Thursday, 30 July 2015

JE, KIPODOZI UKITUMIACHO HAKINA SUMU? SOMA HAPA UPATE KUJUA

Serikali ya Tanzania kupitia mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imevipiga marufuku baadhi ya vipodozi kuuzwa na kutumika kwa matumizi ya binadamu hususani ngozi/urembo kwani imebainika kuwa vina madhara makubwa kwa watumiaji.
Madhara hayo yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni madhara yanayotokea baaada ya muda mfupi na yale yanayotokea baada ya muda mrefu.
Madhara yanayojitokeza kwa muda mfupi ni pamoja na kubabuka ngozi na
ngozi kuwa nyekundu au mabaka meusi.
Madhara yanayojitojeza baada ya muda mrefu ni Kansa ya ngozi, kuharibika kwa figo, zinaangamiza mfumo wa fahamu hasa ubongo na kusababisha matatizo ya kusahau na msongo wa mawazo, magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama vile Asthma/Pumu ya ukubwani, kuharibika kwa mfumo wa homoni kwa akinadada na kusababisha matatizo katika via vya uzazi kama vile maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi, kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa, uvimbe kwenye kizazi, mama mjamzito ni rahisi kujifungua mtoto mwenye matatizo ya akili/taahira n.k

Tangu kuanza kwa udhibiti wa vipodozi nchini, aina 250 za vipodozi vimegundulika kuwa na viambata sumu na hivyo kupigwa marufuku kutumika nchini. Japo idadi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku imeongezeka lakini watumiaji ambao wengi ni akinadada na akinamama wamekuwa wagumu kuacha kiasi kwamba vipodozi hivi vimekuwa vikiuzwa kwa siri na wauzaji hivyo kufanya zoezi la uzuiaji wa vipodozi hivi kuwa gumu. Wanawake wengi wametawaliwa kuwa wakiwa weupe basi ndipo watapendeza au watapendwa zaidi na wanaume.

Cream na Lotion zilizopigwa marufuku zenye kiambato cha HYDROQUINONE ni Mekako Cream, Rico complexion cream, princess cream, extra clear cream, miki cream, viva super lemon cream, ultra skin tone cream, fade out cream, palmer's skin success(pack), fair & white active whitening cream, fair & white strong bleaching treatment cream, fair &white body clearing milk, maxi - tone fade cream, nadinola fade cream, clear essence medicated fade cream, peau claire body lotion, reine clair rico super body lotion, tura lotion, miki beauty cream, extra clair lightening body lotion, clear essence skin beautifying milk, tura skin toning cream, madonna medicated beauty cream, kiss medicated beauty cream, princess patra luxury complexion cream, envi skin toner, zarina medicated skin lightening clere lemon cream, binti jambo cream, malaika medicated beauty ceam, Dear Heart with Hydroquinone Cream, Nish Medicated Cream, Care plus fairness cream, Top clear cream, A3 Skin Lightening Cream, Clear Touch Cream, Rico skin tone, Ultimate skin lightening cream, Immediate Claire Lightening Body Cream, Skin Lightening Lotions containing Hydroquinone, Jaribu skin lightening lotions, Princes Lotion, Clear touch lotion, Super max tone lotion, No Mark Cream.

Pia zimo lotion kama G & G Dynamiclair lotion, G & G Teint Uniforme, G & G Cream Lightening Beauty Cream, Dawmy - lightening body lotion, Maxi White Cream, Bio Claire Lightening body lotion. Kundi lingine ni CREAMS za Amira cream, Jaribu Cream, Peau Claire Cream, Skin balance lemon cream, Skin Success Cream, Miss Caroline Cream, Lemonvate Cream, Movate Cream, Mediven Cream, Diproson Cream, Dermovate Cream, Top Lemon Plus, Lemon cream, Beta Lemon Cream na Unic Clear Super Cream. Kwa ujumla ni vipodozi vingi vilivyopigwa marufuku ambavyo vina viambata vya HYDROQUINONE, MERCURY, ALUMINIUM ZIRCONIUM COMPOUND, PHYTOLACEA, TIN OXIDE, MALIC ACID, APPOCYNUM CANNABIUM ROOT EXTRACT, TUSSILAGO FARFARA, BLUE CAP na STEROIDS.Tambua kuwa viambata hivyo ni sumu. Hivyo uonapo kipodozi chenye mojawapo ya hicyo viambata basi tambua hakifai kwa matumizi ya binadamu. Ushauri uliotolewa ni kutumia vipodozi ambavyo havina viambata hivyo au unaweza kutumia baadhi ya vipodozi vinavyotengenezwa kiasili.

Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000, Tunatoa huduma za Tiba kwa kutumia dawa zisizo na kemikali, dawa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda na ziko katika mfumo wa vidonge.