Thursday, 31 March 2016

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILI WAKO


By: Masha Masanja
Call/txt/whatsapp 0622925000
Email: mashamasanja@gmail.com

Watu wengi tumekuwa tukiishi kwa kutojua miili yetu kama ipo sawa, hii ni kutokana na kile kitendo pengine cha kutougua hutufanya tujisahau kabisa katika kujua undani wa Afya yetu.

Leo napenda tujifunze namna ya kujua jinsi gani utatambua kuwa UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILI WAKO(BODY MASS INDEX kwa kifupi BMI)

Kwa kifupi kitendo hiki huhusisha vitu viwili ambavyo ni uzito wako katika kilogram(kg) pamoja na urefu wako katika mita(m). Tutajifunza kwa kutumia mfano.

Uhusiano huo upo katika mpangilio kama ifuatavyo:
BMI ikiwa chini ya 18.50 hapa inakuwa mtu huyu uzito wake upo chini kuliko kawaida(UNDER WEIGHT)

BMI kuanzia 18.50 hadi 24.99 huyu mtu ni mwenye Afya njema na yuko vizuri kabisa(HEALTHY)

BMI kuanzia 25.00 hadi 29.99 huyu ni mtu ambaye amezidi uzito(OVER WEIGHT) hivyo uzito wake na urefu wake haviendani kabisa.

BMI kuanzia 30.00 na kuendelea basi huyu mtu ni yule aliyepitiliza kabisa kiwango cha uzito na anaingia katika kundi la Obesity.

Sasa unapata vipi uhusiano wa uzito na urefu wako(BMI)?

Angalia hapa chini

Kanuni(BMI)=uzito ÷ (urefu)kipeo cha pili
      
Tuangalie mfano mimi Masha nina uzito wa kg 64 na urefu wa sentimeta 162 ambao ni sawa na mita 1.62

BMI ya Masha=64/1.62×1.62
BMI=64/2.6244
BMI=24.386

Kwa mfano huo basi Masha yupo kwenye kundi salama japo bado kidogo tu afikie 25 ambapo siyo pazuri.

Sasa tufanye ya kwamba Masha ana uzito wa kilo 74 na urefu uleule

BMI= 74/2.6244
BMI=28.196
Hapa anakuwa OVER WEIGHT

Na endapo Masha ana uzito wa kg 91;
BMI=91/2.6244
BMI=34.6745
Hapa ni OBESITY!!

Ndugu msomaji wa makala hii nadhani sasa umeshafahamu namna ya kujua kama una uzito unaoendana na urefu wako, hivyo unaweza kujifanyia tathimini wewe mwenyewe.

NOTE: UREFU WAKO UWE KATIKA KIPIMO CHA MITA(METRE).

Unaweza ku-share zaidi makala hii kwa watu wengi kadri uwezavyo ili nao waweze kujifunza kama ulivyojifunza wewe.

Pia huwa ninatoa ushauri na mafunzo maalumu jinsi ya kupunguza uzito/kitambi na nyamazembe kwa kutumia chakula tu, chakula hicho kitaubadili mwili  uwe mashine ya kuunguza mafuta.

Wednesday, 30 March 2016

Hebu angalia faida 50 za kufanya mazoezi ya viungo ndani ya mwili wako

Umuhimu wa mazoezi kwa afya bora na maisha marefu bila maumivu.

Moja ya mahitaji matano (5) mhimu ili kuishi baada ya oksijeni, maji, chumvi, na potasiamu; ni Mazoezi. Mazoezi ni muhimu kwa ajili ya afya zaidi ya kuwa na maumbile ya kuvutia (sex body), burudani au kitu kingine chochote.

Watu wengi hufuatilia kuhusu chakula tu, hata kama utakula vizuri vipi bila mazoezi mlo haujakamilika, kwa hiyo mazoezi ni mhimu kwa yeyote kama ilivyo kwa maji au chakula.
Hizi ndizo faida 50 za mazoezi

Zifuatazo ni moja ya sababu 50 mhimu za kufanya mazoezi kwa afya bora na maisha marefu bila maumivu:

1. Hukufanya ujisikie vizuri
2. Huongeza uwezo wa kujifunza
3. Hujenga uwezo wa kujistahi
4. Huongeza nguvu ya ubongo kufanya kazi
5. Huuweka mwili wako kuwa unaofaa (fit) na wenye uwezo
6. Huongeza afya ya akili yako
7. Huongeza kinga ya mwili
8. Hupunguza mfadhaiko/stress
9. Hukufanya ujisikie vizuri/mwenye furaha
10. Hukufanya usizeeke mapema
11. Huweka ngozi yenye mng’aro na yenye afya
12. Husaidia kupata usingizi mtulivu
13. Husaidia kuzuia ugonjwa wa kiharusi/strokes
14. Huongeza ufanisi katika makutano/joints za mwili
15. Huongeza nguvu za mishipa
16. Huondoa wasiwasi
17. Huongeza kumbukumbu
18. Husaidia kudhibiti ulevi/uteja
19. Huongeza uzalishaji
20. Huongeza uwezo wa ubunifu
21. Hupendezesha muonekano wa mwili
22. Huongeza uwezo wa kujiamini
23. Husaidia kuongeza nguvu juu ya malengo yako maishani
24. Huondoa tatizo la kukinaishwa na chakula
25. Huongeza miaka ya kuishi
26. Hukomaza mifupa
27. Huongeza afya ya moyo
28. Huongeza hali ya kuwa na msimamo
29. Huondoa homa ndogo ndogo mwilini
30. Huongeza hamu ya kula
31. Hudhibiti usawa wa lehemu/kolesteroli
32. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi ya kansa
33. Hushusha shinikizo la juu la damu/BP
34. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
35. Huzuia kupatwa na ukichaa/uwendawazimu
36. Hupunguza au huzuia maumivu ya mgongo
37. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa mifupa
38. Hupunguza hisia/fikra za kujisikia vibaya au kupiga punyeto kwa vijana
39. Huzuia kupotea kwa mishipa
40. Huongeza nguvu na ustahimilivu
41. Huongeza ufanisi katika michezo
42. Huongeza uwezo wa kuvumilia maumivu
43. Huongeza usawa na ushirikiano wa mwili
44. Huongeza usambazaji wa oksijeni katika seli za mwili
45. Huongeza hali ya ufuatiliaji/concentration
46. Huongeza uwezo wa kujitawala na kujidhibiti nafsi
47. Huondoa uchovu
48. Huongeza nguvu katika tendo la ndoa
49. Hufanya maisha kuwa yenye kuvutia zaidi
50. Huongeza ubora wa maisha

Mazoezi yafuatayo ni mazuri sababu ya thamani yake ya baadaye na hayasababishi maumivu kwenye maungio, nayo ni; kutembea kwa miguu, kuogelea, kuendesha baiskeli, kucheza tenisi, gofu, kukwea, kuruka kamba, kudansi na kadhalika.


Tafadhari share makala hii ili na wengine wajifunze kama wewe

Naitwa Masha Masanja, mshauri wa Afya. Pia ninatoa program maalumu kwa mtu anayehitaji kupungua uzito/kitambi au nyamazembe.

Mawasiliano:
0622925000 - whatsapp
0767925000
0784925000


Wednesday, 16 March 2016

ZIJUE NJIA ZA KUPATA PESA


Robert Kiyosaki ambaye ni mwandishi wa Kitabu kiitwacho “ Rich Dad Poor Dad” ameainisha njia nne za kupata fedha na kuwekeza.
Nimeona ni vema kuwashirikisha wasomaji wangu njia hizo na kuzidi kuwapatia dondoo zaidi za uwekezaji. Kwa jinsi ambavyo Robert Kiyosaki ameandika fedha zinapatikana kwa njia zifuatazo:

1. Kuajiriwa (employment)- ukiajiriwa unalipwa mshahara na malupulupu mbalimbali lakini unafanya kazi ya mtu mwingine.
Ingawa siyo lazima kufanya kazi wakati wote lakini Kiyosaki alisema “fanya kazi ujifunze au kwa kiingereza work to learn”.

2. Kujiajiri (self-employment)- hapa unajiajiri kama mjasiriamali lakini pia biashara yako inakuwa ndogo na unakuwa umeajiriwa lakini kwenye biashara yako.
Faida yake ni kwamba unakuwa huru na unakuwa wa kukua. Lakini usipopambana ukue unaweza kupata kipato kidogo kuliko hata watu walioajiriwa.

3. Biashara (business) –hapa unamiliki biashara ambayo umeajiri watu wengine wanaofanya kazi kwa ajili yako. Kazi yako inakuwa ni usimamizi na kuhahakikisha biashara inakua.
Ukifika hapa uwezekano wa kukua ni mkubwa kama utakuwa kiongozi mwenye mikakati.

4. Kuwekeza (investment) –hapa unawekeza kwenye rasilimali “assets” ambazo zinakupa kipato hata kama haupo (passive income).
Kwa hapa unaweza kuwekeza kwenye nyumba, ardhi, taasisi za fedha (financial institution) kama kwenye account za muda maalum, hati fungate, hisa n.k.
Usikubali hela yako hata shilingi laki moja ikae bure hata kwa mwezi zipo njia za kuwekeza.

Saturday, 12 March 2016

Angalia mtazamo kuhusu Elimu na Ajira, bado Ujasiriamali unahitajika tu


Tatizo la ajira litakoma tu kama mitazamo yetu itabadilika kuanzia ngazi ya familia mpaka ngazi ya kitaifa mtazamo huu:

Familia zetu zinatakiwa kujua tu kuwa mtu haendi shule ili aje afanye tu kazi za kuajiriwa maofisini kwenye kiyoyozi lakini familia zilenge kumpeleka shule mtoto ili apate ujuzi utakao muwezesha kupambana na mazingira na soko la ajira ambalo linahitaji sana ujuzi na uwezo kuliko vyeti.

Familia pia ijenge utamaduni wa kuandaa mifuko ya miradi itakayo wawezesha watoto wao kujiajiri mara wamalizapo shule.

Familia zetu pia ziwe na utamaduni wa kufuatilia masomo ya kijasiriamali kupitia runinga na hata vinginevyo ziweze kuwafungua. Wazazi wajue namna ya kuwa control watoto wao kuangalia vitakavyowajenga katika mtazamo chanya tokea wako watoto.


Pili upande wa makanisa ni kuwa tusi hubiri sana muujiza wa maisha, maisha siyo muujiza ni uhalisia.

Waumini wafundishwe kinaga ubaga kwamba bila kufanya kazi maisha hayatabadilika hata kama mtu ananena kwa lugha.

Familia itengeneze mfumo unaowezekana wa kuwatambua watu wasio na kazi na kanisa liwawezeshe.

Makanisa yaandae semina na vipindi mbalimbali vya kufundisha masomo ya ujasiriamali na Elimu ya kuweka akiba. Makanisa yamekuwa yakihubiri sana Neno la MUNGU na wamesahau kuwa Neno bila fedha haliwezi kuhubiriwa.


Tatu upande wa serikali ni kwamba serikali inahitaji kuingiza somo la ujasiriamali kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu ili kuwajenga wanafunzi waweze kujua umuhimu wa kujiajiri.

Serikali pia inatakiwa kupunguza miaka ya kustaafu kwa watumishi wa umma kwa mtazamo kwamba watumishi wa umma wafanye kazi kwa mkataba say wa miaka 10-15 na walipwe mishahara inayoonekana na wasisitizwe kuwekeza maana baada ya miaka hiyo wataondoka ili kupisha mawazo na watu wengine kuingia kazini.

Haiwezekani unampa mtu astaafu baada ya kufikisha miaka 60. HAPA ndo watu wanajisahau wanakufa maskini Pamoja na kuwa walikuwa wanapokea mishahara mikubwa.

