Friday, 4 December 2015

HIZI NI FAIDA ZA TANGAWIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU



ZIJUE FAIDA ZA KUTUMIA TANGAWIZI.

TANGAWIZI ZINA UWEZO WA KUTIBU MAGONJWA ZAIDI YA 72



Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi.
Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania Tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu Kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.
Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia.

Tangawizi inatumikaje ?:
Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini Kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama Dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga.

Nini Faida ya Tangawizi?
Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.

Pia kiungo hiki kinafaida zaidi kwa Wagonjwa hasa walio athirika na Ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo chonde kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya Maajabu ya Mmea huu wa Tangawizi.

Jinsi ya kuitumia kama Dawa:
Tangawizi ikiwa imesagwa au Mbichi iliyopondwa pondwa inaweza kutumika kama Kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.

Namna rahisi ya kuitumia Tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mbadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na Caffein ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini (soma kuhusu kansa na uzito kupita kiasi kuyajua madhara ya kutumia majani ya chai nyeusi), Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mbogamboga zingine, inaweza kuongezwa katika juisi freshi pia na kuleta radha nzuri ambayo ni dawa pia.

Hutibu Magonjwa gani ?
Tangawizi husaidia yafuatayo:

Kuongeza hamu ya kula,
Kupunguza kichefuchefu
Kutapika, kuharisha,
Kisukari,
Shinikizo la damu,
Kuongeza msukumo wa damu,
Kutoa sumu mwilini,
Maumivu ya tumbo na
Gesi tumboni.
husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni.
husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu na magonjwa mengine mengi.

Kama utakuwa makini au kuwahi kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI basi magonjwa hayo hapo juu ni kati ya Magonjwa nyemelezi yanayo wasumbua sana hawa ndugu zetu hivyo wakitumia Tangawizi basi wataweza kuondokana kabisa na matatizo hayo na kuishi vizuri na kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuepukana na kulala tu kitandani.

Kwa tiba na ushauri kwa Magonjwa tabia yote mfano Kisukari, Presha, Moyo, Vidonda vya tumbo, Kupata choo kigumu, matatizo ya hedhi, ugumba/utasa, upungufu wa nguvu za kiume n.k, wasiliana nasi kwa;
0784925000
0767925000
0622925000 Whatsapp

Masha Masanja - Health Consultant
posted from Bloggeroid

TAMBUA FAIDA ZA TUNDA LA UKWAJU



Hizi Ndio Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!

Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla

Watu waishio bara la Asia, Carribian na America ya kusini wanajua kuwa kula ukwaju maana yake ni Afya Njema.


Ukwaju unaoliwaa katika maeneo hayo una faida nyingi

Kwa hiyo siku nyingine unapoenda kufanya manunuzi ya vyakula
hakikisha unanunua na ukwaju. Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia
ambalo limefungwa na kasha gumu. Ndani ya kasha hilo kuna vifundo vilaini ambavyo ndani yake kuna mbegu nyeusi.
Vifundo hivi ndiyo ambavyo watu wanakula ili kupata virutubisho na
faida za kiafya za ukwaju.

Ukwaju una ladha fulani ya uchachu
ukiwa bado mchanga, lakini kadiri unavyozidi kukomaa unakuwa na ladha tamu. Ingawa ukwaju unakuwa na utamu kadiri
unavyokuwa na kukomaa, kiujumla ukwaju ni mchachu.

Katika nchi kama Jamaica, Mexico, Aruba na India, ukwaju
unachanganjwa na sukari na kuuzwa kama pipi katika mitaa na
madukani. Kula ukwaju au bidhaa zitokanazo na ukwaju kuna faida sana. Ukwaju umejaa Vitamini, fiber, potassium, magnesium na virutubisho vingine muhimu kwa afya njema.

Lakini kati ya faida zingine nyingi za virutubisho na kiafya za
ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni za muhimu zaidi, na ni kama
zifuatazo:
1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha antioxidants ambazo zinasaidia kupigana na saratani. Ukwaju una carotenes, Vitamini C, flavanoids na vitamin B zote.

2. Ukwaju unakuepeusha na ukosefu wa Vitamini C.

3. Ukwaju unasaidia kupunguza homa na kukupa ulinzi dhidi ya
mafua.

4. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni.

5. Ukwaju unakusaidia kutibu matatizo ya nyongo.

6. Juisi ya ukwaju hutumika kama kitu cha kustarehesha mwili.

7. Ukwaju unapunguza cholesterols mwilini.

8. Ukwaju unasaidia kuwa na moyo wenye afya njema.

9. Ukwaju ukiunywa unasaidia kupooza koo.

10. Ukwaju ukiupaka kwenye ngozi unasaidia kutibu uvimbe.

Kwa Tanzania ukwaju unapatikana kwenye masoko
karibu yote.

Kwa tiba na ushauri wa magonjwa tabia yote mfano Kisukari, Presha, Moyo, Vidonda vya tumbo, Kupata choo kigumu, matatizo ya hedhi, ugumba/utasa, upungufu wa nguvu za kiume n.k, wasiliana nasi kwa namba zifuatazo;

0784925000
0767925000
0622925000
Masha Masanja - Health Consultant

posted from Bloggeroid