Saturday, 22 August 2015

KUUMWA MARA KWA MARA NI DALILI TOSHA KUWA KINGA YAKO YA MWILI IMESHUKA

Kinga ya mwili ndiyo kila kitu katika Afya ya binadamu. Kinga ya mwili ni ile hali ya mwili kuwa na uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi mbalimbali. Ukiwa na kinga imara ya mwili huwezi kuugua mara kwa mara.
Kuumwa mara kwa mara ni dalili tosha kabisa kuwa kinga ya mwili wako imeshuka na hivyo unatakiwa kuchukua hatua ili uweze kuiimarisha. Mungu aliumba mwili ukiwa na uwezo wake wa kujikinga na magonjwa yote ikiwa tu mwili utaupatia chakula chake kinachotakiwa kuimarisha kinga yake.
Hapo ndipo tunapotakiwa kujua ni aina gani ya vyakula huimarisha kinga ya mwili na pia ni vyakula gani hupunguza kinga ya mwili. KUMBUKA KINGA NI BORA KULIKO TIBA, hivyo usisubiri upate matatizo ndipo uanze kutafuta suluhisho kwani ukingoja upate matatizo utakuja kutumia gharama kubwa zaidi ambayo hukuitarajia.
EPUKA VITU HIVI
-ULAJI WA SUKARI. Kwa kawaida kiwango cha sukari kinachotakiwa kutumiwa ni kijiko kimoja tu cha chai. Inapozidi hapo tu kinachangia kuharibu mfumo mzima wa kinga ya mwili. Niliwahi kuongelea soda kuwa katika chupa moja ya soda huwa kuna vijiko sita (6) vya sukari. NI HATARI SANA
-EPUKA UNYWAJI WA KAHAWA
Kirutubisho kiitwacho CAFFEINE kilichomo kwenye kahawa kinaweza kuondoa virutubisho muhimu mwilini kama Calcium, Magnesium na Potassium. Kahawa pia huweza kuathiri mfumo wetu wa fahamu na kusababisha wasiwasi na ukosefu wa usingizi. Tukumbuke kuwa usingizi ni muhimu sana kwa ubongo na ni tiba ya magonjwa mbalimbali kwa njia ya asili (natural healing)
-USINYWE KILEVI
Unywaji wa pombe kupita kiasi ni sumu kwa miili yetu. Kitu cha kwanza kuathirika na ulevi kupita kiasi ni INI, halikadhalika mfumo wa fahamu nao huathirika. Hali hiyo pia hudhoofisha uzalishaji wa seli za damu (blood cells)
-EPUKA VYAKULA VIBICHI
Hakikisha unaosha vizuri matunda kabla ya kuyala. Kuna bakteria wa kila aina kwenye vyakula vibichi yakiwemo matunda. Hivyo kuosha matunda kwa umakini ni muhimu sana. Pia ulaji wa mayai mabichi au yaliyochemshwa na kuiva kwa kiasi huweza kuwa na bakteria. Hivyo kinga ya mwili hudhoofika na wale wenye kinga dhaifu wanaweza kupatwa na magonjwa ya mlipuko.
-EPUKA CHIPSI, VYAKULA VYA KUKAANGA NA KUOKA.
Vyakula vya kukaanga kama vile chipsi na vinginevyo pamoja na vyakula vya kuoka huwa huwa na mafuta mabaya (CHOLESTEROLS) ambayo huwa na tabia ya kutengeneza magonjwa mwilini (FREE RADICALS) na huathiri mfumo wa kinga ya mwili pamoja na chembechembe za nasana (DNA). Vyakula hivyo ni vya kuliwa kwa nadra sana siyo kila siku na kikubwa ni kuviepuka tu. Vyakula vingine vya kuepukwa ni VYAKULA VYA KWENYE MAKOPO VINAVYOTENGENEZWA VIWANDANI, NAFAKA ZILIZOKOBOLEWA.
KULA KWA WINGI
-Vyakula vya asili mfano nafaka zisizokobolewa
-Mbogamboga
-Matunda yasiyo na kiwango kikubwa cha sukari
-Viungo kama vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi, uyoga n.k. hivi viungo husaidiana sana kuimarisha kinga ya mwili.
-kunywa maji ya uvuguvugu kila siku
-pata muda wa kulala
Kama tayari unasumbuliwa na tatizo la kuumwa mara kwa mara yaani kinga ya mwili wako imeshuka, wasiliana nasi tutakupatia vidonge vilivyotengenezwa kwa uyoga mwekundu ambao hupandisha sana kinga ya mwili. Vidonge hivi pia ni vizuri sana kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwani huwasaidia wasipatwe na magonjwa nyemelezi.
MAWASILIANO YETU NI 0767925000 AU WHATSAPP 0622925000

