Credit: Masha Products
WhatsApp: 0622925000
Endapo wewe unahisi mwili wako ni mdogo yaani ni mwembamba sana basi tunakushauri uweze kututafuta WhatsApp 0622925000 kisha tueleze changamoto wako tunakushauri nini cha kufanya.
Dawa tunayotoa kwa ni ya unga, lengo lake huwa ni kwenda kuuboresha mwili wako pamoja na kurudisha hamu ya chakula na hivyo kuwa rahisi kwako kuongezeka uzito.
Gharama zetu ni Tsh 37,000 kwa dozi hii ambayo utatumia kwa kunywa kijiko kimoja cha chai kutwa mara mbili unachanganyia kwenye uji mwepesi.
Tutakupatia pia formula ya kujitengenezea juisi ya protein booster.
Hivi vyote ni msaada kwako ili ufikie lengo lako mapema.
Pia tunauza unga wa Msamitu na Mlonge vyote kwa pamoja Tsh 45,000 ambavyo ni msaada mkubwa mno kwa wanaume ambao wana changamoto ya heshima ya ndoa, hizi hutibu hata kama uliathirika na punyeto kwa muda mwingi.
Friday, 29 July 2016
MWILI WAKO NI MDOGO UNATAKA UONGEZEKE?
Monday, 25 July 2016
MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI - 2
Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia uwepo wa hii somo hili ikiwa leo tunaendelea sehemu ya pili. Mada yetu inasomeka hapo juu linawatokea Zaidi wanawake pasipo wao kutambua tatizo karibu asilimia 30%-45% ya wanawake wote wana matatizo haya huwa wanafanya tu tendo la ndoa kuwaridhisha waume zao na wao kutokufurahia tendo hili la kipekee.
~tatizo hili hutokana na sababu tofauti mfano uwiano mbaya wa homoni nk
~Mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na mambo makuu mawili ambayo ni matatizo ya kimwili na matatizo ya kisaikolojia kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya somo hili.
UTAJIGUNDUAJE KAMA UNA TATIHili O HILI?
Hili tulilisema sehemu iliyopita, mojawapo ni kusikia maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa, kingine ni kwamba una uwezo wa kufanya tendo mara moja tu huhitaji tena maana mzunguko wa kwanza wenyewe hata haukufika mwisho, tutakuja kuona mbeleni kabisa madhara ya hali hii kwani hatari ni kubwa kuliko unavyofikiria wewe mpenzi msomaji wa makala hii.
JINSI YA KUJIKINGA NA MATIBABU YAKE
Matibabu yake Hospitali ni magumu kwani hakuna dawa maalumu na Zaidi hufanyika kupitia vipimo vya uchunguzi, historia ya mhusika pamoja na Dalili za magonjwa mbalimbali, pamoja na hayo tatizo hili unaweza kulidhibiti kwa kufanya yafuatayo
-EPUKA KUVUTA SIGARA NA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI
-ZINGATIA ULAJI ULIO SAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI
-ONDOA MAWAZO NA HUZUNI
-BADILISHA MFUMO WA MAISHA YAKO
-ONGEZA UPENDO KATIKA MAHUSIANO YAKO
-WEKA MAZINGIRA MAZURI NA MUDA WA KUFANYA TENDO LA NDOA
-BADILISHA ENEO LA KUFANYIA MAPENZI, SIYO KILA SIKU KITANDANI TU.
Kaa tayari kwa sehemu ya tatu ya somo hili ambapo tutajifunza MWANAUME UFANYE NINI KAMA MKEO/MPENZI WAKO HAFIKI KILELENI.
MASHA MASANJA
Whatsapp 0622925000
TAFADHALI USISAHAU KUSHARE, KU-COMENT, KU-LIKE NA KUWAALIKA WENZAKO KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK "Mimea Yenye Ufumbuzi Wa Matatizo Yako" KWANI KUNA MASOMO KIBAO YAPO PALE KWA AJILI YA AFYA YAKO.
Saturday, 23 July 2016
TATIZO LA MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA - SEHEMU YA 1
VISABABISHI VYA MWANAMKE KUTOFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA
Kufika kileleni ni nini?
Ni kiwango cha juu kabisa cha utamu, hisia, raha, msisimko wakati wa tendo la ndoa wakati ambapo misuli ya uke au uume hukaza.
Kwa mwanaume huambatana na kutoa manii (ejaculation).
Wengine wakifika kileleni hupiga kelele sana, wengine huongea maneno ovyo ovyo hata matusi, wengine huzimia kabisa, wengine huwakwida wapenzi wao kama vile kibaka, wengine hutulia kimya na kupitiliza usingizi na wengine ukiwauliza wanasema mahali walikuwa ni kama vile walikuwa hewani, wengine kama vile walikuwa wananamwona Bwana (Yesu) n.k ilimradi tu ni raha na utamu. Na ni kweli Mungu alitupa zawadi ya ajabu na hii ni kujulisha kwamba Mungu alituumba tena kwa namna ya ajabu. Pia wengine huita kufikia mshindo, wengine huita coming, wapo ambao kwa tendo moja la ndoa huweza kufika kileleni zaidi ya mara moja.
JE, MWANAMKE NA MWANAUME HUFIKA KILELENI KWA PAMOJA?
Kwa wanaume kufika kileleni ni suala ambalo ni automatic, halina mjadala, kitu cha msingi kwake ni kujitahidi asifike mapema kileleni ili amfikishe mke wake pale anatakiwa kufikishwa, kwani mara nyingi mwanaume akifika kileleni hupoteza uwezo wa kuendelea na tendo.
Katika nchi zilizoendelea kama USA na Canada utafiti mwingi unaonesha kwamba asilimia 15 % ya wanawake hufika kileleni mara zote.
Asilimia 48 % ya wanawake mara nyingi hufika kileleni.
Asilimia 19 % ya wanawake ni kawaida kufika kileleni lakini si mara nyingi
Asilimia 11 % ya wanawake ni nadra sana kufika kileleni na
Asilimia 7% ya wanawake hawajawahi kufika kileleni na hawajui ni kitu gani.
Hapa ni wanawake kutoka nchi zilizoendelea ambako elimu kuhusu mapenzi ni kubwa sana.
je, kwetu nchi zilizogoma kuendelea hali itakuwaje?
Ukizingatia wanaume wengi bado hawajajua nini wanawake wanahitaji ili kufikishwa kileleni?
Pia kuna baadhi ya wanawake ambao hata wasipofika kileleni hawana shida wanaridhika tu bora maisha yanaenda.
Nini Kitu muhimu kuhusu mwanamke kufika kileleni?
Wanawake wanaweza kuendelea kupata utamu hata baada ya kufika kileleni hivyo ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anabaki ndani ya uke hadi anahitimisha tendo zima (conclusion) angalau kwa dakika 10 au 15 ndo ukimbie kuoga au kupiga usingizi siyo kumwacha kiumbe wa watu kwenye mataa akiugulia kwa kumuondolea utamu na raha.
Tendo la ndoa huwa ni la kuridhisha sana hasa pale mume anapomfahamu vizuri mwanamke na kile anahitaji kwa kumfanyia utundu wote wa kuchokonoa sehemu zote ambazo zinaweza kumhakikishia kwamba atafika kileleni.
Lakini pia mwanamke ana sehemu kubwa sana ya yeye kujihakikishia anafika kileleni si mwanaume tu ni suala la wote.
Je sababu kubwa za mwanamke kufika kileleni ni nini?
-Kukeketwa (Female Genital Mutilation).
Kukeketwa ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake.
Katika Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya.
Ingawa wanawake waliokeketwa huweza kurudia hali ya kuweza kufika kileleni, walio wengi huathiriwa sana na hiki kitendo na kuwasababishia kushindwa kufika kieleleni.
-Dini, jadi na utamaduni:
Kuna baadhi ya mitazamo na malezi ya dini, jadi au tamaduni huwapa wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na maana kuhusiana na tendo la ndoa.
Katika dini, jadi, na tamaduni nyingi ukiacha jando na unyago, elimu ya mwanamke kuhusu mwili na uzazi havifundishwi wala kutamkwa matokeo yake wanawake wengi hawaijui miili yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa kiume anamuoa binti hajui chochote kuhusu mwili wa huyo mwanamke na mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu mwili wake mwenyewe, akiguswa chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya mtoto, hapo utategemea atafikishwa kileleni kweli?
-Kisaikolojia.
Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.
Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.)
Hofu labda ya kuachwa, mashaka, kutojiamini, kukasirika, donge moyoni, kisirani au mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke kutofika kileleni.
-Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na kupata hisia halisi (sensations).
Kuwa na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa
Mawazo hasi (Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchovu.
-Kibailojia
Kama vile kuwa na mfumo ovyo wa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya viungo vya uzazi pia huchangia.
Anaweza kuwa na uvimbe au kisukari pia huchangia. Pia hitilafu za viungo baada ya kufanyiwa upasuaji hasa sehemu ya uke.
-Umri (Menopause)
Kuna wakati mwanamke kuanzia miaka 45 – 55 hupata mabadiliko ya upungufu wa homoni na huo upungufu husababisha sehemu ya uke kuwa kavu wakati wa tendo la ndoa.
Kuwa na uke mkavu huchangia katika ufanisi wa tendo la ndoa kuwa mdogo na hatimaye kushindwa kufika kileleni
Si kweli kwamba mwanamke akizeeka uwezo wa tendo la ndoa unakuwa mdogo, muhimu ni kutumia vilainisho kama gel au KY jelly na libeneke linaendelea kama kawaida.
-Kutumia madawa (Medicaments).
kama unatumia dawa za kuzuia msongo wa mawazo pia huchangia ile hamu ya tendo la ndoa (libido) na matokeo yake kukosa kufika kileleni.
Pia kuna dawa za uzazi wa mpango hupunguza hamu ya tendo la ndoa hasa zile ambazo huingizwa mwilini (sindano)
Pia dawa za kupunguza pressure hupunguza uwezekano wa kufika kileleni.
-Pombe, madawa ya kulevya na sigara
Alkoholi na madawa ya kulevya hupunguza sana hamu ya tendo la ndoa.
Huathiri mfumo wa Fahamu unaohusika na mzunguko wa hisia za mapenzi kati ya ubongo na uke.
Kama inavyoathiri (alkoholi) mwanaume kudindisha vilevile huathiri mwanamke kufika kileleni.
-Mwonekano, urembo na umaridadi:
Kwa mwanamke jinsi anavyoonekana na jinsi mwanaume anavyoonekana kuna sehemu katika hisia za mapenzi (emotions na feelings).
Kama yeye mwenyewe anajijua kwamba hayupo vizuri kimwonekano (urembo, usafi, harufu) na pia kama mwanaume hayupo sawasawa basi anakuwa ameathirika sana kiasi ambacho hawezi kufika kileleni.
Pia wanawake wana uwezo mkubwa kunusa harufu kuliko mwanaume hivyo harufu yoyote mbaya kwake huwezi kumpeleka nje kabisa ya njia ya kwenda kileleni.
-Mazingira
Kama eneo au chumba mlichopo hakina usalama kama vile anahisi mtu anachungulia au anaweza kuingia, kwa mwanamke hiyo ni ishu kwani hawezi kufika kileleni kwa sababu ya usalama
JE, ZIPO NJIA ZA KUTATUA TATIZO LA KUTOFIKA KILELENI KWA MWANAMKE?
-Kujiruhusu mwenyewe kupenda tendo la ndoa na zaidi kupenda kufika kileleni kwa hamu kubwa.
-Kuwa responsible kwa mambo yote yanayohusu ufanisi wa tendo la ndoa.
-Kujipa elimu na maarifa kuhusu elimu ya mapenzi kwa mwanaume na mwanamke, viungo vinavyohusika na kila kitu kinachoweza kukupa tofauti katika ufanisi na uimarishaji wa tendo la ndoa kama unavyosoma hapa sasa hivi.
-Kuwa na mawasiliano wakati wa tendo la ndoa hasa kubusiana na maeneo yote ambayo unasisimka pale ukiguswa au kuchezewa.
-Kufanyia kazi kila tatizo lolote la kisaikolojia na kupata solution kabla ya tendo la ndoa.
Kwa leo tuishie hapa, jiandae kwa sehemu ya pili ya somo hili.
MASHA MASANJA
Whatsapp: 0622925000
Saturday, 16 July 2016
SIKU YA KUSHIKA MIMBA MZUNGUKO MFUPI - 2
Mungu ndiye muumba watu wote na viumbe vyote juu na chini ya jua, hilo halina pingamizi wala ubishi na lazima tumshukuru Mungu kwa hilo, ila alitoa amri ya ndoa kwamba ZAENI MKAONGEZEKE kwa hiyo kila mtu anayependa kutimiza amri hii yafaa awe na maarifa.
Kwa wale wasiojua namna ya kuhesabu mizunguko yao basi ni muhimu kurudi katika maada zilizopita na kisha kujifunza namna ya kuhesabu mzunguko wako. Tambua ya kwamba mzunguko wa bleed (hedhi) ni tofauti sana na siku za bleed (hedhi).
VITU VYA KUJUA
1. Siku za bleed (hedhi) ni kuanzia na siku ya kwanza unapopata bleed hadi siku ile unamaliza bleed.
2. Wakati mzunguko wa bleed huanza siku umepata bleed mpaka siku moja kabla hujapata bleed nyingine.
Mfano umepata bleed tarehe 1 mwezi wa saba na bleed hiyo ikaisha tarehe 05 basi siku za bleed ni 5 na zimeanza tarehe moja na zikaisha tarehe 5.
Kama bleed nyingine umeipata tarehe 29 mwezi wa 7, basi mzunguko wako wa bleed ya mwezi wa saba umeanza tarehe 01 mwezi wa saba na ukaisha tarehe 28 mwezi wa saba. Mzunguko huo ni wa siku 28. Mzunguko wa mwezi wa 8 Umeanza tarehe 29 mwezi wa 7.
Ukiwa na mzunguko mfupi usiogope kwa kuwa bado unayo nafasi kubwa ya kupata mtoto na watu wengi tu wapo wana watoto.
Lazima ujue mzunguko wako kwanza ni wa siku ngapi. Mfano kama umekuwa na mzunguko wa siku 21 kwa muda wa miezi mitatu mfululizo na mfano umepata bleed tarehe 10 mwezi wa saba basi siku yako ya uzazi haiwezi kuwa siku ya 14 tangu kupata bleed. Bali ni siku ya 7 tangu umepata bleed.
HEBU ZAMA NDANI HAPA UJIFUNZE
Mzunguko wa siku 21 siku ya uzazi ni siku ya (7) tangu upate bleed. Kwa hiyo kama utapata bleed siku 3 basi siku ya tano unatakiwa uanze tendo la ndoa. Mfano mzuri ni kama ufuatao. >>>Marry ameingia bleed leo tarehe 16 mwezi wa 7 na mzunguko wake kila mwezi unamchukua siku 21. Huyu Marry anachukua siku 3 za bleed. Basi siku zake atahesabu hivi tarehe 16 ni siku ya kwanza yaani leo tarehe16 ni siku ya kwanza ya bleed, kesho tarehe 17 ni siku ya pili ya bleed, kesho kutwa tarehe 18 ni siku ya tatu ya bleed, tarehe 19 ni siku ya nne bleed imeisha, tarehe 20 siku ya tano bleed imeisha - anza hapa kukutana na mwenzako, tarehe 21 ni siku ya sita endelea na tendo na tarehe 22 siku ya saba endelea na tendo yai linatoka. Unashauriwa kuanza mapema ili kuongeza nafasi ya mbegu kulikuta yai.
MZUNGUKO WA SIKU 22,23,24,25 na 26
Mzunguko wa siku 22 yai linatoka siku ya 8 wewe anza tendo siku ya 6, 7 na 8
Mzunguko wa siku 23 yai linatoka siku ya 9 wewe anza tendo siku ya 7
Mzunguko wa siku 24 yai linatoka siku ya 10 wewe anza tendo siku ya 8
Mzunguko wa siku 25 yai linatoka siku ya 11 wewe anza tendo siku ya 9
Mzunguko wa siku 26 yai linatoka siku ya 12 wewe anza tendo siku ya 10
Kumbuka kuanza siku moja au mbili kabla ya siku ya yai kutoka pia unaweza ongeza siku 1 au mbili baada ya siku yenyewe hii ni kwa sababu mizunguko huwa inabadilika badilika kutokana na sababu mbalimbali kama ugonjwa na dawa nzitonzito mshituko kama wa kufiwa, kubadilika kwa hali ya hewa na pia mabadiliko ya mwili kama kunenepa.
Kumbuka kama umekaa muda mrefu hujapata mtoto ni lazima ufike hospitalini na kupima na kupata majibu sahihi. Ni muhimu pia ukawa uko karibu na mwenzako, una afya nzuri na mko vizuri kiuhusiano.
UMUHIMU WA CHAKULA BORA
Ni muhimu ule chakula bora na sio bora chakula. Imethibitika ya kwamba asilimia zaidi ya 50 ya matatizo ya hedhi hutokana na kutokula vizuri. Ulaji wa chips, soda, pombe kupindukia, kula wanga mwingi na sukari ni hatari kwa maisha ya ndoa. Unatakiwa kula chakula halisi (Real Food) chakula fresh na chakula cha asili. Vyakula hatari ni pamoja na vyakula vya paketi na makopo na kuku wa kisasa (chicken)
TUNAKUSAIDIAJE?
1.TUNATOA ELIMU YA AFYA KATIKA MAHUSIANO. Endelea kufuatilia mada zetu hapa ili kujifunza mengi zaidi, SHARE NA MARAFIKI ZAKO na pia Elimisha wengine.
2. PEDI ZA NEPLILY – Tumia pedi za neplily pads mara kwa mara. Pedi za Neplily ndio pedi bora kabisa kwa sasa kwa akinadada na akinamama. Zinaondoa miwasho, harufu mbaya UTI na fangasi za ukeni na miguuni. Zinarekebisha uchachu uliozidi ukeni na pia zinarekebisha hedhi zilizovurugika. Zipo MWANZA, SHINYANGA, BUKOBA, DODOMA, IRINGA, BABATI NA DAR
3. KUKOKOTOA SIKU YAKO YA UZAZI – Wasiliana nasi kwa meseji au whatsapp tu ukiwa umeshaandika siku zako za bleed za miezi minne 0622925000
KUOTA NYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA(BAWASIRI) -2
Mmoja wa wasomaji wa gazeti hili aliyejitambulisha kwa jina moja la Michael anauliza: “Katika sehemu zangu za haja kubwa, kuna vivimbe kama vitatu na ninapata taabu kukaa. Nimetumia dawa aina ya Anusol lakini bado sijapata nafuu, je naweza kutibiwa kwa njia gani za kisasa?” Msomaji mwingine nae anauliza: “Je dawa ya ugonjwa wa Bawasiri ni ipi hasa?”
Msomaji wetu mwingine pia anaeleza kuwa amesumbuliwa na maradhi ya Bawasiri kwa zaidi ya miaka kumi sasa na angependa kujua kama ugonjwa huu unatibika. Nae anauliza: “Je nitapata tiba ya ugonjwa huu?” Msomaji mwingine anamuelezea mchumba wake ana kinyama cha Bawasiri kimetoka katika njia ya haja kubwa na anauliza: “Je akienda hospitalini watakikata au atapewa dawa tu na kinyama kitatoka?”
Kutokana na maswali hayo na mengine mengi ambayo sikuyaandika hapa, nimeona kuwa ipo haja kwa siku ya leo tuangalie kwa kina jinsi maradhi haya yanavyotibiwa hospitalini kwa njia ya tiba zenye ushahidi wa kisayansi.
Kwanza kabisa ni vizuri kuelewa kuwa, kuna maradhi ya aina mbalimbali yanayotokea katika njia ya haja kubwa ambayo yanaweza kuwa na dalili zinazofanana na zile za maradhi ya bawasiri. Kwa sababu hiyo, ni vizuri kupata uchunguzi wa kitabibu kabla ya kuamua kuwa unaugua maradhi ya bawasiri.
Uchunguzi na vipimo
Kabla ya matibabu yoyote, daktari mwenye ujuzi wa tiba, atachunguza kwa kuangalia sehemu ya njia ya haja kubwa na kuona kwa macho hali halisi ilivyo. Baada ya hapo daktari anaweza kufanya kipimo kwa kutumia kidole cha shahada. Kidole hiki kikiwa ndani ya mpira wa kuvaa mikononi, kinaweza kulainishwa kwa vilainishi salama na kuingizwa katika njia ya puru ili kubaini hali ya uvimbe.
Daktari pia anaweza kutumia kipimo cha kutazama moja kwa moja katika njia ya haja kubwa kijulikanacho kwa jina la Proctoscopy au kipimo cha kutazama ndani ya utumbo mpana, Sigmoidoscope. Kipimo cha maabara cha kubaini damu iliyofichika; faecal occult blood test, nacho kinaweza kufanyika pale bawasiri daraja la kwanza inapokuwa ndani na inapokuwa vigumu kuibaini kwa kipimo cha kidole au proktoskopi.
Matibabu
Matibabu ya bawasiri kimsingi hutegemea dalili, hali na hatua ya ugonjwa. Kwa kawaida tiba ya awali ni kurekebisha mfumo wa maisha na mtindo wa kula. Mgonjwa hushauriwa kunywa maji mengi na kula vyakula vitakavyolainisha kinyesi kila siku. Vyakula hivyo ni kama vile matunda na mbogamboga kwa wingi, vyakula asili visivyo vya kukoboa, aepuke chumvi nyingi na pombe.
