Thursday, 29 September 2016

MAAMBUKIZI KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE (PID

Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huhusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.



PID husababishwa na nini?

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.

Je mwanamke huambukizwaje PID?


Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na

  • Kufanya ngono isiyo salama
  • Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
  • Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
  • Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
  • Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
Dalili za PID ni zipi?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni

  • Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
  • Kupata maumivu ya mgongo
  • Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
  • Kupata homa
  • Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
  • Pia kutapika
Vipimo vya PID
Ili kuweza kutambua kama mwanamke ameambukizwa ugonjwa huu, tabibu anaweza kufanya vipimo kadhaa vikiwemo

  • Kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba
  • Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
  • Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na uambukizi huo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa kitaalamu huitwa Full Blood Picture.
  • Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa cervical culture
  • Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono.
  • Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yeyote katika mfumo wake wa uzazi.
Matibabu
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa. Hata hivyo ieleweke kuwa matumizi ya dawa hizi hufuata miongozo mbalimbali ambayo imewekwa na wizara au mamlaka za afya zinazohusika. Miongozo hii hutofautiana kati ya sehemu na sehemu au nchi na nchi, ingawa kiujumla Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo limeweka muongozo wake kwa ajili ya kufuatwa na nchi mbalimbali.

Miongoni mwa dawa hizo ni pamoja na Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin na Sulbactam kwa pamoja na Doxycycline; na Ceftriaxone au Cefoxitin pamoja na Doxycycline.
Ieleweke pia haishauriwi kujinunulia na kutumia dawa hizi bila kupata ushauri ushauri wa mtaalamu wa afya. Aidha ili kuondoa maumivu na kushusha homa, dawa kama Paracetamol (Panadol) yaweza kutumika.

Jinsi ya kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi


Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na

  • Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kama ikiwezekana kujizuia kabisa kufanya ngono.
  • Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa
  • Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).
  • Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.
Ped za NEPLILY SANITARY kwa sasa zipo maeneo ya Dar es salaam, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Bukoba, Babati, Iringa na Ngara. Ni ped maalum zenye dawa kwa ajili ya matatizo yote ya akinamama wanapokuwa hedhi. 
Faida kubwa ya ped hizi ni pamoja na kuondoa maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi, kurekebisha mizunguko mibovu ya hedhi, kuondoa miwasho sehemu za siri, kutokwa uchafu wa ajabu sehemu za siri, fangasi n.k

Text/whatsapp 0622925000
Call 0767925000

Tafadhari share kwa ajili ya wengine

ZIJUE FAIDA 48 ZA TANGAWIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU


Huwa inanishangaza sana ninapoutafakari ukuu wa Mungu kwa namna ambayo ametupa mimea mbalimbali muhimu kwa ajili ya afya zetu – Mwanzo 1:29. Maelezo yafuatayo kuhusu tangawizi yatakupa wewe ujuzi wa mmea mwingine wa asili usio na madhara ya kikemikali na kusaidia mwili wako kuwa na afya nzuri na ya kupendeza.

Tafiti mpya zinazidi kuonyesha namna mmea huu ulivyo wa muhimu kwa afya ya binadamu ikihusisha uwezo wake wa kudili na aina mbalimbali za kansa mwilini na tafiti nyingine zinaendelea kufanyika.

Tangawizi inaweza kuwekwa karibu kwenye kila chakula, iwe ni katika kuilainisha nyama nyekundu, kuongeza radha katika nyama au samaki, kama chai, kwenye juisi na kadhalika.

Binafsi napenda ikiwa kwenye juisi ya matunda ndiyo inakuwa tamu zaidi na inaenda kufanya kazi mwilini haraka zaidi.

Tangawizi ni zao la kibiashara na ni rahisi kutoka kimaisha kama utaamua kulima tangawizi ingawa ni zao la miezi mingi lakini ukivumilia utakula bata tu, gunia moja linauzwa kati ya laki 3 hadi 6 wakati wa msimu mzuri.

Tangawizi iliorodheshwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Marekani kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.
Tangawizi huongezwa pia katika vinywaji vingi vya viwandani zikiwemo soda ili kupata radha nzuri zaidi.
Leo nimekuletea hii juisi ya tangawizi, nimetumia tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.

Kazi 48 za tangawizi mwilini
1. Huondoa sumu mwilini haraka sana
2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi
3. Kuna viua vijisumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi
4. Huondoa uvimbe mwilini
5. Huondoa msongamano mapafuni
6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake
7. Huondoa maumivu ya koo
8. Huua virusi wa homa
9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini ikiwemo maumivu wakati wa hedhi
10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)
11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.
12. Tangawizi ina kiinilishe muhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”
13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r
elated cancer)
14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)
15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu(lung cancer)
16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kansa mbalimbali za tumbo
17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kansa za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi
19. Huongeza msukumo wa damu
20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo
21. Huzuia damu kuganda
22. Hushusha kolestro
23. Husafisha damu
24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa
25. Hutibu shinikizo la juu la damu
26. Husafisha utumbo mpana
27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma
28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI
29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu
31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu
32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa
33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
34. Husaidia kuzuia kuharisha
35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu
36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
37. Hutibu homa ya kichwa
38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito
40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)
41. Huimarisha afya ya figo
42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
43. Ina madini ya potassium ya kutosha
44. Ina madini ya manganese ambayo ni muhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha
46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium
47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene
48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

Ped za NEPLILY SANITARY kwa sasa zipo maeneo ya Dar es salaam, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Bukoba, Babati, Iringa na Ngara. Ni ped maalum zenye dawa kwa ajili ya matatizo yote ya akinamama wanapokuwa hedhi.
Faida kubwa ya ped hizi ni pamoja na kuondoa maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi, kurekebisha mizunguko mibovu ya hedhi, kuondoa miwasho sehemu za siri, kutokwa uchafu wa ajabu sehemu za siri, fangasi n.k

Text/whatsapp 0622925000
Call 0767925000


Tafadhari share kwa ajili ya wengine

MWANAMKE: MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOHITAJI KUSHIKA MIMBA


Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu asishike mimba. Sababu hizo zinaweza zikawa zinamhusu mwanamke, mwanamume au wakati mwingine kutojulikana kabisa hali hiyo imesababishwa na nini. Wataalamu wanasema kwamba kwa miaka 20 iliyopita matatizo yanayohusu kushindwa kuzaa yameongezeka kwa kiwango kikubwa na asilimia 25 ya watu wanaotaka kubeba mimba na kuzaa mtoto wanakabiliwa na tatizo hilo. Ni kweli kuwa kwa kawaida watu wengi hubeba mimba na kujaaliwa mtoto pale tu wanapofanya tendo la ndoa. Lakini jambo hilo halitokei kwa watu wote na ingawa kwa baadhi ya watu kila kitu huonekana kwenda sawa lakini pia hushindwa kubeba mimba. Utafiti unaonyesha kwamba katika kila familia au 'couples' 5 zinazojamiiana katika wakati muafaka wa ovulation ni moja tu ndio hufanikiwa kupata mtoto, huku karibu wanawake 9 kati ya 10 wakifanikiwa kushika mimba baada ya kujaribu kutafuta mtoto kwa mwaka mmoja mzima bila kuzuia mimba. Hivyo basi nawaomba wale ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufuata maelekezo ili waweze kushika mimba lakini hawakufanikiwa, wasife moyo kwani ipo siku jitihada zao hizo zitazaa matunda.
 
Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba…
• Kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kabla ya yote unamuona Daktari wako au unakwenda hospitalini na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba. Baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa ni pamoja na:
1. General examination au uchunguzi wa jumla.
2. Kipimo cha kensa au Pap smear.
3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambayo yanaweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.
4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.
5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na kidhahiri anaonekana hana tatizo lolote.
6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyama (red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxopmasmosis infection.
7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:-
• Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwilini.
• Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
• Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanaume baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)
• Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanaume.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomsaidia mwanamke kushika mimba:
• Anza kutumia vidonge vya Folic Acid, vidonge hivyo mbali ya faida nyinginezo humkinga mtoto atakayezaliwa na magonjwa ya ubongo. (Neural Tube Defect) kama vile Spinal Bifida na mengineyo. Dozi ni kwa uchache miligramu 0.4 za Folic acid kwa siku, miezi mitatu kabla ya kuanza hata kutafuta mtoto.
• Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanaume aweze kuboresha na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio. Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.
• Jiepushe kunywa kahawa na vinywaji vinginevyo vyenye caffeine. Wataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.
• Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.
• Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.
• Hakikisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto kali sana kama vile mwanaume wanaofanya kazi kwenye matanuri ya kupika mikate, viwanda vya mafuta na miale hatari baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kutozaa. Hivyo kabla mwanamke hajaanza kujilaumu kwa nini hashiki mimba, mwanaume wake pia anapaswa kufanyiwa uchunguzi kamili kuhusiana na suala hilo.
 Pengine ni suala ambalo wengi hatulijui kwamba katika tiba iwapo mke na mume au mtu na mwenzi wake wana tatizo la kutopata mtoto, wawili hao kwa pamoja hupaswa hufanyiwa vipimo na wala sio mwanamke mwenyewe. Hivyo iwapo unashindwa kushika mimba, hakikisha pia mwenzi wako hana tatizo pia.
Wanaume pia kama walivyo wanawake hukabiliwa na matatizo mengi tu yanayosababisha familia kukosa watoto. Matatizo kama vile upungufu wa mbegu za kiume, uchache wa mbegu, kutokuwa na kasi mbegu na mengineyo ni miongoni mwa matatizo kibao ambayo mwanaume anaweza kuwa nayo na kukosa mtoto. Hivyo tabia ya kuwatizama wanawake kwa jicho la lawama katika jamii na kuwanyooshea kidole pale mimba inaposhindikana kushika ni kinyume cha ukweli wa kitiba na uhalisia.
• Usichoke kufuata mzunguko wako wa Ovulation na kufanya tendo la ndoa katika wakati ambao mwili wako (ewe mwamamke) uko katika siku za kuweza kushika mimba.

Kama huzijui vizuri siku zako za kushika mimba basi usisite kuwasiliana na sisi ili tukueleweshe, na endapo siku zako za hedhi au mzunguko wako haueleweki, unapata maumivu makali wakati wa hedhi au wakati wa tendo la ndoa, una fangasi/miwasho/harufu kali sehemu za siri pia usisite kuwasilina nasi ili tukupatie ped maalumu zinazotibu na kumaliza kabisa matatizo hayo.

MAWASILIANO
0767925000
0622925000 - whatsapp

TAFADHALI SHARE MAKALA HII ILI NA WENGINE WAJIFUNZE