Wednesday, 9 December 2015

VYAKULA NA UNENE - SEHEMU YA 3




JINSI VIAMBATA VYA VYAKULA VINAVYOKUPA KITAMBI NA UZITO MKUBWA NA KUKUPA MAGONJWA SUGU

Napenda niwapongeze sana wote mnaoendelea kukombolewa na kupenda Makala zangu. Jitahidi kualika watu wengi.

Basi somo hili la afya nilisema tumeanza na tatizo la uzito mkubwa na baada ya hapo tutaendelea na magonjwa mengine ,mengi. Nimeanza kutoa ushauri wa kuondoa kitambi, uzito mkubwa na kurekebisha sukari yako kama tayari umeshapata kisukari. Basi elimu hii hakikisha iwe ni nguzo yako katika maisha yako kwani hakuna tiba kubwa ya uzito mkubwa kama elimu ya lishe.

Leo napenda tuzungumze kuhusu viambata mbalimbali vinavyozidi kuangamiza afya za binadamu wengi bila kujijua na wengi wao ni wabishi sana sio kwa kutaka bali wameshakuwa walevi wa vyakula hivyo vyenye kemikali. Siku zote tunapokuwa wazima huwa tuna maneno mengi sana ya kujiimarisha kiafya huku ukizidi kuangamiza kwa kutobadili mwenendo wa maisha.

Kuna viambata vingi vya kemikali ambavyo vimo ndani ya vyakula ambavyo tumekuwa tukivipenda na kuvitumia kila siku.

Viambata hivi vinadanganya mwili wako na kuuficha mwili wako kuhusu ukweli ndani yake, kwa kuchanganya vionja radha vya ulimi wako. Leo nitaongelea kimoja baaada ya kingine na madhara yake.

KUMBUKA SINA MAANA UACHE KUVITUMIA LAKINI KAMA UNALINDA AFYA YAKO JITAHIDI KUVIEPUKA

MSG (Monosodium Glutamate)

Hii ni kemikali ambayo inawekwa katika vyakula vingi sana hapa duniani katika vyakula vya kusindika na kuoka vinavyokuja vimeandikwa “low fats” na “Low Calories” na vingine vikiwa katika maboksi na vyenye label mbalimbali. Hii ni sumu hatari sana kwa mwili zaidi ya pombe na kiini kilichopo kwenye sigara nicotin katika mwili wako kiafya. Kiini hiki kiligunduliwa na bwana Kikunae Ikeda mwanasayansi kutoka japani hapo mwaka 1908 na kujulikana kama “Flavor enhancer”.

Kazi kubwa ya MSG ni kudanganya tezi za ulimi wako kuwa kitu ni asili wakati sio kweli, Najua wote mnajua namna gani nyama ikiwekwa katika friji inavyopoteza radha yake na harufu yake, wote tunajua samaki akikaa kwenye friji anavyopoteza radha yake asilia, basi nyama ambazo zimesindikwa/makopo, na vyakula vyote vilivyosindikwa na kuokwa, vyakula viligandishwa kwa muda mrefu kwa milo ya usiku sehemu za mahoteli makubwa kiini hiki kinatumika sana katika kupunguza gharama katika kutunza uasili wa vyakula na kudanganya radha ya vyakula.
Najua umekuwa ukifurahia radha fulani ambayo ni ya uongo baada ya kununua nyama ya kopo, samaki na vyakula vingine vingi vilivyookwa na kusindikwa.

Viini vifuatavyo LAZIMA VINATUMIA MSG hivyo vichunguze vizuri katikula unavyokula:
i. autolyzed yeast
ii. calcium caseinate
iii. gelatin
iv. glutamate
v. glutamic acid
vi. hydrolyzed protein
vii. monopotassium glutamate
viii. monosodium glutamate
ix. sodium caseinate
x. yeast extract
xi. yeast food
xii. yeast nutrient

Vingine ambavyo sio mara zote huwa vina MSG

I. Flavors (vionjo)
II. Seasoning
III. Natural beef flavoring
IV. Natural pork flavoring
V. Soy protein
VI. Citic acid
VII. Whey protein
VIII. Maltodextrin

NOTE: MSG Inakudanganya kuwa chakula unachokula ndicho ladha yake kumbe radha ile imetengenezwa kiwandani.
Unaweza ukawa unakula vyama ambayo imewekwa katika kopo kwa muda mrefu sana lakini ikawa kama nyama iliyochinjwa siku hio hio. Kwani MSG inakudanganya.

