Tuesday, 8 December 2015

UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)




NAMNA AMBAVYO MTU ANAPATA UGONJWA WA NGIRI (HERNIA)

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni:
-Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla.
-kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu.
-ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa .
Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Mawasiliano
0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

MADHARA YA VYAKULA & UNENE - SEHEMU YA 2

SEHEMU YA PILI:

KWA NINI UNA KITAMBI NA UZITO MKUBWA
BADILI MWILI WAKO KUWA MASHINE INAYOUNGUZA MAFUTA

Napenda tena kukukaribisha mpendwa msomaji wa Makala zangu za afya, nimekuwa nikipewa shukrani nyingi sana na wasomaji wangu jinsi gani walikuwa wakipotoka kuhusu lishe katika jambo zima la kupunguza uzito. Ninapenda pia kuchukua nafasi hii kuwapongeza na kuwaomba tuendelee kuwashauri watu wengi waungane nasi katika jukwaa hili la Makala za afya zilizosheheni maarifa yaliyofanyiwa tafiti za kutosha usisahau kuungana nami facebook kwa kubofya LIKE kwenye ukurasa wangu "Masha Nutrition Health Care".

Basi baada ya jana kujikita sana kuongelea vyakula vya wanga na namna ya kupunguza uzito kwa kupunguza wanga siku ya leo napenda kuengelea kwa upana Zaidi kuhusu VYAKULA VYA MAFUTA NA MAZOEZI mchango wake katika kupunguza uzito.

FIKRA POTOFU NO 1:
ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA VINAKUFANYA UWE NA KITAMBI NA UZITO MKUBWA
Kwanza kabisa napenda tu kuwaambia wote wenye kupenda kupunguza uzito. Najua lengo lenu sio kupunguza uzito lakini ni kuunguza mafuta ili nguo mnazotamani kuzivaa ziweze kuwapendeza na muwe wenye kuvutia. Lakini swala la kuunguza mafuta linaendana na kuboresha afya wapendwa ili mwili wako uzidi kufanya kazi katika uhalisia wake. Kwani ingekuwa lengo lako ni kuunguza mafuta tu,ungeweza kujinyima kula na ukapungua uzito tena ndani ya mwezi tu. Lakini sikushauri kwani utapata maradhi mengi kuzidi matokeo unayoyataka.
Sasa basi ukitaka kupunguza mafuta yako na utimize malengo lazima ufuate ushauri huu ninao kwambia kwani utatimiza malengo yako na afya yako itabaki imara kabisa.

Ingekuwa ulaji wa vyakula vya mafuta unanenepesha basi wale wote ambao majokofu yao majumbani yamejaa vyakula vilivyo andikwa “Low fat”, “Fat Free” wangekuwa umetimiza malengo yao ya kutokuwa na kitambi na uzito mkubwa. Ingawaje wanatumia vyakula vya namna hii bado ongezeko kubwa la matatizo haya ya kitambi na uzito mkubwa yanalikabili taifa kwa ongezeko kubwa sana.
Je unafikiri vyakula vyenye Fat free, No fats vilivyopo katika maduka makubwa ya vyakula vina msaada wowote?
Chochote unachokula kinatoa tafsiri ya jinsi gani mwili ufanye kazi ili uweze kuunguza mafuta, hivyo wewe ndiye mwenye maamuzi. Kitendo cha kutaka kupunguza uzito unatakiwa ujiwekee malengo yako na uyafuate bila kuyapuuza kwani kupunguza uzito ni kazi Zaidi ya kutafuta pesa inahitaji uvumilivu na maamuzi ya kuthubutu ndio maana wengi wameridhika na kuanza kujipotosha kuwa ni wakurithi.
“FAT ISN’T OUR PROBLEM,SUGAR IS”
Tatizo sio mafuta tatizo ni vyakula vinavyotoa sukari nyingi katika damu yako pale unapoviingiza mwilini mwako.

Tangu pale watu walipokuwa wakisumbuka na kiwango kikubwa cha cholesteral na shirika la afya duniani kutoa tamko kupunguza kiwango cha cholesteral mwilini kwa kuepuka vyakula vya mafuta. Basi watu walihamisha mtazamo wao katika aina hizo ya vyakula na kuanza kula vyakula ambavyo vina kiwango kingi cha sukari na vyakula vya wanga vilivyosindikwa na kuwekwa kwenye makopo na vibebeo mbali mbali zikiwa na maandishi ya kibiashara. Watu tumekuwa tukijaza aina hivi ya vinywaji majumbani na vyakula vya namna hii kama mikate, biscuts, chokoleti, sambusa nk hiki ndicho chanzo cha tatizo hili kuongezeka kwa kiwango kikubwa kiasi hiki na kupelekea watu kuugua magonjwa mbalimbali kama kisukari, shinikizo la damu, upungufu wa nguvu za kiume, vimbe kwenye kizazi n.k

UKWELI UPO WAPI KUHUSU MAFUTA?
Katika dunia ya lishe tuna mafuta mazuri na mafuta mabaya, mafuta mazuri ndio yanayoshauriwa kutumika kwa wingi kwa watu wanaotaka kupunguza uzito. Na chakushangaza watu wote wenye uzito mkubwa wanaogopa aina zote za mafuta! Sasa je utapunguaje? Mafuta mazuri siku zote huwa nayaita HEALTHY FATS! Tumia mafuta haya kwa wingi upate faida zifuatazo.
1. Unapokula chakula chenye wanga kidogo na mafuta mazuri kiafya mengi unaufundisha mwili kuanza kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili
2. Pale wanga inapokuwa imeshatumika kuwa nishati ya mwili na kuisha basi mwili utaanza kuunguza mafuta

ZINGATIA
Tafiti zinaonesha kwamba kati ya chakula cha wanga na mafuta mazuri, chakula cha wanga husababisha kupanda kwa kiwango cha insulin (homoni inayo hifadhi sukari iliyozidi katika mfumo wa mafuta ) kwa kiasi kikubwa wakati chakula cha protein kinafuatia na chakula cha mafuta kimeonesha kiwango cha insulin kuwa katika kiwango maalumu muda wote. Tafiti hizi zilifanywa kwa kutumia GTT (Glucose Tolerance Test) kipimo kinaonesha namna gani mwili wako una uwezo wa kuhimili kiasi fulani cha sukari mwilini.

Hivyo basi unapokuwa unatumia vyakula vyenye mafuta mazuri vinakusaidia kuujenga mwili kuanza kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili kukupatia nguvu na pia inapunguza kiwango cha insulin kinachotolewa na kongosho kuja kusawazisha sukari maana vyakula hivi vimeonesha kutoongeza sukari kwa wingi kwenye damu na hivyo basi hakuna mafuta yatakayo hifadhiwa sehemu yoyote na badala yake mwili utaanza kuyaunguza mafuta yaliyo hifadhiwa.

JE UMESHAWAHI KUFIKIRIA UNAHITAJI KIWANGO GANI CHA SUKARI MWILINI UWEZE KUISHI?
Mwili wa binadamu unastahimili kiwango cha sukari chini ya 100mg/dl au 7mmol/l ya damu. Hivyo basi kwa sababu binadamu ana kiwango cha kadirio la lita 5 ya damu ukitaka kupata kiwango gani cha sukari kinahitajika katika lita moja katika kipimo cha gramu utafanya kama ifuatavyo.
1litre=1000mg/litre
Katika lita 5 =5000mg ambayo ni sawa na gramu 5.

Tunakadiria kuwa gramu 5 ni sawa na kijiko kimoja cha sukari. ( hiki ni kiwango cha kawaida ukiwa hujala chochote)
Baada ya kula chakula chako, labda kijiko kimoja cha wali, sukari yako itapanda hadi vijiko 10.

