Saturday, 1 August 2015
ZITAMBUE DALILI ZA MIMBA CHANGA
Habari za leo mpenzi msomaji wa makala zetu, leo tunapenda kugusia kwa kiasi kidogo kuhusu dalili za mimba changa. Hili somo tumeamua kulileta baada ya wasomaji wetu wengi kuendelea kutuuliza maswali kuhusu namna mwanamke anavyoweza kugundua kuwa ni mjamzito hasa kwa akinadada ambao ndiyo mara yao ya kwanza kuwa katika hali hiyo.
Zifuatazo ni baadhi ya dalili ya mimba changa:
KWANZA. Mabadiliko katika siku zako(spotting). Unaweza kupata mimba na ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza katika kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa katika ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo ambazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango cha siku za damu hubadilika.
PILI. Kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa(chuchu). Hii inasababishwa na kuongezeka kwa homoni za estrogen pale unakuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.
TATU. Kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapotoka kulala. Na hii ni kwa sababu ya homoni za progesteron ambazo husababisha kupungua nguvu kwa msuli wa mrija wa chakula au koromeo.
NNE. Uchovu na usingizi usiokuwa wa kawaida na bila sababu. Hali hii husababishwa na ongezeko la homoni ya progesteron na mama utajikuta unapata usingizi kila mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba.
TANO. Kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hii hutokea hasa unapopata mimba ya kwanza utachukia harufu ya baadhi ya vyakula na vinywaji mbalimbali. Wakati mwingine hata harufu za baadhi ya watu zinaweza kukukera. Hapa kidogo panachekesha kwani baadhi ya akinamama huchukia hata harufu ya wapenzi au waume zao.
SITA. Kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinakufanya kujisikia tumbo kujaa.
SABA. Kukojoa mara kwa mara. Hii hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa lishe ya kutosha kwa mama na kiumbe kilichomo tumboni. Kikemia ukiwa na damu nyingi mwilini utakojoa sana. Pili utajisikia kwenda sana haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.
NANE. Kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa akinamama ambao hupima joto lao kwa njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfululizo.
TISA. Kutoona siku zako za hedhi kabisa. Kwa akinamama ambao siku zao hazibadiliki au huenda vizuri yawezekana wakagundua pale wanapokosea siku na pengine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa wale ambao siku zao hubadilika sana wataona ni kawaida ila kama ameshika mimba ataona mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu, kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.
KUMI. Kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. Pharmacy nyingi huuza vipimo ambavyo ukivichovya kwenye mkojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo. Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani au hata kazini. Kipimo hiki ukikichovya kwenye mkojo kama karatasi inavyoelekea utaona mistari baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini, ikitokea mistari miwili basi utakuwa una mimba na ukitokea mmoja itakuwa hauna mimba. Lakini kipimo hiki huwa kina changamoto zake kwa baadhi ya akinamama ambao kulingana na matatizo ya kiwango cha homoni mwilini hakitaweza kuonyesha majibu mpaka wapitishe wiki moja bila kuona siku zao.
Pamoja na dalili hizo hapo juu, ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu zaidi kutoka kwa daktari aliyepo karibu na wewe.
Kama una tatizo lolote la kiafya, mwanaume au mwanamke waweza wasiliana nasi kupitia namba zetu 0767925000 au whatsapp 0622925000 tutakuhudumia popote ulipo Tanzania. Dawa zetu zote zimetengenezwa kutokana na mimea na ziko katika mfumo wa vidonge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment