Friday, 4 November 2016

UTAMBUE MMEA WA GINSENG KATIKA KUTIBU MAGONJWA


Ginseng ni kiambata cha steroid kinachopatikana katika mimea ya aina ya "ginseng" mimea hii ina thamani kubwa na ina historia ndefu sana na watu wa China huiita mfaulme wa mitishamba "king of magic" hii inatokana na kazi ambayo mimea hii hufanya katika mwili wa binadamu

"Inasemekana mimea ya ginseng hutibu mgonjwa yote(King of herb).
Dawa hii hutengenezwa kutokana na mizizi ya mimea ya ginseng (red &white root).

Ginseng ni mitishamba inayouzwa sana katika nchi ya marekani kwa takriban asilimia 15 mpaka 20 ya mitishamba yote inayouzwa marekani ni ginseng.
Steroid ya aina hii hupatikana tu kwenye mimea ya jamii ya ginseng.
Ginseng ni molecule ndogo na inapoingia mwilini huingia katika kila ogani ya mwili sababu ya udogo wake na hufanya kazi yake kwa uhakika zaidi mpaka pale itakapotolewa nje ya mwili.

Udogo wa steroid hii ya ginseng na ueneaji wa dawa hii katika kila organi ya mwili na uwezo wake wa kukaa mwilini kwa muda mrefu huifanya ginseng kuwa dawa imara katika kutibu magonjwa mbalimbali.

GINSENG hii inaundwa na RH2 na RG3 ndizo steroid zinazoweza kupambana na magonjwa mbalimbali na kuzuia kansa, unaweza kuona jinsi gani dawa hii ilivyo ya muhimu

KAZI ZA GINSENOSIDE RG3
Kiambata hiki ni cha muhimu sana na hufanya kazi zifuatazo;
~Hutibu magonjwa ya moyo
~Hutibu magonjwa ya mzunguko wa damu
~Hutibu magonjwa yanayoukumba ubongo
~Magonjwa ya mishipa ya moyo
~Kupooza kwa miguu na mikono
~Hurudisha kumbukumbu hasa kwa watu waliokumbwa na stroke
~Hutibu kansa ya aina mbalimbali,
ginsenoside RG3 hufanya yafuatayo kupambana na kansa;
a)huzuia kutokukua na kuenea kwa kansa
b)ikitumiwa pamoja na dawa zinginee za kansa kama radiotherapy na chemotherapy huweza kuondoa kansa hiyo kwa kiasi kikubwa na kupunguza madhara utakayoyapata kutokana na dawa hizo
c) huongeza kinga ya mwili hasa T..cells hivyoo kuupa mwili uwezo mkubwa wa kupambana na kansa na magonjwa mengine
~Huongeza uwezo mkubwa wa ufikiriaji.
~Huondoa allergy kwani huzuia utolewaji wa histamine
~Husaidia katika kutibu kisukari kwani hufanya ongezeko la utolewaji wa insulin
~Huondoa uchovu wa muda mrefu kwa wagonjwaa wa siku nyingi na wale tunaofanya kazi ngumu bila kupumzika

KAZI YA GINSENG RH2
~Huzuia ukuaji na ueneaji wa kansa
~Husaidia katika uondoaji wa kansa
~Huongeza kinga ya mwili na hivyo kufanya mwili kupambana na kansa na magonjwa mbalimbali.
~Huweka sawa mfumo wa kinga ili kuzuia kansa kutokea,
~Hurudisha kumbukumbu hasa kwa watu walio na stroke.
~Hutibu matatizo ya figo
~Kwa kushirikiana na dawa zingine hutibu na kuzuia kusambaa kwa uvimbe
~Hutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na wanaume wanaoshindwa kuwapa ujauzito wenzi wao

JE GINSENG INAWAFAA WATU GANI???
~wagonjwa wote wa kansa especially stage 1 na 2 ili kuzuia kukua na kuenea kwa kansa,
~Huponyesha vidonda vya operation kwa haraka.
~wagonjwaa wote wanaotumia mionzi na kemikali ili kupunguza madhara ya dawa hizo.
~Watu wenye kinga ndogo ya mwili.
~wazee
~wagonjwaa wa muda mrefu,
~wagonjwa wa kisukari,magonjwa ya moyo, kiharusi.
~Allergy za aina zote.
~Watu wenye uvimbe wa aina yoyote
~Wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume/wanaoshindwa kuwapa ujauzito wenzi wao

Waweza ipata dawa hii ikiwa katika muundo wa vidonge(capsules) na utaweza kutumiwa popote ulipo

MASHA MASANJA
0622925000
Mshauri wa afya.

Friday, 14 October 2016

KUVURUGIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI SEHEMU YA 2


Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi humpata mwanamke yoyote aliyekatika umri wa kuzaa.
Tunaposema mzunguko unavurugika ni kwamba TAREHE MAALUMU YA KUINGIA HEDHI KWA MWANAMKE HAIELEWEKI kwa hiyo mwanamke anashindwa KUTIMIZA MALENGO YAKE kwa kutumia mzunguko huo.

Unaweza kujikuta unapata hedhi ghafla mahali usipotarajia hivyo unabaki na wasiwasi hujui la kufanya kwa kuwa haujajiandaa.
Vilevile unaweza kutokea utapoteza siku zako kabisa mfano ulitarajia tarehe fulani uingie mara hakuna dalili na haungii.
Juzi kanipigia simu dada mmoja analalamika kuwa hajapata hedhi tangu tarehe 20 August au hiyo jana 13 October.

FAIDA ZA KUFAHAMU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
-Itakusaidia kupata mimba uliyotarajia
-Itakusaidia kuepuka kupata mimba usiyoitarajia
-Unaweza kupanga upate mtoto gani/wa kike au kiume

JINSI TATIZO LINAVYOWEZA KUTOKEA
Kuvurugika kwa mzunguko utagundua endapo utafahamu vizuri mzunguko wako, ili kufahamu mzunguko inabidi uijue siku uliyoanza kuona damu hadi siku moja kabla hujaanza hedhi ya mwezi unaofuata.

Tatizo linapotokea linaweza kuwa kwa kurukaruka siku, yaani mwezi mwingine unaona na mwingine hauoni.
Damu ya hedhi inaweza kutokea kidogo kidogo na mabonge mabonge na maumivu makali
Maumivu wakati wa hedhi husambaa chini ya tumbo hadi miguuni na kiunoni

CHANZO CHA TATIZO LA MVURUGIKO WA HEDHI
-Mtu kupata hofu ,woga na mabadiliko ya kisakolojia
-Uwepo wa uvimbe kwenye kizazi
-Matatizo katika mfumo wa homoni
-Matatizo katika vifuko vya mayai na tabaka la ndani la kizazi ni moja wapo ya chanzo cha tatizo hili
-Kuharibika kwa mimba huchangia tatizo hili ambapo unapata damu bila mpangilio na maumivu makali
- Maambukizi sugu ya kizazi ni moja wapo ya sababu
-Dalili ya maambukizi sugu ya kizazi ni maumivu ya TUMBO CHINI YA KITOVU mara kwa mara ambapo kila ukipima unaambiwa unaumwa U.T.I kumbe hauumwi ugonjwa huo.
-Tatizo la kuvurugika kwa hedhi husababishwa na mabadiliko ya mazingira ambapo mfumo wa mwili hubadilika hasa unapotoka sehemu ya joto kwenda sehemu ya baridi au kutoka sehemu ya baridi na kwenda kwenye joto
-Kutokwa na uchafu ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa

MATIBABU YA KUVURUGIKA KWA MZUNGUKO WA HEDHI
Tembelea kituo cha kutolea huduma kilicho karibu na wewe kwa uchunguzi zaidi


Ped za Neplily sasa waweza kuzipata moja kwa moja ukiwa:
Dar mpigie 0752822948
Bukoba/Ngara/Muleba 0764152553
Iringa 0714476764
Arusha 0789836392
Tanga 0655292466
Mbeya 0653223351
Morogoro 0712961194
Mwanza & Shinyanga 0622925000
Zanzibar 0712760871

HIZI HAPA FAIDA ZA NEPLILY PED
-Zimetengenezwa kwa pamba/cotton pekee hivyo ni salama kwa maeneo ya siri kwani hupitisha hewa.
-Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
-Itapunguza siku zako za hedhi kama unachukua siku zaidi ya 7 basi itashuka kidogo
-Kama hedhi yako inaambatana na maumivu makali na kuharisha
-Kama tumbo lako hujaa gesi kabla na baada ya hedhi
-Kuchefu chefu wakati wa hedhi
-Kama hedhi yako ya bila kikomo
-Mzunguko wako wa hedhi unavurugika vurugika hovyo
-Maumivu makali yanayosababisha wengine hufikia hadi kulazwa
-Zinatibu hadi Bawasiri/kuota vinyama sehemu ya haja kubwa, hapa unazitumia kwa maelekezo maalum tutakayokupatia

HEDHI SALAMA NI HAKI YA KILA MWANAMKE

Pia sabuni za Pearl utazipata kupitia kwa hao watu, somo lililopita tulijaribu kuzielezea kiundani.
-hazina kemikali
-humaliza chunusi, madoa, kunuka kikwapa na kulainisha ngozi kwa ujumla.

Maelezo yote unayapata kupitia call/txt/whatsapp 0622925000

Tuesday, 4 October 2016

MAAJABU YA MAJANI YA GINKAGO BILOBA KATIKA KUTIBU MAGONJWA MBALIMBALI



KUTOKANA NA ONGEZEKO LA MARADHI MBALIMBALI KATIKA NYAKATI HIZI TUNAZOISHI KUTOKANA NA MFUMO WA USASA TULIONAO NA AINA YA VYAKULA TUNAVYOKULA ,MARADHI YAMEKUWA YAKIONGEZEKA KILA LEO.