Mara nyingi mgonjwa hutibiwa kwa njia za kawaida zisizohusisha tiba kwa njia ya upasuaji. Mgonjwa mwenye kinyama au kivimbe kinachojitokeza nje, ataelekezwa jinsi ya kukalisha eneo la haja kubwa katika maji ya vuguvugu kwa muda wa dakika 15. Atatakiwa kufanya hivyo mara nyingi kadiri iwezekanavyo hasa kila baada ya kujisaidia.
Mgonjwa pia anaweza kupewa dawa za kupaka kwenye uvimbe ulioko katika njia ya haja kubwa au vidonge vya kuingiza ndani ya tundu la njia ya haja kubwa. Tiba hizi zitasaidia kupunguza uvimbe na maumivu anayoyapata mgonjwa wa bawasiri hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Kama maumivu yatazidi, tiba rahisi iitwayo ‘Rubber band ligation’ inaweza kufanyika kwa bawasiri iliyoko ndani ya puru, yaani pale mishipa inapokuwa haijajitokeza nje. Bawasiri daraja la kwanza na la pili. Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo lililoathirika. Tiba nyingine ni ile ya kuunguza na kufunga uvimbe wa kinyama kwa kifaa maalumu (laser therapy).
Kama uvimbe wa mishipa ya vena ni mkubwa sana na unajitokeza sana nje ya puru (bawasiri daraja la 3 na 4), upasuaji unaweza kufanyika na hapa kinyama hukatwa na kuondolewa, kisha damu inayotoka hudhibitiwa kitaalamu. Tiba hii kitaalamu hujulikana kwa jina la haemorrhoidectomy.
Katika hospitali kubwa, aina nyingine ya upasuaji wa kisasa zaidi inaweza kufanyika pia. Tiba hii kwa jina la kitaalamu hujulikana kama Doppler-guided Haemorrhoidal Artery Ligation Operation (HALO) na wengine hupendelea kuiita Transanal Hemorrhoidal Dearterialization-Hemorrhoidectomy (THD).
Tiba hii ya upasuaji hufanyika bila kukata kinyama na bila kutumia dawa ya usingizi ingawa ganzi inatumika. Ni tiba ambayo haisababishi maumivu na mgonjwa anaweza kuendelea na shughuli zake baada ya saa 48 tokea kipindi cha kufanyiwa upasuaji.
Katika tiba hii, mishipa yote inayojitokeza nje, haikatwi bali inarudishwa ndani ya puru na kushonwa kwa nyuzi zinazoyeyuka zenyewe ili ijishikize kwenye misuli ya ndani ya haja kubwa na mishipa yote inayopeleka damu katika kinyama kinachovimba, hufungwa.
Lengo la kuifunga ni ili kuizuia isipeleke damu nyingi kwenye uvimbe. Baada ya hapo, sehemu hiyo hufunikwa kwa bendeji inayoyeyuka yenyewe baada ya kipindi fulani.
Dk Sushil Maslekar, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Njia ya Haja Kubwa katika Hospitali ya Spire Leeds nchini Uingereza, anasema kuwa tiba hii ni nzuri, haina madhara na inaondosha dalili zote za bawasiri kwa ufanisi mkubwa.
Utafiti wa miaka 10 wa Pravin J. Gupta na Surekha Kalaskar uliochapishwa mwaka 2008 katika jarida la sayansi za tiba liitwalo ‘Annals of Surgical Innovovation and Research’ toleo la 2(5), unabainisha kuwa upasuaji na kushona ngozi ya tundu la haja kubwa katika maeneo matatu ambayo kwa kawaida hutokeza bawasiri, unatoa matokeo mazuri zaidi ya uponaji wa bawasiri.
Pamoja na hayo yote, katika matibabu ya Bawasiri ni muhimu kukumbuka kuwa tiba hizi zinaponyesha lakini tatizo linaweza kujitokeza tena kama vyanzo vyake havikudhibitiwa. Ili kupona kabisa ni lazima mgonjwa arekebishe mfumo wake wa maisha na mtindo wa lishe.
Wednesday, 13 July 2016
SODA TUNAZIPENDA LAKINI .......
Inawezekana una bahati sana kuiona hii makala na itakujenga sana kiafya...tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anapokunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa mwaka.
Japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambapo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo. Biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
Yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.
1. Ugonjwa wa kisukari; kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi kushusha sukari. Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.
2. Unene na kitambi; utafiti ulofanywa na chuo kikuu cha Harvard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda ndugu yangu
3. Upungufu wa madini muhimu mwilini; soda ina kemikali inayoitwa Phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya Calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kwenye mwili wa binadamu.
