Wednesday, 23 December 2015

MADHARA YA KUTUMIA VIDONGE VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME KWA GHAFLA

MADHARA YA KUTUMIA VIDONGE VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME (VIAGRA/VEGA)

Hivi ni vidonge vinavyotumiwa sana na miongoni ya wanaume au vijana wengi kwa lengo la kuongeza uwezo wao wa kufanya mapenzi. Dawa hizi hutumiwa zaidi na wanaume wasioweza kusimamisha uume vizuri(low libido) kwa leo la kumuwezesha kukidhi haja zake au za mwenza wake wa kike. Lakini pia zimekuwa zikitumiwa na vijana wengi kwa lengo la kumkomoa mwanamke au wengine hufanya kwa kuiga kutoka kwa waigizaji video za ngono(pornograph). Madhara ya vidonge hivi ni mengi, leo tutayajua


JINSI VINAVYOFANYA KAZI
Viagra haimfanyi mtu kupata hamu ya ngono bali yenyewe hufanya kazi endapo tu mtu atakuwa na hamu ya kufanya ngono. Hebu tugusie kidogo kuhusu uume unavyoweza kusimama.
Pindi mwanaume anapopata hamu ya kufanya ngono, mishipa ya fahamu iliyoko katika misuli ya uume hutoa chemicals zinazoitwa "nitric oxide" ambayo huamrisha viamshi(enzymes) kuzalisha chemicals nyingine tena zinazoitwa "messenger cyclic guanoside monophosphate". Hali hii huifanya misuli laini ya uume kujiachia na kutanuka ambapo matokeo yake huiruhusu damu kuingia na kujaa vizuri katika mishipa midogomidogo iliyoko katika uume(cappilaries), hapo ndipo uume unakuwa umesimama vizuri.


Hivyo basi, Viagra hufanya kazi ya kusawazisha kiwango cha hii kemikali inayoitwa Cyclic guanosine Monophosphate.


SASA TUONE MADHARA YA VIDONGE HIVYO
Kwa mara ya kwanza dawa hii ilitumika kutibu tatizo la Presha, lakini ilionyesha maajabu pale ilipooneka kuwafanya wagonjwa kuwa na nguvu nyingi za kusimamisha maumbile yao ya uzazi. Baada ya hapo zikazuiliwa kutumika mahospitalini lakini baadae zikafanyiwa uchunguzi na zikaanza rasmi kutumika kwa wanaume wenye matatizo ya kusimamisha. Kipindi hicho watu wenye matatizo ya kusimamisha walikuwa wakipewa dawa hii chini ya uangalizi wa Daktari huku wakipewa ushauri wa kutosha kwamba wataweza kusimamisha na hivyo Saikolojia hiyo ikawakaa na wakasimamisha, lakini baada ya muda fulani, mgonjwa wa tatizo hurudi katika hali yake ya kutosimamisha.


MADHARA
=>Mtu anayetumia vidonge hivi bila usha wa Daktari huku akiwa na matatizo mengine ya Kiafya kama Presha yuko hatarini kupoteza uhai wake.
=>Matumizi makubwa ya dawa hizi hufanya tatizo kuwa kubwa zaidi kwa sababu dawa hizi humfanya mtu kusimamisha kwa muda tu kwani akihitaji kufanya mapenzi siku nyingine inampasa ameze tena. Hali hii ya kuzimeza kila wake inamfanya kuwa dependant(tegemezi) na kumfanya azidi kuongeza dozi zingine na mwiso wa siku hutengeneza sumu mwilini na kuua kabisa nguvu za kiume.
=>Madhara mengine ni kupoteza uwezo wa kusikia(ukiziwi) pamoja na kupoteza uwezo wa kuona.


Kuliko kutumia vidonge hivyo, ni vyema ukatumia vidonge visivyo na madhara ambavyo havina kemikali yoyote. Mimea ya butea superba imeonyesha kiwango kiwango kikubwa cha kutibu kabisa tatizo la upungufu wa uwezo wa kusimamisha. Mmea huu unalimwa nchini Thailand na watafiti wa tiba asili wameamua kuutengeneza mmea huu katika mfumo wa vidonge ili iwe rahisi kupatikana katika nchi zote.
Hata hapa Tanzania vidonge hivi vilivyotengenezwa kwa mmea huu wa Butea Superba vinapatikana kirahisi tu hasa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Tanga na Dar es salaam.

CONTACTS:
0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp

Email: mmasanja86@gmail.com



posted from Bloggeroid

Tuesday, 22 December 2015

WANAUME: CHAKULA NA NGUVU ZA KIUME



Kama tulivyowahi kueleza katika dondoo za afya huko nyuma jinsi ya kuboresha mwenendo wa maisha kiafya ni pamoja na ufanyaji wa tendo la ndoa kwa namna tuliyoieleza.

Na kabla ya kuvitaja hivyo vyakula kwa ufupi tuangalie sababu ya tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa au upungufu wa nguvu za kiume.

SABABU
1.Vyakula hasa vyenye mafuta ya wanyama au mafuta yenye Lehemu(Cholestrols).
Matumizi ya vyakula vye kusindikwa zaidi.
2.Madawa, dawa kama Cimetidine ya vidonda vya tumbo au Adolmet ya shinikizo la damu la kupanda.
3.Miozi kama ya X-ray, Gamma Ray, simu,na vifaa vingine vya Electronic .
4.Magonjwa kama Sonona, Msongo wa mawazo, Kisukari, Kifafa, Ngiri n.k
5.Unene kupita kiasi(Obesity).
6.Kupendelea kuangalia picha za ngono au utupu.
7.Sigara.
8.Pombe.
9.Na nyinginezo.
Hizo ni baadhi ya sababu kwa ujumla wake.

Vyakula vyenye madini ya zinc, folic acid,Omega 3(Mafuta ya samaki), Vitamini B1, B6,B12, E n.k ni katika vyakula vyenye kuongeza hamu ya tendo la ndoa. Pia kuongeza ufanisi wa ufanyaji wa tendo la ndoa(Nguvu).
Baadhi ya vyakula hivyo ni vifuatavyo:
Tangawizi, Kitunguu swaum, Tikiti maji(hasa mbegu zake), Parachichi,Kitunguu maji, Asali, Habat sawda, Tende,Pilipili, Mdalasini, Karanga, Korosho,Pweza, Kiini cha yai, Mkate wa brown,Dark Chocolate, Mbegu za boga, Soya,Karoti, Ndizi mbivu n.k.

Vyakula hivi unaweza kula katika namna ya kuimarisha na kuboresha afya yako,lakini unaweza ukala katika namna ya kuimarisha hamu ya tendo la ndoa(Libido). Kwa leo tutaelezea juisi ya tende na tikiti maji.
Kwa mfano Juisi ya Tende hii ina matokeo ya haraka kama tatizo lako siyo sugu.

JUISI YA TENDE
Chukua tende kiasi kama robo kilo zitoe kokwa ,weka kwenye blenda,tia maziwa fresh kidogo zisage,na utaongeza maziwa kadri uzito wa juisi utakaohitaji na usitie sukari.
Juisi hii unaweza ukaongeza na unga wa habat sawda, unga wa tangawizi na unga wa karanga au soya kiasi kama kijiko cha chai.

Na kama hauna blenda basi kunywa maziwa fresh na tende,na unaweza ukaongeza na karanga mbichi na kipande cha tangawizi au ukatia unga wa tangawizi katika maziwa ya moto pamoja na Habat sawda ya unga na ukaweka asali.
Pia katika juisi ya tende unaweza ukaweka na asali kidogo.

Na unaweza ukatengeneza mchanganyiko wa Asali,Habat sawda,Tangawizi ya unga,Mdalasini ya unga, Kitunguu sawm (Garlic paste) ukawa unatumia kama jam au ukala vijiko viwili asubuhi na jioni huku ukitafunia na karanga au korosho au Brown bread.

JUISI YA TIKITI MAJI.
Andaa juisi ya tikiti maji bila ya kutoa mbegu, weka jikoni kamulia Limao kidogo na ikianza tu kuchemka itoe jikoni,kunywa.

Hivi ni baadhi ya vyakula vinavyopatikana katika mazingira yetu.Tujitahidi kuvitumia ili kuoberesha afya zetu.

Endapo unajua tayari una upungufu wa nguvu za kiume, tambua kuwa tiba yako siyo vyakula bali unatakiwa kupata tiba kwanza kisha ndipo uanze kutumia hivyo vyakula ili usiweze kurudi kwenye tatizo lako kama mwanzo.

Tunayo dawa iliyotengenezwa kutokana na mimea ya Butea Superba inayopatikana katika nchi ya Thailand pekee. Dawa hii ipo katika mfumo wa vidonge na ni vidonge vinne tu kwa dozi moja. Matumizi yake ni kumeza kidonge kimoja tu kwa siku, hivyo dozi inaisha baada ya siku nne pekee.

Upatikanaji wa dawa hii ni rahisi tu kwani unaweza kuipata direct mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Tanga na Dar es salaam. Mikoa mingine tunatuma kupitia Ofisi za mabasi ya mikoani

Mawasiliano
0784925000 
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

Sunday, 20 December 2015

WANAWAKE: JE, UNAJUA PED UNAYOTUMIA INA NINI?




Ndugu zangu huwa nawaambia kila siku kitu cha bei chee, sio chakutumia maana ni ADUI WA AFYA YAKO. Huna haja ya kununua ugonjwa ambao utakugharimu mamilion kwa kuepusha pesa ambayo utaenda kuiepusha hata kwenye vitu ambavyo sio vya KUILINDA AFYA YAKO.
Napenda nikwambie kuwa material yanatumika kutengeneza,pedi hizi za mtaani zinatokana na kuchukua mabaki ya karatasi,plastics na kemikali mbali mbali zikapitishwa kwenye machine (RECYCLING) na hatimaye kupata material ya pedi unazotumia.
Ndugu yangu kundi inayotumika kugundishia pedi hizo kwenye nguo ya ndani ili ikae vizuri imetengenezwa kwa kutumia BENZENE! Nenda google andika madhara ya benzene kwa mwanamke utalia

-Inavuruga mzunguko wa kike

-inaharibu mzunguko wa kike kwa kuleta maumivu,kichefu chefu yani kitaalamu (dysmenorhea)

-Pia inaweza,kusababisha kubleed kwa muda mrefu bila sababu yoyote tena ovyo ovyo (Polymetrohagia)

-Pia inasabisha kukosa kabisa hedhi bila hata sababu ya maana (Amenorhea)


Je inatokeaje?

Endapo ukisha toa pedi, kuna chembe chembe za benzene zinaweza baki na kuingia kwenye sehemu mahusisi za uzazi na kusababisha matatizo yote hayo.

Hili ni janga kila dada ana lalamika mzunguko, ugumba,uvimbe kwnye kizazi watoto wadogo tu, yote haya inategemea jinsi gani mwili wako unaitikia kwenye hii benzene. Km upo sensitive utapata mdhara haraka na km hauko sensitive utachelewa kupata madhara.

Sasa napenda kuwaambia we differ genetically how our body responds to environmentall triggers!

Chukua tahadhari mpendwa kuepusha Afya yako.


PED & PANTLINER ZETU

Ped zetu zimetengenezwa Kwa Technologia ya hali ya juu.ped zetu na Pantliner zinetengenezwa Kwa Anion Chip Technology.Anion ni negative particles ambazo zinatoa oxygen pale zinapogusana na mwili wako. Joto la mwili linapokutana na pedi au pantliner inaachia negative particles ambazo mwisho wa siku inatoa hewa safi ya oxygen.

ANIONS Kwa inapatikana kwenye maporomoko ya Maji, chemichemi ya Maji kwenye misitu, Mvua za acidi, Moshi wa misitu baada ya kuunguzwa n.k.


FAIDA ZA ANION CHIP

1. Ina uwezo wa kuondoa muwasho, bacteria, fungus wa aina yoyote kipindi cha Hedhi

2. Inaondoa harufu mbaya

3. Inarekebisha mzunguko na kuweka homoni sawa.

4. Inatibu Ugumba

5. Inaondoa msongo wa mawazo na uchovu

6. Inarekebisha mfumo wa homoni za mwili

7. Pantliners Pia zinatumika na wanaume wenye prostatic hypertrophy, Bawa siri na kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa

8. Ina uwezo wa kuondoa uvimbe na kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba.

9. Inaimarisha kinga ya mwili na kujikinga na matatizo yote ya uzazi.

10. Inaondoa matatizo yote ya uzazi hasa baada ya kuogelea kwenye mabwawa ya kuogelea.

10. Inatibu UTI.
Kwa ujumla Ped zetu na Pantliner zina uwezo Mkubwa wa kutokomeza matatizo yote yanayowakumba wanawake wakiwa kwenye siku zao, Kama kuumwa kichwa, msongo wa mawazo, kuchoka, kuumwa Tumbo, kuwa na flow kubwa na mengine Mengi

0784925000
0767925000
0622925000 - whatsapp
posted from Bloggeroid

Saturday, 12 December 2015

VYAKULA NA UNENE - SEHEMU YA 5


SEHEMU YA TANO:

LISHE SAHIHI NA JINSI YA KUPANGILIA MLO WAKO



Napenda kusema kwamba ni dhahiri kuwa umekuwa ukitumia kila mbinu uweze kujinasua na uzito mkubwa lakini umekuwa hupati mafanikio yoyote tofauti na kuishia kukata tamaa kabisa. Usikate tamaa kwani nina uhakika umeshindwa kutimiza malengo yako kwa sababu unafikiria kila ushauri wa afya unaoupata unaweza kutimiza malengo yako kumbe sio kweli. Najua umeambiwa kufanya mazoezi, kupunguza kula sana, umekuwa ukiambiwa kuacha kunywa vinywaji vingi vya sukari na vingine vingi vya mfano kama huo lakini umekuwa ukiishia kuongezeka uzito bila hata kupunguza hata kilo moja. Umetumia bidhaa mbalimbali za kupunguza uzito, na umeingia gharama kubwa kwa ajili tu utimize malengo yako, yote hayo ni sahihi ni jinsi gani ulivyo na shauku kubwa ya kuishi na uzito wa kiafya na bila kitambi kabisa.

Mafanikio ya kuishi bila uzito mkubwa na kitambi yapo mikononi mwako rafiki yangu. Kwa sababu ulikuwa hujawahi kusoma na kuelewa ninachoandika basi naomba kuanzia leo anza kufuata hiki ninachotaka kukuambia kupitia kupangilia mlo. Na ili unielewe vizuri kabisa tambua kwamba ushauri wote uliokuwa ukitumia ili kuishi bila uzito mkubwa na kitambi na hukufanikiwa basi ulikuwa na uongo mkubwa ndani yake. Hivyo unatakiwa kuanza kusahau kabisa na kuanza upya safari yako ya kupunguza uzito.

Watu wengi sana nimekuwa nikipokea ujumbe wao wakihitaji japo hata niwaambie wapangilie vyakula gani tangu asubuhi hadi usiku ili waweze kupunguza uzito. Moja ya jibu ambalo wengi nimekuwa nikiwapa ni kurejea kusoma elimu yangu upya kuanzia hatua ya kwanza hadi sasa tulipofika hatua ya sita.

Kama umefuatilia Makala zangu zote basi nina Imani lazima ufikie mafanikio. Ndoto zangu na malengo yangu ni kutaka kuhakikisha kila mtu mwenye kitambi na uzito mkubwa endapo akifuata elimu hii atakuwa shuhuda na daktari katika kizazi chake chote na ukoo wake wote, ndio maana nataka uelewe elimu hii hatua kwa hatua ili uje uwe daktari mzuri wa kitambi na uzito mkubwa katika ukoo wenu na kuondoa fikra potofu kuwa uzito ni moja wapo ya magonjwa ya kurithi na kujisahau kuwa katika familia pia tunarithishana ulaji mbaya wa vyakula na hatimaye kuishia kuwa na uzito mkubwa na kitambi familia nzima kutokana na mwenendo mbaya wa maisha katika familia.

Tangu nianze kufundisha namna gani unaweza kupunguza uzito kiafya,kirahisi kabisa bila gharama yoyote ni kuhakikisha, UNAPUNGUZA VYAKULA VYA WANGA na KULA VYAKULA VYENYE PROTINI YA WASTANI NA VYAKULA VYENYE MAFUTA MAZURI KWA WINGI.

Watu wengi wataguna baada ya kusoma haya kwani sio wewe pekee ambaye umepatwa na hali hiyo kwani wengi hawapendi kufanya uchunguzi na wanapenda kubeba taarifa na kuwa ving’ang’anizi wa kutobadilika.
Miongoni mwa watu walioguna katika aya yangu hapo juu, ndio hao hao ambao hutumia mbinu ya kupunguza uzito kwa kuepuka vinywaji vya sukari na pale pale wanakuwa wanaogopa vyakula vya mafuta vinanenepesha na hatimaye kuishia kupungukiwa viini lishe na kusababisha mwili kutoweza kuendesha shughuli mbalimbali katika kiwango stahiki na hapo ndipo utashangaa mwili wako unavyozidi kunenepa ingawaje unajinyima katika aina fulani ya vyakula. Huku ni kukosa elimu sahihi rafiki! Napenda tu nikumegee kidokezo kuwa unapokula chakula cha wanga gramu moja kitakuja kutumika mwilini mwako na kutoa nishati ya mwili Kalori 4 ambapo unapokula vyakula vya mafuta gramu moja utakuja kupata nishati kalori 9. Unaona rafiki yangu? sayansi hapa ndipo hupotosha fikra za watu! Kwani kwa kawaida sasa ukila vyakula vya mafuta unaweza kusababisha kuhifadhi mafuta! Lakini unapokuja katika swala zima la kuufanya mwili wako kuwa mashine inayounguza mafuta yazingatie haya hapa chini kwani ndio nguzo yako katika zoezi hili unalopenda ufikie malengo kuanzia sasa.

Tafiti zinaonesha kwamba unapokula vyakula vya wanga vina uwezo mkubwa sana wa kupandisha kiwango cha insulin kwenye damu ambayo kazi yake kubwa huwa mbili, Kwanza nataka nikwambie kuwa insulin ni homoni inayotolewa na kongosho ili kuja kuhifadhi sukari iliyozidi katika mfumo wa mafuta na glycogeni. Pili nataka tu tena ujue kuwa insulin inaathiri kupungua kwako uzito inapokuwa katika kiwango kikubwa kwenye damu, kwani inakufanya ujisikie njaa mapema na pia ni homoni inayohifadhi mafuta. Hivyo basi endapo ukihakikisha kiwango cha homoni hii kipo chini muda wote hutaweza kuhifadhi mafuta yoyote tumboni, kiunoni,mgongoni, kifuani,mikononi nk. Njia pekee ya kurekebisha kiwango cha insulin ili kiwe sawa muda wote ni kupunguza kitu kinachosisimua utengenezwaji wake kwa kasi ambapo ni Chakula cha wanga. Hivyo tafiti zimeonesha kwamba watu ambao mlo wao una kiwango kidogo cha wanga huweza kupunguza uzito salama kabisa na bila nguvu zozote.
Lakini sambamba na kupunguza kiwango cha ulaji wa wanga, ili uweze kupunguza uzito zoezi hilo linatakiwa liendane na kuongeza vyakula vya nyuzi sana (Fibers) na vyakula vya protini na mafuta. Endapo ukipunguza wanga katika mlo wako au ukaacha kabisa bila kuongeza kiwango cha mafuta utaishia kupata upungufu wa viini lishe na hatimaye utaongezeka uzito badala ya kupungua. Ndio maana unasoma elimu hii, sitaki ufanye kitu kwa kuambiwa lengo langu nataka utimize malengo yako kwa kusoma na kuelewa na kisha uyaweke katika vitendo utashangaa jinsi gani unavyoshusha uzito wako ndani ya mwezi tu.

Kabla sijagusia mada yangu kiundani Zaidi napenda tu kukuondoa wasiwasi kwani najua umeanza kuwaza sasa, nikiacha kula vyakula vya wanga nitaishi vipi? Ni kweli lazima ujiulize kwa sababu hujawahi kuambiwa elimu sahihi kama hii na inaweza kuwa ni mara yako ya kwanza kusikia, lakini usishangae,Napenda nikupe siri tena katika kupunguza uzito kuna aina kuu mbili ya vyakula vyenye kutoa sukari itokanayo na wanga. Tuna vyakula vyenye kuongeza sukari kwa kiwango kikubwa baada ya kuingia mwilini (High Glycemic Index Foods) na kuna vyakula vyenye kuongeza kiwango kidogo cha sukari baada ya kuingia mwilini (Low Glycemic Index Foods). Mfano wa vyakula vya wanga vyenye kiwango kidogo cha sukari ni viazi vitamu, magimbi,maharage, njegele,matunda mengi, karoti nk kulingana na mazingira ulipo wewe. Pia kuna kundi la kati la aina hii la vyakula ni ngano ambayo haijakobolewa na kundi lenye kutoa sukari nyingi kwenye damu ni ngano nyeupe, popcorn, matunda ni pamoja na tikiti maji,nanasi n.k hivyo vyakula hivi unatakiwa upunguze sana na ndio chanzo kikubwa cha uzito wango kuongezeka kwani inaweza kuwa unakula wanga yenye glycemic index kubwa kila kukicha na ukitegemea kupungua uzito! Najua umeanza kuwaza utakumbukaje na utajuaje kiwango maalumu cha vyakula? Jibu lake ni jepesi sana ndio maana nakushauri utumie mboga za majani kwa wingi na baadhi ya matunda na vyakula vingine vyenye protini na mafuta mazuri kwani ndivyo vyenye kiwango kidogo cha sukari na vyenye kuweza kukufanya mwili wako uache kuhifadhi mafuta na bali uanze kuunguza mafuta.

Basi najua umejifunza kitu, basi kwa sababu unajiuliza sasa utaanzaje safari hii ya kula vyakula sahihi ili uweze kupunguza kitambi hicho na uzito huo, najua kuwa umechoka na uko tayari kuanza safari hii sasa kwani tayari umepata imanivna umefarijika kuwa afya yako sasa inaenda kurudi upya na kuishi maisha ya bila kitambi na uzito mkubwa. Niko tayari kukufanya uyafikie malengo yako kwani dhamira yangu ni kukutimizia ndoto na malengo yako kwa kukupatia elimu sahihi inayozidi kubadili maisha ya watu, sasa ni zamu yako endapo tu ukiwa tayari kuweka katika utekelezaji yote unayosoma katika makala haya. 

HEBU, TUANZE NA MFANO WA VYAKULA VITAKAVYOKUWA MLO WAKO KWA MWEZI HUU UKIWA UNATIMIZA NDOTO ZAKO ZA KUISHI BILA KITAMBI NA UZITO MKUBWA.

VITU VYA KUZINGATIA
1. KULA- Samaki, nyama,mboga za majani aina yote,mayai ya kienyeji na Siagi
2. USILE/PUNGUZA- Vyakula wa Sukari na Wanga ( Wali,mikate,chapati,baga,mandazi na jamii zingine zitokanazo na ngano ,tambi,maharage,viazi vitamu na viazi mviringo)
3. Jitahidi kula pale tu unapokuwa una njaa na sio kwa sababu kuna chakula mbele yako, na hakikisha kila unapokuwa una njaa hakikisha umekula hadi kutosheka chakula sahihi.
4. Tafiti zinaonesha kwamba unapopunguza sukari kwa kupunguza vyakula vya sukari na wanga, Unapunguza kiwango cha insulin kwenye damu kinachofanya kazi ya kuhifadhi nishati katika mfumo wa mafuta na matokeo yake mwili utaanza kuunguza mafuta na kuwa mtu wakutosheka na kushiba haraka na kuondokana na tatizo la ulaji hovyo kuliko kuwa kunasababishwa na kiwango kikubwa cha insulin kwa sababu ya ulaji mbovu.

Baada ya kupata somo kwa ufupi haya basi tusome kwa undani kabisa hapa chini

1. ULAJI WA NYAMA
Kumbuka maada yangu ya aina za mafuta ya protini katika somo langu la sehemu ya tano. Nyama ina protini na pia ina mafuta. Hivyo kama unahitaji kupunguza uzito nakukubalia kabisa katika mlo wako kuweka aina yoyote ya nyama kwani utajipatia aina kuu hizo mbili za viini lishe vikubwa. Kula nyama ya Ng’ombe,mbuzi,kondoo,kuku,wanyama pori,bata nk unaruhusiwa kula aina yoyote ya nyama.
2. SAMAKI
Unaruhusiwa kula samaki wa aina yoyote kwani samaki wana kiwango kingi sana cha mafuta mazuri ambayo huongeza Omega 3 katika mwili wako ambayo kazi kubwa ni kulainisha mishipa na kufanya mzunguko wa damu ufanye kazi katika ufanisi wa hali ya juu kiafya. Kula sangara, sato, samaki wa baharini nk
3. MAYAI
Unatakiwa ujue kuwa mayai ni chanzo kizuri sana cha viini lishe vikuu kama mafuta na protini. Hivyo unaweza kutumia mayai ya kuchemsha au kukaanga na mafuta ya alizeti/olive oil.

4. MBOGA ZA MAJANI ZINAZOSTAWI JUU YA ARDHI
Mboga za majani zina kiwango kingi sana cha nyuzi (fibers) na hivyo zitakufanya muda wote tumbo lako liwe limeshiba na kiwango cha insulin kuwa katika usawa muda wote. Mbali na hivyo utajipatia madini kama manganese, selenium ambayo ni vionjo vinavyosaidia shughuli za mwili zifanyike katika kiwango stahiki na mwili kuweza kuunguza mafuta.
Mfano
-Kabeji
-Spinachi
-sukuma wiki
-Brokoli
-Cauliflower
-Bilinganya
-Uyoga
-Tango
-Vitunguu
-Pilipili
-Asparagus
- Zucchini nk

5. MATUNDA
Usipendelee sana kula matunda kwa sababu matunda, unapokuwa umekula angalau matano kwa siku ni sawa kama umekunywa soda milimeta 500. Hivyo jitahidi kuepuka. Na kama unahitaji kutumia kama juisi hakikisha unatumia blenda ambayo inaitwa (Centrifugal juicer) hii inakuwa na sahani katikati ambacho huzunguka na kupiga kelele. Aina hii ya blenda inakufaa sana kwa wewe unayetaka kupunguza uzito ila hakikisha juisi yako umekunywa ndani ya dakika 15 kwa sababu baada ya dakika hizo vitamin zitakuwa sio hai tena kwa sababu ya mwanga na joto wakati wa kusaga juisi yako. Blenda hii pia huacha nyuzi nyingi sana na hivyo inafaa kwa wewe unayetaka kutimiza malengo yako, Epuka juisi zile cold press juicer ambazo hukamua juisi bila sauti yoyote na inaondoa nyuzi zote itakufanya kuongezeka uzito wako kwa kasi sana maana kutakuwa na sukari nyingi.
Nakushauri glasi moja asubuhi na jioni ya juisi inatosha.
Tumia matunda kama Apple, Parachichi nk

6. Mafuta kwa ajili ya matumizi yako.
Jitahidi utumie mafuta kama Olive oil, alizeti katika kuandaa mlo wako

MFANO NAMNA UNAVYOWEZA KUPANGIA VYAKULA HAPO JUU

Mfano
ASUBUHI UNAPOTAKA KWENDA KAZINI
-Chukua supu yako ya kuku wa kienyeji,kachumbari ya parachichi,tango,kitunguu maji,pilipili hoho. Baada ya nusu saa kunywa maji ya baridi kwa mbali sana. Utajiskia kushiba kuzidi hata yule anayekula vyakula hatari kama chapatti,mandazi,tambi angali bado ana uzito mkubwa

SNACK (KATIKATI YA ASUBUHI NA MCHANA)
Endapo ukijiskia mwenye njaa, Chukua yai lako moja lililochemshwa shushia na maziwa asili ya ng’ombe( Epuka maziwa ya kiwandani namaanisha yaliyohifadhiwa kwenye box). Utajisikia mwenye kushiba na kuridhika na ulicho kula. Mwili wako utakuwa wenye nguvu na utakaa muda mrefu bila njaa kabisa kwani kiwango cha homoni ya insulin kiko chini ya kiwango, kuliko ungelinunua kinywaji chenye sukari kama soda ambacho kinahatarisha maisha yako na uzito wako.

