Showing posts with label tiba kwa wanawake. Show all posts
Showing posts with label tiba kwa wanawake. Show all posts

Monday, 25 July 2016

MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI - 2


Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia uwepo wa hii somo hili ikiwa leo tunaendelea sehemu ya pili. Mada yetu inasomeka hapo juu linawatokea Zaidi wanawake pasipo wao kutambua tatizo karibu asilimia 30%-45% ya wanawake wote wana matatizo haya huwa wanafanya tu tendo la ndoa kuwaridhisha waume zao na wao kutokufurahia tendo hili la kipekee.

~tatizo hili hutokana na sababu tofauti mfano uwiano mbaya wa homoni nk
~Mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na mambo makuu mawili ambayo ni matatizo ya kimwili na matatizo ya kisaikolojia kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya somo hili.

UTAJIGUNDUAJE KAMA UNA TATIHili O HILI?

Hili tulilisema sehemu iliyopita, mojawapo ni kusikia maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa, kingine ni kwamba una uwezo wa kufanya tendo mara moja tu huhitaji tena maana mzunguko wa kwanza wenyewe hata haukufika mwisho, tutakuja kuona mbeleni kabisa madhara ya hali hii kwani hatari ni kubwa kuliko unavyofikiria wewe mpenzi msomaji wa makala hii.


JINSI YA KUJIKINGA NA MATIBABU YAKE
Matibabu yake Hospitali ni magumu kwani hakuna dawa maalumu na Zaidi hufanyika kupitia vipimo vya uchunguzi, historia ya mhusika pamoja na Dalili za magonjwa mbalimbali, pamoja na hayo tatizo hili unaweza kulidhibiti kwa kufanya yafuatayo
-EPUKA KUVUTA SIGARA NA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI
-ZINGATIA ULAJI ULIO SAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI
-ONDOA MAWAZO NA HUZUNI
-BADILISHA MFUMO WA MAISHA YAKO
-ONGEZA UPENDO KATIKA MAHUSIANO YAKO
-WEKA MAZINGIRA MAZURI NA MUDA WA KUFANYA TENDO LA NDOA
-BADILISHA ENEO LA KUFANYIA MAPENZI, SIYO KILA SIKU KITANDANI TU.


Kaa tayari kwa sehemu ya tatu ya somo hili ambapo tutajifunza MWANAUME UFANYE NINI KAMA MKEO/MPENZI WAKO HAFIKI KILELENI.

MASHA MASANJA
Whatsapp 0622925000

TAFADHALI USISAHAU KUSHARE, KU-COMENT, KU-LIKE NA KUWAALIKA WENZAKO KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK "Mimea Yenye Ufumbuzi Wa Matatizo Yako" KWANI KUNA MASOMO KIBAO YAPO PALE KWA AJILI YA AFYA YAKO.


Saturday, 23 July 2016

TATIZO LA MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA - SEHEMU YA 1

VISABABISHI VYA MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA

        Kufika kileleni ni nini?
  Ni kiwango cha juu kabisa cha utamu, hisia, raha, msisimko wakati wa tendo la ndoa wakati ambapo misuli ya uke au uume hukaza.

        Kwa mwanaume huambatana na kutoa manii (ejaculation).
Wengine wakifika kileleni hupiga kelele sana, wengine huongea maneno ovyo ovyo hata matusi, wengine huzimia kabisa, wengine huwakwida wapenzi wao kama vile kibaka, wengine hutulia kimya na kupitiliza usingizi na wengine ukiwauliza wanasema mahali walikuwa ni kama vile walikuwa hewani, wengine kama vile walikuwa wananamwona Bwana (Yesu) n.k ilimradi tu ni raha na utamu. Na ni kweli Mungu alitupa zawadi ya ajabu na hii ni kujulisha kwamba Mungu alituumba tena kwa namna ya ajabu.  Pia wengine huita kufikia mshindo, wengine huita coming, wapo ambao kwa tendo moja la ndoa huweza kufika kileleni zaidi ya mara moja.

        JE, MWANAMKE NA MWANAUME HUFIKA KILELENI KWA PAMOJA?
        Kwa wanaume kufika kileleni ni suala ambalo ni automatic, halina mjadala, kitu cha msingi kwake ni kujitahidi asifike mapema kileleni ili amfikishe mke wake pale anatakiwa kufikishwa, kwani mara nyingi mwanaume akifika kileleni hupoteza uwezo wa kuendelea na tendo.

        Katika nchi zilizoendelea kama USA na Canada utafiti mwingi unaonesha kwamba asilimia 15 % ya wanawake hufika kileleni mara zote.
        Asilimia 48 % ya wanawake mara nyingi hufika kileleni.
        Asilimia 19 % ya wanawake ni kawaida kufika kileleni lakini si mara nyingi
        Asilimia 11 % ya wanawake ni nadra sana kufika kileleni na
        Asilimia 7% ya wanawake hawajawahi kufika kileleni na hawajui ni kitu gani.

        Hapa ni wanawake kutoka nchi zilizoendelea ambako elimu kuhusu mapenzi ni kubwa sana.
        je, kwetu nchi zilizogoma kuendelea hali itakuwaje?
        Ukizingatia wanaume wengi bado hawajajua nini wanawake wanahitaji ili kufikishwa kileleni?

        Pia kuna baadhi ya wanawake ambao hata wasipofika kileleni hawana shida wanaridhika tu bora maisha yanaenda.