MARADHI YAMEKUWA MENGI HIVYO WATU WOTE TUNASHAURIWA KUTUMIA CHAKULA BORA CHENYE VIRUTUBISHO VYOTE STAHIKI VYA MWILI, KUPUMZIKA NA KUFANYA MAZOEZI.

PIA TIBA MBADALA IMEONEKANA KUWA KIMBILIO LA WENGI KWANI NI TIBA AMBAZO ZINATENGENEZWA NA MIMEA NA MATUNDA.

LEO NAKUTAMBULISHA KWAKO MMEA WA ASILI AMBAO UNA UWEZO WA KUTIBU NA KUZUIA MARADHI MENGI SANA.

MTI HUU UNAOPATIKANA KASKAZINI MWA CHINA UNAITWA MTI MTAKATIFU(HOLY TREE) KUTOKANA NA UWEZO WAKE KATIKA KUTIBU NA KUZUIA MARADHI MBALIMBALI.

MAJANI YA MMEA HUU UITWAO GINKAGO BILOBA YAMEWEZA KUTENGENEZWA KITAALAM KATIKA MFUMO WA VIDONGE ILI KUMUWEZESHA MTU YOYOTE SASA HATA KAMA HAYUPO CHINA KUPATA TIBA HII ADIMU KUTOKA KATIKA MAJANI HAYA.

Dozi moja ya vidonge hivi hutumika kwa muda wa mwezi mzima na vinakuwa vidonge 96.

KAZI ZA GINKAGO BILOBA KATIKA MWILI WA BINADAMU NI:
●KAZI YAKE KUBWA NI KUONGEZA UFANISI WA USAFIRISHAJI WA DAMU KWENDA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI KAMA KWENYE UBONGO, MOYO HIVYO BASI KWA KAZI HIZO KUWEZA KUTIBU MARADHI YAFUATAYO.
1. MAUMIVU YA KICHWA YA MUDA MREFU
2. MATATIZO YA GANZI MWILINI
3. MATATIZO YA KIPANDA USO
4. MATATIZO YA KUSIKIA KELELE KWENYE MASIKIO(EAR RINGING)
5. MAUMIVU YA KIFUA UPANDE WA KUSHOTO MFANO CHEMBE MOYO
6. KUONDOA SUMU MWILINI (FREE RADICALS)HII NI OKSJEN AMBAYO HUINGIA MWILINI NA HAITUMIKI NA MWILI HIVYO INAVYOENDELEA KUKAA KWENYE MWILI WAKO INAHARIBU CELL ZA MWILI WAKO NA KULETA MADHARA KAMA KANSA N.K.
7. INAONGEZA KINGA YA MWILI
8. INAONDOA MAFUTA MABAYA YA CHOLESTROL MWILINI MWAKO.

Watu wanaoshauriwa kutumia vidonge hivi ni pamoja na wagonjwa wa shinikizo la damu(presha), wagonjwa wa Kisukari, watu wanaoumwa kichwa mara kwa mara, wenye kipandauso, chembemoyo, wanaojisikia kuchoka kila mara n.k

Unaweza kuyapata majani haya ya Ginkago biloba yakiwa katika mfumo wa vidonge ukiwa mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Manyara, Arusha, Dodoma, Iringa na Dar. Pia sehemu zingine unaweza pata kwa kutumiwa kupitia ofisi za mabasi ya mikoani.

Pia kwa wanawake wenye mizunguko mibovu ya hedhi, maumivu makali wakati wa hedhi, mirija ya uzazi kuziba na mambo mengine yanayoambatana na hedhi unaweza kuzipata ped zetu za Neplily katika mikoa tuliyoitaja

MAWASILIANO
Call 0767925000
Whatsapp 0622925000

Thursday, 29 September 2016

MAAMBUKIZI KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE (PID

Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huhusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.



PID husababishwa na nini?

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.

Je mwanamke huambukizwaje PID?


Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na

  • Kufanya ngono isiyo salama
  • Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
  • Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
  • Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
  • Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
Dalili za PID ni zipi?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni

  • Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
  • Kupata maumivu ya mgongo
  • Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
  • Kupata homa
  • Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
  • Pia kutapika
Vipimo vya PID
Ili kuweza kutambua kama mwanamke ameambukizwa ugonjwa huu, tabibu anaweza kufanya vipimo kadhaa vikiwemo

  • Kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba
  • Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
  • Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na uambukizi huo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa kitaalamu huitwa Full Blood Picture.
  • Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa cervical culture
  • Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono.
  • Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yeyote katika mfumo wake wa uzazi.
Matibabu
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa. Hata hivyo ieleweke kuwa matumizi ya dawa hizi hufuata miongozo mbalimbali ambayo imewekwa na wizara au mamlaka za afya zinazohusika. Miongozo hii hutofautiana kati ya sehemu na sehemu au nchi na nchi, ingawa kiujumla Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo limeweka muongozo wake kwa ajili ya kufuatwa na nchi mbalimbali.

Miongoni mwa dawa hizo ni pamoja na Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin na Sulbactam kwa pamoja na Doxycycline; na Ceftriaxone au Cefoxitin pamoja na Doxycycline.
Ieleweke pia haishauriwi kujinunulia na kutumia dawa hizi bila kupata ushauri ushauri wa mtaalamu wa afya. Aidha ili kuondoa maumivu na kushusha homa, dawa kama Paracetamol (Panadol) yaweza kutumika.

Jinsi ya kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi


Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na

  • Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kama ikiwezekana kujizuia kabisa kufanya ngono.
  • Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa
  • Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).
  • Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.
Ped za NEPLILY SANITARY kwa sasa zipo maeneo ya Dar es salaam, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Bukoba, Babati, Iringa na Ngara. Ni ped maalum zenye dawa kwa ajili ya matatizo yote ya akinamama wanapokuwa hedhi. 
Faida kubwa ya ped hizi ni pamoja na kuondoa maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi, kurekebisha mizunguko mibovu ya hedhi, kuondoa miwasho sehemu za siri, kutokwa uchafu wa ajabu sehemu za siri, fangasi n.k

Text/whatsapp 0622925000
Call 0767925000

Tafadhari share kwa ajili ya wengine

ZIJUE FAIDA 48 ZA TANGAWIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU


Huwa inanishangaza sana ninapoutafakari ukuu wa Mungu kwa namna ambayo ametupa mimea mbalimbali muhimu kwa ajili ya afya zetu – Mwanzo 1:29. Maelezo yafuatayo kuhusu tangawizi yatakupa wewe ujuzi wa mmea mwingine wa asili usio na madhara ya kikemikali na kusaidia mwili wako kuwa na afya nzuri na ya kupendeza.

Tafiti mpya zinazidi kuonyesha namna mmea huu ulivyo wa muhimu kwa afya ya binadamu ikihusisha uwezo wake wa kudili na aina mbalimbali za kansa mwilini na tafiti nyingine zinaendelea kufanyika.

Tangawizi inaweza kuwekwa karibu kwenye kila chakula, iwe ni katika kuilainisha nyama nyekundu, kuongeza radha katika nyama au samaki, kama chai, kwenye juisi na kadhalika.

Binafsi napenda ikiwa kwenye juisi ya matunda ndiyo inakuwa tamu zaidi na inaenda kufanya kazi mwilini haraka zaidi.

Tangawizi ni zao la kibiashara na ni rahisi kutoka kimaisha kama utaamua kulima tangawizi ingawa ni zao la miezi mingi lakini ukivumilia utakula bata tu, gunia moja linauzwa kati ya laki 3 hadi 6 wakati wa msimu mzuri.

Tangawizi iliorodheshwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Marekani kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.
Tangawizi huongezwa pia katika vinywaji vingi vya viwandani zikiwemo soda ili kupata radha nzuri zaidi.
Leo nimekuletea hii juisi ya tangawizi, nimetumia tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.

Kazi 48 za tangawizi mwilini
1. Huondoa sumu mwilini haraka sana
2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi
3. Kuna viua vijisumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi
4. Huondoa uvimbe mwilini
5. Huondoa msongamano mapafuni
6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake
7. Huondoa maumivu ya koo
8. Huua virusi wa homa
9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini ikiwemo maumivu wakati wa hedhi
10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)
11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.
12. Tangawizi ina kiinilishe muhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”
13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r
elated cancer)
14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)
15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu(lung cancer)
16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kansa mbalimbali za tumbo
17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kansa za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi
19. Huongeza msukumo wa damu
20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo
21. Huzuia damu kuganda
22. Hushusha kolestro
23. Husafisha damu
24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa
25. Hutibu shinikizo la juu la damu
26. Husafisha utumbo mpana
27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma
28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI
29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu
31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu
32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa
33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
34. Husaidia kuzuia kuharisha
35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu
36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
37. Hutibu homa ya kichwa
38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito
40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)
41. Huimarisha afya ya figo
42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
43. Ina madini ya potassium ya kutosha
44. Ina madini ya manganese ambayo ni muhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha
46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium
47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene
48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

Ped za NEPLILY SANITARY kwa sasa zipo maeneo ya Dar es salaam, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Bukoba, Babati, Iringa na Ngara. Ni ped maalum zenye dawa kwa ajili ya matatizo yote ya akinamama wanapokuwa hedhi.
Faida kubwa ya ped hizi ni pamoja na kuondoa maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi, kurekebisha mizunguko mibovu ya hedhi, kuondoa miwasho sehemu za siri, kutokwa uchafu wa ajabu sehemu za siri, fangasi n.k

Text/whatsapp 0622925000
Call 0767925000


Tafadhari share kwa ajili ya wengine

MWANAMKE: MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOHITAJI KUSHIKA MIMBA


Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu asishike mimba. Sababu hizo zinaweza zikawa zinamhusu mwanamke, mwanamume au wakati mwingine kutojulikana kabisa hali hiyo imesababishwa na nini. Wataalamu wanasema kwamba kwa miaka 20 iliyopita matatizo yanayohusu kushindwa kuzaa yameongezeka kwa kiwango kikubwa na asilimia 25 ya watu wanaotaka kubeba mimba na kuzaa mtoto wanakabiliwa na tatizo hilo. Ni kweli kuwa kwa kawaida watu wengi hubeba mimba na kujaaliwa mtoto pale tu wanapofanya tendo la ndoa. Lakini jambo hilo halitokei kwa watu wote na ingawa kwa baadhi ya watu kila kitu huonekana kwenda sawa lakini pia hushindwa kubeba mimba. Utafiti unaonyesha kwamba katika kila familia au 'couples' 5 zinazojamiiana katika wakati muafaka wa ovulation ni moja tu ndio hufanikiwa kupata mtoto, huku karibu wanawake 9 kati ya 10 wakifanikiwa kushika mimba baada ya kujaribu kutafuta mtoto kwa mwaka mmoja mzima bila kuzuia mimba. Hivyo basi nawaomba wale ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufuata maelekezo ili waweze kushika mimba lakini hawakufanikiwa, wasife moyo kwani ipo siku jitihada zao hizo zitazaa matunda.
 
Mambo ya kuzingatia iwapo unataka kushika mimba…
• Kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa kabla ya yote unamuona Daktari wako au unakwenda hospitalini na kufanyiwa vipimo ili kujua kama afya yako iko salama au la kwa ajili ya kushika mimba. Baadhi ya vipimo vinavyoshauriwa kufanywa ni pamoja na:
1. General examination au uchunguzi wa jumla.
2. Kipimo cha kensa au Pap smear.
3. Kipimo cha magonjwa ya zinaa (STD) kama vile Chlamydia ambayo yanaweza kuathiri uwezo wako wa kushika mimba.
4. Kipimo cha damu cha kuangalia kama una upungufu wa damu, Rh na kinga yako ya mwili dhidi ya ugonjwa wa Rubella.
5. Kipimo cha mkojo cha kuchunguza iwapo una ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa kisukari huweza kumzuia mtu asishike mimba hata iwapo mzunguko wake wa mwezi uko sawa, anapata Ovulation na kidhahiri anaonekana hana tatizo lolote.
6. Kama una paka nyumbani au unakula sana nyama (red meat) pengine si vibaya pia kupima kipimo cha Toxopmasmosis infection.
7. Kuyajua na kuzingatia baadhi ya mambo yanayoathiri kushika mimba ambayo ni pamoja na:-
• Ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa zaidi ya kilo 50 huweza pia kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia pia huathiri homoni mwilini.
• Kuwa na fikra nyingi na msongo wa mawazo 'stress' huweza pia kauthairi uwezo wa mtu wa kushika mimba.
• Kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanaume baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba (nitazungumzia vyakula vinavyosaidia kushika mimba baadaye)
• Sigara, marijuana na pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba. Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanamume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanaume.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomsaidia mwanamke kushika mimba:
• Anza kutumia vidonge vya Folic Acid, vidonge hivyo mbali ya faida nyinginezo humkinga mtoto atakayezaliwa na magonjwa ya ubongo. (Neural Tube Defect) kama vile Spinal Bifida na mengineyo. Dozi ni kwa uchache miligramu 0.4 za Folic acid kwa siku, miezi mitatu kabla ya kuanza hata kutafuta mtoto.
• Endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanaume aweze kuboresha na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo, Usikimbie chooni au bafuni baada tu ya kukutana kimwili na mwenzio. Kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.
• Jiepushe kunywa kahawa na vinywaji vinginevyo vyenye caffeine. Wataalamu wanasema caffeine huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.
• Jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.
• Usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama spray mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri. Mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate. Vitu kama hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.
• Hakikisha mwenzi wako hafanyi kazi au hawi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kufanya kazi kwenye mazingira ya joto kali sana kama vile mwanaume wanaofanya kazi kwenye matanuri ya kupika mikate, viwanda vya mafuta na miale hatari baadhi ya wakati huwa na matatizo ya kutozaa. Hivyo kabla mwanamke hajaanza kujilaumu kwa nini hashiki mimba, mwanaume wake pia anapaswa kufanyiwa uchunguzi kamili kuhusiana na suala hilo.
 Pengine ni suala ambalo wengi hatulijui kwamba katika tiba iwapo mke na mume au mtu na mwenzi wake wana tatizo la kutopata mtoto, wawili hao kwa pamoja hupaswa hufanyiwa vipimo na wala sio mwanamke mwenyewe. Hivyo iwapo unashindwa kushika mimba, hakikisha pia mwenzi wako hana tatizo pia.
Wanaume pia kama walivyo wanawake hukabiliwa na matatizo mengi tu yanayosababisha familia kukosa watoto. Matatizo kama vile upungufu wa mbegu za kiume, uchache wa mbegu, kutokuwa na kasi mbegu na mengineyo ni miongoni mwa matatizo kibao ambayo mwanaume anaweza kuwa nayo na kukosa mtoto. Hivyo tabia ya kuwatizama wanawake kwa jicho la lawama katika jamii na kuwanyooshea kidole pale mimba inaposhindikana kushika ni kinyume cha ukweli wa kitiba na uhalisia.
• Usichoke kufuata mzunguko wako wa Ovulation na kufanya tendo la ndoa katika wakati ambao mwili wako (ewe mwamamke) uko katika siku za kuweza kushika mimba.

Kama huzijui vizuri siku zako za kushika mimba basi usisite kuwasiliana na sisi ili tukueleweshe, na endapo siku zako za hedhi au mzunguko wako haueleweki, unapata maumivu makali wakati wa hedhi au wakati wa tendo la ndoa, una fangasi/miwasho/harufu kali sehemu za siri pia usisite kuwasilina nasi ili tukupatie ped maalumu zinazotibu na kumaliza kabisa matatizo hayo.

MAWASILIANO
0767925000
0622925000 - whatsapp

TAFADHALI SHARE MAKALA HII ILI NA WENGINE WAJIFUNZE

Monday, 26 September 2016

JINSI YA KUONDOA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI KWA KUTUMIA VYAKULA VYA ASILI


MWANAMKE: NAMNA UNAVYOWEZA KUEPUKA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA HEDHI KWA KULA VYAKULA VYA ASILI

Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.

Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation(siku za kupata mimba), ipo siku tutaongelea kuhusu siku za kupata mimba.

Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili;

Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

Karibu nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia kubwa wanasema kuwa hupata maumivu makali lakini kiafya unatakiwa uingie hedhi bila kupata maumivu makali. Sasa hivi wapo wanawake au wasichana ambao wanapata maumivu hayo hadi wengine huzimia, kulazwa hospitalini na wengine hutumia sindano au vidonge vya kupunguza maumivu ndio wawe vizuri, na hii yote inatokana na tatizo la wanawake wengi vichocheo vyao haviko sawa(hormone imbalances)

SABABU INAYOPELEKEA MAUMIVU.

-kutofanya mazoezi.
-Kutokula matunda kwa wingi.
-Kutokula mboga za majani
-Pia ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa wingi, mfano Chipsi.

Sasa leo nakujuza vyakula vichache endapo utapendelea kuvitumia basi utamaliza au kupunguza kwa kiasi kikubwa maumivu hayo.

PAPAI BICHI

Papai lina uwezo mkubwa wa kulainisha misuli ya mirija ya uzazi hivyo kurahisisha utokaji wa hedhi bila maumivu.
Tunda hili lina manufaa zaidi kwa wasichana hasa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na stress. Utapata faida hizo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi(halijaiva ila limekomaa)

UFUTA

Jinsi unavyoweza kuandaa ufuta kwa tiba ya maumivu wakati wa hedhi ni kusaga ufuta na upate unga wake kisha changanya na maji ya moto. Kunywa mara mbili kwa siku.
Tiba hii huwafaa zaidi wasichana wadogo au wanawake wanaotoka hedhi kidogo zaidi


TANGAWIZI

Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na uweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo kwa siku mara mbili baada ya mlo.
Tutaendelea kuelezea zaidi vyakula vingine.

Tukiwa tunaendelea na kampeni yetu ya MWANAMKE NA HEDHI SALAMA, Bado ped za NEPLILY SANITARY zimebakia kuwa mkombozi wa tatizo hilo pamoja matatizo mengine yanayowasumbua wanawake kama fangasi, UTI, utokwaji wa uchafu, harufu mbaya n.k.



Ubora wa ped hizi unatokana na kuundwa kwa kitambaa cha pamba pekee na kuongezewa dawa maalum(ukiangalia picha ya ped iliyofunguliwa utaona kile kidude cha kijani ndiyo kila kitu katika ped hiyo).
Pia zina harufu nzuri sana itakayokufanya uzidi kuzipenda kuzitumia



Watu wengi wamekuwa wakiniuliza na kulalamika kuhusu upatikanaji wa hizi ped, unaweza kuzipata ped hizi Shinyanga, Mwanza, Bukoba, Iringa, Babati, Dodoma na Dar es salaam

Ili ujibiwe haraka swali lolote tuma sms ya kawaida kwenda 0622925000 au 0767925000.


Maelezo ya kiundani zaidi kuhusu ped wasiliana nasi 0767925000 au whatsapp 0622925000

Share makala hii ili na wengine wajifunze.

Wednesday, 21 September 2016

MZUNGUKO BORA WA HEDHI

MWANAMKE KATIKA  MZUNGUKO BORA WA HEDHI

Imekuwa kawaida kuwasikia wadada wakilalamikia kuhusiana na kuwa na mizunguko mibovu kabisa ya hedhi ambayo imekuwa ikiambatana na maumivu makali ya tumbo la chini, kutokwa damu nyingi na kwa kipindi kirefu.

