Saturday, 15 August 2015
SABABU ZINAZOSABABISHA MWANAMKE ASIPATE MIMBA
Zipo sifa ambazo mwanamke au mwanaume anatakiwa kuwa nazo ili aweze kushika au kumpatia ujauzito mwenzi wake. Kuna wanaume ambao wamekuwa wakiishi maisha ya kutafuta watoto kwa kuwa na uhusiano na wanawake lukuki ndani ya muda mfupi pasipo kutambua kuwa hata wao wana uwezekano mkubwa tu wa kuwa na tatizo la kutozalisha au kutungisha mimba, Wanaume wengi huamini kuwa wanapokuwa na uwezo wa kufanya ngono ndio kigezo cha wao kuweza kuzalisha. DHANA HIYO SIYO KWELI.
Leo tutaziona baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha mwanamke ashindwe kubeba ujauzito. Kwa kawaida mwanamke ili aweze kushika mimba ni lazima aweze kuonekana au kuwa na sifa kama za mwanamke na pia mwanaume ili aweze kumpa mwanamke ujauzito ni lazima awe na sifa kama mwanaume. Hivyo katika sula hili la kutafuta mtoto ni lazima mwanamke na mwanaume washirikiane kwani mwanaume unaweza kujiona kuwa uko fiti kumbe ukija kupima mbegu zako utajikuta una tatizo kubwa.
MATATIZO KWA MWANAMKE
Mwanamke mwenye matatizo ya kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo yafuatayo:
1. Atakuwa amekaa na mwanaume au ameishi katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume kwa zaidi ya mwaka mzima lakini hakuna mafanikio.
2. Hulalamika maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara.
3. Maumivu ya hedhi.
4. Kuvurugika mzunguko wa hedhi.
5. Kutoona ute wa uzazi
6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa na kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa
7. Kuwa na historia ya kutumia njia za uzazi wa mpango au kuharibika/kutoa mimba.
USHAURI: Endapo una muda wa zaidi ya mwaka hujapata ujauzito na unapata baadhi ya dalili nilizozitaja hapo juu, ni vyema uonane na daktari wa magonjwa ya uzazi ambaye hupatikana katika kila Hospitali za Mikoa, Hapo utafanyiwa uchunguzi zaidi hasa katika vichocheo au homoni za uzazi, vipimo vya mirija ya uzazi na vingine ambavyo daktari atakushauri. Uchunguzi huu mara nyingi huchukua muda mrefu hivyo ni vyema kuwa mvumilivu kwani mara nyingine mvurugiko wa homoni, matatizo ndani ya kizazi yanaweza kuwa yamesababishwa na uvimbe au maambukizi.
MATATIZO YA UZAZI KWA MWANAUME
Uchunguzi kwa mwanaume ni kuangalia mbegu za uzazi na kupima korodani, Mwanaume unaweza kujifahamu kama una tatizo endapo utakuwa na dalili zifuatazo:
1. Kuishi na mwanamke au mpenzi kwa zaidi ya mwaka lakini hakuna mimba kwa mwanamke
2. Upungufu wa nguvu za kiume
3. Kutoa manii au shahawa nyepesi sana na zenye harufu mbaya.
4. Maumivu ya muda mrefu ya korodani
5. Maumivu ya kiuno kwa muda mrefu
6. Maambukizi katika njia ya mkojo mara kwa mara
7. Uvutaji wa sigara kwa muda mrefu
8. Unywaji wa pombe kali, matumizi ya dawa za kulevya mfano bangi na mirungi.
USHAURI: Matatizo haya pia hutibika kwa kumuona daktari wa magonjwa ya uzazi. Vipimo vya mbegu na korodani hufanyika. Vipimo vingine hutegemea uwepo wa matatizo mengine kama kuwahi kumaliza tendo la ndoa, upungufu wa nguvu za kiume, uchovu mkali baada ya tendo la ndoa na maumivu katika njia ya mkojo.
Ni vyema kuwahi Hospitali mapema mara tu unapojigundua kuwa una baadhi ya hizo dalili.
Kwa ushauri na tiba za magonjwa yote hususani ya uzazi tafadhali waweza wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000, tunazo dawa zinazotibu matatizo yote hayo, zimetengenezwa kwa mimea na matunda na ziko katika mfumo wa vidonge.
Subscribe to:
Posts (Atom)