        Nini Kitu muhimu kuhusu mwanamke kufika kileleni?
        Wanawake wanaweza kuendelea kupata utamu hata baada ya kufika kileleni hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anabaki ndani ya uke hadi anahitimisha tendo zima (conclusion) angalau kwa dakika 10 au 15 ndo ukimbie kuoga au kupiga usingizi siyo kumwacha kiumbe wa watu kwenye mataa akiugulia kwa kumuondolea utamu na raha.

        Tendo la ndoa huwa ni la kuridhisha sana hasa pale mume anapomfahamu vizuri mwanamke na kile anahitaji kwa kumfanyia utundu wote wa kuchokonoa sehemu zote ambazo zinaweza kumhakikishia kwamba atafika kileleni.
        Lakini pia mwanamke ana sehemu kubwa sana ya yeye kujihakikishia anafika kileleni si mwanaume tu ni suala la wote.

        Je sababu kubwa za mwanamke kufika kileleni ni nini?
        -Kukeketwa (Female Genital Mutilation).
        Kukeketwa ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake.
        Katika Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya.
        Ingawa wanawake waliokeketwa huweza kurudia hali ya kuweza kufika kileleni, walio wengi huathiriwa sana na hiki kitendo na kuwasababishia kushindwa kufika kieleleni.

        -Dini, jadi na utamaduni:
        Kuna baadhi ya mitazamo na malezi ya dini, jadi au tamaduni huwapa wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na maana kuhusiana na tendo la ndoa.
        Katika dini, jadi, na tamaduni nyingi ukiacha jando na unyago, elimu ya mwanamke kuhusu mwili na uzazi havifundishwi wala kutamkwa matokeo yake wanawake wengi hawaijui miili yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa kiume anamuoa binti hajui chochote kuhusu mwili wa huyo mwanamke na mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu mwili wake mwenyewe, akiguswa chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya mtoto, hapo utategemea atafikishwa kileleni kweli?

        -Kisaikolojia.
        Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.
        Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.)
        Hofu labda ya kuachwa, mashaka, kutojiamini, kukasirika, donge moyoni, kisirani au mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke kutofika kileleni.
        -Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na kupata hisia halisi (sensations).
        Kuwa na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa
        Mawazo hasi (Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchovu.

        -Kibailojia
        Kama vile kuwa na mfumo ovyo wa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya viungo vya uzazi pia huchangia.
        Anaweza kuwa na uvimbe au kisukari pia huchangia. Pia hitilafu za viungo baada ya kufanyiwa upasuaji hasa sehemu ya uke.

        -Umri (Menopause)
        Kuna wakati mwanamke kuanzia miaka 45 – 55 hupata mabadiliko ya upungufu wa homoni na huo upungufu husababisha sehemu ya uke kuwa kavu wakati wa tendo la ndoa.
        Kuwa na uke mkavu huchangia katika ufanisi wa tendo la ndoa kuwa mdogo na hatimaye kushindwa kufika kileleni
        Si kweli kwamba mwanamke akizeeka uwezo wa tendo la ndoa unakuwa mdogo, muhimu ni kutumia vilainisho kama gel au KY jelly na libeneke linaendelea kama kawaida.

        -Kutumia madawa (Medicaments).
        kama unatumia dawa za kuzuia msongo wa mawazo pia huchangia ile hamu ya tendo la ndoa (libido) na matokeo yake kukosa kufika kileleni.
        Pia kuna dawa za uzazi wa mpango hupunguza hamu ya tendo la ndoa hasa zile ambazo huingizwa mwilini (sindano)
        Pia dawa za kupunguza pressure hupunguza uwezekano wa kufika kileleni.

        -Pombe, madawa ya kulevya na sigara
        Alkoholi na madawa ya kulevya hupunguza sana hamu ya tendo la ndoa.
        Huathiri mfumo wa Fahamu unaohusika na mzunguko wa hisia za mapenzi kati ya ubongo na uke.
        Kama inavyoathiri (alkoholi) mwanaume kudindisha vilevile huathiri mwanamke kufika kileleni.

        -Mwonekano, urembo na umaridadi:
        Kwa mwanamke jinsi anavyoonekana na jinsi mwanaume anavyoonekana kuna sehemu katika hisia za mapenzi (emotions na feelings).
        Kama yeye mwenyewe anajijua kwamba hayupo vizuri kimwonekano (urembo, usafi, harufu) na pia kama mwanaume hayupo sawasawa basi anakuwa ameathirika sana kiasi ambacho hawezi kufika kileleni.
        Pia wanawake wana uwezo mkubwa kunusa harufu kuliko mwanaume hivyo harufu yoyote mbaya kwake huwezi kumpeleka nje kabisa ya njia ya kwenda kileleni.

        -Mazingira
        Kama eneo au chumba mlichopo hakina usalama kama vile anahisi mtu anachungulia au anaweza kuingia, kwa mwanamke hiyo ni ishu kwani hawezi kufika kileleni kwa sababu ya usalama

JE, ZIPO NJIA ZA  KUTATUA TATIZO LA KUTOFIKA KILELENI KWA MWANAMKE?
        -Kujiruhusu mwenyewe kupenda tendo la ndoa na zaidi kupenda kufika kileleni kwa hamu kubwa.
        -Kuwa responsible kwa mambo yote yanayohusu ufanisi wa tendo la ndoa.
        -Kujipa elimu na maarifa kuhusu elimu ya mapenzi kwa mwanaume na mwanamke, viungo vinavyohusika na kila kitu kinachoweza kukupa tofauti katika ufanisi na uimarishaji wa tendo la ndoa kama unavyosoma hapa sasa hivi.
        -Kuwa na mawasiliano wakati wa tendo la ndoa hasa kubusiana na maeneo yote ambayo unasisimka pale ukiguswa au kuchezewa.
        -Kufanyia kazi kila tatizo lolote la kisaikolojia na kupata solution kabla ya tendo la ndoa.

Kwa leo tuishie hapa, jiandae kwa sehemu ya pili ya somo hili.

MASHA MASANJA
Whatsapp: 0622925000


Saturday, 16 July 2016

SIKU YA KUSHIKA MIMBA MZUNGUKO MFUPI - 2


Mungu ndiye muumba watu wote na viumbe vyote juu na chini ya jua, hilo halina pingamizi wala ubishi na lazima tumshukuru Mungu kwa hilo, ila alitoa amri ya ndoa kwamba ZAENI MKAONGEZEKE kwa hiyo kila mtu anayependa kutimiza amri hii yafaa awe na maarifa.

Kwa wale wasiojua namna ya kuhesabu mizunguko yao basi ni muhimu kurudi katika maada zilizopita na kisha kujifunza namna ya kuhesabu mzunguko wako. Tambua ya kwamba mzunguko wa bleed (hedhi) ni tofauti sana na siku za bleed (hedhi).

VITU VYA KUJUA
1. Siku za bleed (hedhi) ni kuanzia na siku ya kwanza unapopata bleed hadi siku ile unamaliza bleed.
2. Wakati mzunguko wa bleed huanza siku umepata bleed mpaka siku moja kabla hujapata bleed nyingine.
Mfano umepata bleed tarehe 1 mwezi wa saba na bleed hiyo ikaisha tarehe 05 basi siku za bleed ni 5 na zimeanza tarehe moja na zikaisha tarehe 5.
Kama bleed nyingine umeipata tarehe 29 mwezi wa 7, basi mzunguko wako wa bleed ya mwezi wa saba umeanza tarehe 01 mwezi wa saba na ukaisha tarehe 28 mwezi wa saba. Mzunguko huo ni wa siku 28. Mzunguko wa mwezi wa 8 Umeanza tarehe 29 mwezi wa 7.
Ukiwa na mzunguko mfupi usiogope kwa kuwa bado unayo nafasi kubwa ya kupata mtoto na watu wengi tu wapo wana watoto.

Lazima ujue mzunguko wako kwanza ni wa siku ngapi. Mfano kama umekuwa na mzunguko wa siku 21 kwa muda wa miezi mitatu mfululizo na mfano umepata bleed tarehe 10 mwezi wa saba basi siku yako ya uzazi haiwezi kuwa siku ya 14 tangu kupata bleed. Bali ni siku ya 7 tangu umepata bleed.

HEBU ZAMA NDANI HAPA UJIFUNZE

Mzunguko wa siku 21 siku ya uzazi ni siku ya (7)  tangu upate bleed. Kwa hiyo kama utapata bleed siku 3 basi siku ya tano unatakiwa uanze tendo la ndoa. Mfano mzuri ni kama ufuatao. >>>Marry ameingia bleed leo tarehe 16 mwezi wa 7 na mzunguko wake kila mwezi unamchukua siku 21. Huyu Marry anachukua siku 3 za bleed. Basi siku zake atahesabu hivi tarehe 16 ni siku ya kwanza yaani leo tarehe16 ni siku ya kwanza ya bleed, kesho tarehe 17 ni siku ya pili ya bleed, kesho kutwa tarehe 18 ni siku ya tatu ya bleed, tarehe 19 ni  siku ya nne bleed imeisha, tarehe 20 siku ya tano bleed imeisha - anza hapa kukutana na mwenzako, tarehe 21 ni siku ya sita endelea na tendo na tarehe 22 siku ya saba endelea na tendo yai linatoka. Unashauriwa kuanza mapema ili kuongeza nafasi ya mbegu kulikuta yai.

MZUNGUKO WA SIKU 22,23,24,25 na 26

Mzunguko wa siku 22 yai linatoka siku ya 8 wewe anza tendo siku ya 6, 7 na 8
Mzunguko wa siku 23 yai linatoka siku ya 9 wewe anza tendo siku ya 7
Mzunguko wa siku 24 yai linatoka siku ya 10 wewe anza tendo siku ya 8
Mzunguko wa siku 25 yai linatoka siku ya 11 wewe anza tendo siku ya 9
Mzunguko wa siku 26 yai linatoka siku ya 12 wewe anza tendo siku ya 10

Kumbuka kuanza siku moja au mbili kabla ya siku ya yai kutoka pia unaweza ongeza siku 1 au mbili baada ya siku yenyewe hii ni kwa sababu mizunguko huwa inabadilika badilika kutokana na sababu mbalimbali kama ugonjwa na dawa nzitonzito mshituko kama wa kufiwa, kubadilika kwa hali ya hewa na pia mabadiliko ya mwili kama kunenepa.

Kumbuka kama umekaa muda mrefu hujapata mtoto ni lazima ufike hospitalini na kupima na kupata majibu sahihi. Ni muhimu pia ukawa uko karibu na mwenzako, una afya nzuri na mko vizuri kiuhusiano.