MCHANA
Chukua Mboga kama Brocolli chemsha kwa mvuke kisha kata kata kama kachumbari, unaweza kuchanganya na matunda mengine yoyote kama unayo. Unaweza kuchanganya na mchemsho wa samaki. Kisha kula utajisikia umeshiba kuliko yule angeagiza chakula ambacho ni wali, ndizi, pilau, chips, mtoli n.k, huu ni ulaji wa bila kujali afya yako kwani unakula kama vile hufikirii mstakabali wa afya yako na inaonesha umekata tamaa kwa sababu huwezi kula mlo ambao watu ambao hawana kitambi,uzito mkubwa na kisukari wanatumia na wewe utumie. Jitahidi kuepuka vyakula ambavyo vinaweza kutokutimizia malengo yako

USIKU
Pia unaweza kuwa mbunifu wewe mwenyewe kulingana na radha ya chakula unayoitaka. Unaweza kukaanga yai lako moja kwa mafuta ya olive, changanya na kachumbari ya mboga za majani na matunda yasiyokuwa na chachu kama parachichi na tango usisahau kuweka natural antibiotic pilipili kwa mbali. Kisha shushia na maziwa yako ambayo ni ya asili(Organic whole milk)

NOTE: Wengi mnapotaka kupunguza uzito MCHANA Binafsi huu mfumo una uzuri wake na ubora wake lakini ningekushauri kuwa kama unataka kupunguza uzito nimesema mwanzo HAKIKISHA UNAKULA CHAKULA PALE TU UNAPOKUWA UNAJISKIA NJAA NA TUMBO HALINA KITU NA EPUKA KUJINYIMA KULA MAANA KUNAONGEZA UZITO KWA KASI SANA. Hivyo itapendeza usipofuata saa yako kuwa unakula pale tu familia yako inapoivisha chakula, sivyo! Kula chakula pale tu unapokuwa una njaa hii itapunguza ulaji usio na msingi kwa kisingizio chakula kipo mbele yako.

Napenda kusema asante kwa mnaoendelea kufuatilia maada zangu.


Njia pekee ya kupunguza uzito ni kupata ELIMU SAHIHI YA LISHE.

NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUKUOMBA KUSHARE,POST HII POPOTE PALE UTAKAPO ILI KUWEZA KUWAPASHA HABARI WATU WENGI NA WAUNGANE NASI KATIKA JUKWAA HILI LA ELIMU YA LISHE .

Masha
0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

Friday, 11 December 2015

VYAKULA NA UNENE - SEHEMU YA 4


SEHEMU YA NNE

1. JINSI YA KUTAMBUA UZITO AMBAO SIO MZURI KIAFYA

2. AINA KUU TATU ZA VYAKULA WANGA, PROTINI NA MAFUTA (FATS) KATIKA KUPUNGUZA UZITO NA KIAFYA

Nimekuwa nikipokea maswali yenu mengi sana na najitahidi sana kuyajibu lakini wengine nakuwa nashindwa maana message ni nyingi sana zinanizidi uwezo rafiki zangu wa nguvu kupitia mitandao ya kijamii. Nafurahi sana kuona mnapenda maada zangu na mnafuatilia kwa kina maada hizi ambazo zimeamsha hisia za watu sana kutaka kuondokana na uzito mkubwa.

1. JINSI YA KUTAMBUA UZITO AMBAO NI HATARI KWA AFYA YAKO

Watu wengi wamekuwa wakichukia uzito mkubwa sio kwa sababu za kiafya bali wanataka wawe na maumbo mazuri na wenye kupendeza pale wanapokuwa wamevaa nguo fulani popote wakati wa mitoko. Ingawaje hilo ni moja wapo ya faida ya uzito mkubwa lakini kumbuka faida nyingine nyingi za kuwa na uzito wa wastani kwani ni muhimu sana kwa afya yako pale unapokuwa umeepuka magonjwa sugu ambayo yangekutesa maisha yako yote. Usiruhusu uzito mkubwa na kitambi maana ndio ngazi ya magonjwa mengi yanapolipukia.

KIPIMO CHA BMI
Hiki ni kipimo ambacho kinatumia uzito wako na urefu wako kuweza kukutenga katika kundi fulani kulingana na pale utakapoangukia katika alama maalumu zilizopangwa.
Hivyo zoezi hili unaweza kulifanya hata hapo ulipo kaa kwa kuzingatia mfano ufuatao.

Mfano, Mr Masha nina kilo 55 na urefu sm 164.

Hatua 1: Badili urefu kuwa katika kipimo cha mita.

Mita 1 = sm 100
Chukua urefu wangu gawanya kwa 100 kupata urefu katika mita.
Ambapo jibu litakuwa 1.64.

Hatua 2: Zingatia fomula ya BMI = UZITO/M2

Hivyo basi chukua uzito wako gawanya kwa urefu wako kipeo cha pili.
55kg/(1.64)2 ambapo ni sawa na 55/ (1.64 x1.64) = 20.5

Kwa ufupi chukua uzito wako gawanya kwa kipeo cha pili cha urefu wako katika mita.

JE UTAJUAJE KUWA BMI IPO KATIKA KIWANGO SALAMA?

REJEA YA BMI
A. NZURI KWA AFYA YAKO: BMI 19 HADI 24
B. UZITO MKUBWA: BMI 25 HADI 29
C. KITAMBI: BMI ZAIDI YA 30, 35 na 40
Rejea katika mfano wangu pale juu, utagundua kuwa mimi nimeangukia katika UZITO MZURI KWA AFYA YANGU. Sasa unaweza hata wewe ukafanya zoezi hilo sasa hivi kabla hujaendelea na maada hii hapa.
Uzito mkubwa kuanzia BMI 25 na Zaidi tafiti zinaonesha kuwa unakuwa hatarini sana kupata magojwa ambayo ni magonjwa ya moyo na magonjwa tabia kama kisukari, kiharusi, shinikizo la damu, kansa, uvimbe kwenye kizazi nk hivyo ni jukumu lako sasa kuanza safari yako upya kuepuka maadui wote wa vyakula na vinywaji wanaokufanya ufike hapo na BMI kubwa kiasi hicho. Unaweza endapo ukidhamiria kuyatimiza malengo yako.

Baada ya kuona namna gani unaweza kubaini uzito wako kama umekithiri au upo kiwango salama basi naomba nizungumze kwa undani sana kuhusu aina ya vyakula.

MAKUNDI YA VYAKULA NA SAYANSI YAKE KATIKA KUPAMBANA NA UZITO MKUBWA.
Nimekuwa nikitoa maada zangu nyingi sana na tatizo kubwa ambalo nimekuja kuligundua kuwa watu wengi wanashindwa kupungua uzito sio kwamba wanashindwa kufanya utekelezaji bali ni kwa sababu wanafanya utekelezaji nusu nusu ambao haujakamilika. Na wengi hawapendi kujifunza Zaidi na kuchimbua kwa kina kitu ambacho anataka kukifanyia utekelezaji.

Napenda nikupe siri unapotaka kufikia malengo yako kiafya hasa pale unapotaka kuanza safari nzito ambayo wengi imewakatisha tamaa kama ya kupunguza uzito na kitambi. Hakikisha unakuwa na uelewa wakutosha wa kitu ambacho unataka kukifanyia utekelezaji ili kwamba unakuwa unajiongoza kwa lolote ulitendalo.
Pia nimegundua watu wengi hawajui aina kuu ya vyakula na wengi wao fikra zao zinawapeleka kutaka kujua makundi fulani tu ya vyakula na hawataki kujifunza na kujua kwa nini hasa Daktari huyu ananishauri hivi na sio vinginevyo? Uwe mtu unayejiuliza maswali na kuyatafutia majibu, usifanye kitu kwa afya yako kwa kukaririshwa bali jifunze kwa kina ndipo ukiweke katika utekelezaji baada ya kuona ubora wake na ukweli wake kuhusu afya yako hapo baadae.

Basi leo nitakueleza kwa kina kidogo makundi haya ya vyakula na namna gani unaweza kuyatumia pale unapotaka kuondoa kitambi au kupunguza uzito wako kuanzia sasa.

MAKUNDI MAKUU MATATU YA VYAKULA (MACRO NUTRIENTS)
Hizi ni molekyuli kubwa sana za lishe ambazo mwili wako unahitaji kwa kiwango kikubwa sana. Na makundi haya yamegawanywa kama ifuatavyo.
A. WANGA
B. PROTINI
C. MAFUTA (LIPIDS/FATS)

Nitapenda nianze kuchambua aina ya lishe moja baada ya nyingine hii ni kwa sababu ili uweze kupanga mlo lazima ujue elimu ya kile unachokipanga kuhusu afya yako.

1. WANGA ( CARBOHYDRATES)
Wanga ni lishe ambayo imetenegenezwa/kuundwa na vijenga lishe viitwavyo glucose.

Naweza nikafananisha wanga kuwa ni nyumba na glucose ni matofali. Hivyo bila matofali huwezi kupata nyumba yako.
Wanga zimegawanyika katika makundi makuu matatu pia kulingana na kiwango cha glucose zilizo ungana kutengeneza aina hiyo ya wanga.
a) MONOSACCHARIDES
Hii ni aina ya wanga ambayo ndio kiini cha mwisho cha wanga baada ya wanga kuvunjwa vunjwa mwilini mwako pale inapokuwa inatumika.
Mfano: Glucose, Fructose (Inapatikana kwenye matunda), Galactose ( Inapatikana kwenye maziwa)
Hivyo basi wanga inapokuwa katika mifumo rahisi kama Glucose,fructose na Galactose ni virahisi sana kutumika mwilini mwako kupitia utumbo mdogo.
Hivyo unapokuwa unakula tunda, vimeng’enya chakula chako (enzymes) hujitahidi kadri ya uwezo kubadili sukari iliyopo kwenye tunda kuwa katika mfumo rahisi wenye kuweza kutumika na mwili.
Ukinywa maziwa utapata ………Galactose
Ukila tunda utapata………………Fructose Nk

b) DISACCHARIDES
Hii ni aina ya wanga ambayo imepatikana baada ya sukari ambazo zipo katika mifumo rahisi kuungana yaani monosaccharides.
Mfano: Lactose inayopatikana kwenye maziwa inatokana na Glucose pamoja na Galactose.
Hivyo lactose inakuwa inameng’enywa na vimeng’enya chakula hutoa sukari katika mifumo rahisi ambazo ni galactose na glucose.

Mfano mwingine ni sukari ya mezani ambayo tunatumia sana kuweka radha katika vinywaji mbalimbali majumbani, aina hiyo huitwa SUCROSE ambayo inapatikana sana kutokana na miwa hapa Tanzania.
Pia aina nyingine ni maltose ambayo hupatikana kwenye nafaka. Na hupatikana kwa kiwango kikubwa Zaidi pale nafaka inapokuwa imevundikwa .

c) POLYSACCHARIDES
Hupatiakana baada ya sukari ambazo zipo katika hali rahisi kuungana.
Na ningependa tu ujue kuwa sukari inapotaka kuhifadhiwa huungana na kutengenza molekyuli kubwa iitwayo polysaccharides.
Mfano -Sukari katika mimea huhifadhiwa katika mfumo uitwao STARCH. Ambayo unaweza kuipata katika vyakula kama mahindi, mchele,vngano,mihogo, viazi vitamu, viazi ulaya nk. Hivyo unapokuwa unakula vyakula kama hivyo ujue unakula vyakula vya wanga katika mfumo wa starch ambapo vyakula hivyo vikifanyiwa kazi mwilini mwako na vimeng’enya chakula tunapata sukari rahisi iitwayo glucose ambapo ndio inatumika kuzalisha nishati ya mwili wako kuendesha shughuli mbali mbali za mwili.

- Sukari katika mwili wa binadamu huhifadhiwa katika mfumo uitwao GLYCOGEN kwenye misuli na ini.
Unatakiwa ujue kuwa tunapokuwa tunaongelea kuhusu vyakula vya wanga tunaongelea yote ambayo nimeyatamka hapo juu katika makundi makuu matatu.
Hivyo basi kwa ujumla vyakula vyenye wanga kwa KIWANGO KIKUBWA ni kama vifuatavyo
I. Mchele
II. Mahindi
III. Ngano
IV. Mihogo
V. Viazi vitamu
VI. Viazi mviringo nk

Lakini pia kuna vyakula vyenye sukari kwa KIWANGO KIDOGO

VII. Matunda
VIII. Maziwa
Hiyo ni mifano ya vyakula ambavyo unaweza ukajua kutofautisha kirahisi kabisa.

UFANYE NINI ULI UWEZE KUPUNGUZA UZITO KATIKA VYAKULA HIVI VYA WANGA
Jambo la kwanza kukufahamisha kuwa kadri unavyokula kiasi kingi cha wanga ndivyo maji yanayotolewa na kongosho yaani homoni ya insulin inatolewa kuja kusaidia kuhifadhi sukari ambayo ipo juu ya kiwango.

Fikra potofu za watu wengi wanapokuwa wanajaribu kuonisha mambo hujaribu kuipa kazi kubwa insulin kuwa hata ule wanga kiasi gani sukari itaenda kutumika mwilini na kuhifadhiwa na insulin mwilini mwako pale inakuwa imezidi. Ukweli ni kwamba mwili wako unahifadhi kuwango maalumu cha sukari inayozidi kwenye damu katika mfumo wa glycogen kwenye misuli na ini. Hivyo kwa sababu basi kiwango maalumu tu kinaruhusiwa kuhidahiwa katika mfumo wa glycogen mwilini mwako sasa je kiwango kingine kitaenda wapi baada ya kufikiwa kwa hicho kiwango maalumu cha glycogen iliyohifadhiwa?
Jibu lake ni dogo tu, kiasi cha sukari inayozidi huweza kuhifadhiwa katika mfumo wa mafuta mwilini mwako katika sehemu za kuhifadhia mafuta( adipose tissue) kama kiunoni, kifuati, tumbo, mgongoni nk. Hivyo basi ni dhahiri kwamba utakapopunguza kiwango cha wanga utapunguza hata kiwango cha sukari kinachozidi na kubaki hakina kazi muda huo na kuanza kuhifadhiwa.

Nitafurahi endapo ukianza kufanya hivyo kuanzia sasa, punguza wanga katika mlo wako unaoweka mezani mwako.
Nimekuwa nikiona akinadada wana uzito mkubwa na bado wanashindia soda na chips kavu asubuhi na jioni huku wakijidanganya wameepuka mayai.

Afya yako ipo mikononi mwako, na ukitaka kupunguza tumbo na uzito wako lazima kwanza ufuate masharti yale kumi na ukubali kuishi mwenye afya.


ULAJI MZURI WA SAHANI YAKO KAMA UNAHITAJI KUPUNGUZA UZITO
Wanga: Asilimia 10 -15
Protini : Asilimia 15 - 20
Fats (mafuta mazuri): Asilimia 65-75

Hivyo jitahidi kadri uwezavyo kutozidishia mwili wako wanga na kufanya uelemewe na kiwango kikubwa cha sukari na utakapofanya hivyo mwili wako utaanza kuunguza mafuta wenyewe badala ya kuhifadhi mafuta.

Note: KIWANGO CHA WANGA KATIKA SAHANI YAKO WEWE MWENYE KITAMBI NA UZITO MKUBWA USILINGANE NA MTU MZIMA AMBAYE HANA KITAMBI NA UZITO MKUBWA. MAANA UTAKUWA UNAJENGA TASWIRA YA VITU AMBAVYO HAVIENDANI KIAFYA NA ITAKUGHARIMU KUFUATA MLO WA MTU MZIMA.

