Friday, 3 July 2015

TAMBUA MWILI UNAVYOPATA SUMU NA NAMNA YA KUZIONDOA

Sumu ni kitu chochote ambacho huhatarisha utendaji kazi wa mfumo katika mwili.
Sumu huleta madhara ya aina mbili katika mwili
1. Madhara yasiyoweza kurekebishika (irreversible effects).
Madhara haya ni kama vile makovu, upofu, matatizo ya akili, matatizo ya damu, ukiziwi, kulemaa au kupooza n.k
2. Madhara yanayoweza kurekebishika.
Madhara haya ni kama vile uvimbe, kuwashwa kwa ngozi, ngozi kuwa kavu, kutokwa majipu, mwili kubadilika ngozi n.k
VYANZO VYA SUMU KATIKA MIILI YETU
Mwili hupata sumu kupitia njia tofauti kama tatu hivi:
i/ kupitia vitu ambavyo vipo nje ya mwili.
Hivi ni vitu ambavyo binadamu huvitumia na hatimaye humuathiri. Mtu huvitumia kwa kujua au kutojua. Mfano matumizi ya kemikali aina ya Zebaki (Mercury). Hii huathiri sana mapafu na moyo. Pia utumiaji mbovu wa dawa, ulaji mbovu wa vyakula, unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya n.k
ii/ Miili yetu yenyewe huzalisha sumu kupitia mifumo take mbambali ya kazi. Mfano mifumo ya mmeng'enyo wa chakula, mfumo wa hewa n.k. Katika mifumo hiyo baadhi ya sumu huzalishwa na kemikali(free radicals) ambazo hazitakiwi mwilini.
JNSI YA KUZIONDOA SUMU
Zoezi la kuondoa sumu mwilini hutegemea na aina ya sumu yenyewe. Kuna dawa ya kuvunja sumu(antidote). Hapa ni baada ya uchunguzi kufanyika na kugundulika aina ya sumu na kisha kupewa dawa za kuivunja sumu hiyo.
Chakula bora pia ni njia mojawapo ya kuondoa sumu mwilini. Hapa tunakuwa tunamaanisha vyakula vya asili ambavyo ni "antioxidants", hulinda mwili na kemikali hatarishi. Vyakula vya Vitamini A, C na E hupatikana zaidi katika mboga na matunda.
Vyakula vinavyopatikana katika makundi hayo mchicha, spinach, karoti, nanasi, maembe, machenza, mafuta ya alizeti n.k
Swali la kujiuliza katika mboga za majani, je zina ubora unaotakiwa? Maana zinalimwa na zinakuzwa kwa dawa za kuua wadudu. Dawa hizo pamoja na mbolea zake ni kemikali balaa.
Zipo dawa zilizotengenezwa kwa mimea ya aloe vera na militaris zinaondoa sumu mwilini bila madhara yoyote. Mimea hii huota na kustawishwa Barani Afrika na Asia. Dawa hizi zipo katika mfumo wa kawaida kabisa wa vidonge na utavitumia kwa muda wa mwezi mzima.
Wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 ili uweze kujipatia dawa hizo au ushauri wowote kuhusu matatizo ya Kiafya.