Inawezekana una bahati sana kuiona hii makala na itakujenga sana kiafya...tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anapokunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa mwaka.
Japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambapo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo. Biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
Yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.
1. Ugonjwa wa kisukari; kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi kushusha sukari. Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.
2. Unene na kitambi; utafiti ulofanywa na chuo kikuu cha Harvard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda ndugu yangu
3. Upungufu wa madini muhimu mwilini; soda ina kemikali inayoitwa Phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya Calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kwenye mwili wa binadamu.
4. Ugonjwa wa kansa; soda ina kemikali inayoitwa Caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.
5. Huongeza sumu mwilini; soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya ya mtumiaji.
Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha na kuua figo.
6. Hubadilisha rangi ya meno; kila mtu anataka kuwa na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi.hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.
7. Addiction; soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.Hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.
Sababu hii ndiyo inayotusumbua watu wengi na hata tunapoona makala zinazotuasa kuacha soda wala hatuelewi.
8. Huongeza kasi ya uzee; sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yaani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama ana miaka 35.
9. Hupunguza sana maji mwilini ; soda ina kiwango kikubwa cha madini ya Sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.
Mwisho; ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice ya matunda ya kutengeneza mwenyewe ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.
Share Makala hii kwa watu wengi zaidi ili tuwaokoe.
Wednesday, 13 July 2016
SODA TUNAZIPENDA LAKINI .......
Sunday, 10 July 2016
FAHAMU KUHUSU TATIZO SUGU LA CHUNUSI
hivi ni vipele vinavyotokea usoni, kifuani na mgongoni sababu ya kubadilika kwa mfumo wa kutengeneza mafuta wa ngozi.
chanzo ni nini?
hii husababishwa na kuongezeka hormone za uzazi aina ya testosterone kwa jinsia zote hasa hasa kipindi cha kubalehe na kuvunja ungo kwa jinsia zote.
matibabu.
matibabu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo....matibabu kwa chakula, matibabu ya kimwili na matibabu ya dawa za hospitali.
matibabu ya chakula..
- ondoa chumvi kwenye chakula chako au kula chumvi kidogo sana.
- epuka ulaji wa sukari na vyakula vyote vya kukaanga kama chips, maandazi na chapati.
- pendelea kula vyakula vya asili kama wali, ugali, mchicha, maharage, njegere vikiwa vimeungwa mafuta kidogo sana pia kula kwa wingi karoti mbichi kwa sababu zina vitamin A ambayo ni nzuri sana kwa ngozi
- kunywa maji mengi ili kuondoa sumu zote mwilini na kulainisha ngozi.
matibabu ya kimwili.
- acha ngozi yako ipate jua la asubuhi na jioni kila siku.
- weka sura yako kwenye mvuke wa maji ya moto kila siku.
- shiriki mazoezi ya aina yeyote hata kama ni kuruka kamba tu angalau utokwe jasho kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.
- kuna dawa zinasaidia kuondoa chunusi i.e antibiotiki kama doxcycline, vidonge vya vitamini A na vidonge vya hormone kwa wanawake mfano oetrogen, persol tube na kadhalika.
mwisho:
watu wengi hawaponi chunusi kwa sababu ya kupenda kutumia njia moja tu ya matibabu {dawa}, ni vizuri kuchanganya njia zote hapo juu kwa matokeo mazuri na inaposhindikana ni vizuri kumuona daktari bingwa wa ngozi kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
MAUMIVU MAKALI YA MGONGO
![]() |
| (Mgongo) |
![]() |
| (Maumivu yanayosambaa) |
- Maumivu yasiyohama (yapo katika eneo la mgongo husika haijalishi unafanya nini - localized pain). Mara nyingi maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli/mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa eneo la mgongoni. Au, ni yale yanayotokana na mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo hivyo kusababisha kuchanika kwa misuli ya ndani ya mgongo na kusababisha maumivu!!
- Maumivu yanayosambaaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili wako mbali na mgongo kama vile miguu. Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo wako kwa kupigwa/kuanguka. Mfano: shida ipo mgongoni ila unahisi ganzi kwenye miguu au miguu kuwaka moto).
- Moja ya visababishi vikuu vya maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama ni kichocheo cha kupata maumivu ya mgongo.
- Mkao: nyumbani, kazini, shuleni, n.k wakati unafanya shughuli zako za kila siku, una nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza hatari ya kupata maumivu ya mgongo
- Ubebaji wa mizigo mizito (kufikia kilo 5 au zaidi) usiozingatia afya ya mgongo.
- Kulalia godoro laini na lililobonyea/linalobonyea katikati
wakati wa kulaa. Hii husababisha misuli ya mgongo kuvutika kupita kiasi wakati
umelala na kupelekea kuchanika hivyo kuishia
katika kupata maumivu ya mgongo na ambayo hudumu kwa muda mrefu (wote) utakokuwa unalalia godoro hilo au hata zaidi..jpg)
(Godoro la kubonyea) - Kujeruhi(wa) mgongo wako kunakotokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe (kansa) katika uti wa mgongo.