VYAKULA VYENYE FIBER NYINGI ( NYUZI NYUZI)
Vyakula hivi vya fiber ni aina pia ya wanga inayopatikana kwa wingi wenye mimea. Kwani fiber huwa haiwezi kumeng’enywa kiurahisi na vimeng’enya chakula (enzymes) mwilini mwako.hivyo basi baada ya kufika kwenye utumbo mpana bacteria marafiki huweza kuanza kuimeng’enya na kutengeneza lishe muhimu mwilini na pia kiini maarufu kama BUTYRIC ACID hutengenezwa ambacho kimeonesha uwezo mkubwa wa kusawazisha sukari mwilini na kuzuia magonjwa mbalimbali ya moyo.

JE VYAKULA VYA FIBER VINAKAZI GANI KUBWA KATIKA KUPUNGUZA UZITO AU KITAMBI?
Vyakula hivi vina uwezo mkubwa wa kuhakikisha sukari yako inakuwa katika kiwango sawia muda wote na pia itakata ile hali ya kujisikia njaa muda wote( ulaji hovyo) kwa sababu vyakula hivi hufanya umeng’enyaji chakula katika mfumo wa chakula uende polepole, nadhani rudia tena kutamka , pole pole ndio maana unapokuwa umekuwa vyakula vya fiber utajisikia muda wote tumbo lako umeshiba na sukari yako muda wote itakuwa katika kiwango kizuri kabisa.
Tumia vyakula hivi kupata vyuzi nyuzi nyingi
1. MATUNDA KAMA TIKITI MAJI, APPLE, TANGO
Kumbuka kama unataka kutumia kama juisi hakikisha juisi yako umetengeneza kwa blende zenye kuacha nyuzi nyuzi na sio zenye kumaliza nyuzi zote.
Pia hakikisha juisi yako unavyoweka ndani ya dakika 15 kwani vitamin na madini yanaathiriwa haraka sana na joto na mwanga.

2. MBOGA ZA MAJANI
Mboga za majani unaweza kutumia kama kachumbali au kama juisi yako nyumbani utajisikia mwenye Amani na utashangaa maajabu yake.
Mfano: Kabeji, spinachi,kale, beet root, brokoli nk

UTAFURAHIA SANA JINSI GANI UTAKAVYOEPUKA TABIA YA KULA KULA PALE UTAKAPOTUMIA VYAKULA VYA FIBER.

B. PROTINI
Hili pia ni kundi kubwa sana mwilini mwako katika makundi ya vyakula ambayo yanahitajika katika kiasi kikubwa kiutendaji.
Kwani vyakula vya protini vinatengenezwa na vijenga protein viitwavyo AMINO ACIDS. Hivyo basi kwa lugha nyepesi ukitaka kunielewa namaanisha nini, basi amino acids ni matofali yanayotumika kujenga molekyuli kubwa ya lishe iitwayo protini.

KAZI KUBWA YA PROTINI MWILINI MWAKO
-Kujenga mwili
-Kutengeneza homoni
-Kutengeneza visafirisha hewa kama hemoglobin
-Kuongeza kinga ya mwili kwa kutengeneza Antibodies ambazo hupambana na maambukizi.

AINA KUU MBILI ZA AMINO ACIDS
Napenda nikwambie kuwa mwili una uwezo wa kutengeneza amino acids wenyewe na aina hii huitwa NON-ESSENTIAL AMINO ACIDS, maana hutengenezwa na mwili wenyewe ambapo takribani idadi ya amino acids 11 kutengenezwa na mwili wako kati ya idadi yote 20. Lakini pia nataka nikwambie kuwa mwili unahitaji kiasi fulani cha amino acids ambazo hupatikana mwilini mwako kupitia kula vyakula vya protini aina hii huitwa ESSENTIAL AMINO ACIDS ambapo mwili unahitaji Zaidi ya amino acids 9 kutoka kwenye vyakula vya protini.
Sitaweza kukuchambulia kwa majina lakini nataka ujue kuwa aina hizo tisa tunatakiwa tuzipate kupitia vyakula vyetu tunavyo andaa majumbani.
Pia napenda nikuwekee aina ya protini katika makundi makuu mawili ambapo nadhani hutakuwa na swali tena la kumuuliza Daktari pale unapotaka kubaini protini gani utumie.

1. PROTINI ILIYO KAMILI (COMPLETE PROTEIN)
Hii ni protini yenye aina zote za essential amino acids ( amino acids zinazohitajika na mwili kutokana na lishe)
Aina hii ya protini inapatikana kwenye nyama za mifugo mbalimbali kama ng’ombe, mbuzi,kondoo, kuku nk

2. PROTEIN ISIYO KAMILI
Hii ni aina ya protini yenye amino acids kiasi katika zile zinazohitajika na mwili kupitia lishe. Aina hii hupatikana kwenye matunda na mimea mbalimbali. Hivyo unapokula tunda mfano parachichi unakuwa unakula protein pia lakini sio kwamba amino acids zote zile 9 zinazohitajika zinapatikana katika tunda hilo ndio maana ya aina hizi mbili.

VYAKULA VYA PROTINI NA KUPUNGUZA UZITO
Napenda nikwambie kuwa unapotaka kufikia malengo yako kuhusu afya yako lazima ujue kuna viwango maalumu lazima uzingatie kama ifuatavyo;
KIWANGO MAALUMU CHA PROTINI KILA SIKU

Mtoto mdogo chini ya mwaka ni gramu 14
Mtoto wa mwaka mmoja hadi 4 ni gramu 16
Mama mjamzito gramu 60
Mama anaye nyonyesha gramu 65
Mtu mzima gramu 60
ANGALIA MIFANO YA MAKADIRIO YA VYAKULA BAADHI HAPA ILI UWEZE KUJUA UNAFIKIA KIWANGO HICHO MAALUMU.
Kipande cha nyama (Sm 4 x2) Ng’ombe, kuku, mbuzi nk. . . . 7gram
Kipande cha siagi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7gram
Glasi moja ya maziwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8 gram
Nusu kikombe cha maharage . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6 gram
Yai moja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8 gram
Vijiko viwili vya peanut butter . . . . . . . . . . . . . . . . 8 gram

Kwa kuhitimisha vyakula vya protini vipo vingi sana lakini baadhi amabavyo vinatumika kila matabaka ndivyo nilivyoweka hapo juu.
Hivyo angalia kwa siku kama unahitajika kutumia protini gm 60 unatakiwa uchanganye lishe katika aina ya protini hadi utakapokaribia kiwango maalumu.

B. VYAKULA VYA MAFUTA (LIPIDS /FATS)
Vyakula hivi vimeonesha kuepukwa sana na watu wengi kwa sababu ya kuonekana vinasababisha magonjwa ya moyo, uzito mkubwa na kisukari.
Lakini katika jukwaa hili kuna aina kuu mbili za vyakula vyenye mafuta (fats) hapa duniani na leo ningependa uzijue ili uweze kuepuka vizuri

1. VYAKULA VYENYE SATURATED FATS
Hivi ni vyakula vyenye mafuta ambayo yana madhara mwilini mwako kwani hupelekea kuongeza cholesteral mbaya mwilini na hatimaye kukupa magonjwa ya moyo na mengine.
Aina hii ya mafuta huwa yameganda katika mazingira ya kawaida ya joto la ndani. Mfano mafuta yote yatokanayo na wanyama (animal fats) mfano, Butter Hivyo unapokuwa unachagua vyakula vyako vya protini jaribu kupunguza protini itokanayo na nyama na weka aina zingine kufikia malengo.

2. VYAKULA VYENYE UNSATURATED FATS
Hivi ni vyakula vyenye mafuta mazuri ambavyo vinapunguza mafuta ya cholesteral na kukuepusha na magonjwa ya moyo,kisukari , uzito mkubwa ba shinikizo la damu.
Mafuta haya mengi yanapatikana katika mimea na siku zote ukitaka kuyagundua ni pale unapoyakuta hayajaganda katika joto la kawaida la ndani.
Mafano, Alizeti, parachichi,Olive, canola, peanut nk hivi ni baadhi ya vyakula vinatupa kiwango kingi cha unsaturated fats.

Kuna fikra potofu kuwa mafuta yote yatokanayo na mimea ni salama kwa afya na hivyo watu wamekuwa wakiyakimbilia bila kujiuliza mara mbili.
Ni kweli mafuta yatokanayo na mimea ni mazuri kwa afya zetu lakini sio yote kuna baadhi yana kiwango kingi sana cha saturated fats ambazo ni adui mkubwa wa afya yetu.
Mfano mafuta ya Coconut oil, palm kernel oils, and cocoa butter ni mafuta hatari kwa afya yako kwani yana kiwango kingi sana cha mafuta mabaya na kiwango kidogo cha mafuta mazuri.

HEBU CHUNGUZA MTIRIRIKO HUU, KUANZIA JUU NI MAFUTA MABAYA NA KADRI UNAVYOSHUKA CHINI NDIVYO YANAZIDI KUWA BORA ZAIDI KWA AFYA YAKO.

Angalia hapa

Coconut
Corn
Walnut
Soybean
Peanut
Canola
Almond
Safflower
Fat or oil
Avocado
Olive
Sunflower
Lard
Palm
Beef tallow
Cocoa butter
Table cream
Butter
Palm kernel

Note: UKITAKA KUCHAGUA MAFUTA MAZURI KWA AFYA YAKO KUMBUKA KUANZIA CHINI UKIFUATA ORODHA HIO.

Huo mchoro unaonesha ubora wa mafuta ambayo yamekuwa yakitangazwa kila kona
Mfano: Mafuta ya alizeti yana kiwango cha saturated fats asilimia 10 ambapo Coconut oil ni asilimia 80 ya saturated fats HIVYO MAFUTA YA ALIZETI NI MAZURI SANA
Mfano wa pili ni kati ya OLIVE oil na coconut oil ambapo oil ina kiwango cha unsaturated fats asilimia 10 ambapo coconut oil ina asilimia 80. HIVYO MAFUTA YA OLIVE OIL MAZURI SANA

KUTOKANA NA KUWEPO KWA MAFUTA MABAYA NA MAZURI KATIKA AINA MOJA YA CHANZO CHA MAFUTA NI JUHUDI ZAKO KUTAFUTA KIPI KIZURI KWA AFYA YAKO

Mafuta pia yatokanayo na samaki yamekuwa yakionesha umahili mkubwa kwa afya za binadamu kwa sababu yana kiwango kikubwa cha omega 3. Mfano mafuta ya SALMON ni mazuri sana kama umekuwa ukiyatumia nyumbani kwako.

Kwa kuhitimisha vyakula vyenye mafuta unaweza kuvipata katika vyanzo vingi sana mfano wake ni huu hapa
- Matunda kama parachichi
- Samaki
- Karanga
- Coconut
- Alizeti
- Olive nk
Vyakula vya mafuta mazuri vinaonesha kupunguza kasi ya uzito kwani vimeonesha kwa kiwango kikubwa kutopandisha sukari kwa wingi na kuufanya mwili kuanza kuyaunguza mafuta mwilini mwako
Kikubwa ambacho unatakiwa kujali, ni kutafuta soko la viwanda linatoa bidhaa gani na kudanganywa na watu wanaotumia mafuta hayo jinsi gani wanakula vyakula vitamu. Jiulize kwanza kabla ya kushawishika na matangazo maana afya ni hazina yako na sio ya mtu mwingine.

NAJUA LEO UMEJIFUNZA KUHUSU MAKUNDI MAKUU 3 YA VYAKULA KWA KINA ZAIDI

Nina matumaini kuwa Makala zangu zijazo zitakzoendelea nikitamka kitu fulani basi utakuwa unajua na hivyo kilichobaki sasa na kuanza kupangilia mlo na hilo zoezi litaanza kuanzia muda wowote. Kama upo pamoja nami tangu darasa hili lianze naomba kuhitimisha hapa na ninashukuru kwa moyo wako wakujifunza endelea kukaribisha watu wengi sana kuendelea kuungana nasi katika jukwaa hili la Afya.

Whatsapp: 0622925000
Email: mashamasanja@gmail.com
Blog: www.mashahealth.blogspot.com
posted from Bloggeroid

Thursday, 10 December 2015

TIBA ASILI YA MAFUA

Njia Rahisi za Kiasili za Kutibu Mafua.

Mafua ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanapoanza kutokea mabadiliko ya hali ya hewa, kutoka msimu wa joto kuingia baridi au kutoka msimu wa kiangazi kuingiza masika. Ili kujikinga na ugonjwa wa mafua, ni lazima mwili uwe na kinga ya kutosha.


Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi kikubwa cha protini na virutubisho vingine.


SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa na virutubisho vinavyosaidia kupunguza utokaji wa makamasi. Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza supu ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.


VITUNGUU SAUMU
Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya ‘allicin’ ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza. Kitunguu saumu kinatoa kinga halikadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua. Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje zake.


CHAI
Chai, hasa ya kijani, (green tea) ina virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal of the American College of Nutrition) umeonesha kuwa watu wanaotumia chai kwa mpangilio maalum hawasumbuliwi mara kwa mara na mafua pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza, huwa salama na mafua au siku za kuumwa mafua hupungua kwa asilimia 36 ukilinganisha na wale wasiokuwa na kinga imara.


Hata hivyo, tahadhari inatolewa kwa watoto wa shule kutokupewa kiasi kingi cha chai kwa siku. Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku kwa mtoto wa shule siyo mbaya. Kwa mtu mzima, asizidishe vikombe vitatu kwa siku. Ikumbukwe kuwa chai inapotumika kwa wingi kupita kiasi, huweza kusababisha pia tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu. Kunywa kiasi kwa afya yako.


MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Ili kupata kiasi kingi cha Vitamin C, inashauriwa machungwa yaliwe pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.


ASALI
Kama inavyojulikana, asali ni tiba ya matatizo mengi ya kiafya, miongoni mwa hayo ni pamoja na mafua. Asali inasaida kuondoa kikohozi na muwasho kwenye koo. Halikadhalika, asali inaweza kutumiwa na watoto wadogo kama dawa.


Watoto wanaoruhusiwa kutumia asali kama tiba ni wa umri kati ya miaka 2 hadi 5. Hawa dozi yao ni nusu kijiko kidogo cha asali, wenye umri wa miaka 6-11 wapewe kijiko kimoja kidogo na wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 18, wapewe vijiko vidogo viwili vya asali wakati wa kulala.

MTINDI
Kutokana na kiwango kikubwa cha protini ilichonacho, Mtindi ni chakula kingine kinachofaa kuliwa na mtu mwenye mafua ili kupunduza siku za kusumbuliwa na ugonjwa kukohoa.

