Friday, 31 July 2015
TAMBUA MUDA SAHIHI WA KULA MATUNDA
Watu wengi hula matunda kipindi wanapojisikia wao pasipo kutambua kuwa inatupasa kula matunda kipindi maalumu na pia hilo tunda inabidi liwe na sifa maalumu, siyo kula tunda tu mradi ni tunda.
Kama nilivyosema hapo awali kuwa watu wengi hupenda kula tunda kwa muda wanaoutaka wao au wanakula kwa kujikuta tu wanakula matunda pasipo kupanga au wengi wamekariri kula matunda baada ya mlo. Hii siyo sahihi.
Basi leo ndugu zangu napenda kuwaelezea somo hili kuhusu ulaji sahihi wa matunda. Kwanza inabidi tuzitambue faida za matunda katika miili yetu. Matunda yana faida nyingi sana kwa Afya ya binadamu, hivyo yatupasa kuyapa kipaumbele mkubwa katika milo yetu ya kila siku. Matunda ni chanzo kikubwa cha Vitamin mwilini, hulinda mwili kwa kuongeza kinga ya mwili, hupunguza uzito wa mwili kwa watu wanene, hulainisha ngozi, huondoa sumu mwilini, hufanya mishipa ya damu kusafirisha damu vizuri, huongeza na kuimarisha nguvu ya mwili/nguvu za kiume n.k.
JINSI YA KULA MATUNDA ILI UFAIDIKE
1. KULA TUNDA KIPINDI UKIWA NA NJAA
Unapokula tunda wakati tumbo likiwa wazi/njaa, matunda husagika kwa urahisi. Baada ya saa moja au zaidi unaweza kula sasa mlo wako mwingine wa kawaida.
2. USILE MATUNDA BAADA YA MLO
Imezoeleka watu wengi kula matunda baada ya mlo kamili. Hata kwenye Hafla na Taafrija, matunda huliwa mwishoni baada ya chakula, HII SIYO SAHIHI KABISA na hayo ni miongoni mwa makosa mengi yanayofanyika kwa sababu ya mazoea tu. Inaelezwa kuwa ulaji wa matunda baada ya mlo siyo sahihi kwa sababu matunda huyeyuka haraka kuliko chakula cha kawaida . Tunda linapokuwa tayari kutoka tumboni kuelekea kwenye utumbo mwembamba huzuiliwa na chakula. Baada ya muda tunda huchanganyikana na chakula na kuoza na hatimaye huzalisha asidi ambayo humfanya mtu kuumwa tumbo baada ya kula matunda, lakini pia virutubisho vyake hupotea.
Ili kuepukana na hali hiyo ya msongamano kwenye tumbo, kula matunda saa moja kabla ya mlo au angalau masaa mawili baada ya mlo. UKIZINGATIA UTARATIBU HUO UTAKUWA UMETOA NAFASI YA CHAKULA KUSAGIKA NA BILA KUZUIA UYEYUKAJI WA MATUNDA
3. ZINGATIA KIWANGO CHA SUKARI KWA BAADHI YA MATUNDA
Baadhi ya matunda kama vile papai, ndizi mbivu yana kiasi kingi cha sukari, japo karibu kila matunda yana sukari lakini baadhi yana kiasi kingi zaidi. Hivyo inashauriwa kula matunda kwa kiwango cha wastani kila siku bila kuzidisha kiwango cha sukari cha gramu 25 kinachohitajika kwa siku.
Aidha unapokula tunda hakikisha unakula kwa ukamilifu wake ili kupata virutubisho vyake. Kwa mfano unapokula chungwa hakikisha unakula pamoja na nyama zake ili kupata virutubisho vyote muhimu vilivyomo. Pia ulapo tango jitahidi baada ya kuliosha ule pamoja na maganda yake.
Jiwekee tabia ya kula matunda ya aina mbalimbali kwa nyakati tofauti ili kupata Vitamin na Madini tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mwili. Hii ni kwa kuwa matunda ndiyo yanayojenga na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi na kamwe hutasumbuliwa na magonjwa mara kwa mara.
Mpendwa msomaji wa makala zetu endelea kufuatilia masomo mbalimbali ndani ya Blog hii. Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment