaidi ni pale ambako kabla hujakwenda kupiga mswaki ndiyo unatakiwa kuyanywa haya maji.  Tunapata vitamin B12 ambazo zinazalishwa mdomoni wakati binadamu akiwa amelala na mojawapo ya vitamin hiyo ni pamoja na kusaidia msagiko (mmeng'enyo) ule wa vyakula."

Tatizo la wengi kukaa na vyakula kwa muda mrefu tumboni ni moja ya sababu pia ya kuwa na tumbo kubwa yaani kuwa na mafuta ya ziada tumboni na wengine wanakuwa na vyakula vingi wanavyoingiza kuliko wanavyovitoa.



"Asubuhi kabla hujapiga mswaki ukaondoa zile vitamin mdomoni zinywe pamoja na maji, kunywa maji ya vuguvugu glasi nne mpaka sita kila siku unapoamka asubuhi mfululizo mpaka siku 21, baada ya muda fanya hivyo kwa wakati mwingine na wakati ukifanya hivyo pia epuka vile vitu vitakufanya uendelee kuwa na tumbo ili unachokifanya kiweze kuwa na majibu na si kuoga na kujipaka tope," anasema na kuongeza kuwa kupunguza vyakula vya wanga ni njia mojawapo itakayomfanya mhusika kupata majibu ya haraka

MAUMIVU MAKALI YA MGONGO


UTANGULIZI

Maumivu ya mgongo ni ile hali ya kuhisi maumivu au kutojiskia vizuri/kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako (eneo lililopo kati ya kiuno na shingo).

(Mgongo)
Maumivu haya yanatofautiana baina ya mtu na mtu na pia yanategemea sana wapi ilipo shida katika mgongo wako; nini kisababishi na kiungo kilichoathiriwa (kilichoumizwa/jeruhiwa).

Vivyo hivyo dalili nazo hutegemea na kisababishi na hivyo baadhi ya watu huwa na dalili zinazofanana huku wengine wakiwa na dalili za aina mbalimbali kuanzia maumivu ya mgongo, kushindwa kufanya shughuli za kawaida za kila siku kutokana na maumivu, homa na kutetemeka, kupungua uzito (hasa baada ya ajali/magonjwa ya mifupa), kupungua nguvu katika misuli ya miguu, miguu kuwaka moto/kuchomwa chomwa mithili ya sindano au miiba, ganzi kwenye miguu hadi kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa.

Aina kuu za maumivu ya mgongo:
Mara nyingi, maumivu ya mgongo hujitokeza katika aina kuu mbili ambayo ni:
(Maumivu yanayosambaa)
  1. Maumivu yasiyohama (yapo katika eneo la mgongo husika haijalishi unafanya nini - localized pain). Mara nyingi maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli/mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa eneo la mgongoni. Au, ni yale yanayotokana na mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo hivyo kusababisha kuchanika kwa misuli ya ndani ya mgongo na kusababisha maumivu!!
  2. Maumivu yanayosambaaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili wako mbali na mgongo kama vile miguu. Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo wako kwa kupigwa/kuanguka. Mfano: shida ipo mgongoni ila unahisi ganzi kwenye miguu au miguu kuwaka moto).


Visababishi vya maumivu ya mgongo:
(Ubebaji wa mizigo)
  1. Moja ya visababishi vikuu vya maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama ni kichocheo cha kupata maumivu ya mgongo.
  2. Mkao: nyumbani, kazini, shuleni, n.k wakati unafanya shughuli zako za kila siku, una nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza hatari ya kupata maumivu ya mgongo
  3. Ubebaji wa mizigo mizito (kufikia kilo 5 au zaidi) usiozingatia afya ya mgongo.
  4. Kulalia godoro laini na lililobonyea/linalobonyea katikati wakati wa kulaa. Hii husababisha misuli ya mgongo kuvutika kupita kiasi wakati umelala na kupelekea kuchanika hivyo kuishia
    (Godoro la kubonyea)
    katika kupata maumivu ya mgongo na ambayo hudumu kwa muda mrefu (wote) utakokuwa unalalia
      godoro hilo au hata zaidi.
  5. Kujeruhi(wa) mgongo wako kunakotokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe (kansa) katika uti wa mgongo.
  6. Ujauzito/uzito wa kupita kiasi (kitambi): wengi wanashtuka wanaposikia kuwa uzito (kitambi) husababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimam. Kuelemewa kwa misuli/mfupa hii husababisha mabadliko ya mwili katika kutafuta namna ya kufidia hali hiyo… mwisho ni maumivu!!!
  7. Msongo wa mawazo (stress): msongo wa mawazo humfanya mtu kukaa katika mkao mbaya akiwaza na kuwazua hivyo kuishia katika kupata maumivu ya mgongo
    kama nilvyotangulia kusema hapo juu.
  8. Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo na misuli ya pembeni mwa mifupa hiyo na kusababisha maumivu katika eneo husika.
  9. Kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgongo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ajali.
    (Msongo wa mawazo)
  10. Umri wa uzeeni: kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabdiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa-na-misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.[Wanawake huathiriwa mapema katika uzee wao kuliko wanaume kutokana na mfumo wa vichocheo (homoni) vya miili yao kupungua kwa haraka zaidi baada ya miaka kati ya 45-55 ya umri wao wa kuishi).
  11. Wanaume kujihusisha na UPIGAJI PUNYETO wakati wa ujana wao. Vijana wengi ukiwauliza watakwambia wameufanya sana mchezo huu na hadi wengine kufikia kuuhalalisha kuwa ni kawaida kufanya hivyo. Kitendo hiki huhusisha kwa sana uti wa mgongo na ubongo hivyo ni chanzo kimojawapo cha maumivu ya mgongo na hata upungufu wa NGUVU ZA KIUME


Matibabu:
  • Mumivu ya kwaida hasa yale yanayotokana na mshtuko wa misuli ya mgongo au mkao mbaya huwa yanaisha yenyewe ndani ya siku 4 -14, hivo mgonjwa anashauriwa kutumia dawa za kawaida za kutuliza mamivu.
  • Maumivu yanayotokana na kujeruhiwa mgongo ikiwa ni pamoja na ajali/kupigwa/kuangukia mgongo n.k) unashauriwa kufika hospitalini au kituo cha afya kilicho karibu nawe ili upate uchunguzi yakinifu na ushauri/tiba.
  • Maumivu yanayoamabatana na kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa, maumivu makali ya miguu, miguu kuwaka moto/ganzi yanahitaji tiba ya haraka na dharura kwa sababu tayari mfumo wa fahamu/neva utakuwa ulishaguswa/athiriwa kwa namna moja au nyingine.


Namna ya kuzuia maumivu ya mgongo:

(Namna ya kunyenyua mzigo)
  • Mwone daktari wa tiba viungo (PHYSIOTHERAPIST) aliye karibu nawe kwa ushauri kuhusu namna ya:
  • Kukaa vizuri ukiwa nyumbani, kazini au shuleni 
  • Namna ya kubeba mizigo kwa kujali na kuingatia afya ya mgongo wako ili kuepusha kujeruhi misuli ya mgongo wako.
  • Mpangilio na uboreshaji wa mazingira ya kazi yako ili kuzuia hatari za kupata maumivu ya kimfumo (misuli-na-mifupa)
  • Mazoezi muhimu kwa ajili ya afya ya mgongo wako.
  • Tiba ya mazoezi ya viungo (na mgongo kwa ujumla) inayoendana na shida yako husika.

***Kumbuka, tiba ya mtu mmoja mmoja hutaofautiana kwa kuwa dalili hutofautiana kutokana na kisababishi cha maumivu hayo***

***Usifanye mazoezi uliyoona mwenzako akifanya ukidhani unajitibu kumbe ukawa unaongeza tatizo badala ya kupunguza. Ni vizuri umwone mtaalam akuelekeze tiba stahiki***

NJIA SALAMA ZA KUPUNGUZA UZITO


Ukizungumza na watu wengi wanene watakwambia wanataka kujua njia ya kupunguza mafuta tumboni. 
Njia rahisi na salama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kitambi ni ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.

Kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi.

Vyakula kama viazi mviringo, wali, mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku tatu, pia unywaji wa vinwaji vitamu vyenyw sukari nyingi unasababisha kuongezeka uzito na pia huongeza ukubwa wa tumbo.

Vyakula hivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi kidogo sana. Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko kawaida hali hiyo inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi, kutokunywa maji ya kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum.

Vyakula vya wanga na mafuta hufanya mtu kunenepa, acha au kupunguza kula vyakula hivyo.
Tumbo kuwa kubwa ni dalili kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada inafanya mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya mwili.
Kwa kuwa chakula hiki cha ziada huwa hakitakiwi, mwili hukibadilisha na kuweka akiba katika mfumo wa mafuta kitaalam kama glycogem.

Unaweza kukabiliana na kuzidi kwa protini zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba kwa mfumo huo wa mafuta. Mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia mlo wake kwa siku kama ifuatavyo:
Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika hali inayotakiwa.

Watu wengi wanatumia chakula cha wanga mwingi wakati wa usiku, muda ambao wanakwenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa tumboni na kwenye makalio.

Mazoezi ya viungo husaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili. Wanaume huwa na asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na wanawake ni asilimia 13 hadi 25.
Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni katika mapafu na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili. 
Kwa ushauri zaidi wasiliana na daktari.