Sunday, 12 July 2015

MAUMIVU MAKALI YA KIFUA (ANGINA PECTORIS)

 Huu ni ugonjwa wa Moyo unaohusisha mgonjwa kupata maumivu makali upande wa kushoto wa kifua na maumivu hayo huenda mpaka shavuni, shingoni, mkono wa kushoto na hata mpaka mgongoni. Kwa hiyo mtu aliye na dalili hizo basi tambua ana tatizo la moyo na ugonjwa huo huitwa Angina Pectoris.
  Ugonjwa huo husababishwa hasa na kupungua kwa ujazo wa mishipa ya moyo na hivyo kuufanya moyo wenyewe usiweze kupata damu ya kutosha na kusababisha hewa ya Oxygen kupungua katika minofu ya moyo(myocard).
 Tatizo hili la mishipa hutokana na kula mafuta mengi hasa ya wanyama kama kitimoto, mafuta ya pamba, kula vyakula vya wanga kwa wingi na unywaji wa bia. Hivyo vyote vikiingia mwilini huendelea kuhifadhiwa kama mafuta. Vyanzo vingine vya tatizo hili ni uvutaji wa sigara, kutofanya mazoezi, kuwa na wasiwasi/mawazo kila mara na ugonjwa wa shinikizo la damu(B.P).
 Ugonjwa huu wa Angina Pectoris umegawanyika katika sehemu tatu(3);
1. Maumivu ayapatayo mtu wakati akifanya kazi ngumu au anatembea zaidi ya mita 100. Maumivu hayo hutokana na moyo kuongezeka kufanya kazi lakini damu ya Oxygen inakuwa haitoshi.
2. Maumivu yatokeayo wakati mtu akitembea chini ya mita 100 au kufanya kazi kidogo tu au kupanda ngazi ya ghorofa.
3. Maumivu ayapatayo mtu wakati amekaa au amepumzika tu.
NB: kama ukiwa na maumivu ya aina hizo tatu, tafadhali acha shughuli zote utakazokuwa unazifanya muda huo kisha hakikisha unafungua madirisha ya nyumba ili upate hewa ya kutosha.
Wagonjwa wa tatizo hili hushauriwa mara zote kutembea na vidonge vya Nitroglycerin kwa ajili ya kuondoa maumivu hayo pindi tu yanapowapata. Lakini vidonge hivyo huishia kuondoa maumivu tu na siyo kutibu tatizo.
Ugonjwa huu huweza kutibika kwa kiasi fulani kwa kubadili tabia zetu mfano kuacha kabisa kunywa pombe kali, kutokula mafuta mengi, kula chakula kwa wakati unaotakiwa, kuacha kuvuta sigara, kufanya mazoezi japo kwa kutembea kwa kasi hata kwa muda wa nusu saa au saa moja tu mara tatu kwa wiki na kutibu shinikizo la damu.
Pia kuna dawa iliyotengenezwa kwa majani ya *biloba*. Majani hayo yanapatikana nchini China na Thailand pekee. Dawa hii imeboreshwa na kuweza kutengenezwa katika mfumo wa vidonge na hivyo kuwa rahisi kupatikana sehemu zote hata hapa Tanzania.
 Endapo una ndugu au mtu wako wa karibu mwenye tatizo hilo tafadhali wasiliana nasi kwa 0767925000 au Whatsapp 0622925000 ili ujipatie dawa hiyo popote ulipo.

No comments:

Post a Comment