CHOKOLETI NYEUSI
Wataalamu wanakubaliana kuwa ulaji wa ‘chocolate’ nyeusi (dark chocolate) huimarisha kinga ya mwili, hivyo inapoliwa na mgonjwa wa mafua huweza kumpa ahueni mgonjwa kwa namna moja ama nyingine. Halikadhalika huwa kinga kwa maambukizi mengine.

PWEZA
Samaki aina ya pweza wana virutubisho vingi vya kuongeza kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana na bakteria pamoja na virusi vya mafua. Kiasi kidogo cha pweza, awe wa kukaangwa au kuchemshwa kama supu, anafaa kuliwa mara kwa mara kuimarisha kinga ya mwili.


VIAZI VITAMU
Kirutubisho aina ya ‘Beta-carotene’ huimarisha kinga ya mwili. Kirutubisho hicho huwa ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa kinga mwilini na kinapatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu na vyakula vingine kama vile karoti, maboga na mayai, (kiini).


Kwa ujumla, suala la kuimarisha kinga ya mwili ni muhimu kwa afya zetu. Ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu na vingine, unatakiwa kuwa ni wa mara kwa mara kama siyo wa kudumu, kwa sababu mwili unapokosa kinga imara, ni rahisi kushambuliwa na maradhi ya kuambukiza.

Kila dawa na Ugonjwa wake..
posted from Bloggeroid

CHAKULA NA UNENE - 4



SEHEMU YA 4:

MAMBO KUMI YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUANZA SAFARI YA KUPUNGUZA UZITO

Nimekuwa nikitamka sentensi hii mara kwa mara kuhusu kupunguza uzito na laiti ungekuwa unaijua maana yake usingekuwa unasumbuka tena na uzito mkubwa kiasi hicho!
Napenda kurudia tena, Je upo tayari kuifuata? Najua kwa jinsi gani umekuwa ukijaribu kujinasua itakuwa na mara yako ya kwanza kuitilia maanani sentensi hii,
“Njia pekee yakupunguza uzito ni kuwa mwenye afya” Maana yake kama mwili wako unashambuliwa na changamoto mbalimbali hasa zinazoharibu shughuli za mwili na hatimaye mwili kushindwa kuendesha shughuli zake ipasavyo. Inapofikia hapo mwili wako hauwezi kupunguza uzito haijalishi unatumia nguvu kiasi gani.

Na njia pekee ili uweze kuwa mwenye afya na kuufanya mwili wako ufanye kazi katika misingi yake bila kuchanganyikiwa kiutendaji basi unatakiwa kuanzia leo ubadili chakula kinachoingia kinywani mwako na sio kupunguza kiasi cha chakula ambacho umekuwa ukiweka kinywani mwako. Kitendo cha kujinyima kula kunasababisha homoni kama adrenaline na noradrenalines (stress hormones) kutolewa kwa wingi na zinauwezo mkubwa wa kukusababishia hamu Zaidi ya chakula na uzito kuongezeka.

Hivyo kujinyima bila chakula kumeonyesha kunaongeza uzito kwa hali kubwa sana kulingana na tafiti zilizofanyika. Siri kubwa sio KUJINYIMA CHAKULA bali ni KUJITAHADHALI CHAKULA KINACHOINGIA KINYWANI MWAKO NI CHA AINA GANI NA KINA UBORA GANI KULINGANA NA TATIZO LAKO?
Unatakiwa kujua kuwa LISHE YA MTU ambaye hana uzito mkubwa au kitambi ni tofauti kabisa na yule mwenye uzito mkubwa na kitambi. Ndio maana basi inashangaza unapokuwa una ndoto ya kupunguza uzito lakini mlo wako unafanana na mlo wa watu wengine ambao hawana ndoto kama yako kiafya.

Basi leo nataka nizungumzie mambo kumi ambayo lazima uyafuate unapotaka kupunguza uzito wako. Na kama umekuwa ukitaka kupunguza uzito kilo kumi ndani ya siku 7 basi hizi Makala hazita kufaa kwani bado una fikra potofu ya kupunguza uzito bila kujali afya yako na ni bora kutoendelea kupoteza muda kusoma haya! Kama HUNA HARAKA! Basi endelea rafiki! Kama unapenda na unaamini kitendo cha kupunguza uzito ni safari ya polepole na hasa Zaidi unapotaka kupunguza uzito kiafya basi zingatia ushauri huu ambao nimekuwa nikikupatia.

1. USIHIFADHI CHAKULA NDANI MWAKO KILE AMBACHO UNAKIEPUKA
Moja ya kitu cha pekee ambacho utatakiwa ukizingatie ni kutokuwa na chakula chochote ambacho ni hatari kwa afya yako. Hata familia yako ijengee mazingira ya kuepuka tatizo maana siku akipata tatizo kama lako ni kazi sana kuliondoa kama unavyofikiria.
Napenda nikupe siri moja tu kwamba, endapo ukiweka mbali vyakula na vinywaji hatari kwa afya yako, unakuwa unajisikia uvivu kwenda na kuvifuatilia na hivyo hutaweza kuvitumia. Pia unaweza ukawa unauhitaji nacho lakini huna pesa uta ahirisha! Lakini endapo vyakula hivyo vimo ndani ni virahisi kutojizuia kuvitumia.
Hii hatua ni ngumu sana kwani nimekuwa nikiongea na watu wengi na wengi wao mtihani huu umewashinda kabisa. Hivyo endapo unauchukia uzito naomba unipe ahadi rafiki yangu kuanzia leo utakaa mbali na vyakula ambavyo ni hatari kwa afya yako

2. KULA CHAKULA BORA KABLA HUJALA CHAKULA AMBACHO UNAJUA SIO BORA KWA AFYA YAKO
Watu wengi sana hupenda kutumia vyakula ambavyo ni hatari kwa afya zao na hivyo wanapokutana na chakula bora hushindwa kabisa kumudu kula chakula hicho na hatimaye afya hudhoofika. Nataka nikwambie kuwa tafiti zinaonesha kuwa watu wengi wenye uzito uliokithiri wana kabiliwa pia na upungufu wa madini na vitamin muhimu mwilini maana hivyo ndivyo vinavyohakikisha shughuli zote za mwili zinatembea katika mwendo sahihi na wenye kukufanya mwenye afya daima. Hivyo basi kukosa baadhi ya lishe kunasababishwa na kutoa kipaumbele kwa vyakula ambavyo sio bora kwa afya yako. Hivyo hakikisha umekula matunda kwanza kama unataka kunywa soda yako kwa wale ambao huwezi kabisa kujizuia kutumia vyakula vyenye sukari nyingi ( Sugary drinks). Hapa naaamanisha hakikisha unatoa kipaumbele kwa chakula sahihi ndipo utumie chakula ambacho hata nafsi yako inajua sio salama kwa afya yako.

3. KULA CHAKULA BORA KWA AFYA YAKO PALE UNAPOKUWA UNA NJAA
Nimekuwa nikijiuliza sana watu wanao fanya kazi katika maofisi makubwa ya serikali kwa nini unene na uzito mkubwa umekithiri? Nimejitahidi kufanya tafiti hii na swala dogo sana nimekuja kuligundua ni kwamba hawana mazoezi muda mwingi wako na kazi na kibaya Zaidi wanakula vyakula ambavyo ni hatari kwa afya zao kwani hawana jinsi kwa sababu yumo ofsini.
Nimekuwa nikiona ofsi nyingi sana zinatumia vyakula hatari kwa afya yako, kama mikate na mchana unakula viazi vilivyo okwa na nyama ya kuku pembeni. Hii ni ishara kuwa unakula chakula ambacho sio bora wakati una njaa. Na pia niekuwa nikiona watu wengi sana wanapokuwa wananjaa basi ananunua au anafungua soda yake apate sukari kwanza huku akiendelea na kazi. Na bado anahitaji kupungua uzito! Umeona jinsi gani unavyo enda kinyume na zoezi zima la kupungua uzito? Nimekuwa nikiambiwa na wazazi wangu usemi “Ukitaka kizuri lazima ulipe gharama” Maana yake ukitaka kupungua uzito fuata mashart utafurahia kama wenzako wanaofuata mashariti ndio maana unatamani kuwa kama wao.

Pia hakikisha unaandaa chakula na unakuwa na muda sahihi wa kupata chakula ili pindi tu unapopata njaa upate chakula ambacho ni bora kwa afya yako ili utimize malengo yako. Changamoto ipo pale unapokuwa una njaa na hauna chakula ambacho unatakiwa ulishe mwili wako na hatimaye unaishia kula vyakula ambavyo ni hatari kwa afya yako.

4. EPUKA VYAKULA VYOTE AMBAVYO UNAONA UNAWEZA KUVIEPUKA NA USIVIJALI
Hapa wengi hujitahidi kuepuka kwa maneno na baada tu ya kutoka nje na marafiki zao hujificha na kutumia kile kitu ambacho nafsi inashuhudia kuwa ulikiacha. Naomba unapo amua kuvunja agano ujue utakuja unalipa gharama yake ya kutofikia malengo yako unayo yataka

5. BADILI MLO WAKO NA MWENENDO WAKO POLE POLE
Watu wengi wanaohitaji kupunguza uzito au kitambi siku zote huwa wana haraka kwani wanasahau kitambi na uzito mkubwa alivipata kwa muda mrefu. Hivyo hakikisha kwamba unafuata mashariti haya kama unahitaji kupunguza uzito wako kiafya na salama kabisa.
Na hivyo unajua kwa nini umekuwa ukijitahidi kubadili tabia na ujaribu kupungua na umeshindwa? Jibu ni dogo tu najua utashangaa! Lakini hata usishangae kwa sababu ni haraka zako za kufikia malengo yasiyo ya kiafya yanakukosesha mafanikio ya kuishi bila kitambi, hebu sikiliza! Ukitaka kuacha vyakula fulani jitahidi kuacha kimoja kimoja, na pole pole kwani watu wengi wameonesha kushindwa kuacha kutumia kitu fulani na kuishi maisha ya mazoezi kwa kujaribu kuacha vitu vyote kwa wakati mmoja. Nakushauri kuwa kama unataka kupunguza uzito basi anza kuacha tabia au chakula ambacho unajua ni hatari pole pole lazima utafanikiwa.

6. USIJIPONGEZE KWA VYAKULA
Watu wengi tunapopata pesa baada ya mihangaiko ya utafutaji huwa tunajipongeza! Na wengi wetu hujipongeza kwa nguo,chakula na sherehe maalumu kwa ajili ya pongezi hio. Jiulize wewe huwa unajipongeza kwa namna gani upatapo pesa? Kwa kwenda kula viazi vilivyo kaangwa kwa mafuta, kuku na pombe? Nakuomba upunguze au kuacha kabisa kujipongeza kwa vyakula kwani vinakupotezea mpangilio wa milo yako na hatimaye kuchanganya ubongo ulivyozoea katika kufanyia kazi chakula unachoweka mwilini mwako. Ukiweza hili hutarudi nyuma daima katika zoezi la kufikia mafanikio ya kuishi bila kitambi.

7. KUWA NA DAFTARI LA LISHE
Hili sio daftari la kuhesabu kiwango cha sukari unachokula kwa siku wala kuhesabu vipande vya karoti ulivyokula kwa siku. Hiki kitabu kinatakiwa kitumike kuandika na kuanisha maamuzi yako unayoyafanya unapotaka kupiga hatua na kuepuka kitambi. Mfano umechukua maamuzi ya kuacha kunywa vinywaji vyenye kemikali ya vionjo, rangi, radha na sukari basi umeamua kuwa unatengeneza juisi ya matunda na mboga za kijani ambapo utakunywa juisi hiyo ndani ya dakika 15 baada ya kutengeneza. Huu ni mfano wa kuandika mikakati yako ili kwamba ukikiuka kitabu hiki cha kumbukumbu ya maamuzi kitakushtaki. Kama una nia ya dhati najua tutafika endelea kutambua kuwa wengi wao wameridhika na uzito mkubwa na kitambi kwa sababu wanashindwa kumudu hatua hizi kwa sababu vyakula vimeshawadhuru na hawana tena mamlaka juu ya miili yao katika maamuzi ya vyakula gani na vinywaji gani anatakiwa atumie.

Najua umedhamiria hakikisha sasa unajiwekea malengo yanayotimilika kama unachukia hali hio ya kitambi.

8. JICHUNGUZE UNAKULA CHAKULA KIASI GANI NA KWA MUDA GANI
Watu wengi hawajali kabisa zoezi zima la kula, hata anapokuwa amemaliza kula ukimuuliza ametumia dakika ngapi hajui na hakumbuki kabisa...
Hii ni kwa sababu watu wengi hufanya zoezi hili bila kujitambua kuwa wanakula ambapo ni hatari sana kwani huwezi kuchukua maamuzi ya kuamua kuongeza lishe fulani na upunguze kitu fulani katika mlo wako. Na kumbuka hata ule muda wa kutafuna chakula chako kinywani kinasaidia sana vimeng’enya chakula (enzymes) kufanya kazi katika kiwango stahiki. Hivyo kuanzia leo kuwa mwangalizi wa zoezi lako unapokuwa unakula utajikuta unapata mabadiliko hadi utashangaa unapokuwa unaelekea kuondoa kitambi na kupunguza uzito wako

9. Jitahidi kula vyakula vya mafuta mazuri kwa wingi na protini kwa wingi na punguza ulaji wa kiwango kikubwa cha wanga.

Tafiti zinaonyesha kwamba vyakula vya protini vina uwezo mkubwa wa kusisimua mwili wako kuchovya Vipunguza hamu ya chakula (appetite suppressants) ambavyo ni leptin na kufanya kazi yake ya kukufanya kutokuwa mtu wa kula hovyo bila kukata kiu ya njaa.
Chakula aina ya pili kinachofanya kazi kama protini ni vyakula vyenye mafuta mazuri. Na hivyo basi tafiti zinaonyesha kuwa vyakula vya wanga hupunguza na kusababisha kutofanya kazi yake ipasavyo endapo tu unapokuwa unakula wanga kwa kiwango kikubwa kupita kiasi.
Napenda kurudia na kusema kuwa kipimo cha wanga kwa mtu ambaye ana kisukari au uzito mkubwa na kitambi ni tofauti sana na mtu ambaye hana matatizo kama hayo. Ndio maana tunashauri kupunguza vyakula vya wanga unapokuwa unataka kufikia malengo yako.
Kuanzia kesho nitafundisha aina kuu ya vyakula na utajua wewe mwenyewe chakula gani upange na ufike unapotaka.

10. WEKA MALENGO
Hadi hapa ulipo fikia ni asilimia 80 ya kufanikiwa kuondoa kitambi na uzito mkubwa au kutofanikiwa. Maamuzi yote yako ndani ya uwezo wako kwani ndiye unayetakiwa kupanga mikakati ya kuyatimiza yote ambayo umeyasoma katika elimu yangu hii ya afya.