Friday, 21 August 2015

HIZI HAPA NDIYO SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA WANAUME WENGI

Habari za leo mpenzi msomaji wa makala zangu, leo napenda niongelee hili janga la wanaume wengi kuwa wahanga wa tatizo la upungufu au kuishiwa nguvu za kiume kabisa. Tatizo hili ni pana sana ila ntalizungumzia kwa kifupi tu hasa sababu zinazosababisha tatizo hili.
Kwa kufuata ukweli, hakuna mwanaume anayekubali kuwa na tatizo hili, kila mmoja anapohisi ametumbukia katika tatizo hili hujaribu kwa haraka kutafuta suluhu ya tatizo lake. Wengi huamua kununua madawa wanayoyajua wao kuwa yanaweza kuwasaidia lakini wengi wao hujikuta wakishindwa kupata tiba ya kudumu kwani huwalazimu kila wanapohitaji kushiriki tendo huenda kununua dawa au kolezo ili waweze kupata angalau mzuka wa kushiriki. Hii ni Kazi ngumu sana kwani kadri unapoendelea kutumia hizo kolezo ndivyo unavyozidi kujimaliza. Unatakiwa utafute suluhisho la tatizo hata kama gharama ni kubwa lakini tatizo liishe. La sivyo kwa watu wenye ndoa familia au ndoa zao huwa mashakani au unaweza kumfanya mkeo atoke nje ya ndoa (KUCHEPUKA) ili apate tu kutimiza haja zake za kimwili.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu za tatizo hilo kwa wanaume wengi:
1. Kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu. Hii wanaifanya sana vijana wengi na hata watu wazima. Unakuta kijana haipiti siku bila kuifanya hii kitu. Matokeo yake misuli ya uume hudhoofika na kufanya wasiweze kusimamisha vizuri hasa wanapokuwa na wapenzi wao kwani wamezoea kufanya kwa mkono (punyeto) hivyo wanapokutana na sehemu laini za mwanamke wanashindwa.

2. Mitindo ya maisha
Wanaume wengi kwa sasa wameshaingia katika mitindo ya ulaji mbovu wa vyakula.Vyakula vyenye mafuta mengi au ulaji wa chipsi na nyama choma kila siku. Hivi vyakula hudhoofisha mzunguko wa damu na kufanya damu kushindwa kuzunguka vizuri hasa kwenye uume. Hapa ndipo tatizo la wengi linapoanzia. Mwanaume ambaye hakupata tatizo hili kutokana na kujichua basi atalipata kwenye chakula. Pia unywaji wa pombe, soda na juisi za viwandani, vyakula vilivyokobolewa kama sembe, uvutaji wa sigara n.k

3. Msongo wa mawazo/Kisaikolojia
Kuna wanaume wanaoweza kusababishiwa tatizo hili na wapenzi wao. Mfano mpenzi wako anakwambia "yaani siku hizi sijui umekuwaje tu, yaani huwezi kazi kabisa". Hapa mwanaume kwa hakika ni lazima uchanganyikiwe na utaliweka kichwani na kuwa tatizo. Mengine ni kusikia maneno ya watu wakiongelea ufanyaji wa ngono kwa kiwango cha juu zaidi na wewe kujiona huwezi.

4. Maumivu ya kiuno kwa muda mrefu. Hili linaweza kuwakuta hasa watu wanaofanya kazi wakiwa wamekaa kwa muda mrefu. Madereva wa magari wanaoendesha kwa umbali mrefu na wanaofanya kazi maofisini wapo hatarini. Utakuta mtu yupo ofisini amekaa tangu asubuhi hadi muda wa kutoka kazini. Hata chai na chakula cha mchana anaagiza aletewe ofisini. HII NI HATARI SANA

5. Kuwa na magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu, ulemavu wa kupata ajali navyo pia huchangia tatizo hili. Matatizo ya Unene/uzito, matatizo ya tezi dume, figo, ini pia ni vyanzo vingine vya tatizo hili.

