Tatizo la ajira litakoma tu kama mitazamo yetu itabadilika kuanzia ngazi ya familia mpaka ngazi ya kitaifa mtazamo huu:
Familia zetu zinatakiwa kujua tu kuwa mtu haendi shule ili aje afanye tu kazi za kuajiriwa maofisini kwenye kiyoyozi lakini familia zilenge kumpeleka shule mtoto ili apate ujuzi utakao muwezesha kupambana na mazingira na soko la ajira ambalo linahitaji sana ujuzi na uwezo kuliko vyeti.
Familia pia ijenge utamaduni wa kuandaa mifuko ya miradi itakayo wawezesha watoto wao kujiajiri mara wamalizapo shule.
Familia zetu pia ziwe na utamaduni wa kufuatilia masomo ya kijasiriamali kupitia runinga na hata vinginevyo ziweze kuwafungua. Wazazi wajue namna ya kuwa control watoto wao kuangalia vitakavyowajenga katika mtazamo chanya tokea wako watoto.
Pili upande wa makanisa ni kuwa tusi hubiri sana muujiza wa maisha, maisha siyo muujiza ni uhalisia.
Waumini wafundishwe kinaga ubaga kwamba bila kufanya kazi maisha hayatabadilika hata kama mtu ananena kwa lugha.
Familia itengeneze mfumo unaowezekana wa kuwatambua watu wasio na kazi na kanisa liwawezeshe.
Makanisa yaandae semina na vipindi mbalimbali vya kufundisha masomo ya ujasiriamali na Elimu ya kuweka akiba. Makanisa yamekuwa yakihubiri sana Neno la MUNGU na wamesahau kuwa Neno bila fedha haliwezi kuhubiriwa.
Tatu upande wa serikali ni kwamba serikali inahitaji kuingiza somo la ujasiriamali kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu ili kuwajenga wanafunzi waweze kujua umuhimu wa kujiajiri.
Serikali pia inatakiwa kupunguza miaka ya kustaafu kwa watumishi wa umma kwa mtazamo kwamba watumishi wa umma wafanye kazi kwa mkataba say wa miaka 10-15 na walipwe mishahara inayoonekana na wasisitizwe kuwekeza maana baada ya miaka hiyo wataondoka ili kupisha mawazo na watu wengine kuingia kazini.
Haiwezekani unampa mtu astaafu baada ya kufikisha miaka 60. HAPA ndo watu wanajisahau wanakufa maskini Pamoja na kuwa walikuwa wanapokea mishahara mikubwa.
Serikali pia ifanye mpango wa kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mkubwa wa kuanzisha makampuni na iwawezeshe ili wanafunzi hao waajiri wanafunzi wengine. Serikali itoe fursa kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho kuandika mawazo ya kibiashara na yale yanayowezekana yawezeshwe na watu waanze mara moja wamalizapo.
Mwisho upande wa mtu binafsi.
Kimsingi tatizo hili linaanza na sisi wenyewe.
Jim Rhon anasema "kama utabadilika kila kitu kitabadilika".
Kuna haja sasa mtu binafsi kuanza kubadili mtazamo wake hasa kwa wasomi.
Amini kuwa siyo lazima uajiriwe na mtu ofisini na kumbe unaweza fanya mambo yako na ukifika mbali.
Anza na kile ulichonacho (capital accumulation) na baade utafika mbali usisubiri mitaji mikubwa.
Penda maarifa kwa kusoma vitu vizur vitakavyo kusaidia.
Maisha ni vile utakavyoamua wewe yawe. Hakuna mtu mwenye uweze wa kutengeneza maisha yako. Wewe ndo pekee wa kuweza kubadilisha maisha kwa kuwa ndo dereva wa maisha yako.
Namaliza kwa kusema Inawezekana "what was impossible yesterday is possible today".
Wajibika..!!
Masha Masanja
0622925000