UMUHIMU WA CHAKULA BORA
Ni muhimu ule chakula bora na sio bora chakula. Imethibitika ya kwamba asilimia zaidi ya 50 ya matatizo ya hedhi hutokana na kutokula vizuri. Ulaji wa chips, soda, pombe kupindukia, kula wanga mwingi na sukari ni hatari kwa maisha ya ndoa. Unatakiwa kula chakula halisi (Real Food) chakula fresh na chakula cha asili. Vyakula hatari ni pamoja na vyakula vya paketi na makopo na kuku wa kisasa (chicken)

TUNAKUSAIDIAJE?
1.TUNATOA ELIMU YA AFYA KATIKA MAHUSIANO. Endelea kufuatilia mada zetu hapa ili kujifunza mengi zaidi, SHARE NA MARAFIKI ZAKO na pia Elimisha wengine.
2. PEDI ZA NEPLILY – Tumia pedi za neplily pads mara kwa mara. Pedi za Neplily ndio pedi bora kabisa kwa sasa kwa akinadada na akinamama. Zinaondoa miwasho, harufu mbaya UTI na fangasi za ukeni na miguuni. Zinarekebisha uchachu uliozidi ukeni na pia zinarekebisha hedhi zilizovurugika.  Zipo MWANZA, SHINYANGA, BUKOBA, DODOMA, IRINGA, BABATI NA DAR 
3. KUKOKOTOA SIKU YAKO YA UZAZI – Wasiliana nasi kwa meseji au whatsapp tu ukiwa umeshaandika siku zako za bleed za miezi minne 0622925000

Friday, 8 July 2016

ITAMBUE SIKU YAKO YA UZAZI

SIKU YA UZAZI MZUNGUKO WA KAWAIDA NA MREFU SIKU 28-35

****NOTE, KAMA HUJUI KUHESABU SIKU ZA MZUNGUKO WAKO BASI TAFUTA MAKALA IPO HAPA CHINI
》》》》》

Kwa wale wanandoa wenye uhakika na MIZUNGUKO YAO ya mwezi. Mfano una uhakika kabisa ya kwamba mzunguko wako wa hedhi ni siku 28 au 32 au 35 na kwamba mzunguko huu umeuona kwa muda wa miezi mitatu basi leo nawapa SIRI YENYE UHAKIKA WA 70% kujua siku zako za uzazi.

MZUNGUKO WA SIKU 28 KWA MFANO
SIKU YA 14 NDIO SIKU YA UZAZI.
FORMULA IKO HIVI

>>>>hesabu siku 15 kuanzia siku ya 28 na kurudi nyuma, yaani tarehe 28 siku ya 1, tarehe27 ya pili,26 ya tatu,25 ya nne ,24 ya tano,23 ya sita,22,21,20,19,18,17,16,15, na tarehe 14 ni siku ya kumi na tano

Katika mzunguko huu siku nzuri ya kuanza kuwa karibu na mwenzako ni kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16.

Mfano huu ni kwamba kama umepata bleed tarehe 1 mwezi wa 7 na mzunguko wako ni siku 28 basi tarehe 14 ndio SIKU YA UZAZI, lakini wewe anza shughuli tarehe 12 hadi 16. Hii ni kwa sababu yai likitoka katika nyumba yake ya mayai linaweza ishi masaa24 tu wakati mbegu za kiume zinaweza ishi masaa hadi 72 na zaidi

MZUNGUKO WA SIKU 34 KWA MFANO
SIKU YA 20 NDIO SIKU YA UZAZI
FORMULA IKO HIVI

Hakikisha mzunguko huu ni mzunguko ulioupata katika miezi mitatu iliyopita. Kama mzunguko unarukaruka basi formula hii haiwezi kukufaa.

Mfano Umepata hedhi mwezi wa saba tarehe 1 manayake siku ya 34 ni mwezi wa 8 tarehe 3. Sasa hesabu siku 15 kuanzia tarehe 3 mwezi wa 8 na kurudi nyuma.
Yaani tarehe 3 mwezi wa 8 itakuwa siku ya kwanza ,tarehe 2 mwezi wa 8 itakuwa siku ya 2,tarehe 1 mwezi wa nane itakuwa siku ya 3 ,tarehe 31 mwezi wa 7 itakuwa siku ya 4, tarehe 30 siku ya 5, endelea 29,28,27,26,25,24,23,22,21, hadi tarehe 20 itakuwa siku ya 15.

>>>Katika mfano huu ni kuwa kama umepata bleed tarehe 1 mwezi wa 7 basi SIKU YAKO YA UZAZI ni tarehe 20. Kwa hiyo unatakiwa kuwa karibu na mwenzio kuanzia tarehe 18 hadi 22.

USHAURI WA BURE ni kwamba katika siku hizi Epuka kuwa mgomvi na mnyimi kuwa mkarimu na mpole ili uongeze furaha ya mwenzako afanye kazi kwa bidii na vizuri.

Sasa tarehe zinaambatana pia na dalili moja kubwa ya kuwa na UTEUTE UKENI, ute huu ni ule kama utaingiza vidole viwili katika uke na kisha ukitoa vitanue kama unaweka alama ya V. UTAONA UTE UNAOVUTIKA KAMA UZI.

BASI JUA KWA HAKIKA HIYO NDIYO SIKU YAKO YA UZAZI. Kama utajaribu miezi kadhaa na kukosa kushika mimba basi tambua ya kwamba kuna tatizo lingine kubwa ama kwa mwenzako au kwa wewe mwenyewe.

>>>> IKIWA UNA MATATIZO YA BLEED AU HEDHI YENYE KURUKA RUKA AU HAIPO KABISA AU UNATOA DAMU NYINGI AU INAKAA MUDA MREFU ZAIDI YA SIKU 7 AU NI ILE INATOKA SIKU MOJA TU BASI USISITE KUWASILIANA NASI KWA USHAURI ZAIDI <<<<<

PI UNAKARIBISHWA KUNUNUA PEDI ZETU ZENYE DAWA NA ZENYE UWEZO WA KUTIBU MIWASHO, FANGASI NA MAUMIVU WAKATI WA SIKU ZA HEDHI

Call/txt 0767925000
Watsap 0622925000


Saturday, 18 July 2015

MWANAMKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa au kukosa nyege huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, lakini wanaume hukerwa zaidi kuliko wanawake, ifahamike kuwa mwanaume akikosa hamu ya tendo la ndoa mwanamke au mke wake atajua tu, ila mwanamke akikosa hamu ya tendo la ndoa siyo rahisi mwanaume kujua kama hatamwambia au hatakuwa muwazi. Tatizo hili linaathiri asilimia 20 ya wanaume wakati wanawake ni mara mbili ya wanaume.

Hali ya kujisikia kufanya mapenzi kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalimbali yanayomtokea katika maisha yake. 

MATUKIO YANAYOATHIRI MWANAMKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
-Kuisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanaume
-Kuwa na matatizo/ugomvi wa mara kwa mara katika mapenzi/mahusiano
-Kupata ujauzito
-Kuwa na magonjwa mbalimbali
-Kuwa na mawazo au stress hasa kwa wanawake waliokosa kushika mimba kwa muda mrefu


JINSI YA KUTAMBUA KAMA UNA TATIZO HILI
Kwanza ifahamike kuwa tatizo hili halitokei ghafla tu kama kuugua mafua, huanza taratibu sana na pengine mwanamke anaweza asigundue. Sanasana pima mwenendo wako wa masuala ya mapenzi kwa mwaka uliopita na miezi ya hivi karibuni. Tatizo hili halitokei kwa kutofanya mapenzi kwa muda mrefu au kuhesabu kuwa umeshafanya mapenzi mara ngapi. Mawazo yako kuhusu tendo la ndoa ndiyo ya muhimu katika kujipima.


Viashiria vingine ni vyaweza kuwa kila mara uwapo chumbani na mpenzi wako na anakutomasa sehemu mbalimbali zenye kuleta hisia lakini kwa muda mrefu husikii chochote au hupati nyege basi tambua tayari una tatizo hilo.



Thursday, 16 July 2015

ZIJUE DALILI NA VISABABISHI VYA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER)

 Ugonjwa wa Kansa ya shingo ya kizazi ni ugonjwa unaoshambulia kizazi cha mwanamke. Tukumbuke kuwa sehemu hii ipo chini ya mji wa mimba ambayo huunganisha uke na mji wa mimba. Urefu wake ni karibu inchi mbili hivi.

DALILI ZAKE NI:
1. Kutokwa na uchafu sehemu za siri.
2. Kutokwa damu nyingi kuliko kawaida siku za hedhi
3. Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
4. Kupata siku za hedhi bila mpangilio (siku za hedhi kubadilikabadilika kila mwezi)
5. Maumivu makali chini ya kitovu

VIHATARISHI/VISABABISHI VYA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI
1. Magonjwa ya zinaa
2. Akinamama wanaojifungua mapacha kila mara
3. Mwanamke kuwa na wapenzi wengi
4. Mwanamke kuanza kuzaa akiwa na umri mdogo
5. Uvutaji wa sigara
6. Utumiaji wa vidonge vya uzazi wa mpango/Vitanzi
7. Ulaji mbovu wa vyakula hasa vyenye mafuta mengi
8. Upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI)

AINA ZA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI
1. SQUMOUS CELL CANCER.
    Hii hushambulia kwa nje ya kizazi.
2. ADENOR CARCINOMAR CELL CANCER.
    Hii hushambulia ndani ya ngozi ya kizazi.

HABARI NJEMA KWA TIBA YA UGONJWA HUU
Wataalamu wa utafiti wa dawa kwa kutumia mimea kutoka Thailand na China wamegundua na kutengeneza dawa katika mfumo wa vidonge ambavyo vimetokana kwa mimea ya nyanya, maharage ya soya, uyoga mwekundu na ginsen. 
Dawa hizi zitumike kwa muda wa miezi mitatu na mgonjwa atapona kabisa.

Kama una mgonjwa ana tatizo au dalili hizo waweza wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 ili umchukulie dawa hizo popote ulipo Tanzania.
















Saturday, 11 July 2015

MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(URINARY TRACT INFECTIONS)

Maambukizi katika njia ya mkojo hujulikana zaidi kwa jina la UTI, kirefu chake ni Urinary Tract Infections.
Maambukizi haya tunaweza kuyaweka katika makundi makuu mawili:
(1) Maambukizi ya chini katika njia ya mkojo(lower urinary tract infections).
   Hii inahusisha mrija wa mkojo(urethra) na kibofu cha mkojo.
(2) Maambukizi ya juu katika njia ya mkojo(upper urinary tract infections.
  Haya ni maambukizi ambayo hupanda na kusababisha maambukizi kwenye figo.

Pia tunaweza kuchanganua ugonjwa huu katika namna kuu mbili.
(1) Acute UTI.
  Hii ni UTI ya kawaida tu. Haya ni maambukizi yanayoambatana na dalili zinzosababishwa na usumbufu wa maradhi kwenye njia ya mkojo. Kwa mfano kuumia wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara n.k.
(2) Chronic UTI.
  Hii mara nyingi huwa tunaiita UTI sugu. Katika hali hii huambatana na dalili za hatari kama kukojoa damu inayoweza kuonekana kwa macho tu bila msaada wa Microscope au kukojoa mkojo wenye chembechembe za damu nyekundu ambazo haziwezi kuonekana kwa macho. Sasa ukiona dalili hizo unaweza kujua kama una UTI sugu. Na unapofikia hali hii mara nyingi tunaamini kuwa tayari figo imeshambuliwa(pyelonephritis). Hapa ni kitendo cha kushambuliwa kwa kuta za nje za njia ya mkojo. Hapa mgonjwa anakuwa anasikia maumivu makali sana kwenye pingili za chini ya mgongo zikiambatana na dalili za tumbo kuuma chini ya kitovu na kukojoa mkojo wenye damu.

KWANINI WATU WENGI KILA KONA NI UTI?
Hii ni kwa sababu watu hawafuati utaratibu au kanuni za kuchukua vipimo maabara. Mfano kipimo cha UTI kwa Maabara tunapima kipimo cha mwanzo kwa kutumia mkojo wa katikati yaani MID STREAM URINE. Tatizo wengi wetu tukienda Hospitali tunaambiwa KAKOJOE HUMU ULETE MKOJO!
Mkojo wa mwanzo ni lazima upitie normal flora(bacteria rafiki/wasio na madhara), na kipimo cha mkojo huwa hakibagui, hapo ni lazima kitasoma una bacteria wengi kumbe wala siyo bacteria wenye madhara. Hapo inatakiwa ukojoe mkojo wa mwanzo umwagike kwanza ndipo uje uchukue mkojo unaofuata(wa katikati au mid stream urine catch).

WATU AMBAO WAPO HATARINI KUPATA UTI
=>Watoto wadogo wanaotumia Nepi maana wao hujikojolea humohumo. Hivyo mtoto mdogo kama humbadilishii Nepi mara kwa mara, huzinyooshi ili ziwe safi ana hatari ya kuugua UTI.
=>Wanaume wa umri mkubwa ambao hawajafanyiwa tohara.
=>Mwanamke yeyote yupo hatarini kupata UTI kwa sababu njia ya haja kubwa ipo karibu sana na njia ya uzazi. Na hivyo wengi wa wanawake wanapokuwa katika zoezi la kujisafisha hujisafisha kwa kupeleka uchafu mbele badala ya kusukuma huo uchafu kwa nyuma. Pia wanawake njia yao ya mkojo(urethra) ni fupi ukilinganisha na ya mwanaume. Kwa wanaume ni nadra sana bacteria kufika kwenye kibofu. Maambukizi ya kibofu huitwa CYSTIS.
=>Watu wenye wapenzi wengi yaani michepuko mingi na hawatumii kinga wakati wa kufanya mapenzi.
=>Wanawake wanaotumia nguo wakati wa kujihifadhi hedhi bila kuzikausha vizuri na kuzinyoosha. Kuna wanawake wengi hufua nguo na kuanika ndani nguo wanazotumia wakati wa hedhi.
=>Wanawake wanaotumia ped za madukani ambazo hazina viwango na kuchelewa kubadilisha ped.
=>Matumizi mabaya ya Antibiotics husababisha walinzi wa sehemu za siri kufa na kufanya bacteria nyemelezi kuvamia na kuanza kuharibu mazingira. Hivyo antibiotics ni nzuri lakini zitumiwe kwa misingi maalumu maana normal flora wakifa basi utashambuliwa na kila bacteria au fangasi ambao ni nyemelezi.

JE, VYOO VICHAFU NI CHANZO CHA UTI?
Watu wengi tumekuwa na visingizio kuwa bacteria wa chooni huwezi kuruka na kuingia katika via vya uzazi na kusababisha ugonjwa wa UTI. Ukweli ni kwamba hao bacteria hawana mabawa ya kuwafanya waruke ila sisi watu ndio huwa tunakiuka taratibu za kujisafisha tuwapo chooni. Kwa maana hiyo utaweza kuambukizwa UTI kupitia hivyo vyoo vichafu hasa vya jumuia endapo tu hautatumia Tishu zenye Antibiotics kujifutia.

SASA TUANGALIE TIBA YA UGONJWA HUU KWA KUTUMIA PED ZENYE ANIONS CHIP ZISIZO NA MADHARA.
Anions hizi zimewekwa katikati ya ped kwa kutumia pamba nyepesi. Hali hii huifanya sehemu husika ikilowa maji au damu, inafyonza damu yote na kuruhusu hewa kupenya na kusafisha joto lote kukausha unyevunyevu wote. Hewa inapopita inaondoa joto lote na kuondoa mazingira ya bacteria waharibifu kuweza kuota au kuishi maeneo hayo. Pia inasafisha na kukausha unyevunyevu wote ambao ukiachwa wadudu kama bacteria au fangasi huweza kuchekelea na kuzaliana kwa fujo. Hivyo kwa staili hiyo mwanamke au msichana unakuwa mkavu na hakuna joto kabisa kama vile kuna AC kwa jinsi utakavyojisikia mwenye amani.