Leo tutaona visababishi vya matatizo hayo pamoja na suluhisho lake ambapo litakuweka wewe binti/mwanamke/mama ufurahie siku zako za hedhi na siyo kuzichukia

SABABU ZA KUWA NA MZUNGUKO MBOVU/UNAOBADILIKA MARA KWA MARA

■MAZINGIRA - Mazingira yanaweza kumfanya mwanamke kuwa na mzunguko usioeleweka. Kuhama kutoka eneo pengine lenye baridi kwenda eneo lenye joto inaweza kusababisha hali hiyo

■Kuwa na hofu/Uoga/Stress

■Uwepo wa uvimbe katika kizazi

■Matatizo ya mfumo wa homoni - hii ndiyo tatizo kuu kwa akinadada hasa kutokana na vyakula wanavyopenda kuvitumia

■Matatizo katika vifuko vya mayai na tabaka la ndani la kizazi

■Maambukizi sugu katika kizazi, mara nyingi unapoenda Hospitali unaambiwa una UTI(yutiai), lakini ukweli siyo hivyo.

■Kutokwa na uchafu ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hupelekea mwanamke kutofurahia tendo la ndoa

UCHUNGUZI
Uchunguzi  hufanyika katika Kliniki za magonjwa ya Akinamama ambapo vipimo mbalimbali hufanyika ikiwemo vipimo vya damu, mkojo, ultrasound na vingine

ATHARI ZA MZUNGUKO USIOELEWEKA
Siyo suala la kufurahia au kuishia kusikitika unapokuwa na tatizo tatizo. Madhara yake ni kama yafuatayo:
●KUTOPATA UJAUZITO
●MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA KUZAZI
●KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI
●KUPOTEZA HAMU YA TENDO LA NDOA IKIWA NI PAMOJA NA KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

PED ZA NEPLILY
Hizi ni ped zilizotengenezwa kwa kutumia "COTTON" PEKEE, Faida kubwa iliyomo katika ped hizi ni kuwepo kwa dawa maalum/chip ambayo ndiyo msaada mkubwa kwa wanawake wenye matatizo yaliyotajwa kwenye makala hii lakini pia hata ambaye hana matatizo maana ni msaada mkubwa wa kujiweka katika mazingira safi muda wote ili usishambuliwe na matatizo yaliyotajwa

HIZI HAPA NDIYO KAZI AMBAZO HUFANYWA NA PED HIZO
1. Husafisha via vya uzazi na kukufanya uwe hali nzuri katika mazingira yako muda wote

2. Hutibu magonjwa yote ya sehemu za siri kwa mwanamke mfano fangasi, UTI, Kutokwa uchafu sehemu za siri, harufu mbaya sehemu za siri n.k

3. Hurekebisha siku za  mzunguko wa hedhi

4. Hutibu tatizo la kutokuwa na uwiano wa homoni/hormonal imbalances

5. Husaidia kwa watu wenye matatizo ya kutopata watoto

6. Huzibua mirija ya uzazi

7. Hurudisha hamu ya tendo la ndoa

MATUMIZI
Unatumia kama unavyotumia ped zingine ulizozizoea, ni kipindi unapokuwa katika siku zako za hedhi.
Zipo aina mbili, za wakati wa kawaida(day use) na za wakati wa usiku(night use), hazitofauti matumizi. Uwezo wake wa kufyonza damu ni mls 250 - 280

Unaweza kujipatia ped hizi ukiwa Shinyanga, Mwanza, Bukoba na mikoa mingine pia tunatuma kupitia ofisi za mabasi ya mikoani.

MAWASILIANO
0767925000
0622925000-WHATSAPP


Friday, 29 July 2016

MWILI WAKO NI MDOGO UNATAKA UONGEZEKE?

Credit: Masha Products
WhatsApp: 0622925000

Endapo wewe unahisi mwili wako ni mdogo yaani ni mwembamba sana basi tunakushauri uweze kututafuta WhatsApp 0622925000 kisha tueleze changamoto wako tunakushauri nini cha kufanya.

Dawa tunayotoa kwa ni ya unga, lengo lake huwa ni kwenda kuuboresha mwili wako pamoja na kurudisha hamu ya chakula na hivyo kuwa rahisi kwako kuongezeka uzito.

Gharama zetu ni Tsh 37,000 kwa dozi hii ambayo utatumia kwa kunywa kijiko kimoja cha chai kutwa mara mbili unachanganyia kwenye uji mwepesi.

Tutakupatia pia formula ya kujitengenezea juisi ya protein booster.

Hivi vyote ni msaada kwako ili ufikie lengo lako mapema.

Pia tunauza unga wa Msamitu na Mlonge vyote kwa pamoja Tsh 45,000 ambavyo ni msaada mkubwa mno kwa wanaume ambao wana changamoto ya heshima ya ndoa, hizi hutibu hata kama uliathirika na punyeto kwa muda mwingi.


Monday, 25 July 2016

MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI - 2


Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia uwepo wa hii somo hili ikiwa leo tunaendelea sehemu ya pili. Mada yetu inasomeka hapo juu linawatokea Zaidi wanawake pasipo wao kutambua tatizo karibu asilimia 30%-45% ya wanawake wote wana matatizo haya huwa wanafanya tu tendo la ndoa kuwaridhisha waume zao na wao kutokufurahia tendo hili la kipekee.

~tatizo hili hutokana na sababu tofauti mfano uwiano mbaya wa homoni nk
~Mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na mambo makuu mawili ambayo ni matatizo ya kimwili na matatizo ya kisaikolojia kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya somo hili.

UTAJIGUNDUAJE KAMA UNA TATIHili O HILI?

Hili tulilisema sehemu iliyopita, mojawapo ni kusikia maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa, kingine ni kwamba una uwezo wa kufanya tendo mara moja tu huhitaji tena maana mzunguko wa kwanza wenyewe hata haukufika mwisho, tutakuja kuona mbeleni kabisa madhara ya hali hii kwani hatari ni kubwa kuliko unavyofikiria wewe mpenzi msomaji wa makala hii.


JINSI YA KUJIKINGA NA MATIBABU YAKE
Matibabu yake Hospitali ni magumu kwani hakuna dawa maalumu na Zaidi hufanyika kupitia vipimo vya uchunguzi, historia ya mhusika pamoja na Dalili za magonjwa mbalimbali, pamoja na hayo tatizo hili unaweza kulidhibiti kwa kufanya yafuatayo
-EPUKA KUVUTA SIGARA NA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI
-ZINGATIA ULAJI ULIO SAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI
-ONDOA MAWAZO NA HUZUNI
-BADILISHA MFUMO WA MAISHA YAKO
-ONGEZA UPENDO KATIKA MAHUSIANO YAKO
-WEKA MAZINGIRA MAZURI NA MUDA WA KUFANYA TENDO LA NDOA
-BADILISHA ENEO LA KUFANYIA MAPENZI, SIYO KILA SIKU KITANDANI TU.


Kaa tayari kwa sehemu ya tatu ya somo hili ambapo tutajifunza MWANAUME UFANYE NINI KAMA MKEO/MPENZI WAKO HAFIKI KILELENI.

MASHA MASANJA
Whatsapp 0622925000

TAFADHALI USISAHAU KUSHARE, KU-COMENT, KU-LIKE NA KUWAALIKA WENZAKO KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK "Mimea Yenye Ufumbuzi Wa Matatizo Yako" KWANI KUNA MASOMO KIBAO YAPO PALE KWA AJILI YA AFYA YAKO.


Saturday, 23 July 2016

TATIZO LA MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA - SEHEMU YA 1

VISABABISHI VYA MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA

        Kufika kileleni ni nini?
  Ni kiwango cha juu kabisa cha utamu, hisia, raha, msisimko wakati wa tendo la ndoa wakati ambapo misuli ya uke au uume hukaza.

        Kwa mwanaume huambatana na kutoa manii (ejaculation).
Wengine wakifika kileleni hupiga kelele sana, wengine huongea maneno ovyo ovyo hata matusi, wengine huzimia kabisa, wengine huwakwida wapenzi wao kama vile kibaka, wengine hutulia kimya na kupitiliza usingizi na wengine ukiwauliza wanasema mahali walikuwa ni kama vile walikuwa hewani, wengine kama vile walikuwa wananamwona Bwana (Yesu) n.k ilimradi tu ni raha na utamu. Na ni kweli Mungu alitupa zawadi ya ajabu na hii ni kujulisha kwamba Mungu alituumba tena kwa namna ya ajabu.  Pia wengine huita kufikia mshindo, wengine huita coming, wapo ambao kwa tendo moja la ndoa huweza kufika kileleni zaidi ya mara moja.

        JE, MWANAMKE NA MWANAUME HUFIKA KILELENI KWA PAMOJA?
        Kwa wanaume kufika kileleni ni suala ambalo ni automatic, halina mjadala, kitu cha msingi kwake ni kujitahidi asifike mapema kileleni ili amfikishe mke wake pale anatakiwa kufikishwa, kwani mara nyingi mwanaume akifika kileleni hupoteza uwezo wa kuendelea na tendo.

        Katika nchi zilizoendelea kama USA na Canada utafiti mwingi unaonesha kwamba asilimia 15 % ya wanawake hufika kileleni mara zote.
        Asilimia 48 % ya wanawake mara nyingi hufika kileleni.
        Asilimia 19 % ya wanawake ni kawaida kufika kileleni lakini si mara nyingi
        Asilimia 11 % ya wanawake ni nadra sana kufika kileleni na
        Asilimia 7% ya wanawake hawajawahi kufika kileleni na hawajui ni kitu gani.

        Hapa ni wanawake kutoka nchi zilizoendelea ambako elimu kuhusu mapenzi ni kubwa sana.
        je, kwetu nchi zilizogoma kuendelea hali itakuwaje?
        Ukizingatia wanaume wengi bado hawajajua nini wanawake wanahitaji ili kufikishwa kileleni?

        Pia kuna baadhi ya wanawake ambao hata wasipofika kileleni hawana shida wanaridhika tu bora maisha yanaenda.