KWA NINI MSG INAKUFANYA UWE NA KITAMBI NA UZITO MKUBWA?

Kwanza kama MSG ni SUMU KATIKA NEVA ZA FAHAMU na huathiri kwa kiasi kikubwa neva za fahamu za kwenye ubongo na mfumo mzima wa ufahamu. Tunajuwa kuwa uchovyaji wa homoni za kuratibu chakula huongozwa kwa kiasi kikubwa na ubongo na mfumo wa fahamu kiujumla. Nadhani umeshawahi kuona unaweza ukala chakula fulani ukashiba sana lakini baada ya muda kidogo tu unapata njaa unahitaji mfuko mwingine wa chakula.

Hii ni ishara kuwa leptin ambacho ni kichocheo ambacho hutolewa na seli zinahifadhi mafuta baada ya mamlaka kutoka kwenye ubongo, Leptin huenda kuwaambia ubongo tena kuwa umetosheka na umeshiba. Maana yake leptin ikishindwa kufanya kazi haipo siku utajisikia umeshiba. Watu wengi wenye uzito mkubwa wana kizuizi cha utendaji wa leptin ( Leptin Resistance) hivyo huwa wanakula sana na kila mara njaa inakuuma. Hii yote inaweza kusababishwa na ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi na ulaji wa vyakula vyenye vionjo vyenye kemikali nyingi kama MSG.
Hivyo basi MSG imekuwa ikiwekwa sehemu mbali mbali ya vyakula. Hii ni kwa sababu inaweza kumfanya mtu akawa mlevi wa chakula fulani kupita kiasi ( Addicted) na wote wenye viwanda wanapenda kutumia ili uendelee kukipenda kukuza biashara yake.

“USISEME KITAMU,JIULIZE KWA NINI NI KITAMU”?

TAFAKARI❗❗

Hivi umeshawahi kujiuliza kila kukicha tafiti mbalimbali zinafanyika kuoanisha uzito na magonjwa mbalimbali kama presha, uvimbe kwenye kizazi, kisukari nk wanatumia nini? Mara nyingi hutumia panya katika maabara ambao wana kitambi, je unafikiria hawa panya wanawakuta wakiwa na kitambi? HAPANA, Hilo halipo na halitakuja kutokea.
Panya wa majaribio kujaribu kuonisha Uzito na kitambi hupatikana kwa kuchomwa MSG na kusababisha homoni ya insulin kupanda juu, na kuanza kuhifadhi mafuta na hatimaye kuleta kitambi. Huu ni mfano, dhahiri kuwa namna gani MSG inavyoweza kukutengenezea kitambi na kukusababishia insulin kutofanya kazi na leptin kutofanya kazi ukaishia kuwa na uzito mkubwa na ulaji hovyo wa vyakula bila kujizuia na bila kukata hamu ya chakula.

KESHO NITAWALETEA HATUA ZA KUANZA SAFARI MPYA NA MAISHA MAPYA YA BILA KITAMBI NA UZITO MKUBWA.

❗Nitakupa maboresho ambayo unatakiwa uyafanye ufike unapotaka kiafya katika kupunguza uzito wako

❗Nitakufundisha namna gani unaweza kupangilia mlo wako wewe mwenyewe bila uwepo wako

❗Namna gani unaweza kuhakikisha uzito wako hauongezeki na kuendelea kuwa na umbo unalotaka na kufurahia mavazi yako

Basi usisahau kushare na rafiki yako dondoo zangu hizi za afya.

Hakikisha unakaribisha marafiki zako wengi kuanza kutembelea ukurasa wangu facebook unaitwa "Masha Nutrition Health Care"

Blog: www.mashahealth.blogspot.com

Mawasiliano
0784925000
0767925000
0622925000 whatsapp
posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment