Saturday, 16 July 2016

SIKU YA KUSHIKA MIMBA MZUNGUKO MFUPI - 2


Mungu ndiye muumba watu wote na viumbe vyote juu na chini ya jua, hilo halina pingamizi wala ubishi na lazima tumshukuru Mungu kwa hilo, ila alitoa amri ya ndoa kwamba ZAENI MKAONGEZEKE kwa hiyo kila mtu anayependa kutimiza amri hii yafaa awe na maarifa.

Kwa wale wasiojua namna ya kuhesabu mizunguko yao basi ni muhimu kurudi katika maada zilizopita na kisha kujifunza namna ya kuhesabu mzunguko wako. Tambua ya kwamba mzunguko wa bleed (hedhi) ni tofauti sana na siku za bleed (hedhi).

VITU VYA KUJUA
1. Siku za bleed (hedhi) ni kuanzia na siku ya kwanza unapopata bleed hadi siku ile unamaliza bleed.
2. Wakati mzunguko wa bleed huanza siku umepata bleed mpaka siku moja kabla hujapata bleed nyingine.
Mfano umepata bleed tarehe 1 mwezi wa saba na bleed hiyo ikaisha tarehe 05 basi siku za bleed ni 5 na zimeanza tarehe moja na zikaisha tarehe 5.
Kama bleed nyingine umeipata tarehe 29 mwezi wa 7, basi mzunguko wako wa bleed ya mwezi wa saba umeanza tarehe 01 mwezi wa saba na ukaisha tarehe 28 mwezi wa saba. Mzunguko huo ni wa siku 28. Mzunguko wa mwezi wa 8 Umeanza tarehe 29 mwezi wa 7.
Ukiwa na mzunguko mfupi usiogope kwa kuwa bado unayo nafasi kubwa ya kupata mtoto na watu wengi tu wapo wana watoto.

Lazima ujue mzunguko wako kwanza ni wa siku ngapi. Mfano kama umekuwa na mzunguko wa siku 21 kwa muda wa miezi mitatu mfululizo na mfano umepata bleed tarehe 10 mwezi wa saba basi siku yako ya uzazi haiwezi kuwa siku ya 14 tangu kupata bleed. Bali ni siku ya 7 tangu umepata bleed.

HEBU ZAMA NDANI HAPA UJIFUNZE

Mzunguko wa siku 21 siku ya uzazi ni siku ya (7)  tangu upate bleed. Kwa hiyo kama utapata bleed siku 3 basi siku ya tano unatakiwa uanze tendo la ndoa. Mfano mzuri ni kama ufuatao. >>>Marry ameingia bleed leo tarehe 16 mwezi wa 7 na mzunguko wake kila mwezi unamchukua siku 21. Huyu Marry anachukua siku 3 za bleed. Basi siku zake atahesabu hivi tarehe 16 ni siku ya kwanza yaani leo tarehe16 ni siku ya kwanza ya bleed, kesho tarehe 17 ni siku ya pili ya bleed, kesho kutwa tarehe 18 ni siku ya tatu ya bleed, tarehe 19 ni  siku ya nne bleed imeisha, tarehe 20 siku ya tano bleed imeisha - anza hapa kukutana na mwenzako, tarehe 21 ni siku ya sita endelea na tendo na tarehe 22 siku ya saba endelea na tendo yai linatoka. Unashauriwa kuanza mapema ili kuongeza nafasi ya mbegu kulikuta yai.

MZUNGUKO WA SIKU 22,23,24,25 na 26

Mzunguko wa siku 22 yai linatoka siku ya 8 wewe anza tendo siku ya 6, 7 na 8
Mzunguko wa siku 23 yai linatoka siku ya 9 wewe anza tendo siku ya 7
Mzunguko wa siku 24 yai linatoka siku ya 10 wewe anza tendo siku ya 8
Mzunguko wa siku 25 yai linatoka siku ya 11 wewe anza tendo siku ya 9
Mzunguko wa siku 26 yai linatoka siku ya 12 wewe anza tendo siku ya 10

Kumbuka kuanza siku moja au mbili kabla ya siku ya yai kutoka pia unaweza ongeza siku 1 au mbili baada ya siku yenyewe hii ni kwa sababu mizunguko huwa inabadilika badilika kutokana na sababu mbalimbali kama ugonjwa na dawa nzitonzito mshituko kama wa kufiwa, kubadilika kwa hali ya hewa na pia mabadiliko ya mwili kama kunenepa.