SASA TUONE KAZI NA FAIDA YA HIZO ANION CHIP
=>Tujue kuwa hizo anions chip ni negative charged, yaani anions inapokuwa inatolewa inakuwa inatengeneza oxygen ambayo hii huzuia bacteria wote wanaoweza kustawi bila kuhitaji oxygen yaani Anaerobic Bacteria. Mfano mzuri ni mtu anayekuwa na kidonda cha anaerobes huwa kinanuka sana . Hivyohivyo harufu mbaya sehemu za siri kwa wanawake husababishwa na kuoteana kwa bacteria hawa. Hivyo kwa kutumia ped hizo hii hali huondoka kabisa.
=>Huzuia kansa ya shingo ya kizazi.
=>Hutibu kabisa UTI ya aina yoyote
=>Huzibua mirija ya uzazi kwa watu wenye matatizo ya uzazi
=>Huzuia harufu mbaya sehemu za siri
=>Inazuia maambukizi yote ya kizazi hasa unapokuwa katika mazingira hatarishi kama mabwawa ya kuogelea
=>Zinarekebisha tatizo la uwiano wa vichocheo au hormonal imbalances
=>Hurekebisha siku za hedhi kwa wanawake ambao siku zao za hedhi hubadilikabadilika.
=>Huondoa tatizo la kuumwa kichwa na tumbo wakati wa hedhi.
Ped hizo zinapatikana sehemu nyingi hapa nchini. Piga simu namba 0767925000 au whatsapp 0622925000 utazipata popote utakapokuwa. Pia zinapatikana kwa bei ya jumla na rejareja.

Thursday, 2 July 2015

AKINAMAMA: KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI(MENORRHAGIA)

Hili ni tatizo linalosumbua akinadada/mama. Hiki ni kitendo cha mwanamke kutumia siku nyingi akiwa hedhi au damu kutoka kwa wiki kuliko kawaida.
CHANZO CHA TATIZO
1. FIBROIDS - Hizi ni vimbe katika kizazi na zinaweza kuwa ndani ya kizazi au nje
2. ENDOMETRIASIS - Hii ni hali ambayo seli za ukuta wa kizazi huenda kujiotesha sehemu nyingine. Automatically mwanamke akiwa na hali hii anaweza kupata hedhi hata mara mbili kwa mwezi au mara moja lakini akatumia siku nyingi kuliko kawaida.
3. Hormones imbalances. Ni kipindi ambacho kiwango cha vichocheo kinapokuwa hakiko katika usawa wake, hasa estrogen homoni.
4. Maambukizi katika mfuko wa kizazi
5. Kansa ya mfuko wa kizazi
DALILI ZA TATIZO
=>Kupata hedhi kwa zaidi ya siku saba
=>Kubadili ped zaidi ya moja ndani ya saa moja
=>Damu inayotoka kuonekana kuwa na dalili ya kuganda
=>Kuonyesha dalili za kuishiwa damu kipindi ukiwa kwenye hedhi
Tatizo hili kwa sasa linaathiri mwanamke mmoja kati ya wanawake watano.
USHAURI NA TIBA
Unapoona dalili hizo tafadhali jitahidi umuone daktari kwa matibabu maana siyo hali ya kawaida. Usitumie vidonge vya maumivu au vyovyote vya kemikali maana utakuwa unaongeza kama mbolea tu mwili hivyo tatizo la vichocheo(hormone imbalance) kuwa kubwa zaidi na zaidi. Akinamama wengi wanaumia na tatizo hili kwa kutokujua madhara ya vidonge wanavyovitumia pindi wakiwa kwenye hedhi.
Tumia matibabu ya mmea,  Tunayo dawa ya mmea ambayo iko katika mfumo wa vidonge utakayoitumia kwa mwezi mmoja. Inamaliza kabisa tatizo hilo.
Kama una tatizo hili au una ndugu yako ana shida hiyo basi usisite kuwasiliana nasi kwa namba 0767925000 au whatsapp 0622925000

Sunday, 28 June 2015

UVIMBE KWENYE KIZAZI(UTERINE FIBROIDS/MYOMA)

Kumekuwa na ongezeko kubwa la tatizo la akinamama kuwa na uvimbe kwenye kizazi. Suala hili ni gumu na hupelekea akinamama wengi kutozaa tena katika maisha yao japo hutegemeana na sehemu uvimbe ulipo.
Kwa leo tutaona ni jinsi gani ugonjwa huu tunavyoupata, dalili na matibabu yake yanavyokuwa. Tukumbuke kuwa mgonjwa wa uvimbe kwenye kizazi haendi hospitali kwa sababu ya ukubwa wa uvimbe bali anaenda Hospitali kutokana na dalili atakazokuwa anazipata. Wanawake wengi tu wanakuwa na tatizo hili lakini wanajikuta wanabeba hata mimba hadi wanajifungua salama. Hii ni kutokana kuwa bado hawajapata dalili za ugonjwa huu/yaani hawajaanza kusumbuliwa.

HIZI HAPA NDIYO DALILI ZA KUWA NA UVIMBE KWENYE KIZAZI
1. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
2. Kupata hedhi mara nyingi zaidi ya siku za kawaida
3. Kuumwa na tumbo la hedhi zaidi ya kawaida
4. Kutokwa na uchafu na majimaji yenye harufu kali sehemu za siri
5. Kukojoa mara kwa mara
6. Figo kujaa maji na kusababisha kiuno kuuma sana(uvimbe umekandamiza ureter moja)
HIZO NDIYO DALILI ZINAZOMFANYA MGONJWA KWENDA HOSPITALI NA SIYO UKUBWA WA UVIMBE.

