Thursday, 25 June 2015

TATIZO LA MIGUU KUUMA/KUFA GANZI

Matatizo ya miguu/mikono kuhisi ganzi au maumivu husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa Neva za pembezoni mwa mwili(peripheral neuropathy), hivyo kusababisha kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika eneo husika(miguuni au mikononi).
DALILI ZA TATIZO
~Mtu kuhisi miguu kufa ganzi
~Maumivu au kuhisi kama vile moto unawaka miguuni au mikononi
~Kuhisi kama vile umevaa soksi au gloves wakati hujavaa
~Kuhisi kama vile kuna kitu chenye ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole
HIZI NDIZO SABABU ZA KUDHOOFIKA KWA NEVA HIZO
~Kupungua kwa virutubisho mwilini. Hapa tunamaanisha mwili kutokuwa na Vitamin za kutosha hasa mkusanyiko wa Vitamini B Complex
~Matumizi ya dawa fulani kwa muda mrefu mfano TB na ARV
~Uzito mkubwa wa mwili. Hii hupelekea maumbile ya viungo vya mwili mfano umbile la uti wa mgongo huonekana tofauti na ilivyo kawaida. Kubadilika huku husababisha baadhi ya Neva katika uti wa mgongo zikandamizwe zaidi na misuli/uzito wa mwili na hivyo kusababisha Neva hizo zishindwe kufanya kazi vizuri, matokeo yake unaanza kuhisi maumivu au miguu/mikono kufa ganzi.
~ugonjwa wa kisukari
~shinikizo la damu
HIZO NDIZO SABABU ZA TATIZO HILO, HIVYO TUSIEGEMEE KWENYE MAMBO YA KISHIRIKINA KABISA
MATIBABU
**Kubadili tabia hasa vyakula vinavyochangia tatizo hili kama nilivyotaja hapo juu
**Kutumia virutubisho ambavyo vitaweza kukurejesha katika hali ya zamani, pia dawa zilizotengenezwa kwa mimea zitakusaidia kufurahia Afya njema.
Wasiliana nasi kwa 0767925000 au 0784925000
Whatsapp 0622925000