4. Ugonjwa wa kansa; soda ina kemikali inayoitwa Caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.
5. Huongeza sumu mwilini; soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya ya mtumiaji.
Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha na kuua figo.
6. Hubadilisha rangi ya meno; kila mtu anataka kuwa na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi.hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.
7. Addiction; soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.Hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.
Sababu hii ndiyo inayotusumbua watu wengi na hata tunapoona makala zinazotuasa kuacha soda wala hatuelewi.
8. Huongeza kasi ya uzee; sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yaani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama ana miaka 35.
9. Hupunguza sana maji mwilini ; soda ina kiwango kikubwa cha madini ya Sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.
Mwisho; ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice ya matunda ya kutengeneza mwenyewe ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.
Share Makala hii kwa watu wengi zaidi ili tuwaokoe.
Sunday, 10 July 2016
HATUA 5 ZA KUPATA MTOTO WA KIUME
FAHAMU KUHUSU TATIZO SUGU LA CHUNUSI
hivi ni vipele vinavyotokea usoni, kifuani na mgongoni sababu ya kubadilika kwa mfumo wa kutengeneza mafuta wa ngozi.
chanzo ni nini?
hii husababishwa na kuongezeka hormone za uzazi aina ya testosterone kwa jinsia zote hasa hasa kipindi cha kubalehe na kuvunja ungo kwa jinsia zote.
matibabu.
matibabu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo....matibabu kwa chakula, matibabu ya kimwili na matibabu ya dawa za hospitali.
matibabu ya chakula..
- ondoa chumvi kwenye chakula chako au kula chumvi kidogo sana.
- epuka ulaji wa sukari na vyakula vyote vya kukaanga kama chips, maandazi na chapati.
- pendelea kula vyakula vya asili kama wali, ugali, mchicha, maharage, njegere vikiwa vimeungwa mafuta kidogo sana pia kula kwa wingi karoti mbichi kwa sababu zina vitamin A ambayo ni nzuri sana kwa ngozi
- kunywa maji mengi ili kuondoa sumu zote mwilini na kulainisha ngozi.
matibabu ya kimwili.
- acha ngozi yako ipate jua la asubuhi na jioni kila siku.
- weka sura yako kwenye mvuke wa maji ya moto kila siku.
- shiriki mazoezi ya aina yeyote hata kama ni kuruka kamba tu angalau utokwe jasho kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.
- kuna dawa zinasaidia kuondoa chunusi i.e antibiotiki kama doxcycline, vidonge vya vitamini A na vidonge vya hormone kwa wanawake mfano oetrogen, persol tube na kadhalika.
mwisho:
watu wengi hawaponi chunusi kwa sababu ya kupenda kutumia njia moja tu ya matibabu {dawa}, ni vizuri kuchanganya njia zote hapo juu kwa matokeo mazuri na inaposhindikana ni vizuri kumuona daktari bingwa wa ngozi kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Uvimbe sehemu ya haja kubwa - bawasiri/bawasili (HAEMORRHOIDS)
- Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
- Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
- Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
- Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
- Tatizo sugu la kuharisha
- Kupata kinyesi kigumu
- Ujauzito
- Uzito kupita kiasi (obesity)
- Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
- Kwa ujumla mambo yanayoongeza shinikizo katika tumbo.
- Umri mkubwa
- Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
- Maumivu au usumbufu
- Kinyesi kuvuja
- Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
- Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
- Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
- Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
- Strangulated hemorrhoids
- Digital rectal examination
- Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
- Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
- Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
- Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
- Coagulation (infrared, laser and bipolar)
- Hemorrhoidectomy
- Stapled hemorrhoidopexy
- High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
- Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
- Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
Njia sahihi ya kupunguza Kitambi na Unene
MAUMIVU MAKALI YA MGONGO
(Mgongo) |
(Maumivu yanayosambaa) |
- Maumivu yasiyohama (yapo katika eneo la mgongo husika haijalishi unafanya nini - localized pain). Mara nyingi maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli/mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa eneo la mgongoni. Au, ni yale yanayotokana na mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo hivyo kusababisha kuchanika kwa misuli ya ndani ya mgongo na kusababisha maumivu!!
- Maumivu yanayosambaaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili wako mbali na mgongo kama vile miguu. Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo wako kwa kupigwa/kuanguka. Mfano: shida ipo mgongoni ila unahisi ganzi kwenye miguu au miguu kuwaka moto).
- Moja ya visababishi vikuu vya maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama ni kichocheo cha kupata maumivu ya mgongo.
- Mkao: nyumbani, kazini, shuleni, n.k wakati unafanya shughuli zako za kila siku, una nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza hatari ya kupata maumivu ya mgongo
- Ubebaji wa mizigo mizito (kufikia kilo 5 au zaidi) usiozingatia afya ya mgongo.
- Kulalia godoro laini na lililobonyea/linalobonyea katikati
wakati wa kulaa. Hii husababisha misuli ya mgongo kuvutika kupita kiasi wakati
umelala na kupelekea kuchanika hivyo kuishia
(Godoro la kubonyea) - Kujeruhi(wa) mgongo wako kunakotokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe (kansa) katika uti wa mgongo.
- Ujauzito/uzito wa kupita kiasi (kitambi): wengi wanashtuka wanaposikia kuwa uzito (kitambi) husababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimam. Kuelemewa kwa misuli/mfupa hii husababisha mabadliko ya mwili katika kutafuta namna ya kufidia hali hiyo… mwisho ni maumivu!!!
- Msongo wa mawazo
(stress): msongo wa mawazo humfanya mtu kukaa katika mkao mbaya akiwaza na
kuwazua hivyo kuishia katika kupata maumivu ya mgongo
- Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo na misuli ya pembeni mwa mifupa hiyo na kusababisha maumivu katika eneo husika.
- Kuvunjika au kuhama
kwa mifupa ya mgongo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu
mbali mbali ikiwemo ajali.
(Msongo wa mawazo) - Umri wa uzeeni: kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabdiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa-na-misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.[Wanawake huathiriwa mapema katika uzee wao kuliko wanaume kutokana na mfumo wa vichocheo (homoni) vya miili yao kupungua kwa haraka zaidi baada ya miaka kati ya 45-55 ya umri wao wa kuishi).
- Wanaume kujihusisha na UPIGAJI PUNYETO wakati wa ujana wao. Vijana wengi ukiwauliza watakwambia wameufanya sana mchezo huu na hadi wengine kufikia kuuhalalisha kuwa ni kawaida kufanya hivyo. Kitendo hiki huhusisha kwa sana uti wa mgongo na ubongo hivyo ni chanzo kimojawapo cha maumivu ya mgongo na hata upungufu wa NGUVU ZA KIUME
- Mumivu ya kwaida hasa yale yanayotokana na mshtuko wa misuli ya mgongo au mkao mbaya huwa yanaisha yenyewe ndani ya siku 4 -14, hivo mgonjwa anashauriwa kutumia dawa za kawaida za kutuliza mamivu.
- Maumivu yanayotokana na kujeruhiwa mgongo ikiwa ni pamoja na ajali/kupigwa/kuangukia mgongo n.k) unashauriwa kufika hospitalini au kituo cha afya kilicho karibu nawe ili upate uchunguzi yakinifu na ushauri/tiba.
- Maumivu yanayoamabatana na kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa, maumivu makali ya miguu, miguu kuwaka moto/ganzi yanahitaji tiba ya haraka na dharura kwa sababu tayari mfumo wa fahamu/neva utakuwa ulishaguswa/athiriwa kwa namna moja au nyingine.
- Mwone daktari wa tiba viungo (PHYSIOTHERAPIST) aliye karibu nawe kwa ushauri kuhusu namna ya:
- Kukaa vizuri ukiwa nyumbani, kazini au shuleni
- Namna ya kubeba mizigo kwa kujali na kuingatia afya ya mgongo wako ili kuepusha kujeruhi misuli ya mgongo wako.
- Mpangilio na uboreshaji wa mazingira ya kazi yako ili kuzuia hatari za kupata maumivu ya kimfumo (misuli-na-mifupa)
- Mazoezi muhimu kwa ajili ya afya ya mgongo wako.
- Tiba ya mazoezi ya viungo (na mgongo kwa ujumla) inayoendana na shida yako husika.
NJIA SALAMA ZA KUPUNGUZA UZITO
Vyakula vya wanga na mafuta hufanya mtu kunenepa, acha au kupunguza kula vyakula hivyo.
Saturday, 9 July 2016
HIVI HAPA VYAKULA 7 VIZURI ZAIDI KWA NGUVU ZA KIUME
Mwanaume mmoja kati ya watatu wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.
Sababu za kukosa nguvu za kiume
- Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
- Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
- Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
1. Blueberry
2. Mtini (Figs)
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
4. Karanga
5. Vitunguu saumu
6. Ndizi
7. Chocolate
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.