Sunday, 16 August 2015
TATIZO LA NGOZI (ECZEMA)
ECZEMA au pumu ya ngozi au kwa kitaalamu huitwa atopic dermatitis ni tatizo la ngozi litokanalo na mzio au allergy ya ngozi na reactions za mazingira yanayomzunguka mtu au baadhi ya familia zenye historia ya ugonjwa wa Pumu/Asthma.
Neno Eczema ambalo ndiyo jina la ugonjwa huu ni la Kigiriki linamaanisha kututumka sehemu ya ngozi, hali amabayo huonekana pindi mgonjwa anapopata maradhi haya. Maradhi haya ya ngozi yanachangia asilimia arobaini (40%) ya magonjwa yote ya ngozi yanayoripotiwa Hospitalini.
Maradhi haya hushambulia zaidi watoto na huweza kupitiliza hadi ukubwani, lakini watu wengi huweza kupona au kupungua kadri mtoto anavyozidi kukua. Watafiti wanasema kuwa kumekuwa na ongezeko la maradhi haya katika kipindi cha miaka ya usoni hali inayoashiria kuwa maradhi haya ni ya kurithi (atopic eczema).
Maradhi haya huweza pia kujitokeza ukubwani ingawa ni mara chache Maradhi haya huathiri watu wa jinsia zote kwa uwiano sawa yaani wanaume na wanawake.
DALILI ZA TATIZO
Maradhi haya ni ya muda mrefu, kwa hiyo mtu huweza kukaa nayo kwa muda mrefu ingawa siyo muda wote ngozi itaonyesha dalili za maradhi. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za ugonjwa huu:
-Muwasho wa ngozi usio wa kawaida na kupelekea ngozi kupata vipele kisha kuwa kavu na ngumu
-Kuvimba kwa ngozi
-Sehemu ya ngozi iliyoathirika huwa inatutumka
-Ngozi huwa inakuwa na mipasuko inayoweza kuruhusu vimelea vya maradhi kushambulia sehemu ya ndani ya ngozi
-Maeneo ya ngozi yaliyoathirika huweza pia kuwa na malengelenge na hata kutoa maji
-Bila matibabu ya haraka ngozi inaweza fanya vidonda
-Ingawa maeneo yenye kuathirika huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini pumu ya ngozi hupenda kushambulia sehemu za mikono hususani eneo baada ya kiwiko kwenda chini, miguu, viganja vya mikono, eneo la nyuma ya magoti (mkunjo wa mguu kwenye eneo la goti), maungio ya mkono kwenye kiwiko, shingo, sehemu ya juu ya kifua, wagonjwa wengune hupata maambukizi kwenye maeneo yanayozunguka macho, watoto wengi hupata pumu ya ngozi kwenye uso.
Kwa wenye pumu ya ngozi mbaya kabisa sehemu kubwa zaidi ya mwili hututumka na vidonda pamoja na kutokwa na majimaji kwenye maeneo yenye vidonda. Wakati maradhi haya yanapoanza hunyesha dalili za muwasho ambao husababisha mgonjwa kujikuna na kumsababishia mikwaruzo kwenye ngozi ambayo nayo husababisha vimelea vya maradhi kuweza kupenya na kusababisha vidonda vikubwa zaidi kutokea kwenye eneo la ngozi. Vidonda vinapotokea hasa kwa mtoto huweza kumsababishia msongo wa mawazo, kama hali hii ikimtokea kwa mtoto wa shule basi hata mahudhurio yake shuleni yatakuwa mabovu au hata kufeli mitihani.
SABABU ZA MASHAMBULIZI ZAIDI
-Kuogea maji ya moto kwa mrefu
-Kuruhusu ngozi ya mwili kukaa ikiwa kavu kwa mrefu (bila kupaka mafuta)
-Kuwa na msongo wa mawazo
-Kubadili joto la mwili yaani kusafiri kutoka kwenye eneo la joto kwenda eneo lenye baridi au kinyume chake
-Kuvaa mavazi yasiyo ya pamba (cotton)
-Uvutaji wa sigara
-Kukaa kwenye vumbi
-Kukaa kwenye mchanga
-Matumizi ya mafuta ya mwili yanayosababisha mzio wa mwili
-Matumizi ya sabuni zinazosababisha mzio wa mwili
-Ulaji wa chakula kinachosabisha mzio wa mwili, mfano wale wenye mzio wa vyakula vinavyopatikana kwenye maji au baharini.
SABABU ZA PUMU YA NGOZI
Wataalamu wanasema kwamba maradhi haya mtu huzaliwa nayo na kuwa huwa yanarithiwa. Athari za maradhi haya huzidi kutokana na sababu nyingine za ndani au nje ya mwili.
Vitu kama manyoya ya wanyama au mbegu za mimea huweza kusababisha mzio ambao huweza kuleta madhara makubwa zaidi kutokea kwenye ngozi.
Mtu mwenye dalili au tatizo hili ni vyema awahi kuanza matibabu au anaweza kuwasiliana na sisi kwa namba 0767925000 au whatsapp 0622925000 tutampatia dawa za vidonge atakazozitumia kwa miezi mitatu na tatizo hilo litaisha. Dawa hizi huanza kwa kuondoa chanzo cha tatizo na kuiacha ngozi yako ibaki kuwa nzuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nahangaika na pumu, naimba kwaya imefikia siwezi nakohoa kifua kinabana,
ReplyDeleteOoh good article I have never read
ReplyDelete