        Nini Kitu muhimu kuhusu mwanamke kufika kileleni?
        Wanawake wanaweza kuendelea kupata utamu hata baada ya kufika kileleni hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anabaki ndani ya uke hadi anahitimisha tendo zima (conclusion) angalau kwa dakika 10 au 15 ndo ukimbie kuoga au kupiga usingizi siyo kumwacha kiumbe wa watu kwenye mataa akiugulia kwa kumuondolea utamu na raha.

        Tendo la ndoa huwa ni la kuridhisha sana hasa pale mume anapomfahamu vizuri mwanamke na kile anahitaji kwa kumfanyia utundu wote wa kuchokonoa sehemu zote ambazo zinaweza kumhakikishia kwamba atafika kileleni.
        Lakini pia mwanamke ana sehemu kubwa sana ya yeye kujihakikishia anafika kileleni si mwanaume tu ni suala la wote.

        Je sababu kubwa za mwanamke kufika kileleni ni nini?
        -Kukeketwa (Female Genital Mutilation).
        Kukeketwa ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake.
        Katika Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya.
        Ingawa wanawake waliokeketwa huweza kurudia hali ya kuweza kufika kileleni, walio wengi huathiriwa sana na hiki kitendo na kuwasababishia kushindwa kufika kieleleni.

        -Dini, jadi na utamaduni:
        Kuna baadhi ya mitazamo na malezi ya dini, jadi au tamaduni huwapa wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na maana kuhusiana na tendo la ndoa.
        Katika dini, jadi, na tamaduni nyingi ukiacha jando na unyago, elimu ya mwanamke kuhusu mwili na uzazi havifundishwi wala kutamkwa matokeo yake wanawake wengi hawaijui miili yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa kiume anamuoa binti hajui chochote kuhusu mwili wa huyo mwanamke na mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu mwili wake mwenyewe, akiguswa chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya mtoto, hapo utategemea atafikishwa kileleni kweli?

        -Kisaikolojia.
        Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.
        Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.)
        Hofu labda ya kuachwa, mashaka, kutojiamini, kukasirika, donge moyoni, kisirani au mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke kutofika kileleni.
        -Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na kupata hisia halisi (sensations).
        Kuwa na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa
        Mawazo hasi (Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchovu.

        -Kibailojia
        Kama vile kuwa na mfumo ovyo wa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya viungo vya uzazi pia huchangia.
        Anaweza kuwa na uvimbe au kisukari pia huchangia. Pia hitilafu za viungo baada ya kufanyiwa upasuaji hasa sehemu ya uke.

        -Umri (Menopause)
        Kuna wakati mwanamke kuanzia miaka 45 – 55 hupata mabadiliko ya upungufu wa homoni na huo upungufu husababisha sehemu ya uke kuwa kavu wakati wa tendo la ndoa.
        Kuwa na uke mkavu huchangia katika ufanisi wa tendo la ndoa kuwa mdogo na hatimaye kushindwa kufika kileleni
        Si kweli kwamba mwanamke akizeeka uwezo wa tendo la ndoa unakuwa mdogo, muhimu ni kutumia vilainisho kama gel au KY jelly na libeneke linaendelea kama kawaida.

        -Kutumia madawa (Medicaments).
        kama unatumia dawa za kuzuia msongo wa mawazo pia huchangia ile hamu ya tendo la ndoa (libido) na matokeo yake kukosa kufika kileleni.
        Pia kuna dawa za uzazi wa mpango hupunguza hamu ya tendo la ndoa hasa zile ambazo huingizwa mwilini (sindano)
        Pia dawa za kupunguza pressure hupunguza uwezekano wa kufika kileleni.

        -Pombe, madawa ya kulevya na sigara
        Alkoholi na madawa ya kulevya hupunguza sana hamu ya tendo la ndoa.
        Huathiri mfumo wa Fahamu unaohusika na mzunguko wa hisia za mapenzi kati ya ubongo na uke.
        Kama inavyoathiri (alkoholi) mwanaume kudindisha vilevile huathiri mwanamke kufika kileleni.

        -Mwonekano, urembo na umaridadi:
        Kwa mwanamke jinsi anavyoonekana na jinsi mwanaume anavyoonekana kuna sehemu katika hisia za mapenzi (emotions na feelings).
        Kama yeye mwenyewe anajijua kwamba hayupo vizuri kimwonekano (urembo, usafi, harufu) na pia kama mwanaume hayupo sawasawa basi anakuwa ameathirika sana kiasi ambacho hawezi kufika kileleni.
        Pia wanawake wana uwezo mkubwa kunusa harufu kuliko mwanaume hivyo harufu yoyote mbaya kwake huwezi kumpeleka nje kabisa ya njia ya kwenda kileleni.

        -Mazingira
        Kama eneo au chumba mlichopo hakina usalama kama vile anahisi mtu anachungulia au anaweza kuingia, kwa mwanamke hiyo ni ishu kwani hawezi kufika kileleni kwa sababu ya usalama

JE, ZIPO NJIA ZA  KUTATUA TATIZO LA KUTOFIKA KILELENI KWA MWANAMKE?
        -Kujiruhusu mwenyewe kupenda tendo la ndoa na zaidi kupenda kufika kileleni kwa hamu kubwa.
        -Kuwa responsible kwa mambo yote yanayohusu ufanisi wa tendo la ndoa.
        -Kujipa elimu na maarifa kuhusu elimu ya mapenzi kwa mwanaume na mwanamke, viungo vinavyohusika na kila kitu kinachoweza kukupa tofauti katika ufanisi na uimarishaji wa tendo la ndoa kama unavyosoma hapa sasa hivi.
        -Kuwa na mawasiliano wakati wa tendo la ndoa hasa kubusiana na maeneo yote ambayo unasisimka pale ukiguswa au kuchezewa.
        -Kufanyia kazi kila tatizo lolote la kisaikolojia na kupata solution kabla ya tendo la ndoa.

Kwa leo tuishie hapa, jiandae kwa sehemu ya pili ya somo hili.

MASHA MASANJA
Whatsapp: 0622925000


Saturday, 16 July 2016

SIKU YA KUSHIKA MIMBA MZUNGUKO MFUPI - 2


Mungu ndiye muumba watu wote na viumbe vyote juu na chini ya jua, hilo halina pingamizi wala ubishi na lazima tumshukuru Mungu kwa hilo, ila alitoa amri ya ndoa kwamba ZAENI MKAONGEZEKE kwa hiyo kila mtu anayependa kutimiza amri hii yafaa awe na maarifa.

Kwa wale wasiojua namna ya kuhesabu mizunguko yao basi ni muhimu kurudi katika maada zilizopita na kisha kujifunza namna ya kuhesabu mzunguko wako. Tambua ya kwamba mzunguko wa bleed (hedhi) ni tofauti sana na siku za bleed (hedhi).

VITU VYA KUJUA
1. Siku za bleed (hedhi) ni kuanzia na siku ya kwanza unapopata bleed hadi siku ile unamaliza bleed.
2. Wakati mzunguko wa bleed huanza siku umepata bleed mpaka siku moja kabla hujapata bleed nyingine.
Mfano umepata bleed tarehe 1 mwezi wa saba na bleed hiyo ikaisha tarehe 05 basi siku za bleed ni 5 na zimeanza tarehe moja na zikaisha tarehe 5.
Kama bleed nyingine umeipata tarehe 29 mwezi wa 7, basi mzunguko wako wa bleed ya mwezi wa saba umeanza tarehe 01 mwezi wa saba na ukaisha tarehe 28 mwezi wa saba. Mzunguko huo ni wa siku 28. Mzunguko wa mwezi wa 8 Umeanza tarehe 29 mwezi wa 7.
Ukiwa na mzunguko mfupi usiogope kwa kuwa bado unayo nafasi kubwa ya kupata mtoto na watu wengi tu wapo wana watoto.

Lazima ujue mzunguko wako kwanza ni wa siku ngapi. Mfano kama umekuwa na mzunguko wa siku 21 kwa muda wa miezi mitatu mfululizo na mfano umepata bleed tarehe 10 mwezi wa saba basi siku yako ya uzazi haiwezi kuwa siku ya 14 tangu kupata bleed. Bali ni siku ya 7 tangu umepata bleed.

HEBU ZAMA NDANI HAPA UJIFUNZE

Mzunguko wa siku 21 siku ya uzazi ni siku ya (7)  tangu upate bleed. Kwa hiyo kama utapata bleed siku 3 basi siku ya tano unatakiwa uanze tendo la ndoa. Mfano mzuri ni kama ufuatao. >>>Marry ameingia bleed leo tarehe 16 mwezi wa 7 na mzunguko wake kila mwezi unamchukua siku 21. Huyu Marry anachukua siku 3 za bleed. Basi siku zake atahesabu hivi tarehe 16 ni siku ya kwanza yaani leo tarehe16 ni siku ya kwanza ya bleed, kesho tarehe 17 ni siku ya pili ya bleed, kesho kutwa tarehe 18 ni siku ya tatu ya bleed, tarehe 19 ni  siku ya nne bleed imeisha, tarehe 20 siku ya tano bleed imeisha - anza hapa kukutana na mwenzako, tarehe 21 ni siku ya sita endelea na tendo na tarehe 22 siku ya saba endelea na tendo yai linatoka. Unashauriwa kuanza mapema ili kuongeza nafasi ya mbegu kulikuta yai.

MZUNGUKO WA SIKU 22,23,24,25 na 26

Mzunguko wa siku 22 yai linatoka siku ya 8 wewe anza tendo siku ya 6, 7 na 8
Mzunguko wa siku 23 yai linatoka siku ya 9 wewe anza tendo siku ya 7
Mzunguko wa siku 24 yai linatoka siku ya 10 wewe anza tendo siku ya 8
Mzunguko wa siku 25 yai linatoka siku ya 11 wewe anza tendo siku ya 9
Mzunguko wa siku 26 yai linatoka siku ya 12 wewe anza tendo siku ya 10

Kumbuka kuanza siku moja au mbili kabla ya siku ya yai kutoka pia unaweza ongeza siku 1 au mbili baada ya siku yenyewe hii ni kwa sababu mizunguko huwa inabadilika badilika kutokana na sababu mbalimbali kama ugonjwa na dawa nzitonzito mshituko kama wa kufiwa, kubadilika kwa hali ya hewa na pia mabadiliko ya mwili kama kunenepa.

