Tuesday, 23 June 2015

ZIJUE FAIDA ZA KUNYWA MAJI GLASS 7 KWA SIKU

Suala la kunywa maji tumekuwa tukihimizwa kila mara na wataalamu wa Afya. Lakini zoezi hili limekuwa gumu kwa kuwa watu wengi huona kama adhabu. Imekuwa ikihimizwa angalau kunywa Lita mbili(2) za maji kila siku kwa kila mtu.
Nimekuwa nikiwasikia watu wengi wakidai wameenda Hospitali kutibiwa wameambiwa wanywe maji ya kutosha ili yawasaidie. Pia wengine wakithubutu kusema kuwa ukinywa maji mengi basi waweza tibu ugonjwa wa UTI kirahisi kabisa. Hili ni kweli lakini tatizo watu wengi hatuwezi kunywa hayo maji mengi.
Leo nitakupa mpangilio rahisi kabisa wa kunywa maji glass 7 kwa siku na faida zake mwilini. Hii itakusaidia zaidi maana glass 7 ni sawa na Lita 2 karibu na nusu.
GLASS 1. kunywa maji glass moja mara baada ya kuamka. Hii husaidia viungo vya ndani vya mwili kama figo, moyo, n.k
GLASS 1. Nusu saa kabla ya kunywa chai. Husaidia katika mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kuoga asubuhi. Husaidia kushusha shinikizo la moyo
GLASS 1. Nusu saa kabla ya chakula cha mchana. Pia husaidia katika mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kuoga jioni. Pia husaidia kushusha shinikizo la moyo
GLASS 1. Nusu saa kabla ya chakula cha usiku. Vilevile husaidia katika suala la mmeng'enyo wa chakula
GLASS 1. Kabla ya kulala. Husaidia kuepuka kupata shambulio la moyo
Hiyo ndiyo ratiba nzuri ya kunywa maji glass 7 bila kuhangaika.
Endelea kufuatilia makala zangu zingine za Afya ndani ya blog hii ya www.mashahealth.blogspot.com
Kwa maoni, ushauri au chochote unachopenda tukiweke humu wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000

No comments:

Post a Comment