Tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa au kukosa nyege huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, lakini wanaume hukerwa zaidi kuliko wanawake, ifahamike kuwa mwanaume akikosa hamu ya tendo la ndoa mwanamke au mke wake atajua tu, ila mwanamke akikosa hamu ya tendo la ndoa siyo rahisi mwanaume kujua kama hatamwambia au hatakuwa muwazi. Tatizo hili linaathiri asilimia 20 ya wanaume wakati wanawake ni mara mbili ya wanaume.
Hali ya kujisikia kufanya mapenzi kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalimbali yanayomtokea katika maisha yake.
MATUKIO YANAYOATHIRI MWANAMKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
-Kuisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanaume
-Kuwa na matatizo/ugomvi wa mara kwa mara katika mapenzi/mahusiano
-Kupata ujauzito
-Kuwa na magonjwa mbalimbali
-Kuwa na mawazo au stress hasa kwa wanawake waliokosa kushika mimba kwa muda mrefu
JINSI YA KUTAMBUA KAMA UNA TATIZO HILI
Kwanza ifahamike kuwa tatizo hili halitokei ghafla tu kama kuugua mafua, huanza taratibu sana na pengine mwanamke anaweza asigundue. Sanasana pima mwenendo wako wa masuala ya mapenzi kwa mwaka uliopita na miezi ya hivi karibuni. Tatizo hili halitokei kwa kutofanya mapenzi kwa muda mrefu au kuhesabu kuwa umeshafanya mapenzi mara ngapi. Mawazo yako kuhusu tendo la ndoa ndiyo ya muhimu katika kujipima.
Viashiria vingine ni vyaweza kuwa kila mara uwapo chumbani na mpenzi wako na anakutomasa sehemu mbalimbali zenye kuleta hisia lakini kwa muda mrefu husikii chochote au hupati nyege basi tambua tayari una tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment