MWANAMKE: NAMNA UNAVYOWEZA KUEPUKA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA HEDHI KWA KULA VYAKULA VYA ASILI
Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.
Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation(siku za kupata mimba), ipo siku tutaongelea kuhusu siku za kupata mimba.
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili;
Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
Karibu nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kubwa wanasema kuwa hupata maumivu makali lakini kiafya unatakiwa uingie hedhi bila kupata maumivu makali. Sasa hivi wapo wanawake au wasichana ambao wanapata maumivu hayo hadi wengine huzimia, kulazwa hospitalini na wengine hutumia sindano au vidonge vya kupunguza maumivu ndio wawe vizuri, na hii yote inatokana na tatizo la wanawake wengi vichocheo vyao haviko sawa(hormone imbalances)
SABABU INAYOPELEKEA MAUMIVU.
-kutofanya mazoezi.
-Kutokula matunda kwa wingi.
-Kutokula mboga za majani
-Pia ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa wingi, mfano Chipsi.
Sasa leo nakujuza vyakula vichache endapo utapendelea kuvitumia basi utamaliza au kupunguza kwa kiasi kikubwa maumivu hayo.
PAPAI BICHI
Papai lina uwezo mkubwa wa kulainisha misuli ya mirija ya uzazi hivyo kurahisisha utokaji wa hedhi bila maumivu.
Tunda hili lina manufaa zaidi kwa wasichana hasa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na stress. Utapata faida hizo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi(halijaiva ila limekomaa)
UFUTA
Jinsi unavyoweza kuandaa ufuta kwa tiba ya maumivu wakati wa hedhi ni kusaga ufuta na upate unga wake kisha changanya na maji ya moto. Kunywa mara mbili kwa siku.
Tiba hii huwafaa zaidi wasichana wadogo au wanawake wanaotoka hedhi kidogo zaidi
TANGAWIZI
Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na uweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo kwa siku mara mbili baada ya mlo.
Tutaendelea kuelezea zaidi vyakula vingine.
Tukiwa tunaendelea na kampeni yetu ya MWANAMKE NA HEDHI SALAMA, Bado ped za NEPLILY SANITARY zimebakia kuwa mkombozi wa tatizo hilo pamoja matatizo mengine yanayowasumbua wanawake kama fangasi, UTI, utokwaji wa uchafu, harufu mbaya n.k.
Ubora wa ped hizi unatokana na kuundwa kwa kitambaa cha pamba pekee na kuongezewa dawa maalum(ukiangalia picha ya ped iliyofunguliwa utaona kile kidude cha kijani ndiyo kila kitu katika ped hiyo).
Pia zina harufu nzuri sana itakayokufanya uzidi kuzipenda kuzitumia
Watu wengi wamekuwa wakiniuliza na kulalamika kuhusu upatikanaji wa hizi ped, unaweza kuzipata ped hizi Shinyanga, Mwanza, Bukoba, Iringa, Babati, Dodoma na Dar es salaam
Ili ujibiwe haraka swali lolote tuma sms ya kawaida kwenda 0622925000 au 0767925000.
Maelezo ya kiundani zaidi kuhusu ped wasiliana nasi 0767925000 au whatsapp 0622925000
Share makala hii ili na wengine wajifunze.