Nimeamua kuongea hizi hatua kumi kwanza kabla sijagusia maada halisi ili kujua kama kweli hutaweza kupuuzia hatua hata moja. Kuna mwingine ataruka kwa kujidanganya katika nafsi yake kuwa haina haja ya kuzingatia vipengele vyote tabia hio haitaweza kukutimizia malengo yako kamwe.

Napenda nihitimishe hapa kwa siku ya leo kesho kutakuwa na mada fupi na iliyo jaa elimu nzito kuhusu mwanzo wa mlo sahihi na makundi ya vyakula kwa ujumla. Watu wengi wamekuwa wakinitafuta kutaka kuwatajia ni vyakula gani watumie wapungue. Lakini mimi sitapenda kuwakaririsha bali nataka muwe waalimu wa vizazi vyenu wote maana hadi sasa matatizo ya uzito mkubwa, kitambi, shinkizo la damu, kisukari yameshamiri zaidi hata ya magonjwa hatari ya kuambukiza. Na bado dunia inayumba kutokana na jinsi gani viwanda vinavyoendelea kufurahi kukosa ufahamu kwa jamii yetu hasa katika vyakula tunavyoweka kinywani.

Naomba tena kukuomba na kukupongeza kwa ushirikiano wako wa kuendelea kuwakaribisha watu wengi kushiriki jukwaa hili kwa kunifuatilia facebook katika ukurasa wangu "Masha Nutrition Health Care"

Asanteni kwa kujumuika nami.


0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

Wednesday, 9 December 2015

ZIJUE FAIDA ZA NDIZI


JE WAJUA NDIZI NI MOJA YA CHAKULA MUHIMU SANA?

Ndizi ni tunda ambalo limezoeleka na watu wengi, linapatikana karibu kila mahali. Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa tunda hili mwilini mwako. Taarifa ifuatavyo itabadilisha mtazamo wako.

Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako, sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya sucrose, fructose na glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako.

Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika tisini (90) ambazo ni sawa na saa moja na nusu.
Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika.

Nishati si faida pekee inayopatikana kwenye ndizi mbivu, tunda hili lina faida nyingine ambayo ni kuusaidia mwili wako kupambana na kuulinda na maradhi kadhaa.

Msongo wa mawazo/mfadhaiko wa akili (stress & Depression) Kwa mujibu wa utafiti kadhaa watu wengi wanaopata mfadhaiko au msongo wa mawazo hujisikia nafuu pale wanapokula ndizi mbivu.
Hii ni kwa sababu ndizi mbivu zina virutubisho aina ya TRYPTOPHAN ambayo ni aina ya protini ambayo mwili huigeuza na kuwa SEROTONIN ambayo kazi yake ni kukufanya upate utulivu na kukurejeasha katika hali ya kawaida mpaka utakapo pata furaha na kuondokana na msongo wa mawazo.

Zaidi ya hapo ndizi mbivu huongeza vitamin B6 mwilini ambayo inasimamia usambazaji wa glucose au sukari na hivyo kusaidia kutuliza msongo wa mawazo.

UPUNGUFU WA DAMU MWILINI ( Anemia)

Ndizi zina madini ya chuma na zinasaidia uzalishaji haemoglobin ambayo ni mzalishaji mkuu wa damu mwilini mwako, hivyo huwasaidia wale wenye upungufu wa damu mwilini.

PRESHA YA DAMU

Ndizi mbivu zina madini ya potassium na una madini chumvi kwa kiwango cha chini jambo ambalo linafanya tunda hili kuwa dawa ya kupambana na matatizo ya presha.
Mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani imetambua uwezo wa ndizi mbivu katika hili kiasi cha kuigiza wazalishaji na viwanda vya ndizi kufanya tunda hili kuwa rasmi katika mapambano ya kupunguza vifo vitokanavyo na presha na kiharusi (stroke)

NGUVU YA UBONGO/AKILI (Brain power)

Katika utafiti uliofanywa huko Twickenham Middlesex) nchini England wanafunzi 200 walifaidika kwa kufaulu kwa mitihani yao mwaka huu kwa kula mlo wa ndizi mbivu asubuhi na mchana .
Ndizi imebainika kuwa uwezo wa kuusaidia ubongo kuongeza nguvu yake. Utafiti umeonyesha madini ya potassium yanaweza kusaidia ubongo kuwa na kasi na uwezo zaidi ya hali ya kawaida.

KUFUNGA CHOO/ CONSTIPATION

Fibre inayopatikana kwenye ndizi mbivu ina uwezo wa kuurejesha utumbo ambao umesababisha kufunga choo kufanya kazi kama kawaida.

MADHARA YA MATUMIZI YA KILEVI/ HANGOVER

Moja ya njia ya haraka ya kurudi katika hali ya kawaida baada ya madhara ya matumizi ya kilevi hasa asubuhi unapoamka ni kutumia ndizi mbivu au bidhaa zitokanazo na ndizi mfano banana milkshake. Ndizi hituliza tumbo na kurejesha kiwango cha kawaida cha sukari mwilini huku ikirutubisha mfumo wa maji mwilini.

KIUNGULIA/ HEARTBURN

Ndizi mbivu ina uwezo wa kupambana na kemikali au acid zinazosababisha kiungulia. Jaribu kula ndizi mbivu na utakuwa shahidi Kwa hili.

Kuumwa asubuhi kwa wajawazito/ MORNING SICKNESS

Matumizi ya ndizi mbivu yamegundulika kusaidia kuepusha kuugua asubuhi ambako kunawapata kina mama wajawazito, hii ni kutokana na uwezo wa tunda hili kuweka katika ulinganifu kiwango cha sukari mwilini.

ALAMA ZA KUNG'ATWA NA MBU

Kwa wale wanaotokwa na vile vipele vidogo vyekundu baada ya kung'atwa na mbu jaribu kufuta eneo hilo lenye kipele kama hicho kwa upande wa ndani wa ganda la ndizi ni ajabu lakini hufanya kazi kuwa hii hupunguza uvimbe na muwasho.

NEVA/NERVES

Ndizi husaidia sana kutibu mfumo wa neva (nervous system) hata kwa wale watu wenye matatizo ya uzito unaotokana na tabia zisizo salama za ulaji hasa kutokana na kukosa muda wa kula na kulazimika kula vyakula vyenye mafuta mengi vinavyopikwa haraka ndizi mbivu zinaweza kuwa msaada mkubwa

VIDONDA VYA TUMBO/ ULCERS

Ndizi zinatumika kama chakula ambacho kinaweza kuwa msaada kwa watu wenye matatizo kwenye tumbo hii kutokana na ulaini wake na hupunguza acid ambayo husababisha vidonda tumboni na pia hupunguza maumivu kutokana na kuziba baadhi ya vidonda hivyo.

KUPUNGUZA HALI JOTO MWILINI

Ndizi ni tunda ambalo huweza kusaidia kupunguza joto. Nchini Thailand kina mama wajawazito hula ndizi ili kuhakikisha wanawazaa watoto wao katika hali ya joto pungufu.


NB. Hivyo basi ndizi mbivu ni tunda ambalo lina uwezo wa kusaidia matatizo mengi ya afya ya mwanadamu. Unapolifananisha na Apple ndizi hulizidi tunda hili kwa protini kwa angalau mara nne, madini ya wanga au carbohydrates mara mbili , madini ya phosphorus mara tatu, vitamin A, na madini chuma mara tano na mara mbili kwenye vitamin nyingine na madini ni muda wa kubadili ule misemo kuwa apple moja hukuweka mbali na daktari na kusema ndizi moja mbivu hukuweka mbali na daktari na hospitali.

Pia tunazo dawa zilizotengenezwa kutokana na mimea ila zipo katika mfumo wa vidonge. Dawa zetu zinatibu kabisa magonjwa tabia yote kama Kisukari, Presha, Matatizo ya Moyo, Uzazi/mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa, matatizo ya hedhi, upungufu wa nguvu za kiume n.k

Masha Masanja
0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

VYAKULA NA UNENE - SEHEMU YA 3




JINSI VIAMBATA VYA VYAKULA VINAVYOKUPA KITAMBI NA UZITO MKUBWA NA KUKUPA MAGONJWA SUGU

Napenda niwapongeze sana wote mnaoendelea kukombolewa na kupenda Makala zangu. Jitahidi kualika watu wengi.

Basi somo hili la afya nilisema tumeanza na tatizo la uzito mkubwa na baada ya hapo tutaendelea na magonjwa mengine ,mengi. Nimeanza kutoa ushauri wa kuondoa kitambi, uzito mkubwa na kurekebisha sukari yako kama tayari umeshapata kisukari. Basi elimu hii hakikisha iwe ni nguzo yako katika maisha yako kwani hakuna tiba kubwa ya uzito mkubwa kama elimu ya lishe.

Leo napenda tuzungumze kuhusu viambata mbalimbali vinavyozidi kuangamiza afya za binadamu wengi bila kujijua na wengi wao ni wabishi sana sio kwa kutaka bali wameshakuwa walevi wa vyakula hivyo vyenye kemikali. Siku zote tunapokuwa wazima huwa tuna maneno mengi sana ya kujiimarisha kiafya huku ukizidi kuangamiza kwa kutobadili mwenendo wa maisha.

Kuna viambata vingi vya kemikali ambavyo vimo ndani ya vyakula ambavyo tumekuwa tukivipenda na kuvitumia kila siku.

Viambata hivi vinadanganya mwili wako na kuuficha mwili wako kuhusu ukweli ndani yake, kwa kuchanganya vionja radha vya ulimi wako. Leo nitaongelea kimoja baaada ya kingine na madhara yake.

KUMBUKA SINA MAANA UACHE KUVITUMIA LAKINI KAMA UNALINDA AFYA YAKO JITAHIDI KUVIEPUKA

MSG (Monosodium Glutamate)

Hii ni kemikali ambayo inawekwa katika vyakula vingi sana hapa duniani katika vyakula vya kusindika na kuoka vinavyokuja vimeandikwa “low fats” na “Low Calories” na vingine vikiwa katika maboksi na vyenye label mbalimbali. Hii ni sumu hatari sana kwa mwili zaidi ya pombe na kiini kilichopo kwenye sigara nicotin katika mwili wako kiafya. Kiini hiki kiligunduliwa na bwana Kikunae Ikeda mwanasayansi kutoka japani hapo mwaka 1908 na kujulikana kama “Flavor enhancer”.

Kazi kubwa ya MSG ni kudanganya tezi za ulimi wako kuwa kitu ni asili wakati sio kweli, Najua wote mnajua namna gani nyama ikiwekwa katika friji inavyopoteza radha yake na harufu yake, wote tunajua samaki akikaa kwenye friji anavyopoteza radha yake asilia, basi nyama ambazo zimesindikwa/makopo, na vyakula vyote vilivyosindikwa na kuokwa, vyakula viligandishwa kwa muda mrefu kwa milo ya usiku sehemu za mahoteli makubwa kiini hiki kinatumika sana katika kupunguza gharama katika kutunza uasili wa vyakula na kudanganya radha ya vyakula.
Najua umekuwa ukifurahia radha fulani ambayo ni ya uongo baada ya kununua nyama ya kopo, samaki na vyakula vingine vingi vilivyookwa na kusindikwa.

Viini vifuatavyo LAZIMA VINATUMIA MSG hivyo vichunguze vizuri katikula unavyokula:
i. autolyzed yeast
ii. calcium caseinate
iii. gelatin
iv. glutamate
v. glutamic acid
vi. hydrolyzed protein
vii. monopotassium glutamate
viii. monosodium glutamate
ix. sodium caseinate
x. yeast extract
xi. yeast food
xii. yeast nutrient

Vingine ambavyo sio mara zote huwa vina MSG

I. Flavors (vionjo)
II. Seasoning
III. Natural beef flavoring
IV. Natural pork flavoring
V. Soy protein
VI. Citic acid
VII. Whey protein
VIII. Maltodextrin

NOTE: MSG Inakudanganya kuwa chakula unachokula ndicho ladha yake kumbe radha ile imetengenezwa kiwandani.
Unaweza ukawa unakula vyama ambayo imewekwa katika kopo kwa muda mrefu sana lakini ikawa kama nyama iliyochinjwa siku hio hio. Kwani MSG inakudanganya.

KWA NINI MSG INAKUFANYA UWE NA KITAMBI NA UZITO MKUBWA?

Kwanza kama MSG ni SUMU KATIKA NEVA ZA FAHAMU na huathiri kwa kiasi kikubwa neva za fahamu za kwenye ubongo na mfumo mzima wa ufahamu. Tunajuwa kuwa uchovyaji wa homoni za kuratibu chakula huongozwa kwa kiasi kikubwa na ubongo na mfumo wa fahamu kiujumla. Nadhani umeshawahi kuona unaweza ukala chakula fulani ukashiba sana lakini baada ya muda kidogo tu unapata njaa unahitaji mfuko mwingine wa chakula.

Hii ni ishara kuwa leptin ambacho ni kichocheo ambacho hutolewa na seli zinahifadhi mafuta baada ya mamlaka kutoka kwenye ubongo, Leptin huenda kuwaambia ubongo tena kuwa umetosheka na umeshiba. Maana yake leptin ikishindwa kufanya kazi haipo siku utajisikia umeshiba. Watu wengi wenye uzito mkubwa wana kizuizi cha utendaji wa leptin ( Leptin Resistance) hivyo huwa wanakula sana na kila mara njaa inakuuma. Hii yote inaweza kusababishwa na ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi na ulaji wa vyakula vyenye vionjo vyenye kemikali nyingi kama MSG.
Hivyo basi MSG imekuwa ikiwekwa sehemu mbali mbali ya vyakula. Hii ni kwa sababu inaweza kumfanya mtu akawa mlevi wa chakula fulani kupita kiasi ( Addicted) na wote wenye viwanda wanapenda kutumia ili uendelee kukipenda kukuza biashara yake.

“USISEME KITAMU,JIULIZE KWA NINI NI KITAMU”?

TAFAKARI❗❗

Hivi umeshawahi kujiuliza kila kukicha tafiti mbalimbali zinafanyika kuoanisha uzito na magonjwa mbalimbali kama presha, uvimbe kwenye kizazi, kisukari nk wanatumia nini? Mara nyingi hutumia panya katika maabara ambao wana kitambi, je unafikiria hawa panya wanawakuta wakiwa na kitambi? HAPANA, Hilo halipo na halitakuja kutokea.
Panya wa majaribio kujaribu kuonisha Uzito na kitambi hupatikana kwa kuchomwa MSG na kusababisha homoni ya insulin kupanda juu, na kuanza kuhifadhi mafuta na hatimaye kuleta kitambi. Huu ni mfano, dhahiri kuwa namna gani MSG inavyoweza kukutengenezea kitambi na kukusababishia insulin kutofanya kazi na leptin kutofanya kazi ukaishia kuwa na uzito mkubwa na ulaji hovyo wa vyakula bila kujizuia na bila kukata hamu ya chakula.

KESHO NITAWALETEA HATUA ZA KUANZA SAFARI MPYA NA MAISHA MAPYA YA BILA KITAMBI NA UZITO MKUBWA.

❗Nitakupa maboresho ambayo unatakiwa uyafanye ufike unapotaka kiafya katika kupunguza uzito wako

❗Nitakufundisha namna gani unaweza kupangilia mlo wako wewe mwenyewe bila uwepo wako

❗Namna gani unaweza kuhakikisha uzito wako hauongezeki na kuendelea kuwa na umbo unalotaka na kufurahia mavazi yako

Basi usisahau kushare na rafiki yako dondoo zangu hizi za afya.

Hakikisha unakaribisha marafiki zako wengi kuanza kutembelea ukurasa wangu facebook unaitwa "Masha Nutrition Health Care"

Blog: www.mashahealth.blogspot.com

Mawasiliano
0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

Tuesday, 8 December 2015

UGONJWA WA NGIRI(HERNIA)




NAMNA AMBAVYO MTU ANAPATA UGONJWA WA NGIRI (HERNIA)

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni:
-Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla.
-kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu.
-ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa .
Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Mawasiliano
0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

MADHARA YA VYAKULA & UNENE - SEHEMU YA 2

SEHEMU YA PILI:

KWA NINI UNA KITAMBI NA UZITO MKUBWA
BADILI MWILI WAKO KUWA MASHINE INAYOUNGUZA MAFUTA

Napenda tena kukukaribisha mpendwa msomaji wa Makala zangu za afya, nimekuwa nikipewa shukrani nyingi sana na wasomaji wangu jinsi gani walikuwa wakipotoka kuhusu lishe katika jambo zima la kupunguza uzito. Ninapenda pia kuchukua nafasi hii kuwapongeza na kuwaomba tuendelee kuwashauri watu wengi waungane nasi katika jukwaa hili la Makala za afya zilizosheheni maarifa yaliyofanyiwa tafiti za kutosha usisahau kuungana nami facebook kwa kubofya LIKE kwenye ukurasa wangu "Masha Nutrition Health Care".

Basi baada ya jana kujikita sana kuongelea vyakula vya wanga na namna ya kupunguza uzito kwa kupunguza wanga siku ya leo napenda kuengelea kwa upana Zaidi kuhusu VYAKULA VYA MAFUTA NA MAZOEZI mchango wake katika kupunguza uzito.

FIKRA POTOFU NO 1:
ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA VINAKUFANYA UWE NA KITAMBI NA UZITO MKUBWA
Kwanza kabisa napenda tu kuwaambia wote wenye kupenda kupunguza uzito. Najua lengo lenu sio kupunguza uzito lakini ni kuunguza mafuta ili nguo mnazotamani kuzivaa ziweze kuwapendeza na muwe wenye kuvutia. Lakini swala la kuunguza mafuta linaendana na kuboresha afya wapendwa ili mwili wako uzidi kufanya kazi katika uhalisia wake. Kwani ingekuwa lengo lako ni kuunguza mafuta tu,ungeweza kujinyima kula na ukapungua uzito tena ndani ya mwezi tu. Lakini sikushauri kwani utapata maradhi mengi kuzidi matokeo unayoyataka.
Sasa basi ukitaka kupunguza mafuta yako na utimize malengo lazima ufuate ushauri huu ninao kwambia kwani utatimiza malengo yako na afya yako itabaki imara kabisa.

Ingekuwa ulaji wa vyakula vya mafuta unanenepesha basi wale wote ambao majokofu yao majumbani yamejaa vyakula vilivyo andikwa “Low fat”, “Fat Free” wangekuwa umetimiza malengo yao ya kutokuwa na kitambi na uzito mkubwa. Ingawaje wanatumia vyakula vya namna hii bado ongezeko kubwa la matatizo haya ya kitambi na uzito mkubwa yanalikabili taifa kwa ongezeko kubwa sana.
Je unafikiri vyakula vyenye Fat free, No fats vilivyopo katika maduka makubwa ya vyakula vina msaada wowote?
Chochote unachokula kinatoa tafsiri ya jinsi gani mwili ufanye kazi ili uweze kuunguza mafuta, hivyo wewe ndiye mwenye maamuzi. Kitendo cha kutaka kupunguza uzito unatakiwa ujiwekee malengo yako na uyafuate bila kuyapuuza kwani kupunguza uzito ni kazi Zaidi ya kutafuta pesa inahitaji uvumilivu na maamuzi ya kuthubutu ndio maana wengi wameridhika na kuanza kujipotosha kuwa ni wakurithi.
“FAT ISN’T OUR PROBLEM,SUGAR IS”
Tatizo sio mafuta tatizo ni vyakula vinavyotoa sukari nyingi katika damu yako pale unapoviingiza mwilini mwako.

Tangu pale watu walipokuwa wakisumbuka na kiwango kikubwa cha cholesteral na shirika la afya duniani kutoa tamko kupunguza kiwango cha cholesteral mwilini kwa kuepuka vyakula vya mafuta. Basi watu walihamisha mtazamo wao katika aina hizo ya vyakula na kuanza kula vyakula ambavyo vina kiwango kingi cha sukari na vyakula vya wanga vilivyosindikwa na kuwekwa kwenye makopo na vibebeo mbali mbali zikiwa na maandishi ya kibiashara. Watu tumekuwa tukijaza aina hivi ya vinywaji majumbani na vyakula vya namna hii kama mikate, biscuts, chokoleti, sambusa nk hiki ndicho chanzo cha tatizo hili kuongezeka kwa kiwango kikubwa kiasi hiki na kupelekea watu kuugua magonjwa mbalimbali kama kisukari, shinikizo la damu, upungufu wa nguvu za kiume, vimbe kwenye kizazi n.k

UKWELI UPO WAPI KUHUSU MAFUTA?
Katika dunia ya lishe tuna mafuta mazuri na mafuta mabaya, mafuta mazuri ndio yanayoshauriwa kutumika kwa wingi kwa watu wanaotaka kupunguza uzito. Na chakushangaza watu wote wenye uzito mkubwa wanaogopa aina zote za mafuta! Sasa je utapunguaje? Mafuta mazuri siku zote huwa nayaita HEALTHY FATS! Tumia mafuta haya kwa wingi upate faida zifuatazo.
1. Unapokula chakula chenye wanga kidogo na mafuta mazuri kiafya mengi unaufundisha mwili kuanza kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili
2. Pale wanga inapokuwa imeshatumika kuwa nishati ya mwili na kuisha basi mwili utaanza kuunguza mafuta

ZINGATIA
Tafiti zinaonesha kwamba kati ya chakula cha wanga na mafuta mazuri, chakula cha wanga husababisha kupanda kwa kiwango cha insulin (homoni inayo hifadhi sukari iliyozidi katika mfumo wa mafuta ) kwa kiasi kikubwa wakati chakula cha protein kinafuatia na chakula cha mafuta kimeonesha kiwango cha insulin kuwa katika kiwango maalumu muda wote. Tafiti hizi zilifanywa kwa kutumia GTT (Glucose Tolerance Test) kipimo kinaonesha namna gani mwili wako una uwezo wa kuhimili kiasi fulani cha sukari mwilini.

Hivyo basi unapokuwa unatumia vyakula vyenye mafuta mazuri vinakusaidia kuujenga mwili kuanza kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili kukupatia nguvu na pia inapunguza kiwango cha insulin kinachotolewa na kongosho kuja kusawazisha sukari maana vyakula hivi vimeonesha kutoongeza sukari kwa wingi kwenye damu na hivyo basi hakuna mafuta yatakayo hifadhiwa sehemu yoyote na badala yake mwili utaanza kuyaunguza mafuta yaliyo hifadhiwa.

JE UMESHAWAHI KUFIKIRIA UNAHITAJI KIWANGO GANI CHA SUKARI MWILINI UWEZE KUISHI?
Mwili wa binadamu unastahimili kiwango cha sukari chini ya 100mg/dl au 7mmol/l ya damu. Hivyo basi kwa sababu binadamu ana kiwango cha kadirio la lita 5 ya damu ukitaka kupata kiwango gani cha sukari kinahitajika katika lita moja katika kipimo cha gramu utafanya kama ifuatavyo.
1litre=1000mg/litre
Katika lita 5 =5000mg ambayo ni sawa na gramu 5.

Tunakadiria kuwa gramu 5 ni sawa na kijiko kimoja cha sukari. ( hiki ni kiwango cha kawaida ukiwa hujala chochote)
Baada ya kula chakula chako, labda kijiko kimoja cha wali, sukari yako itapanda hadi vijiko 10.

Umeona jinsi gani tunavyo hitaji kiwango kidogo cha sukari kinachoweza kutufanikisha tuishi na tusiwe na nyama uzembe? Hili unaweza kuliepuka kwa kupunguza wanga katika mlo wako na kuongeza mafuta mazuri ,mboga za majani na matunda kwa wingi bila kusau protein

JE KATIKA KIWANGO GANI?
Wengi huwa wanapenda kuniambia watumie vyakula gani kuanzia asubuhi hadi jioni lakini hili linakunyima uhuru wako wa kuchagua chakula cha namna gani katika kundi lile lile utumie kulingana na unavyojisikia siku hiyo. Ndio maana natoa elimu hii yote ili uweze kupangilia mwenyewe. Hebu zingatia hili

ULAJI MBAYA KATIKA SAHANI YAKO KAMA UNAHITAJI KUPUNGUZA UZITO
Wanga; 48.7%
Protein: 15.7%
Mafuta au Fats: 33.7%
Umeona jinsi gani watu walivyo na fikra potofu kuhusu lishe, wanga ni nyingi kwani wanajua ndio chanzo kikubwa cha nishati ya mwili na woga wa kutumia mafuta. Kadri wanga inavyozidi kiwango,ndivyo sukari nyingi itahifadhiwa kama mafuta tumboni,kifuani,mgongoni na kiunoni pia kwenye ini ( Fat liver).

Kadri sukari inavyozidi kuwa juu ndivyo homoni ya insulin inavyozidi kupanda kuja kufanya kazi yake ya kuhifadhi sukari iliyozidi.

ULAJI MZURI WA SAHANI YAKO KAMA UNAHITAJI KUPUNGUZA UZITO
Wanga: Asilimia 10-15
Protini : Asilimia 15-20
Fats (mafuta mazuri): Asilimia 65-75
Ukingalia katika takwimu hizo utajua kuwa hesabu hazidanganyi, kadri unavyozidi kuimarisha mlo wako kuweka mafuta mazuri mengi na kupunguza wanga. Unaufanya mwili wako kuwa na kiwango sawia cha insulin na hakuna mafuta yatakayo hifadhiwa kwani hakuna sukari iliyozidi. Na mwili wako utaujengea mazoea ya kuanza kutumia mafuta kama nishati baada tu ya sukari kuisha na hapo ndipo mwili wako utabadilika kuwa mashine inayounguza mafuta na kadri siku zinavyokwenda utashitukia tumbo linapungua na nyama uzembe kupungua na hatimaye kuisha na kuboreka kwa afya yako.

ZINGATIA: Watu wengi husema kuwa mazoezi ndio suluhisho la uzito mkubwa, ni kweli napenda kukubaliana nao kabisa, lakini nimekuwa nikipokea taarifa za watu ambao wamejitahidi sana kufanya mazoezi katika gym za kisasa bila mafanikio na wameridhika na uzito huo. Hii ni kwa sababu unaweza kupungua kupitia mazoezi endapo ukiwa mvumlivu kwani itakuchukua muda mrefu sana sivyo kama unavyofikiria na kutaka matokeo yatokee pale pale.

Siku zote mazoezi katika stesheni za gym huimarisha mwili na kukukinga na magonjwa tu, lakini JIKONI NDIO KUNA SULUHISHO LA UZITO MKUBWA. Lishe iwe ndio ngao yako ya kwanza na sio mazoezi. Hii ndio maana nimekuwa nikikutana na wahudhuriaji wazuri wa gym lakini bado wanasumbuka na kuvurugika kwa homoni na uzito kutoshuka.

Baada ya mada hii basi siku zijazo nitajibu swali lako Je ni vyakula gani tunaweza kula vina mafuta mazuri na vyakula gani vina wanga kidogo tunaweza kula kuendana na utaratibu wa LOW CARBOHYDRATES HIGH FAT DIET PROGRAM itakayolenga kukusaidia kufikia malengo yako.
Kama una maswali yatunze yote nitayajibu kwa Makala zangu zijazo kupitia ukurasa wangu wa facebook "Masha Nutrition Health Care" jaribu kujumuika nasi upate elimu hii bure.

Mawasiliano
0784925000
0622925000 whatsapp
0767925000
posted from Bloggeroid

Monday, 7 December 2015

SOMO MAALUMU KUHUSU VYAKULA & UNENE. SEHEMU YA 1

 KWA NINI UNA UZITO MKUBWA NA KITAMBI?

JINSI YA KUUFANYA MWILI WAKO KUWA MASHINE INAYOUNGUZA MAFUTA

Kwa mwenendo mzuri wa maisha utakayoishi nayo unaweza kuubadili mwili wako kuanzia leo kuwa mashine inayounguza mafuta bila hata kuwa unahangaika kutumia bidhaa za kupunguza uzito zenye gharama kubwa zinazokuweka na kukubakiza mifuko iliyotoboka kwa kutumia ushauri huu hapa leo.
Watu wengi wamekuwa wakitumia bidhaa mbalimbali za kupunguza uzito lakini baada ya muda fulani uzito unakuja kuongezeka kwa kasi sana na kurudia hali yako ya mwanzo. Hivyo hii inaonesha kuwa mbali na matumizi ya bidhaa hizo za kupunguza uzito uwe na elimu hii ambayo itakusaidia maishani mwako daima.

FIKRA POTOFU 1
Watu wengi tunajua na tunashauriwa na baadhi ya vyakula vimeainisha kiwango cha sukari (kalori) ambazo unatakiwa utumie kwa siku moja. Basi watu wengi wamekuwa wakijitahidi kuhesabu na kujinyima kiwango kingi cha kalori kwa kutumia vyakula vyenye kiwango kidogo ili kuweza kuepukana na uzito mkubwa. Nimekuwa nikikutana na vinywaji vimeandikwa ‘ Kiwango maalumu cha kalori” na vyakula vingine vimeandikwa ” low fats” chakushangaza karibia vinywaji vingi vimeandikwa hivyo na watu wanajichunga sana kwani wanajua nini maana ya maneno hayo, LAKINI BADO SUALA LA UZITO MKUBWA NI CHANGAMOTO.

Ina maana kuwa siri nyingine ambayo wewe unatakiwa kuijua kuhusu mwili wako ndipo uweze kulinda uzito wako kiafya.
Usemi huo ni mzuri kuwa tule vyakula vyenye mafuta kidogo na vyakula vyenye kiwango fulani cha kalori, lakini usemi huo unatumika sana PALE VICHOCHEO VYA MIILI YETU VINAPOKUWA KATIKA USAWA (NORMAL RANGE) hapo ndipo mwili utakuwa katika utendaji wake kiuhalisia. Lakini kutokana na miili yetu imekuwa ikipata misuko suko mingi kiafya kuanzia kwenye vyakula tunavyokula, hewa tunayovuta na vyote tunavyoweka juu ya ngozi homoni za kutumia mafuta zimevurugika na ule usemi wa mafuta kidogo na kalori chache upungue uzito hautatumika tena.

Inatakiwa tushughulikie mwili uanze kuunguza mafuta pale vichocheo vyetu vinapokuwa vimevurugika na uzito unaongezeka kila siku.
“Tunapozungumzia viwango vya homoni mwilini, vitu vingi vinaweza kusambaratisha homoni zako na kusababisha kupoteza uwezo wa mwili wako kuunguza mafuta mwilini, kama msongo wa mawazo,hasira nyingi,kiwango sahihi cha usingizi, mazoezi yako na mengineyo, Lakini MLO SAHIHI ndio kiini pekee cha kukuwezesha kupungua uzito kwa kuunguza mafuta, kwani kiwango cha homoni mwilini mwako kinategemea sana MLO SAHIHI KIAFYA.

Kitendo cha watu wengi kuhesabu kiasi cha kalori kinaweza kukufanya ukafurahia kupungua kwa kilo mwanzoni na ukafurahia zoezi hilo, LAKINI kimwenendo wa mwili wako zoezi hilo halitaendelea hivyo hivyo milele mwili baadae hubadili mtazamo na hii ndio sababu watu wengi ambao ni wazuri sana wa kuhesabu kalori wanazotumia kwa siku huishia kutoona matokeo baada ya muda flani.

FIKRA POTOFU 2:
UZITO NI WAKURITHI

Watu wengi tumekuwa tukikutana na maelezo mengi sana kuhusu kurithi kwa magonjwa kutoka kwa wazazi wetu kupitia Genes (vibeba taarifa) au DNA.

Ukipata kisukari, utaambiwa umerithi DNA za kisukari kwa wazazi wako kama kilikuwepo

>Ukipata Kansa utaambiwa umerithi Gene au DNA za kisukari kutoka kwa wazazi wako
>Ukipata Shinikizo la damu na uzito mkubwa utaambiwa umerithi kutoka kwa wazazi wako.
IMEKUWA NI KURITHI GENES,KURITHI GENES,KURITHI GENES kila ugonjwa na watu tunafurahia kutamkiwa kurithi huku na kutofikiria Zaidi namna gani unaweza kuikinga familia yako na vizazi vyako.
Hebu soma hiki kitu,
“Ukweli ni kwamba VINA SABA (DNA)/GENES hazijawahi kubadilika takribani miaka 40,000 hadi sasa. Lakini umekuwa ukiona ongezeko kubwa la magonjwa kama kisukari,shinikizo la damu,uzito mkubwa anavyoendelea kushambulia binadamu hadi sasa. Swali la kujiuliza kama tumerithi magonjwa haya mbona enzi hizo hakukuwa na magonjwa mengi kiasi hiki na watu wengi wenye matatizo kama haya?
Kwa nini sasa unaendelea kuzilaumu GENES au DNA za urithi kila siku? Tafuta chanzo kuanzia leo”

NOTE: Ni asilimia 0.01% ya magonjwa yanayofikirika kuwa ni magonjwa yakurithi na miongoni mwa hayo UZITO MKUBWA SIO MIONGONI MWAO.

Tafakari! Hivyo fikra potofu kuwa uzito ni wakurithi unakukosesha uwezo mpana na kubaini tatizo kwa kutafuta taarifa Zaidi za tatizo lako.

“ The best way to lose weight is to Get healthy” Hivyo basi lishe sahihi ni muhimu na nguzo kubwa sana katika safari yako kiafya.
Ni kweli inaweza kuwa genes/DNA za urithi zina mchango kiasi katika kukufanya uzito uwe mkubwa lakini sio kwa mtizamo wako.

Uzito mkubwa unasababishwa na kuishi maisha ambayo yanapingana na uhalisia wa mazingira ya seli za mwili zilivyotengenezwa kufanya kazi katika uhalisia flani. Hivyo basi chochote unachoweka ndani ya kinywa chako kinaenda kubadili uhalisia wa mwili wako kufanya kazi na hatimaye kuishia kupata madhara mbalimbali ya kiafya.

KWA NINI UNAKUWA NA KITAMBI AU NYAMA UZEMBE
Katika miili yetu kuna makundi makundi makuu mawili ya lishe
1. MACRO –NUTRIENTS
Hizi ni molekyuli kubwa za lishe kama WANGA,PROTINI, MAFUTA NA POMBE.
Mwili unapokuwa unahitaji nishati huanza kwanza kutumia wanga, na unapokuwa umepungukiwa wanga unatumia Mafuta( Fats) na mwisho hutumia Protein wakati kama hakuna vyanzo vingine vyote vya nishati

2. MICRO-NUTRIENTS
Hizi ni molekyuli ndogo za lishe ambazo hujumuisha madini yote na vitamin zote. Madini kama zinc,selenium manganese, Chuma nk na vitamin kama vitamin A,B,C,D,E K nk


SABABU KUU MBILI KWA NINI UNAPATA KITAMBI
Baada ya kuona mchanganuo wa lishe kwa upana hebu sasa kabla sijasema sababu ya kwa nini uzito wako unaongezeka kila siku na hupati suluhisho.
“ Ukitaka kutibu tatizo lolote la magonjwa yanayosababishwa na lishe kuzidi,kupungua au usahihi wake basi angalia chimbuko la tatizo kuanzia kwenye molekyuli za chakula na seli za mwili zinavyofanya kazi, utalibaini tatizo na kulipatia ufumbuzi wa moja kwa moja ndicho ambacho nataka ujifunze leo”

SABABU YA KWANZA:
Kukosa taalamu sahihi ya lishe kamili kwa mtu mwenye tatizo la uzito mkubwa au kitambi, kwani wengi tumekuwa tukitumia ushauri ambao sio sahihi na hatimaye kuishia kuongezeka uzito.
Ulaji wa kiwango kikubwa cha wanga ni chanzo kikubwa sana cha wewe uzito kuwa mkubwa kila kukicha!
Kwani chakula cha wanga chote hubadilishwa kwenye damu na kuwa sukari (glucose) ili tuweze kupata nishati ya mwili kuendesha shughuli za mwili.
Kadri kiwango cha wanga kinavyozidi kuwa kikubwa katika mlo wako, ndivyo kiwango kikubwa cha sukari kitakachozalishwa kwenye mzunguko wa damu.
Miili yetu ina tabia ya kutokubali kupoteza chanzo cha nishati ya mwili yaani glucose hovyo, hivyo baada ya kiwango kuwa kingi sana mwili unachovya maji kutoka kwenye kongosho yaitwayo Insulin. Maji haya ni homoni ambayo hutolewa kwa lengo la kuja kuhifadhi sukari kwa matumizi ya baadae (sio kupunguza sukari kama wengi tunavyojua) kupungua kwa sukari kwenye damu ni matokeo ya kazi ya insulin hili wengi hupotosha!

NAMNA GANI INSULIN INAPUNGUZA SUKARI?
Insulini inafanya kazi kubwa ya kubadili sukari iliyozidi kiwango kuwa mafuta kwa kiwango kikubwa na kuhifadhi mafuta haya katika sehemu za kuhifadhia mafuta kama kiunoni,kifuani,mgongoni,tumboni,kwenye mikono nk.
Hivyo basi homoni ya insulin ni homoni ambayo ningependa kusema ni FAT STORING HORMON
>Kadri kiwango cha wanga kinavyoongezeka ndivyo kiwango cha sukari kinavyo ongezeka
>Kadri kiwango cha sukari kinavyoongezeka ndivyo kiwango kikubwa cha insulin homoni kitatolewa kwenda kupunguza kiwango kwa kuhifadhi kwa matumizi ya baadae
>Kadri Kiwango kingi cha insulin kilivyo juu ndivyo kiwango kingi cha mafuta kitahifadhiwa sehemu maalumu kama kiunoni,tumboni,mikononi,mgongoni nk

Nadhani umenielewa jinsi gani mwili wako unashugulika na kiwango kingi cha wanga mwilini mwako!


MASWALI YA KUJULIZA
SWALI NO 1.
Je ulaji wa nafaka ambayo haijakobolewa kunapunguza kiwango cha sukari inayozalishwa kwenye damu baada ya wanga kutumika kutengeneza glucose kwenye damu? Hapana!

SWALI NO 2.
Je kama kwenye nafaka ambayo haijakobolewa kina kiwango kingi cha fiber ( Nyuzi), jiulize hizo nyuzi zinapunguza kiwango cha sukari kitakacho tengenezwa baada ya kiwango flani cha wanga kutumika? Hapana! Kwani moja ya kazi kubwa ya fibers kwenye kupunguza uzito ni kupunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula na kukufanya ukae muda wote unajisikia umeshiba! Lakini kumbuka kuna aina zingine za vyakula vyenye fibers nyingi ambavyo vinakiwango kidogo sana cha wanga! Kwa nini hufukirii hilo?

Watu wengi wanaopenda kula kiwango kikubwa cha wanga na vyakula vingine vya wanga na sukari vilivyo andaliwa viwandani kama mikate,biskuti,chokoleti na vinywaji vyenye sukari,vionjo,rangi na kemikali za kuhifadhia vinywaji vyakula vinavyokuja wana matatizo yafuatayo:

1. Wote ni wanene kupita kiasi
2. Wote muda mwili hujisikia wachovu( kusinzia hovyo)
3. Hawawezi kufuata mpangilio wa mlo (over eating)
4. Matunda na mboga mboga haziwezi kuwakatia kiu ya njaa
5. Wanafikiria kachumbali ya matunda na mboga za kijani sio chakula sahihi kwao wao wanahitaji kula chakula kizito kuweza kushinda bila njaa
6. Muda mwingi hujisikia wenye njaa na hupenda kula sana vitu vitamu vitamu na hawawezi kujizuia wanaona kama mateso


UNAJITAMBUAJE WEWE UMEATHIRIWA NA KIWANGO KINGI CHA WANGA?
Unaweza kufanya zoezi hili hata ukiwa nyumbani kwako, chukua mchemsho wa samaki (protein), kachumbari ya mboga za majani ( Asparagus,cauliflower, spinach, kabeji,sukuma wiki) na Tango pembeni katakata. Baada ya muda mchache tu utajiskia kama vile hujala chochote kabisa! Pole kama umekumbwa na tatizo hilo, na hongera kama hujakuta tatizo hilo endelea kupata mlo sahihi kwa kutumia elimu hii.

SABABU YA PILI KWA NINI UNA UZITO MKUBWA NA KITAMBI
Moja ya sababu kubwa watu wengi wamekuwa wakifanya mazoezi mengi katika gymes mbalimbali na wamekuwa wakijitahidi kufanya mazoezi mengi na kuishia kuumia viungo vya mwili bila kiu yao ya kupunguza uzito kukatika. Hii ni kwa sababu ya upungufu wa madini na vitamin mwilini mwako.
Madini kama manganese na selenium yanafanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha shughuli za mwili zinafanyika katika kiwango kinachostahiki. Hivyo basi endapo kuna upungufu wa madini kama haya pamoja na baadhi ya vitamin muhimu mwili wako hauwezi hata kuunguza mafuta katika kiwango kinachotakiwa maana shughuli zote zinakuwa zinafanyika katika kiwango cha chini sana.
KWANINI INAWEZEKANA UNA UPUNGUFU WA MADINI NA VITAMIN KWA SABABU YA UZITO MKUBWA?
Nimeongelea kuhusu vyakula vya wanga jinsi gani vinavyoathiri utendaji kazi wa mwili wako endapo unapokuwa unatumia wanga katika kiwango kikubwa sana kupita kiasi. Kiwango kikubwa cha madini na vitamin kinapatikana katika matunda na mboga za kijani. Sasa watu wengi wenye uzito mkubwa nimeeleza kuwa kiu yao huwa haikatwi na vyakula kama matunda na mboga za majani wengi hupenda kusema kuwa wanastahili chakula kizito kuweza kuhimili miili yao hadi kesho (Ndio maana atatumia viazi vya kukaanga na soda pembeni amejitahidi sana juisi iliyotengenezwa masaa kumi yaliyopita sio fresh imemaliza vitamin zote kwani vitamin huwa zina athiriwa kiurahisi sana na joto na mwanga hivyo juisi ya tiba inahitaji uhifadhi maalumu kama usipoinywa pale pale baada ya kuitengeneza)
Hivyo basi nadhani umeona kwa nini uzito wako unazidi kuongezeka bila sababu kwa sababu tu ya kukosa vitamin na madini mwilini mwako bila hiari yako ni kwa sababu homoni zako zimevurugika kwa sababu ya ulaji mbovu zinakulazimu kupenda vyakula fulani ambavyo vinazidi kupeleka afya yako pabaya.

Basi ningependa kukomea hapa kwa siku ya leo, bali kitu ambacho unatakiwa ujifunze ni kwamba tupunguze kiwango cha wanga katika sahani unayo weka mezani kwako, asilimia 75 ziwe mboga za kijani, protini, fats na matunda na asilimia 15 iwe wanga. Pia tuache kuogopa neno FATS (MAFUTA) kwani hili neno kila mtu huwa ananiambia sasa hivi nimeacha kabisa mafuta, kesho nitaeleza namna gani unaweza kuufanya mwili wako kuwa mashine inayounguza mafuta na ukapunguza uzito kwani watu hatujui hata umuhimu wa mafuta mazuri katika kuunguza mafuta na kuondoa kitambi.
Napenda tu niendelee kuwapongeza wote mnaoendelea kufuatilia Makala zangu, hebu endelea kuwakaribisha watu wengine waweze kutufuatilia katika jukwaa letu la afya utafurahia mada yangu ijayo ambayo nitairusha kwenye group blog hii. 

UNGANA NAMI KATIKA MAKALA IJAYO NITAKAYOJIKITA KUONGELEA NAMNA YA KUPANGILIA AINA YA VYAKULA VYAKO

MAWASILIANO:
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid