Wednesday, 16 March 2016

ZIJUE NJIA ZA KUPATA PESA


Robert Kiyosaki ambaye ni mwandishi wa Kitabu kiitwacho “ Rich Dad Poor Dad” ameainisha njia nne za kupata fedha na kuwekeza.
Nimeona ni vema kuwashirikisha wasomaji wangu njia hizo na kuzidi kuwapatia dondoo zaidi za uwekezaji. Kwa jinsi ambavyo Robert Kiyosaki ameandika fedha zinapatikana kwa njia zifuatazo:

1. Kuajiriwa (employment)- ukiajiriwa unalipwa mshahara na malupulupu mbalimbali lakini unafanya kazi ya mtu mwingine.
Ingawa siyo lazima kufanya kazi wakati wote lakini Kiyosaki alisema “fanya kazi ujifunze au kwa kiingereza work to learn”.

2. Kujiajiri (self-employment)- hapa unajiajiri kama mjasiriamali lakini pia biashara yako inakuwa ndogo na unakuwa umeajiriwa lakini kwenye biashara yako.
Faida yake ni kwamba unakuwa huru na unakuwa wa kukua. Lakini usipopambana ukue unaweza kupata kipato kidogo kuliko hata watu walioajiriwa.

3. Biashara (business) –hapa unamiliki biashara ambayo umeajiri watu wengine wanaofanya kazi kwa ajili yako. Kazi yako inakuwa ni usimamizi na kuhahakikisha biashara inakua.
Ukifika hapa uwezekano wa kukua ni mkubwa kama utakuwa kiongozi mwenye mikakati.

4. Kuwekeza (investment) –hapa unawekeza kwenye rasilimali “assets” ambazo zinakupa kipato hata kama haupo (passive income).
Kwa hapa unaweza kuwekeza kwenye nyumba, ardhi, taasisi za fedha (financial institution) kama kwenye account za muda maalum, hati fungate, hisa n.k.
Usikubali hela yako hata shilingi laki moja ikae bure hata kwa mwezi zipo njia za kuwekeza.