Kumbuka kama umekaa muda mrefu hujapata mtoto ni lazima ufike hospitalini na kupima na kupata majibu sahihi. Ni muhimu pia ukawa uko karibu na mwenzako, una afya nzuri na mko vizuri kiuhusiano.

UMUHIMU WA CHAKULA BORA
Ni muhimu ule chakula bora na sio bora chakula. Imethibitika ya kwamba asilimia zaidi ya 50 ya matatizo ya hedhi hutokana na kutokula vizuri. Ulaji wa chips, soda, pombe kupindukia, kula wanga mwingi na sukari ni hatari kwa maisha ya ndoa. Unatakiwa kula chakula halisi (Real Food) chakula fresh na chakula cha asili. Vyakula hatari ni pamoja na vyakula vya paketi na makopo na kuku wa kisasa (chicken)

TUNAKUSAIDIAJE?
1.TUNATOA ELIMU YA AFYA KATIKA MAHUSIANO. Endelea kufuatilia mada zetu hapa ili kujifunza mengi zaidi, SHARE NA MARAFIKI ZAKO na pia Elimisha wengine.
2. PEDI ZA NEPLILY – Tumia pedi za neplily pads mara kwa mara. Pedi za Neplily ndio pedi bora kabisa kwa sasa kwa akinadada na akinamama. Zinaondoa miwasho, harufu mbaya UTI na fangasi za ukeni na miguuni. Zinarekebisha uchachu uliozidi ukeni na pia zinarekebisha hedhi zilizovurugika.  Zipo MWANZA, SHINYANGA, BUKOBA, DODOMA, IRINGA, BABATI NA DAR 
3. KUKOKOTOA SIKU YAKO YA UZAZI – Wasiliana nasi kwa meseji au whatsapp tu ukiwa umeshaandika siku zako za bleed za miezi minne 0622925000

KUOTA NYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA(BAWASIRI) -2

Mmoja wa wasomaji wa gazeti hili aliyejitambulisha kwa jina moja la Michael anauliza: “Katika sehemu zangu za haja kubwa, kuna vivimbe kama vitatu na ninapata taabu kukaa. Nimetumia dawa aina ya Anusol lakini bado sijapata nafuu, je naweza kutibiwa kwa njia gani za kisasa?” Msomaji mwingine nae anauliza: “Je dawa ya ugonjwa wa Bawasiri ni ipi hasa?”

Msomaji wetu mwingine pia anaeleza kuwa amesumbuliwa na maradhi ya Bawasiri kwa zaidi ya miaka kumi sasa na angependa kujua kama ugonjwa huu unatibika. Nae anauliza: “Je nitapata tiba ya ugonjwa huu?” Msomaji mwingine anamuelezea mchumba wake ana kinyama cha Bawasiri kimetoka katika njia ya haja kubwa na anauliza: “Je akienda hospitalini watakikata au atapewa dawa tu na kinyama kitatoka?”

Kutokana na maswali hayo na mengine mengi ambayo sikuyaandika hapa, nimeona kuwa ipo haja kwa siku ya leo tuangalie kwa kina jinsi maradhi haya yanavyotibiwa hospitalini kwa njia ya tiba zenye ushahidi wa kisayansi.

Kwanza kabisa ni vizuri kuelewa kuwa, kuna maradhi ya aina mbalimbali yanayotokea katika njia ya haja kubwa ambayo yanaweza kuwa na dalili zinazofanana na zile za maradhi ya bawasiri. Kwa sababu hiyo, ni vizuri kupata uchunguzi wa kitabibu kabla ya kuamua kuwa unaugua maradhi ya bawasiri.

Uchunguzi na vipimo
Kabla ya matibabu yoyote, daktari mwenye ujuzi wa tiba, atachunguza kwa kuangalia sehemu ya njia ya haja kubwa na kuona kwa macho hali halisi ilivyo. Baada ya hapo daktari anaweza kufanya kipimo kwa kutumia kidole cha shahada. Kidole hiki kikiwa ndani ya mpira wa kuvaa mikononi, kinaweza kulainishwa kwa vilainishi salama na kuingizwa katika njia ya puru ili kubaini hali ya uvimbe.

Daktari pia anaweza kutumia kipimo cha kutazama moja kwa moja katika njia ya haja kubwa kijulikanacho kwa jina la Proctoscopy au kipimo cha kutazama ndani ya utumbo mpana, Sigmoidoscope. Kipimo cha maabara cha kubaini damu iliyofichika; faecal occult blood test, nacho kinaweza kufanyika pale bawasiri daraja la kwanza inapokuwa ndani na inapokuwa vigumu kuibaini kwa kipimo cha kidole au proktoskopi.

Matibabu
Matibabu ya bawasiri kimsingi hutegemea dalili, hali na hatua ya ugonjwa. Kwa kawaida tiba ya awali ni kurekebisha mfumo wa maisha na mtindo wa kula. Mgonjwa hushauriwa kunywa maji mengi na kula vyakula vitakavyolainisha kinyesi kila siku. Vyakula hivyo ni kama vile matunda na mbogamboga kwa wingi, vyakula asili visivyo vya kukoboa, aepuke chumvi nyingi na pombe.

Mara nyingi mgonjwa hutibiwa kwa njia za kawaida zisizohusisha tiba kwa njia ya upasuaji. Mgonjwa mwenye kinyama au kivimbe kinachojitokeza nje, ataelekezwa jinsi ya kukalisha eneo la haja kubwa katika maji ya vuguvugu kwa muda wa dakika 15. Atatakiwa kufanya hivyo mara nyingi kadiri iwezekanavyo hasa kila baada ya kujisaidia.

Mgonjwa pia anaweza kupewa dawa za kupaka kwenye uvimbe ulioko katika njia ya haja kubwa au vidonge vya kuingiza ndani ya tundu la njia ya haja kubwa. Tiba hizi zitasaidia kupunguza uvimbe na maumivu anayoyapata mgonjwa wa bawasiri hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa.

Kama maumivu yatazidi, tiba rahisi iitwayo ‘Rubber band ligation’ inaweza kufanyika kwa bawasiri iliyoko ndani ya puru, yaani pale mishipa inapokuwa haijajitokeza nje. Bawasiri daraja la kwanza na la pili. Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo lililoathirika. Tiba nyingine ni ile ya kuunguza na kufunga uvimbe wa kinyama kwa kifaa maalumu (laser therapy).

Kama uvimbe wa mishipa ya vena ni mkubwa sana na unajitokeza sana nje ya puru (bawasiri daraja la 3 na 4), upasuaji unaweza kufanyika na hapa kinyama hukatwa na kuondolewa, kisha damu inayotoka hudhibitiwa kitaalamu. Tiba hii kitaalamu hujulikana kwa jina la haemorrhoidectomy.

Katika hospitali kubwa, aina nyingine ya upasuaji wa kisasa zaidi inaweza kufanyika pia. Tiba hii kwa jina la kitaalamu hujulikana kama Doppler-guided Haemorrhoidal Artery Ligation Operation (HALO) na wengine hupendelea kuiita Transanal Hemorrhoidal Dearterialization-Hemorrhoidectomy (THD).

Tiba hii ya upasuaji hufanyika bila kukata kinyama na bila kutumia dawa ya usingizi ingawa ganzi inatumika. Ni tiba ambayo haisababishi maumivu na mgonjwa anaweza kuendelea na shughuli zake baada ya saa 48 tokea kipindi cha kufanyiwa upasuaji.

Katika tiba hii, mishipa yote inayojitokeza nje, haikatwi bali inarudishwa ndani ya puru na kushonwa kwa nyuzi zinazoyeyuka zenyewe ili ijishikize kwenye misuli ya ndani ya haja kubwa na mishipa yote inayopeleka damu katika kinyama kinachovimba, hufungwa.

Lengo la kuifunga ni ili kuizuia isipeleke damu nyingi kwenye uvimbe. Baada ya hapo, sehemu hiyo hufunikwa kwa bendeji inayoyeyuka yenyewe baada ya kipindi fulani.

Dk Sushil Maslekar, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Njia ya Haja Kubwa katika Hospitali ya Spire Leeds nchini Uingereza, anasema kuwa tiba hii ni nzuri, haina madhara na inaondosha dalili zote za bawasiri kwa ufanisi mkubwa.

Utafiti wa miaka 10 wa Pravin J. Gupta na Surekha Kalaskar uliochapishwa mwaka 2008 katika jarida la sayansi za tiba liitwalo ‘Annals of Surgical Innovovation and Research’ toleo la 2(5), unabainisha kuwa upasuaji na kushona ngozi ya tundu la haja kubwa katika maeneo matatu ambayo kwa kawaida hutokeza bawasiri, unatoa matokeo mazuri zaidi ya uponaji wa bawasiri.

Pamoja na hayo yote, katika matibabu ya Bawasiri ni muhimu kukumbuka kuwa tiba hizi zinaponyesha lakini tatizo linaweza kujitokeza tena kama vyanzo vyake havikudhibitiwa. Ili kupona kabisa ni lazima mgonjwa arekebishe mfumo wake wa maisha na mtindo wa lishe.