Sunday, 28 June 2015

UVIMBE KWENYE KIZAZI(UTERINE FIBROIDS/MYOMA)

Kumekuwa na ongezeko kubwa la tatizo la akinamama kuwa na uvimbe kwenye kizazi. Suala hili ni gumu na hupelekea akinamama wengi kutozaa tena katika maisha yao japo hutegemeana na sehemu uvimbe ulipo.
Kwa leo tutaona ni jinsi gani ugonjwa huu tunavyoupata, dalili na matibabu yake yanavyokuwa. Tukumbuke kuwa mgonjwa wa uvimbe kwenye kizazi haendi hospitali kwa sababu ya ukubwa wa uvimbe bali anaenda Hospitali kutokana na dalili atakazokuwa anazipata. Wanawake wengi tu wanakuwa na tatizo hili lakini wanajikuta wanabeba hata mimba hadi wanajifungua salama. Hii ni kutokana kuwa bado hawajapata dalili za ugonjwa huu/yaani hawajaanza kusumbuliwa.

HIZI HAPA NDIYO DALILI ZA KUWA NA UVIMBE KWENYE KIZAZI
1. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
2. Kupata hedhi mara nyingi zaidi ya siku za kawaida
3. Kuumwa na tumbo la hedhi zaidi ya kawaida
4. Kutokwa na uchafu na majimaji yenye harufu kali sehemu za siri
5. Kukojoa mara kwa mara
6. Figo kujaa maji na kusababisha kiuno kuuma sana(uvimbe umekandamiza ureter moja)
HIZO NDIYO DALILI ZINAZOMFANYA MGONJWA KWENDA HOSPITALI NA SIYO UKUBWA WA UVIMBE.

Mgonjwa anapofika na dalili hizo hubidi kufanyiwa kipimo cha picha ya tumbo(ultrasound) lengo na madhumuni ya kipimo hicho ni kujua uvimbe upo wapi, kujua uvimbe uko mmoja au zaidi, kutambua kama uvimbe umeathiri sehemu zingine kama kuziba ureter kama upo nje ya kizazi. Kipimo hicho kitamsaidia Daktari kujua anamsaidiaje mgonjwa wake kimatibabu.
VISABABISHI VYA UVIMBE KWENYE KIZAZI
-Kisababishi kikuu ni kuharibika kwa uwiano wa vichocheo vya estrogen na kusababisha kiwango cha estrogen kuwa kikubwa.
-ulaji wa vyakula vya viwandani vilivyovundikwa au kuhifadhiwa kwa msaada wa kemikali
-unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi (added sugar), kionjo na rangi ambavyo ni industrial products
-unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara

WATU AMBAO WAPO HATARINI KUPATA UGONJWA HUU
~Wanawake wote ambao hawajawahi kupata mtoto
~wanawake wote ambao wapo katika umri wa kuweza kuzaa, maana yake wote kuanzia umri wa kubalehe hadi kikomo cha kuzaa ~wanawake wanene kupita kiasi n.k

MATIBABU
Matibabu yake yanaweza kuwa kama ifuatavyo kutegemeana sehemu uvimbe ulipo
=>kupewa vidonge vya kutuliza maumivu tu, vidonge hivyo ni ghali sana lakini pia mgonjwa hushauriwa kutumia kwa muda mfupi tu kwani vina madhara ya kuweza kumfanya mwanamke kuwa na muonekano wa kiume kana vile kuota ndevu n.k
=>kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe tu endapo uvimbe upo pembeni ya kizazi. Ukifanyiwa hiyo Huduma bado mwanamke unaweza kupata mimba na kuzaa.
=>kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kabisa kizazi endapo Uvimbe upo ndani ya kizazi. Hapa mwanamke akifanyiwa upasuaji huu hawezi kuzaa tena katika maisha yake yote
NB: KUMBUKA KUWA HATA KAMA UTAUONDOA UVIMBE HUO, HAIMAANISHI KUWA UVIMBE UMEISHA, TATIZO HUJIRUDIA TENA MAANA BADO UNAKUWA HUJATIBU VYANZO VYA TATIZO AMBAVYO NI PAMOJA NA UWIANO MBOVU WA HORMONES NA MENGINE.

Vipo vidonge vilivyotengenezwa kwa mimea na uyoga mwekundu unaopatikana katika nchi za China na Thailand vinatibu kabisa tatizo hilo la uvimbe kwenye kizazi kwa kusambaza, kukausha na hatimaye kuumaliza kabisa uvimbe huo. Vidonge hivyo vinapatikana sasa Tanzania na kama wewe una tatizo hilo au ndugu na rafiki zako wana tatizo hilo basi wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 uweze kujipatia vidonge hivyo

Thursday, 25 June 2015

TATIZO LA MIGUU KUUMA/KUFA GANZI

Matatizo ya miguu/mikono kuhisi ganzi au maumivu husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa Neva za pembezoni mwa mwili(peripheral neuropathy), hivyo kusababisha kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika eneo husika(miguuni au mikononi).
DALILI ZA TATIZO
~Mtu kuhisi miguu kufa ganzi
~Maumivu au kuhisi kama vile moto unawaka miguuni au mikononi
~Kuhisi kama vile umevaa soksi au gloves wakati hujavaa
~Kuhisi kama vile kuna kitu chenye ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole
HIZI NDIZO SABABU ZA KUDHOOFIKA KWA NEVA HIZO
~Kupungua kwa virutubisho mwilini. Hapa tunamaanisha mwili kutokuwa na Vitamin za kutosha hasa mkusanyiko wa Vitamini B Complex
~Matumizi ya dawa fulani kwa muda mrefu mfano TB na ARV
~Uzito mkubwa wa mwili. Hii hupelekea maumbile ya viungo vya mwili mfano umbile la uti wa mgongo huonekana tofauti na ilivyo kawaida. Kubadilika huku husababisha baadhi ya Neva katika uti wa mgongo zikandamizwe zaidi na misuli/uzito wa mwili na hivyo kusababisha Neva hizo zishindwe kufanya kazi vizuri, matokeo yake unaanza kuhisi maumivu au miguu/mikono kufa ganzi.
~ugonjwa wa kisukari
~shinikizo la damu
HIZO NDIZO SABABU ZA TATIZO HILO, HIVYO TUSIEGEMEE KWENYE MAMBO YA KISHIRIKINA KABISA
MATIBABU
**Kubadili tabia hasa vyakula vinavyochangia tatizo hili kama nilivyotaja hapo juu
**Kutumia virutubisho ambavyo vitaweza kukurejesha katika hali ya zamani, pia dawa zilizotengenezwa kwa mimea zitakusaidia kufurahia Afya njema.
Wasiliana nasi kwa 0767925000 au 0784925000
Whatsapp 0622925000

Tuesday, 23 June 2015

ZIJUE FAIDA ZA KUNYWA MAJI GLASS 7 KWA SIKU

Suala la kunywa maji tumekuwa tukihimizwa kila mara na wataalamu wa Afya. Lakini zoezi hili limekuwa gumu kwa kuwa watu wengi huona kama adhabu. Imekuwa ikihimizwa angalau kunywa Lita mbili(2) za maji kila siku kwa kila mtu.
Nimekuwa nikiwasikia watu wengi wakidai wameenda Hospitali kutibiwa wameambiwa wanywe maji ya kutosha ili yawasaidie. Pia wengine wakithubutu kusema kuwa ukinywa maji mengi basi waweza tibu ugonjwa wa UTI kirahisi kabisa. Hili ni kweli lakini tatizo watu wengi hatuwezi kunywa hayo maji mengi.
Leo nitakupa mpangilio rahisi kabisa wa kunywa maji glass 7 kwa siku na faida zake mwilini. Hii itakusaidia zaidi maana glass 7 ni sawa na Lita 2 karibu na nusu.
GLASS 1. kunywa maji glass moja mara baada ya kuamka. Hii husaidia viungo vya ndani vya mwili kama figo, moyo, n.k
GLASS 1. Nusu saa kabla ya kunywa chai. Husaidia katika mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kuoga asubuhi. Husaidia kushusha shinikizo la moyo
GLASS 1. Nusu saa kabla ya chakula cha mchana. Pia husaidia katika mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kuoga jioni. Pia husaidia kushusha shinikizo la moyo
GLASS 1. Nusu saa kabla ya chakula cha usiku. Vilevile husaidia katika suala la mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kulala. Husaidia kuepuka kupata shambulio la moyo
Hiyo ndiyo ratiba nzuri ya kunywa maji glass 7 bila kuhangaika.
Endelea kufuatilia makala zangu zingine za Afya ndani ya blog hii ya www.mashahealth.blogspot.com
Kwa maoni, ushauri au chochote unachopenda tukiweke humu wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000

Sunday, 21 June 2015

SULUHISHO LA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI


Hiki kimekuwa kilio cha wanawake wengi na kimesababisha wengi kukubaliana na hali hiyo na kubakia kuwa wahanga wa maumivu hayo.

Zipo sababu nyingi zinazochangia uwepo wa tatizo hili ikiwepo kubwa la kutokuwepo uwiano wa vichocheo (hormones imbalance), kuwepo kwa magonjwa mbalimbali kama endometriasis ambapo ni tatizo la seli za ndani ya mfuko wa kizazi kujitokeza nje ya kizazi, adenomyosis ambapo ni hali ya mwanamke kuota Uvimbe katika mfuko wa kizazi, magonjwa ya zinaa yanayotokana na bacteria, mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu kutoka kwa urahisi.
Hizo ndizo baadhi ya sababu za maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.

Mara nyingi wanawake wengi hutumia dawa za kutuliza maumivu kama Ibuprofen, Naproxen au aina nyinginezo zisizokuwa na Steroids (NSAIDS). 

Madakatari baadhi huwashauri wanawake kutumia vidonge vya kuzuia mimba ili kukata maumivu hayo. Lakini tatizo kubwa ni kwamba njia hizo humaliza maumivu ndani ya kipindi hicho tu, yaani mwezi utakaofuata maumivu yapo palepale na itakulazimu kuzitumia tena hizo njia. Kwa kifupi siyo njia za kudumu katika kumaliza maumivu hayo.

Kuna dawa maalumu ya kamaliza tatizo hili pamoja na ped zake maalum. Ped  hizo zimewekwa ANIONS CHIP ambayo ni dawa maalumu inayokusaidia kumaliza maumivu hayo, kusawazisha viwango vya homoni, ni kinga na tiba ya ugonjwa wa UTI, miwasho na fangasi sehemu za siri, pia zina uwezo mkubwa wa kufyonza damu hadi 250mls wakati wa hedhi na mengine mengi. 

Dawa hizi pia husawazisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake wenye tatizo la mzunguko usioeleweka na husaidia sana mambo ya uzazi. Dawa zipo katika mfumo wa vidonge na hazina madhara yoyote kwani zimetengezwa kwa mimea pasipo kuongezewa kemikali yoyote.

Wasiliana nasi kwa:
0767925000
0622925000 - whatsapp

JINSI YA KUTAMBUA KAMA MWILI WAKO UMEJAA SUMU

Wimbi la watu kuugua na vifo vya ghafla limeongezeka kwa sasa. Katika makala hii fupi tutaangalia baadhi ya sababu zinazotupelekea kuugua kila mara tena bila kujua sababu. Hii inapelekea hata baadhi kuamini kuwa wamerogwa kwani hata waendapo Hospitali wakifanyiwa vipimo majibu huonyesha hawana ugonjwa wowote.
Sasa leo tutambue kuwa hakuna mchawi yeyote isipokuwa wewe mwenyewe ndiye mchawi wa matatizo yako.
Kutokana na tabia zetu za ulaji mbovu wa vyakula visivyo MLO KAMILI pia na UNYWAJI WA VINYWAJI VYENYE SUKARI NYINGI ndivyo vinavyochangia sisi kupata maradhi yasiyotibika Hospitalini. Ulaji na unywaji huo hupelekea miili yetu kujaa sumu.
UTATAMBUAJE KAMA MWILI WAKO UNA SUMU?
Ukiwa na dalili zifuatazo basi tambua kuwa mwili wako una sumu balaa;
-mwili wako unakuwa mchovu kila mara
-unaugua homa mara kwa mara
-unajisikia kuumwa lakini ukienda kufanya vipimo unaambiwa hauna ugonjwa wowote
-unakosa usingizi au unapata usingizi mpaka umeze dawa za usingizi
-unaugua mafua yasiyopona
-maumivu ya kiuno, mgongo na miguu kuwaka moto
-maumivu ya kichwa mara kwa mara
-mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa
-mwanamke kupata maumivu makali wakati wa hedhi
-mwanamke kubadilikabadilika siku zake za hedhi
-unene kupitiliza
-mwanaume kuishiwa nguvu za kiume
-kuwa na magonjwa tabia mbalimbali kama Kisukari, Presha, Uvimbe kwenye kizazi n.k
Tunao msaada kwa watu wote wenye tatizo hilo la mwili kuwa na sumu. Tunazo dawa za Aloe, Lycopene na Yongcordyceps zinazotumika kuondoa sumu zote mwilini bila madhara yoyote kwani zimetengenezwa kwa mimea tu pasipo kuongezwa kemikali zozote. Ziko katika mfumo wa vidonge. Dozi zake ni miezi miwili mpaka mitatu.
Tunao mawakala sehemu zote.
Wasiliana nasi kwa:
0767925000
0622925000 whatsapp

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa hivi karibuni limekuwa likizidi kushamiri siku hadi siku. Hii inatokana na baadhi ya vijana au wanaume kutokubali kubadilika katika baadhi ya tabia zao.
Zipo baadhi ya sababu nyingi zinazochangia kwa wingi tatizo hili ikiwemo:
1. Upigaji wa punyeto kwa vijana hasa wale wanaobalehe au waliopo mashuleni. Wapo pia wanaume watu wazima wanaofanya tabia hii hats wakiwa kwenye ndoa zao. Hii tabia huwa inabaki kuwa siri ya mhusika maana hufanya akiwa peke yake. Matokeo yake misuli ya uume huwa dhaifu kutokana na kuzoeshwa kutumia vidole ambavyo ni vigumu kulinganisha na uke.
2. Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.
3. Utumiaji wa pombe, sigara na madawa ya kulevya
4. Kuwa na hofu au msongo wa mawazo
5. Matumizi mabaya ya dawa hasa zile za kusisimua nguvu za kiume, pia utumiaji ovyo wa dawa pasipo kufuata ushauri wa kitaalamu
6. Kuwa na magonjwa kama Kisukari, Shinikizo la damu na Moyo pia ni chanzo cha tatizo hili
7. Kutopata usingizi wa kutosha. Mwili unahitaji muda wa kupumzika hasa usiku ili kuweza kukaa katika hali yake nzuri, hivyo mwili ukikosa hiyo Huduma ya usingizi inapelekea kusababisha hilo tatizo kwa kiasi fulani.
Zipo dawa nyingi zinazoweza kutibu tatizo la nguvu za kiume kupungua au kutokuwepo kabisa. Dawa iliyotengenezwa kwa mimea ya  butea superba. Ni msaada mkubwa kwa wanandoa na vijana wengi. Haina madhara kwani haina kemikali kabisa na imetengenezwa kwa mimea na samaki wa baharini bila kuongezwa kemikali zozote.
Wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000