Watu wengi wamekuwa wakibabaika wanapokabiliwa na watu Kuchagua kampuni ya mtandao wanaowafuata na kuwashawishi kujiunga na kampuni za mitandao au pale wanapokuwa wameamua kwa mapenzi yao kuingia kwenye biashara za mtandao wasijue namna ya kutoa maamuzi sahihi kwamba ni kampuni ipi au zipi ndizo bora kujiunga nazo.
Kwa maoni yangu, hii ndiyo hatua muhimu kuliko zote kwa sababu endapo utaangukia kwenye mikono ya kampuni mbovu, nguvu zako na mtaji wako vyote ni bure. Leo katika ukurasa huu tutaona vigezo vya kuvitumia katika kuchagua kampuni ya mtandao ya kujiunga nayo. Moja kwa moja nitaanza kwa kuviorodhesha vigezo hivyo au sifa za kampuni bora na kuvitolea maelezo.
1. Historia Ya Kampuni
Zipo kampuni ambazo zinaanza biashara na baada ya muda mfupi zinapotea au kufilisika. Kama ulikuwa mmoja wa wanachama wa kampuni ya namna hiyo, lazima utakuwa umeathirika kwa namna fulani. Inabidi upate kampuni ambayo ina historia ya kufanya biashara kwa muda mrefu, kwa ufanisi na ambayo biashara yake bado inaendelea kukua na si ile ambayo imefikia ukomo. Njia rahisi ya kupata taarifa hii ni kupitia internet ingawa kuwauliza ndugu na marafiki wengine inaweza kusaidia pia.
2. Bidhaa Za Kampuni
Kampuni bora ya mtandao ni ile ambayo bidhaa zake zinalenga kutatua matatizo ya wateja katika jamii unayoishi na zimethibika kufaulu katika kufanya hivyo. Bidhaa ambazo zitatangazwa halafu zikashindwa kukidhi mahitaji ya wateja zitakuwa na muda mfupi sana wa mauzo kabla ya wateja kugundua kuwa haziwafai. Bidhaa zitakazokidhi haja ya wateja zitakurahisishia kazi wewe muuzaji kwani baadaye zitajiuza zenyewe. Bidhaa hizo pamoja na kutatua matatizo ya wateja ziwe na bei ambazo wateja wengi wataweza kuzimudu kwani pamoja na ubora wake bidhaa ambayo bei yake itakuwa juu mno itauzika kwa wateja wachache sana wenye uwezo. Kumbuka kuwa wewe kama mwuzaji utanufaika zaidi pale unapouza bidhaa kwa wingi zaidi.
3. Mpango Mzuri Wa Ulipaji (Compensation Plan)
Mpango mzuri wa ulipaji na ambao ni rahisi kuuelewa ndio utakaokupa wewe pesa. Kama kampuni haina mpango mzuri wa ulipaji kamwe hutapata pesa ya kutosha na kama mpango wao si rahisi kueleweka utakosa pesa nyingi kwa sababu ya kutojua namna ya kuitumia kampuni yako vizuri.
Kwa vile ulijiunga na kampuni ya mtandao ili upate pesa ya kuboresha maisha yako, kitu cha kwanza cha kutazama ni mpango wao wa ulipaji na kuusoma au kuupitia kwa makini. Hili ndilo kosa ambalo watu wengi hulifanya, kujiunga na kampuni na kuanza kuchakarika bila kuujua kwa undani mpango wa ulipaji wa kampuni yake.
Unaweza share makala hii kwa watu wengi zaidi ili nao wajifunze.
Kwa ushauri khs biashara na jinsi ya kuanza biashara ya Mtandao wasiliana nami kwa:
0767925000
0622925000(whatsapp).