Umeona jinsi gani tunavyo hitaji kiwango kidogo cha sukari kinachoweza kutufanikisha tuishi na tusiwe na nyama uzembe? Hili unaweza kuliepuka kwa kupunguza wanga katika mlo wako na kuongeza mafuta mazuri ,mboga za majani na matunda kwa wingi bila kusau protein

JE KATIKA KIWANGO GANI?
Wengi huwa wanapenda kuniambia watumie vyakula gani kuanzia asubuhi hadi jioni lakini hili linakunyima uhuru wako wa kuchagua chakula cha namna gani katika kundi lile lile utumie kulingana na unavyojisikia siku hiyo. Ndio maana natoa elimu hii yote ili uweze kupangilia mwenyewe. Hebu zingatia hili

ULAJI MBAYA KATIKA SAHANI YAKO KAMA UNAHITAJI KUPUNGUZA UZITO
Wanga; 48.7%
Protein: 15.7%
Mafuta au Fats: 33.7%
Umeona jinsi gani watu walivyo na fikra potofu kuhusu lishe, wanga ni nyingi kwani wanajua ndio chanzo kikubwa cha nishati ya mwili na woga wa kutumia mafuta. Kadri wanga inavyozidi kiwango,ndivyo sukari nyingi itahifadhiwa kama mafuta tumboni,kifuani,mgongoni na kiunoni pia kwenye ini ( Fat liver).

Kadri sukari inavyozidi kuwa juu ndivyo homoni ya insulin inavyozidi kupanda kuja kufanya kazi yake ya kuhifadhi sukari iliyozidi.

ULAJI MZURI WA SAHANI YAKO KAMA UNAHITAJI KUPUNGUZA UZITO
Wanga: Asilimia 10-15
Protini : Asilimia 15-20
Fats (mafuta mazuri): Asilimia 65-75
Ukingalia katika takwimu hizo utajua kuwa hesabu hazidanganyi, kadri unavyozidi kuimarisha mlo wako kuweka mafuta mazuri mengi na kupunguza wanga. Unaufanya mwili wako kuwa na kiwango sawia cha insulin na hakuna mafuta yatakayo hifadhiwa kwani hakuna sukari iliyozidi. Na mwili wako utaujengea mazoea ya kuanza kutumia mafuta kama nishati baada tu ya sukari kuisha na hapo ndipo mwili wako utabadilika kuwa mashine inayounguza mafuta na kadri siku zinavyokwenda utashitukia tumbo linapungua na nyama uzembe kupungua na hatimaye kuisha na kuboreka kwa afya yako.

ZINGATIA: Watu wengi husema kuwa mazoezi ndio suluhisho la uzito mkubwa, ni kweli napenda kukubaliana nao kabisa, lakini nimekuwa nikipokea taarifa za watu ambao wamejitahidi sana kufanya mazoezi katika gym za kisasa bila mafanikio na wameridhika na uzito huo. Hii ni kwa sababu unaweza kupungua kupitia mazoezi endapo ukiwa mvumlivu kwani itakuchukua muda mrefu sana sivyo kama unavyofikiria na kutaka matokeo yatokee pale pale.

Siku zote mazoezi katika stesheni za gym huimarisha mwili na kukukinga na magonjwa tu, lakini JIKONI NDIO KUNA SULUHISHO LA UZITO MKUBWA. Lishe iwe ndio ngao yako ya kwanza na sio mazoezi. Hii ndio maana nimekuwa nikikutana na wahudhuriaji wazuri wa gym lakini bado wanasumbuka na kuvurugika kwa homoni na uzito kutoshuka.

Baada ya mada hii basi siku zijazo nitajibu swali lako Je ni vyakula gani tunaweza kula vina mafuta mazuri na vyakula gani vina wanga kidogo tunaweza kula kuendana na utaratibu wa LOW CARBOHYDRATES HIGH FAT DIET PROGRAM itakayolenga kukusaidia kufikia malengo yako.
Kama una maswali yatunze yote nitayajibu kwa Makala zangu zijazo kupitia ukurasa wangu wa facebook "Masha Nutrition Health Care" jaribu kujumuika nasi upate elimu hii bure.

Mawasiliano
0784925000
0622925000 whatsapp
0767925000
posted from Bloggeroid