Hivyo unapotafuta suluhisho la tatizo lako ni vyema ukajua chanzo chake ili utibiwe kwa kutatua chanzo na upate tiba ya moja kwa moja. Nimefanya hivi ili kuwasaidia wengi mjitambue ili hata unapopata tiba tatizo lako lisijirudie tena.

Tiba ya tatizo hili tunayo na utamaliza dozi ndani ya mwezi mmoja hadi miwili kutegemeana na ukubwa wa tatizo lako.
Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000. TUPO MWANZA NA SHINYANGA. MIKOA MINGINE TUNAO MAWAKALA PIA

Sunday, 16 August 2015

UGONJWA WA PRESHA (BLOOD PRESSURE)


Huu ni ugonjwa ambao kwa sasa ni kama janga la jamii yote kwani imekuwa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kipindi cha nyuma. Miaka ya nyuma ilizoeleka kuwa ugonjwa huu ni kwa ajili ya watu wanene, wazee au matajiri tu, jambo hilo kwa sasa ni tofauti kabisa kwani watoto, maskini na hata watu wembamaba wanaupata tu.

PRESHA ni hali inayotokea endapo MOYO UNASUKUMA DAMU KWA HALI AMBAYO SIYO YA KAWAIDA. Kwa kawaida Presha ndiyo inayosaidia katika kusukuma damu, lakini Presha hiyo inapokuwa juu au chini zaidi ya kawaida huleta matatizo makubwa kiafya. Watu wazima zaidi ya miaka 18 presha ya diastole inatakiwa kuwa kipimo cha juu cha 120mmHg na Presha ya diastole ambacho ni kipimo cha chini inatakiwa iwe 80mmHg. Hapa ndipo tunaposema Presha inatakiwa kuwa 120/80mmHg.

Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote mkubwa au mtoto kulingana na maisha tunayoishi. Presha huathiri vitu vingi mfano idadi ya maji mwilini, idadi ya chumvi, homoni mwilini, hali ya joto au baridi, hali ya hisia au figo, mfumo wa neva na mishipa ya damu.

Kama Presha itakuwa juu na kuachwa kutodhibitiwa, moyo na mishipa haitofanya kazi vizuri kama ipasavyo. Kwa sababu neva na seli za mwili tayari zinakuwa zimeshaathiriwa na presha.
HAPO NDIPO MTU ANAPOTUMIA DAWA ZENYE KEMIKALI INAKUWA NGUMU SANA KUPONA TATIZO HILO. Lakini usijali kama utafuata maelekezo nitakayokupatia ndani ya makala hii ya Presha.

Kwa kawaida tunautofautisha huu ugonjwa katika makundi makuu mawili:
1. Presha ya juu (high blood pressure au Hypertension)
2. Presha ya chini/kushuka (low blood pressure au Hypotension)

VISABABISHI VYA PRESHA KUWA JUU
-Chumvi nyingi
-Unene uliozidi
-Umri mkubwa au uzee
-Figo ikiwa haifanyi kazi
-Historia ya ugonjwa wa Presha katika familia
-Ugonjwa wa kisukari

DALILI ZA MTU MWENYE UGONJWA WA PRESHA
Mara nyingi Presha huwa haina dalili hadi ilete madhara na hivyo imefanya kuitwa "SILENT KILLER" yaani muuaji wa kimyakimya.
Hizi ni baadhi ya dalili:
-Kichwa kuuma
-Kizunguzungu
-Pumzi kubana
-Kutokuona vizuri
-Kichefuchefu

VITU VINAVYOCHANGIA HALI YA MGONJWA WA PRESHA KUWA MBAYA ZAIDI
-Kula chumvi nyingi
-Unene uliozidi
-Kutofanya mazoezi mara kwa mara
-Kunywa pombe nyingi
-Uvutaji wa sigara

TIBA YA UGONJWA WA PRESHA
Mojawapo ya tiba za ugonjwa huu wa Presha ni kuepukana na vitu nilivyovitaja hapo juu vinavyochangia hali ya mgonjwa wa Presha kuwa mbaya yaani kuacha kula vyakula vyenye chumvi au unaweza kuweka kidogo sana, kufanya mazoezi ya angalau nusu saa kwa siku kwa wiki hata mara tatu, epuka vyakula vyenye mafuta mengi na lehemu (cholesterols) maana huwa vinaganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha presha, kula zaidi mboga za majani na matunda.
Daktari anapobaini kuwa presha yako yako iko juu kulingana na aina na kiwango cha presha atakushauri kuhusiana na vyakula na jinsi ya kubadili mwenendo wa maisha au atakuanzishia dawa mara moja. Kwa dawa za Hospitali au za kemikali ni muhimu kujua kuwa mara utakapoanzishiwa dawa ujue hautaacha kutumia dawa maisha yako yote la sivyo tatizo litarudi kama mwanzo.