Mgonjwa anapofika na dalili hizo hubidi kufanyiwa kipimo cha picha ya tumbo(ultrasound) lengo na madhumuni ya kipimo hicho ni kujua uvimbe upo wapi, kujua uvimbe uko mmoja au zaidi, kutambua kama uvimbe umeathiri sehemu zingine kama kuziba ureter kama upo nje ya kizazi. Kipimo hicho kitamsaidia Daktari kujua anamsaidiaje mgonjwa wake kimatibabu.
VISABABISHI VYA UVIMBE KWENYE KIZAZI
-Kisababishi kikuu ni kuharibika kwa uwiano wa vichocheo vya estrogen na kusababisha kiwango cha estrogen kuwa kikubwa.
-ulaji wa vyakula vya viwandani vilivyovundikwa au kuhifadhiwa kwa msaada wa kemikali
-unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi (added sugar), kionjo na rangi ambavyo ni industrial products
-unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara

WATU AMBAO WAPO HATARINI KUPATA UGONJWA HUU
~Wanawake wote ambao hawajawahi kupata mtoto
~wanawake wote ambao wapo katika umri wa kuweza kuzaa, maana yake wote kuanzia umri wa kubalehe hadi kikomo cha kuzaa ~wanawake wanene kupita kiasi n.k

MATIBABU
Matibabu yake yanaweza kuwa kama ifuatavyo kutegemeana sehemu uvimbe ulipo
=>kupewa vidonge vya kutuliza maumivu tu, vidonge hivyo ni ghali sana lakini pia mgonjwa hushauriwa kutumia kwa muda mfupi tu kwani vina madhara ya kuweza kumfanya mwanamke kuwa na muonekano wa kiume kana vile kuota ndevu n.k
=>kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe tu endapo uvimbe upo pembeni ya kizazi. Ukifanyiwa hiyo Huduma bado mwanamke unaweza kupata mimba na kuzaa.
=>kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kabisa kizazi endapo Uvimbe upo ndani ya kizazi. Hapa mwanamke akifanyiwa upasuaji huu hawezi kuzaa tena katika maisha yake yote
NB: KUMBUKA KUWA HATA KAMA UTAUONDOA UVIMBE HUO, HAIMAANISHI KUWA UVIMBE UMEISHA, TATIZO HUJIRUDIA TENA MAANA BADO UNAKUWA HUJATIBU VYANZO VYA TATIZO AMBAVYO NI PAMOJA NA UWIANO MBOVU WA HORMONES NA MENGINE.

Vipo vidonge vilivyotengenezwa kwa mimea na uyoga mwekundu unaopatikana katika nchi za China na Thailand vinatibu kabisa tatizo hilo la uvimbe kwenye kizazi kwa kusambaza, kukausha na hatimaye kuumaliza kabisa uvimbe huo. Vidonge hivyo vinapatikana sasa Tanzania na kama wewe una tatizo hilo au ndugu na rafiki zako wana tatizo hilo basi wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 uweze kujipatia vidonge hivyo

Sunday, 21 June 2015

SULUHISHO LA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI


Hiki kimekuwa kilio cha wanawake wengi na kimesababisha wengi kukubaliana na hali hiyo na kubakia kuwa wahanga wa maumivu hayo.

Zipo sababu nyingi zinazochangia uwepo wa tatizo hili ikiwepo kubwa la kutokuwepo uwiano wa vichocheo (hormones imbalance), kuwepo kwa magonjwa mbalimbali kama endometriasis ambapo ni tatizo la seli za ndani ya mfuko wa kizazi kujitokeza nje ya kizazi, adenomyosis ambapo ni hali ya mwanamke kuota Uvimbe katika mfuko wa kizazi, magonjwa ya zinaa yanayotokana na bacteria, mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu kutoka kwa urahisi.
Hizo ndizo baadhi ya sababu za maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.

Mara nyingi wanawake wengi hutumia dawa za kutuliza maumivu kama Ibuprofen, Naproxen au aina nyinginezo zisizokuwa na Steroids (NSAIDS). 

Madakatari baadhi huwashauri wanawake kutumia vidonge vya kuzuia mimba ili kukata maumivu hayo. Lakini tatizo kubwa ni kwamba njia hizo humaliza maumivu ndani ya kipindi hicho tu, yaani mwezi utakaofuata maumivu yapo palepale na itakulazimu kuzitumia tena hizo njia. Kwa kifupi siyo njia za kudumu katika kumaliza maumivu hayo.

Kuna dawa maalumu ya kamaliza tatizo hili pamoja na ped zake maalum. Ped  hizo zimewekwa ANIONS CHIP ambayo ni dawa maalumu inayokusaidia kumaliza maumivu hayo, kusawazisha viwango vya homoni, ni kinga na tiba ya ugonjwa wa UTI, miwasho na fangasi sehemu za siri, pia zina uwezo mkubwa wa kufyonza damu hadi 250mls wakati wa hedhi na mengine mengi. 

Dawa hizi pia husawazisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake wenye tatizo la mzunguko usioeleweka na husaidia sana mambo ya uzazi. Dawa zipo katika mfumo wa vidonge na hazina madhara yoyote kwani zimetengezwa kwa mimea pasipo kuongezewa kemikali yoyote.

Wasiliana nasi kwa:
0767925000
0622925000 - whatsapp