Kumbuka kama umekaa muda mrefu hujapata mtoto ni lazima ufike hospitalini na kupima na kupata majibu sahihi. Ni muhimu pia ukawa uko karibu na mwenzako, una afya nzuri na mko vizuri kiuhusiano.

UMUHIMU WA CHAKULA BORA
Ni muhimu ule chakula bora na sio bora chakula. Imethibitika ya kwamba asilimia zaidi ya 50 ya matatizo ya hedhi hutokana na kutokula vizuri. Ulaji wa chips, soda, pombe kupindukia, kula wanga mwingi na sukari ni hatari kwa maisha ya ndoa. Unatakiwa kula chakula halisi (Real Food) chakula fresh na chakula cha asili. Vyakula hatari ni pamoja na vyakula vya paketi na makopo na kuku wa kisasa (chicken)

TUNAKUSAIDIAJE?
1.TUNATOA ELIMU YA AFYA KATIKA MAHUSIANO. Endelea kufuatilia mada zetu hapa ili kujifunza mengi zaidi, SHARE NA MARAFIKI ZAKO na pia Elimisha wengine.
2. PEDI ZA NEPLILY – Tumia pedi za neplily pads mara kwa mara. Pedi za Neplily ndio pedi bora kabisa kwa sasa kwa akinadada na akinamama. Zinaondoa miwasho, harufu mbaya UTI na fangasi za ukeni na miguuni. Zinarekebisha uchachu uliozidi ukeni na pia zinarekebisha hedhi zilizovurugika.  Zipo MWANZA, SHINYANGA, BUKOBA, DODOMA, IRINGA, BABATI NA DAR 
3. KUKOKOTOA SIKU YAKO YA UZAZI – Wasiliana nasi kwa meseji au whatsapp tu ukiwa umeshaandika siku zako za bleed za miezi minne 0622925000

KUOTA NYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA(BAWASIRI) -2

Mmoja wa wasomaji wa gazeti hili aliyejitambulisha kwa jina moja la Michael anauliza: “Katika sehemu zangu za haja kubwa, kuna vivimbe kama vitatu na ninapata taabu kukaa. Nimetumia dawa aina ya Anusol lakini bado sijapata nafuu, je naweza kutibiwa kwa njia gani za kisasa?” Msomaji mwingine nae anauliza: “Je dawa ya ugonjwa wa Bawasiri ni ipi hasa?”

Msomaji wetu mwingine pia anaeleza kuwa amesumbuliwa na maradhi ya Bawasiri kwa zaidi ya miaka kumi sasa na angependa kujua kama ugonjwa huu unatibika. Nae anauliza: “Je nitapata tiba ya ugonjwa huu?” Msomaji mwingine anamuelezea mchumba wake ana kinyama cha Bawasiri kimetoka katika njia ya haja kubwa na anauliza: “Je akienda hospitalini watakikata au atapewa dawa tu na kinyama kitatoka?”

Kutokana na maswali hayo na mengine mengi ambayo sikuyaandika hapa, nimeona kuwa ipo haja kwa siku ya leo tuangalie kwa kina jinsi maradhi haya yanavyotibiwa hospitalini kwa njia ya tiba zenye ushahidi wa kisayansi.

Kwanza kabisa ni vizuri kuelewa kuwa, kuna maradhi ya aina mbalimbali yanayotokea katika njia ya haja kubwa ambayo yanaweza kuwa na dalili zinazofanana na zile za maradhi ya bawasiri. Kwa sababu hiyo, ni vizuri kupata uchunguzi wa kitabibu kabla ya kuamua kuwa unaugua maradhi ya bawasiri.

Uchunguzi na vipimo
Kabla ya matibabu yoyote, daktari mwenye ujuzi wa tiba, atachunguza kwa kuangalia sehemu ya njia ya haja kubwa na kuona kwa macho hali halisi ilivyo. Baada ya hapo daktari anaweza kufanya kipimo kwa kutumia kidole cha shahada. Kidole hiki kikiwa ndani ya mpira wa kuvaa mikononi, kinaweza kulainishwa kwa vilainishi salama na kuingizwa katika njia ya puru ili kubaini hali ya uvimbe.

Daktari pia anaweza kutumia kipimo cha kutazama moja kwa moja katika njia ya haja kubwa kijulikanacho kwa jina la Proctoscopy au kipimo cha kutazama ndani ya utumbo mpana, Sigmoidoscope. Kipimo cha maabara cha kubaini damu iliyofichika; faecal occult blood test, nacho kinaweza kufanyika pale bawasiri daraja la kwanza inapokuwa ndani na inapokuwa vigumu kuibaini kwa kipimo cha kidole au proktoskopi.

Matibabu
Matibabu ya bawasiri kimsingi hutegemea dalili, hali na hatua ya ugonjwa. Kwa kawaida tiba ya awali ni kurekebisha mfumo wa maisha na mtindo wa kula. Mgonjwa hushauriwa kunywa maji mengi na kula vyakula vitakavyolainisha kinyesi kila siku. Vyakula hivyo ni kama vile matunda na mbogamboga kwa wingi, vyakula asili visivyo vya kukoboa, aepuke chumvi nyingi na pombe.

Mara nyingi mgonjwa hutibiwa kwa njia za kawaida zisizohusisha tiba kwa njia ya upasuaji. Mgonjwa mwenye kinyama au kivimbe kinachojitokeza nje, ataelekezwa jinsi ya kukalisha eneo la haja kubwa katika maji ya vuguvugu kwa muda wa dakika 15. Atatakiwa kufanya hivyo mara nyingi kadiri iwezekanavyo hasa kila baada ya kujisaidia.

Mgonjwa pia anaweza kupewa dawa za kupaka kwenye uvimbe ulioko katika njia ya haja kubwa au vidonge vya kuingiza ndani ya tundu la njia ya haja kubwa. Tiba hizi zitasaidia kupunguza uvimbe na maumivu anayoyapata mgonjwa wa bawasiri hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa.

Kama maumivu yatazidi, tiba rahisi iitwayo ‘Rubber band ligation’ inaweza kufanyika kwa bawasiri iliyoko ndani ya puru, yaani pale mishipa inapokuwa haijajitokeza nje. Bawasiri daraja la kwanza na la pili. Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo lililoathirika. Tiba nyingine ni ile ya kuunguza na kufunga uvimbe wa kinyama kwa kifaa maalumu (laser therapy).

Kama uvimbe wa mishipa ya vena ni mkubwa sana na unajitokeza sana nje ya puru (bawasiri daraja la 3 na 4), upasuaji unaweza kufanyika na hapa kinyama hukatwa na kuondolewa, kisha damu inayotoka hudhibitiwa kitaalamu. Tiba hii kitaalamu hujulikana kwa jina la haemorrhoidectomy.

Katika hospitali kubwa, aina nyingine ya upasuaji wa kisasa zaidi inaweza kufanyika pia. Tiba hii kwa jina la kitaalamu hujulikana kama Doppler-guided Haemorrhoidal Artery Ligation Operation (HALO) na wengine hupendelea kuiita Transanal Hemorrhoidal Dearterialization-Hemorrhoidectomy (THD).

Tiba hii ya upasuaji hufanyika bila kukata kinyama na bila kutumia dawa ya usingizi ingawa ganzi inatumika. Ni tiba ambayo haisababishi maumivu na mgonjwa anaweza kuendelea na shughuli zake baada ya saa 48 tokea kipindi cha kufanyiwa upasuaji.

Katika tiba hii, mishipa yote inayojitokeza nje, haikatwi bali inarudishwa ndani ya puru na kushonwa kwa nyuzi zinazoyeyuka zenyewe ili ijishikize kwenye misuli ya ndani ya haja kubwa na mishipa yote inayopeleka damu katika kinyama kinachovimba, hufungwa.

Lengo la kuifunga ni ili kuizuia isipeleke damu nyingi kwenye uvimbe. Baada ya hapo, sehemu hiyo hufunikwa kwa bendeji inayoyeyuka yenyewe baada ya kipindi fulani.

Dk Sushil Maslekar, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Njia ya Haja Kubwa katika Hospitali ya Spire Leeds nchini Uingereza, anasema kuwa tiba hii ni nzuri, haina madhara na inaondosha dalili zote za bawasiri kwa ufanisi mkubwa.

Utafiti wa miaka 10 wa Pravin J. Gupta na Surekha Kalaskar uliochapishwa mwaka 2008 katika jarida la sayansi za tiba liitwalo ‘Annals of Surgical Innovovation and Research’ toleo la 2(5), unabainisha kuwa upasuaji na kushona ngozi ya tundu la haja kubwa katika maeneo matatu ambayo kwa kawaida hutokeza bawasiri, unatoa matokeo mazuri zaidi ya uponaji wa bawasiri.

Pamoja na hayo yote, katika matibabu ya Bawasiri ni muhimu kukumbuka kuwa tiba hizi zinaponyesha lakini tatizo linaweza kujitokeza tena kama vyanzo vyake havikudhibitiwa. Ili kupona kabisa ni lazima mgonjwa arekebishe mfumo wake wa maisha na mtindo wa lishe.


Wednesday, 13 July 2016

SODA TUNAZIPENDA LAKINI .......

Inawezekana una bahati sana kuiona hii makala na itakujenga sana kiafya...tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anapokunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa mwaka.
Japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambapo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo. Biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.

Yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.
1. Ugonjwa wa kisukari; kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi kushusha sukari. Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.