Serikali pia ifanye mpango wa kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mkubwa wa kuanzisha makampuni na iwawezeshe ili wanafunzi hao waajiri wanafunzi wengine. Serikali itoe fursa kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho kuandika mawazo ya kibiashara na yale yanayowezekana yawezeshwe na watu waanze mara moja wamalizapo.


Mwisho upande wa mtu binafsi.
Kimsingi tatizo hili linaanza na sisi wenyewe.

Jim Rhon anasema "kama utabadilika kila kitu kitabadilika".

Kuna haja sasa mtu binafsi kuanza kubadili mtazamo wake hasa kwa wasomi.

Amini kuwa siyo lazima uajiriwe na mtu ofisini na kumbe unaweza fanya mambo yako na ukifika mbali.

Anza na kile ulichonacho (capital accumulation) na baade utafika mbali usisubiri mitaji mikubwa.

Penda maarifa kwa kusoma vitu vizur vitakavyo kusaidia.

Maisha ni vile utakavyoamua wewe yawe. Hakuna mtu mwenye uweze wa kutengeneza maisha yako. Wewe ndo pekee wa kuweza kubadilisha maisha kwa kuwa ndo dereva wa maisha yako.

Namaliza kwa kusema Inawezekana "what was impossible yesterday is possible today".
Wajibika..!!

Masha Masanja
0622925000

Friday, 11 March 2016

YAONE MAAJABU YA SABUNI HII ILIYOTENGENEZWA KWA MAGAMBA YA VIUMBE WA BAHARINI



Ni sabuni iliyotengenezwa kutokana na magamba ya viumbe wa baharini kama simbi, konokono na viumbe wengine wa baharini.
Magamba hayo yanasagwa na kutolewa ili kutengeneza sabuni hii bora.

Sabuni hii ina aina18 za amino acid..zaid ya aina 30 za Trace Element na vitamins ambazo zinasafirisha material yenye virutubisho ndani ya ngozi na kuondoa vitu vigeni katika ngozi yako

KAZI ZAKE
1. Kutengeneza uzuri wa ngozi iwe na ubora wake.
2. Inaimarisha uasili wa ngozi.
3. Inaondoa mafuta na jasho na kuifanya ngozi kubaki kavu na safi.
4. Inasafisha na inaondoa sumu ndani ya ngozi.
5. Inaondoa mabaka na upele.
6. Kuponya muendelezo wa tishu zilizoharibika ndani ya ngozi.
7. Kuondoa mafuta yaliyoganda na kuziba vinyweleo na kuifanya ipumue vizuri
8. Inaondoa chunusi na kuifanya sura ing'ae.
9. Inang'arisha ngozi
10. Inazuia uharibifu wa ngozi unaotokana na miale ya jua na miali yenye kemikali nyingine kupitia ngozi.
11. Inaondoa mba wa shingoni, mwilini na hata kichwani.
12. Inaondoa Fangasi za aina zote hata kwa wanaonuka miguu wameliwa vidole wakivua viatu.

Utaalamu huu wa kutumia viumbe wa bahari katika usafi na uimara wa ngozi ulianza karne nyingi nchini china na unaendelea hadi leo na hata wazee wa Kichina hawachoki ngozi na akili.
Ni nzuri kwa wanawake, wanaume watoto, vijana na wazee...!!


MATUMIZI
1. Loweka ngozi kwa maji safi.
2. Paka sabuni juu ya ngozi.
3. Sugua kwa dakika 1 - 3.
4. Suuza kwa maji safi.
5. Tumia mara 2 kwa siku kupata matokeo mazuri

Enjoy harufu nzuri na isiyoumiza pua zako yenye kukufanya upende kuendelea kuoga tu muda wote...! Harufu salama ya maua na zabibu..!

ANGALIZO
Sabuni hii haijatengenezwa kwa kemikali za viwandani ni Tiba mbadala, hivyo unashauriwa kuitumia na kutokupaka vipodozi vya kemikali, hasa Lotion zenye hydroquinone, ina maana utakuwa unatibu Kisha unajeruhi tena, Tumia Lotion zisizo na kemikali.

Kwa kuzipata sabuni hizi wasiliana nami hakika hutaogea sabuni nyingine yenye kemikali tena maana ni sabuni salama kabisa.

Whatsapp 0622925000
Call 0767925000

Monday, 7 March 2016

MAMBO MUHIMU YA KUFANYA UNAPOTAKA KUANZA BIASHARA YA MTANDAO



Watu wengi wamekuwa wakibabaika wanapokabiliwa na watu Kuchagua kampuni ya mtandao wanaowafuata na kuwashawishi kujiunga na kampuni za mitandao au pale wanapokuwa wameamua kwa mapenzi yao kuingia kwenye biashara za mtandao wasijue namna ya kutoa maamuzi sahihi kwamba ni kampuni ipi au zipi ndizo bora kujiunga nazo.

Kwa maoni yangu, hii ndiyo hatua muhimu kuliko zote kwa sababu endapo utaangukia kwenye mikono ya kampuni mbovu, nguvu zako na mtaji wako vyote ni bure. Leo katika ukurasa huu tutaona vigezo vya kuvitumia katika kuchagua kampuni ya mtandao ya kujiunga nayo. Moja kwa moja nitaanza kwa kuviorodhesha vigezo hivyo au sifa za kampuni bora na kuvitolea maelezo.



1. Historia Ya Kampuni
Zipo kampuni ambazo zinaanza biashara na baada ya muda mfupi zinapotea au kufilisika. Kama ulikuwa mmoja wa wanachama wa kampuni ya namna hiyo, lazima utakuwa umeathirika kwa namna fulani. Inabidi upate kampuni ambayo ina historia ya kufanya biashara kwa muda mrefu, kwa ufanisi na ambayo biashara yake bado inaendelea kukua na si ile ambayo imefikia ukomo. Njia rahisi ya kupata taarifa hii ni kupitia internet ingawa kuwauliza ndugu na marafiki wengine inaweza kusaidia pia.



2. Bidhaa Za Kampuni
Kampuni bora ya mtandao ni ile ambayo bidhaa zake zinalenga kutatua matatizo ya wateja katika jamii unayoishi na zimethibika kufaulu katika kufanya hivyo. Bidhaa ambazo zitatangazwa halafu zikashindwa kukidhi mahitaji ya wateja zitakuwa na muda mfupi sana wa mauzo kabla ya wateja kugundua kuwa haziwafai. Bidhaa zitakazokidhi haja ya wateja zitakurahisishia kazi wewe muuzaji kwani baadaye zitajiuza zenyewe. Bidhaa hizo pamoja na kutatua matatizo ya wateja ziwe na bei ambazo wateja wengi wataweza kuzimudu kwani pamoja na ubora wake bidhaa ambayo bei yake itakuwa juu mno itauzika kwa wateja wachache sana wenye uwezo. Kumbuka kuwa wewe kama mwuzaji utanufaika zaidi pale unapouza bidhaa kwa wingi zaidi.


3. Mpango Mzuri Wa Ulipaji (Compensation Plan)

Mpango mzuri wa ulipaji na ambao ni rahisi kuuelewa ndio utakaokupa wewe pesa. Kama kampuni haina mpango mzuri wa ulipaji kamwe hutapata pesa ya kutosha na kama mpango wao si rahisi kueleweka utakosa pesa nyingi kwa sababu ya kutojua namna ya kuitumia kampuni yako vizuri.

Kwa vile ulijiunga na kampuni ya mtandao ili upate pesa ya kuboresha maisha yako, kitu cha kwanza cha kutazama ni mpango wao wa ulipaji na kuusoma au kuupitia kwa makini. Hili ndilo kosa ambalo watu wengi hulifanya, kujiunga na kampuni na kuanza kuchakarika bila kuujua kwa undani mpango wa ulipaji wa kampuni yake.

Unaweza share makala hii kwa watu wengi zaidi ili nao wajifunze.

Kwa ushauri khs biashara na jinsi ya kuanza biashara ya Mtandao wasiliana nami kwa:
0767925000
0622925000(whatsapp).