- Ujauzito/uzito wa kupita kiasi (kitambi): wengi wanashtuka wanaposikia kuwa uzito (kitambi) husababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimam. Kuelemewa kwa misuli/mfupa hii husababisha mabadliko ya mwili katika kutafuta namna ya kufidia hali hiyo… mwisho ni maumivu!!!
- Msongo wa mawazo
(stress): msongo wa mawazo humfanya mtu kukaa katika mkao mbaya akiwaza na
kuwazua hivyo kuishia katika kupata maumivu ya mgongo kama nilvyotangulia kusema hapo juu.
- Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo na misuli ya pembeni mwa mifupa hiyo na kusababisha maumivu katika eneo husika.
- Kuvunjika au kuhama
kwa mifupa ya mgongo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu
mbali mbali ikiwemo ajali.
.jpg)
(Msongo wa mawazo) - Umri wa uzeeni: kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabdiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa-na-misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.[Wanawake huathiriwa mapema katika uzee wao kuliko wanaume kutokana na mfumo wa vichocheo (homoni) vya miili yao kupungua kwa haraka zaidi baada ya miaka kati ya 45-55 ya umri wao wa kuishi).
- Wanaume kujihusisha na UPIGAJI PUNYETO wakati wa ujana wao. Vijana wengi ukiwauliza watakwambia wameufanya sana mchezo huu na hadi wengine kufikia kuuhalalisha kuwa ni kawaida kufanya hivyo. Kitendo hiki huhusisha kwa sana uti wa mgongo na ubongo hivyo ni chanzo kimojawapo cha maumivu ya mgongo na hata upungufu wa NGUVU ZA KIUME
- Mumivu ya kwaida hasa yale yanayotokana na mshtuko wa misuli ya mgongo au mkao mbaya huwa yanaisha yenyewe ndani ya siku 4 -14, hivo mgonjwa anashauriwa kutumia dawa za kawaida za kutuliza mamivu.
- Maumivu yanayotokana na kujeruhiwa mgongo ikiwa ni pamoja na ajali/kupigwa/kuangukia mgongo n.k) unashauriwa kufika hospitalini au kituo cha afya kilicho karibu nawe ili upate uchunguzi yakinifu na ushauri/tiba.
- Maumivu yanayoamabatana na kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa, maumivu makali ya miguu, miguu kuwaka moto/ganzi yanahitaji tiba ya haraka na dharura kwa sababu tayari mfumo wa fahamu/neva utakuwa ulishaguswa/athiriwa kwa namna moja au nyingine.
- Mwone daktari wa tiba viungo (PHYSIOTHERAPIST) aliye karibu nawe kwa ushauri kuhusu namna ya:
- Kukaa vizuri ukiwa nyumbani, kazini au shuleni
- Namna ya kubeba mizigo kwa kujali na kuingatia afya ya mgongo wako ili kuepusha kujeruhi misuli ya mgongo wako.
- Mpangilio na uboreshaji wa mazingira ya kazi yako ili kuzuia hatari za kupata maumivu ya kimfumo (misuli-na-mifupa)
- Mazoezi muhimu kwa ajili ya afya ya mgongo wako.
- Tiba ya mazoezi ya viungo (na mgongo kwa ujumla) inayoendana na shida yako husika.
Sunday, 22 May 2016
ZIJUE TABIA 10 ZINAZOHARIBU FIGO
By Masha Masanja
Call/txt/whatsapp 0622925000
Kwa kifupi sana leo tunakutajia baadhi ya Tabia zinazochangia kuharibika kwa Figo. Tutambue kuwa tatizo hili la kufeli kwa figo limeshawakumba wengi na baadhi yao wameshapoteza maisha.
Ukiwa mzima mshukuru Mungu na ni vyema ukasoma makala hii ili kujinusuru na janga hili la kuharibikiwa figo.
Hizi hapa ni baadhi ya tabia 10 zinazoharibu figo:
1. Kubana mkojo kwa muda mrefu
2. Kutokunywa maji ya kutosha
3. Kutumia chumvi nyingi
4. Kula nyama mara nyingi zaidi
5. Kutokula chakula cha kutosha
6. Kuchelewa kujitibu maambukizi madogomadogo
7. Kutumia visivyo dawa za maumivu
8. Utumiaji wa madawa kwa ajili ya Insulin
9. Kunywa pombe kupita kiasi
10. Kutopata muda wa kutosha kupumzika
Tafadhari share makala hii kwa watu wengi zaidi ili nao wapate kujifunza na kisha kujinusuru na tatizo hili.
whatsapp 0622925000



.jpg)
.jpg)
.jpg)