2. Unene na kitambi; utafiti ulofanywa na chuo kikuu cha Harvard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda ndugu yangu

3. Upungufu wa madini muhimu mwilini; soda ina kemikali inayoitwa Phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya Calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kwenye mwili wa binadamu.

4. Ugonjwa wa kansa; soda ina kemikali inayoitwa Caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.

5. Huongeza sumu mwilini; soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya ya mtumiaji.
Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha na kuua figo.

6. Hubadilisha rangi ya meno; kila mtu anataka kuwa na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi.hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.

7. Addiction; soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.Hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.
Sababu hii ndiyo inayotusumbua watu wengi na hata tunapoona makala zinazotuasa kuacha soda wala hatuelewi.

8. Huongeza kasi ya uzee; sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yaani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama ana miaka 35.

9. Hupunguza sana maji mwilini ; soda ina kiwango kikubwa cha madini ya Sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.
Mwisho; ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice ya matunda ya kutengeneza mwenyewe ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.

Share Makala hii kwa watu wengi zaidi ili tuwaokoe.


Sunday, 10 July 2016

HATUA 5 ZA KUPATA MTOTO WA KIUME




Kupata mtoto wa kiume ni jambo linalohitaji ushirikiano wa pande zote mbili, yaani mke na mume na ni jambo linalohitaji hatua kwa hatua na kwa umakini, ingawa njia nitakayoeleza hapa haimaanishi kuwa inaweza kufanya kazi kwa asilimia 100.  Bali ni njia ambayo imekuwa ikitumika mara kwa mara na ndiyo njia rahisi na ukiifuata unaweza ukapata kwa asilimia 75.

Mwaka 1960 mwanasayansi Landrum Shettles aliandika kitabu kinachohusu uchaguzi wa jinsi ya mtoto.  Mwanasayansi huyo wa tiba ndiye aliyeileta nadharia yake iliyojikita zaidi katika vitu vilivyomo ndani ya seli, yaani malighafi za kijenetiki ziitwazo chromosomes ambayo ndiyo inayotumika na kama ikifuatwa vizuri basi huweza kuwa na mafanikio.

Sayansi ya kijenetiki inaeleza kuwa mwanamke huwa na mbegu ya XX na wa kiume huwa na XY, na pale yai la kike linaporutubishwa hutokea mgawanyiko wa seli na mbadilishano wa malighafi za kijenetiki hutokea.

Hivyo kiumbe kinachotungwa yaani mtoto, huwa na nusu ya malighafi za kijenetiki kutoka kwa mama na nusu nyingine kutoka kwa baba, na akipata mbegu XX huwa ni jinsi ya kike na akipata XY ni wa kiume.
Kiasilia mbegu Y huwa ni ndogo kimaumbo, zina mwendokasi mkubwa lakini hufa mapema ukilinganisha na za kike X ni kubwa, hazina kasi, lakini huishi kwa muda mrefu.  Kwa kutumia ufahamu huu ndipo mwanasayansi Shettels aliweka nadharia ambazo zinatumika katika uchaguzi wa jinsia.

Kuna hatua tano za kufuata kwa umakini ili uweze kufanikiwa, ingawa haimaanishi kuwa ni lazima ufanikiwe kwani hatua hizi huongeza nafasi zaidi ya kupata jinsi ya kiume na kwa yule atakayehitaji jinsi ya kike afanye kinyume cha hatua hizi.

Hatua ya kwanza
Hatua ya kwanza ni kugundua wakati wa ovulation, ama siku ambayo yai la kike linatoka.  Hiki ni kipindi ambacho yai la mwanamke lipo tayari kurutubishwa na mbegu ya kiume hivyo mimba huweza kutungishwa.

Ili kugundua kuwa upo katika ovulation, inabidi kufuatilia yafuatayo: Inabidi uwe na chati ya kuangalia na kufuatilia ute wa kizazi unaotoka ukeni, maana muda mfupi kabla ya ovulation ute huwa wa majimaji na wa kuvutika hufanana kama vile wa mayai ya kawaida, nikimaanisha ya kuku, ambayo yamezoeleka kwa wengi.

Ni vizuri kupanga chati hii kwa zaidi ya miezi mitatu ili kusudi uwe na uzoefu wa kugundua tofauti ya ute.  Vilevile inabidi uwe na chati ya kuweka rekodi ya joto la chini la mwili wakati ukiwa umepumzika, nikiwa na maana mara nyingi ukiwa umelala.

Joto la chini la mwili hupanda kwa nyuzi joto 0.5 sentigredi kipindi cha ovulation.  Ni vizuri chati hii iwe pamoja na ya ute wa kizazi, kusudi uweze kufuatilia mabadiliko haya kwa pamoja.

Kipimo cha kugundua ovulation ni kipimo ambacho huangalia wingi wa homoni aina ya Lutenizing ambayo hutolewa kwa wingi kipindi hiki.  Kipimo hiki ni vizuri kufanya mara mbili kwa siku, kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 9:00 mchana.  Vilevile kati ya saa 11:00 jioni na saa 4:00 usiku.

Hatua ya pili
Hii ni hatua ya kutegea wakati muafaka wa kufanya tendo la ndoa.  Ni vizuri kufanya tendo la ndoa kipindi cha saa 24 kabla ya ovulation na saa 12 baada ya ovulation.  Kwa sababu tindikali na utelezi katika ute wa kizazi hupungua na hivyo husaidia mbegu za mwanaume hasa aina ya Y kusafiri haraka na kulifikia yai la mwanamke na kulirutubisha.

Hatua ya tatu
Pendelea mtindo au staili inayofanywa na wanyama kama mbuzi wakati wa tendo la ndoa, yaani mtindo wa mwenza wako kuinama.
Mtindo huu huwezesha mlango wa uzazi kuwa karibu na sehemu ya kiume pia kuingia umbali mrefu zaidi ndani ya uke, hivyo basi mbegu za kiume humwagwa karibu na shingo ya kizazi na kulifikia yai haraka zaidi.

Hatua ya nne
Ni muhimu mwanamke kufika kileleni kabla ya mwanaume; kufika kileleni kwa mwanamke husaidia kubadili mazingira katika uke kuwa ya ukakasi (alkaline) hivyo kusaidia mbegu za kiume “Y” kuwa imara zaidi.  Uke kuwa na tindikali huipunguza uimara wa mbegu ya kiume.

Hatua ya tano
Hii ni kwa upande wa mwanaume.  Ni vizuri kuvaa nguo zisizoweka joto kali na kubana.  Unapaswa kuvaa chupi au nguo ambazo hupwaya na zimetengenezwa kwa pamba.  Nguo za ndani zinazobana ambazo huongeza joto hupunguza idadi ya mbegu za kiume.  Joto pia hupunguza ubora na utengenezaji wa mbegu za kiume.

Vilevile inabidi kunywa vinywaji vyenye caffeine kabla ya tendo la ndoa.  Hii huongeza nguvu ya mbegu za kiume aina ya Y.

Mambo mengine ya kuzingatia ni mlo.  Hakikisha unakula vizuri wiki moja kabla na siku ya tendo.  Tafiti zinaonyesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye sukari huiwezesha mbegu ya Y kuimarika zaidi na kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume.  Vyakula hivi ni kama matunda matamu, vyakula vya wanga na vinywaji vyenye glukosi.

Vyakula vingine ni kama vile nyama nyekundu, mayai, maziwa, vyakula vya baharini kama vile samaki, kamba na pweza.

Kwa upande wa mwanamke, anapaswa kula zaidi vyakula visivyo na tindikali kama vile kuepuka kula matunda yenye uchachu na vyakula jamii ya kunde kupitia kiasi.

Mambo mengine ni kuzingatia mazingira ya tendo lenyewe, hakikisha upo vizuri kiafya, kimwili na kiakili.  Usiwe na msongo wa mawazo na sonona kwa sababu huleta mwingiliano na tendo, hivyo kulifanya kuwa dhaifu.


Ni vyema pia kutafuta mazingira mazuri ya kufanyika kwa tendo lenyewe.  Lengo ni kuwa na utulivu wa kimwili na kiakili pia.  Hii itakuepusha pia na usumbufu utakaoweza kuleta mwingiliano na tendo lenyewe

FAHAMU KUHUSU TATIZO SUGU LA CHUNUSI

chunusi ni nini? 
hivi ni vipele vinavyotokea usoni, kifuani na mgongoni sababu ya kubadilika kwa mfumo wa kutengeneza mafuta wa ngozi.

chanzo ni nini?
hii husababishwa na kuongezeka hormone za uzazi aina ya testosterone kwa jinsia zote hasa hasa kipindi cha kubalehe na kuvunja ungo kwa jinsia zote.

matibabu.
matibabu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo....matibabu kwa chakula, matibabu ya kimwili na matibabu ya dawa za hospitali.


matibabu ya chakula..

  •  ondoa chumvi kwenye chakula chako au kula chumvi kidogo sana.
  •  epuka ulaji wa sukari na vyakula vyote vya kukaanga kama chips, maandazi na chapati.           
  • pendelea kula vyakula vya asili kama wali, ugali, mchicha, maharage, njegere vikiwa vimeungwa mafuta kidogo sana  pia kula kwa wingi karoti mbichi kwa sababu zina vitamin A ambayo ni nzuri sana kwa ngozi
  • kunywa maji mengi ili kuondoa sumu zote mwilini na kulainisha ngozi.

matibabu ya  kimwili.

  •  acha ngozi yako ipate jua la asubuhi na jioni kila siku.
  • weka sura yako kwenye mvuke wa maji ya moto kila siku. 
  • shiriki mazoezi ya aina yeyote hata kama ni kuruka kamba tu angalau utokwe jasho kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.                                                                                                                                          
 matibabu ya dawa

  • kuna dawa zinasaidia kuondoa chunusi i.e antibiotiki kama doxcycline, vidonge vya vitamini A na vidonge vya hormone kwa wanawake mfano oetrogen, persol tube na kadhalika. 

 mwisho:
 watu wengi hawaponi chunusi kwa sababu ya kupenda  kutumia njia moja tu ya matibabu {dawa}, ni vizuri kuchanganya njia zote hapo juu kwa matokeo mazuri na inaposhindikana ni vizuri kumuona daktari bingwa wa ngozi kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Uvimbe sehemu ya haja kubwa - bawasiri/bawasili (HAEMORRHOIDS)



Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
  • Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
  • Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
  • Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
  • Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
                 
Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;
  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayoongeza shinikizo katika tumbo.
  • Umri mkubwa
Dalili za bawasiri
  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri
  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids
Vipimo na uchunguzi
  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
Upasuaji;
  • Hemorrhoidectomy
  • Stapled hemorrhoidopexy
Njia za kuzuia Bawasiri
  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
Njia zingine za kuzuia Bawasiri
1. Jaribu kunywa maji ya kutosha na kula chakula chenye fiber nyingi ili uepuke kupata Choo kigumu.
2. Epuka kusimama muda mrefu au kukaa muda mrefu kama ulikuwa unafanya hivo awali
3. Fanya mazoezi ili kuongeza intenstine motility
4. Epuka kujikamua sana ukipatwa na haja kubwa
NB: Huu ugonjwa hauhusiani na matatizo ya uzazi
Baadhi ya sababu zinazopelekea hali hiyo ni

-kufunga choo ama kupata choo ngumu 
-ujauzito
-sababu za kiurithi-baadhi ya watu wanaweza kuwa na kuta dhaifu

Njia sahihi ya kupunguza Kitambi na Unene



Mtindo wa maisha, vyakula na shughuli za kila siku za mwanadamu ni baadhi ya vitu vinavyosababisha idadi kubwa ya wake kwa waume kuwa na uzito au unene kupita kiasi na wakati mwingine kuwa na vitambi.
Matatizo haya yamekuwa yakiwapata watu wa jinsia zote na kuwanyima raha wanawake wengi, ambao hufikia hatua ya kutumia mikanda maalumu ya kufunga tumbo au kuhangaika kupitia njia mbalimbali ili kupunguza kadhia hiyo kwao.

Kutokana na kuongezeka kwa tatizo hilo, kumezuka dawa nyingi zinazodaiwa kuwa na uwezo wa kupunguza vitambi na uzito mkubwa, lakini wataalamu wa afya wanaonya kuwa ni sumu.

Tafiti nyingi za kisayansi zinaonesha kuwa dawa hizi kwa kiasi kikubwa zina kemikali kama vile phentermine, sibutramine, phenolphthalein, caffein, hydroxycitric acid (HCA) na senna ambazo zina madhara makubwa kwa afya ya mwanadamu.
Dk. Phil McGraw anasema baadhi ya dawa hizo huathiri sehemu ya ubongo inayohusika na hamu ya chakula.  "Hamu ya chakula ni muhimu kwa ajili ya ubora wa afya na maisha.  Dawa yoyote inayoharibu hamu ya chakula kwa kipindi kirefu, inaweza kusababisha madhara ya kiafya", anasema Dk. Phil.
Mama mwenye uzito wa kilo 108, Doreen Shayo anasema amewahi kujaribu dawa za kupunguza mwili, lakini akapatwa na homa kali iliyohatarisha maisha yake baada ya wiki moja, hivyo alishindwa kuendelea na dozi hiyo.

"Nilishawishiwa kununua dawa hiyo ya kupunguza uzito na nilishauriwa kula mbogamboga, matunda na maji kwa wingi wakati wa dozi, sikuwa nakula wanga wala chakula kamili.  Nilipata homa ya ghafla madaktari wakanishauri kwamba dawa zile hazikuwa nzuri kwangu hivyo niachane nazo, wakati huo nilikuwa na kilo 120 lakini nilipungua kutokana na maelekezo ya madaktari", anasema Doreen.
Baadhi ya madaktari bingwa wa afya ya binadamu wanasema msukumo wa dawa hizo unaowafanya wahusika kuharisha mafuta mengi kwa wakati mmoja, ni njia isiyo sahihi ambayo pia huathiri baadhi ya viungo ndani ya tumbo, huku madhara yake yakijitokeza miaka kadhaa mbeleni.

Tabibu mmoja wa tiba mbadala anasema asilimia kubwa ya dawa za kupunguza kitambi na mwili kwa uharaka ni sumu.
"Mtu anapewa dawa anaharisha sana, swali la kujiuliza nini dawa inafanya tumboni na kusababisha kupata choo laini au kuyeyusha mafuta kwa muda mfupi?  Lazima tujue kwamba zina madhara baada ya muda, wengi wanauziwa vitu vibaya na mbegu fulani ambazo ni sumu halafu mwili unabadilika anaharisha sana, anaambiwa dawa ndio inafanya kazi yanatoka mafuta mengi, si njia sahihi ya kupunguza uzito wa mwili au kitambi."

Dk. Samuel Shita kutoka Hospitali ya Mwananyamala anasema kwa kawaida kuharisha humfanya mtu kupunguza maji mengi na chumvichumvi mwilini na hivyo huathiri kazi ya seli na mfumo wa fahamu.

"Dawa hizo nyingi hazijaruhusiwa kutumika na Wizara ya Afya na wala hazijathibitika kwamba ni sahihi kwa matumizi ya binadamu, lakini wanazitumia na madhara yake yanaanza kujitokeza baada ya kutumia mtu anaharisha sana na yeye anadhani ana mafuta lakini ule ni uteute unaokaa tumboni unaosaidia tumbo kufanya kazi.

"Utafiti unaonesha kuwa watu wanaopendelea kula katika migahawa mikubwa ndio wanaoongoza kuwa na miili mikubwa, teknolojia zipo na dawa zitumikazo lazima ziwe zimefanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 10.  Kuna madhara mengi yanayoweza kuwakuta watu ikiwamo ya figo, moyo, ini na mishipa ya damu."


Dk Shita anasema kuna njia sahihi za kupunguza tumbo ambazo pia ni salama.  "Mtu anatakiwa kufanya mazoezi mepesi na matumizi sahihi ya vyakula, tunatakiwa kupunguza vyakula vya wanga kupita kiasi, sukari na mafuta.
Anasema soda, pipi na chocolate ni vyakula ambavyo havitakiwi kutumika kupita kiasi.

Tabibu wa tiba mbadala anazitaja hatua sahihi za kupunguza kitambi na kuondoa sumu mwilini akisema: "Kutumia juisi za matango na nyanya kila siku kwa muda wa mwezi mmoja sumu zote zinaondoka."
Hata hivyo, Mwaka anasema mtu anapokula chakula ni lazima kiishe tumboni kabla ya kuingiza kingine, vinginevyo anakuwa ametunza sumu mwilini kutokana na kuwa na mabaki mengi ya chakula cha takriban hata mwaka mmoja.

"Mfuko wa chakula una uwezo wa kutunza chakula kwa muda mrefu, ndiyo maana binadamu hufa akikosa chakula kwa siku nyingi.  Miongoni mwa vitu vinavyofanya uondoe sumu mwilini ni kufuata sheria za ulaji na njia za asili za kuondoa sumu hiyo na si njia za haraka kwani zina madhara," alisema.
Wataalamu wa masuala ya dawa Deborah Mitchel na David Dadson, katika kitabu chao kilichochapishwa mwaka 2002 cha "The Diet Pill Guide: The Consumer's Book of Over-the-Counter and Prescription Weight -Loss Pills and Supplements," wanasema:

"Ingawa ushahidi wa dawa hizi unazidi kuongezeka, bado watu wengi wanaaminishwa kwa uongo kuwa zina manufaa.  Hata hivyo, pia watu wanaendelea kuamini kuwa dawa hizi zinazotokana na mimea na ni dawa salama za asili zinazofanyiwa utafiti wa kina na kuthibitishwa na mamlaka za udhibiti na usalama wa dawa kama nyingine za hospitalini."

Namna ya kupunguza kitambi


Maji ya moto yakitumiwa kwa umakini yana uwezo wa kupunguza kitambi, tumbo au uzito mkubwa wa mwili kwa asilimia 60.
"Maji ya moto yana uwezo wa kupunguza tumbo kwa zaidi ya asilimia 60, unachotakiwa kufanya ni kuyachemsha yawe ya vuguvugu kiasi kunywa kati ya glasi nne mpaka sita na iwe ni katikati ya mlo mpaka mlo ndiyo maana kuna watu wanashauri unywe asubuhi au iwe katikati ya mlo wa jana usiku na ule utakaokwenda kuula baadaye.

"Lakini pagumu zaidi ni pale ambako kabla hujakwenda kupiga mswaki ndiyo unatakiwa kuyanywa haya maji.  Tunapata vitamin B12 ambazo zinazalishwa mdomoni wakati binadamu akiwa amelala na mojawapo ya vitamin hiyo ni pamoja na kusaidia msagiko (mmeng'enyo) ule wa vyakula."

Tatizo la wengi kukaa na vyakula kwa muda mrefu tumboni ni moja ya sababu pia ya kuwa na tumbo kubwa yaani kuwa na mafuta ya ziada tumboni na wengine wanakuwa na vyakula vingi wanavyoingiza kuliko wanavyovitoa.



"Asubuhi kabla hujapiga mswaki ukaondoa zile vitamin mdomoni zinywe pamoja na maji, kunywa maji ya vuguvugu glasi nne mpaka sita kila siku unapoamka asubuhi mfululizo mpaka siku 21, baada ya muda fanya hivyo kwa wakati mwingine na wakati ukifanya hivyo pia epuka vile vitu vitakufanya uendelee kuwa na tumbo ili unachokifanya kiweze kuwa na majibu na si kuoga na kujipaka tope," anasema na kuongeza kuwa kupunguza vyakula vya wanga ni njia mojawapo itakayomfanya mhusika kupata majibu ya haraka