Tunazo dawa zilizotengenezwa kwa mimea katika mfumo wa vidonge ambazo hazina kemikali kabisa na zinatibu kabisa tatizo kwa kuzitumia kwa muda wa miezi mitatu tu.
Wasiliana nasi kwa namba 0767925000 au whatsapp 0622925000. Tunatoa huduma popote Tanzania


TATIZO LA NGOZI (ECZEMA)



ECZEMA au pumu ya ngozi au kwa kitaalamu huitwa atopic dermatitis ni tatizo la ngozi litokanalo na mzio au allergy ya ngozi na reactions za mazingira yanayomzunguka mtu au baadhi ya familia zenye historia ya ugonjwa wa Pumu/Asthma.

Neno Eczema ambalo ndiyo jina la ugonjwa huu ni la Kigiriki linamaanisha kututumka sehemu ya ngozi, hali amabayo huonekana pindi mgonjwa anapopata maradhi haya. Maradhi haya ya ngozi yanachangia asilimia arobaini (40%) ya magonjwa yote ya ngozi yanayoripotiwa Hospitalini.


Maradhi haya hushambulia zaidi watoto na huweza kupitiliza hadi ukubwani, lakini watu wengi huweza kupona au kupungua kadri mtoto anavyozidi kukua. Watafiti wanasema kuwa kumekuwa na ongezeko la maradhi haya katika kipindi cha miaka ya usoni hali inayoashiria kuwa maradhi haya ni ya kurithi (atopic eczema).


Maradhi haya huweza pia kujitokeza ukubwani ingawa ni mara chache Maradhi haya huathiri watu wa jinsia zote kwa uwiano sawa yaani wanaume na wanawake.


DALILI ZA TATIZO
Maradhi haya ni ya muda mrefu, kwa hiyo mtu huweza kukaa nayo kwa muda mrefu ingawa siyo muda wote ngozi itaonyesha dalili za maradhi. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za ugonjwa huu:
-Muwasho wa ngozi usio wa kawaida na kupelekea ngozi kupata vipele kisha kuwa kavu na ngumu
-Kuvimba kwa ngozi 
-Sehemu ya ngozi iliyoathirika huwa inatutumka
-Ngozi huwa inakuwa na mipasuko inayoweza kuruhusu vimelea vya maradhi kushambulia sehemu ya ndani ya ngozi
-Maeneo ya ngozi yaliyoathirika huweza pia kuwa na malengelenge na hata kutoa maji
-Bila matibabu ya haraka ngozi inaweza fanya vidonda
-Ingawa maeneo yenye kuathirika huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini pumu ya ngozi hupenda kushambulia sehemu za mikono hususani eneo baada ya kiwiko kwenda chini, miguu, viganja vya mikono, eneo la nyuma ya magoti (mkunjo wa mguu kwenye eneo la goti), maungio ya mkono kwenye kiwiko, shingo, sehemu ya juu ya kifua, wagonjwa wengune hupata maambukizi kwenye maeneo yanayozunguka macho, watoto wengi hupata pumu ya ngozi kwenye uso.

Kwa wenye pumu ya ngozi mbaya kabisa sehemu kubwa zaidi ya mwili hututumka na vidonda pamoja na kutokwa na majimaji kwenye maeneo yenye vidonda. Wakati maradhi haya yanapoanza hunyesha dalili za muwasho ambao husababisha mgonjwa kujikuna  na kumsababishia mikwaruzo kwenye ngozi ambayo nayo husababisha vimelea  vya maradhi kuweza kupenya na kusababisha vidonda vikubwa zaidi kutokea kwenye eneo la ngozi. Vidonda vinapotokea hasa kwa mtoto huweza kumsababishia msongo wa mawazo, kama hali hii ikimtokea kwa mtoto wa shule basi hata mahudhurio yake shuleni yatakuwa mabovu au hata kufeli mitihani.


SABABU ZA MASHAMBULIZI ZAIDI
-Kuogea maji ya moto kwa mrefu
-Kuruhusu ngozi ya mwili kukaa ikiwa kavu kwa mrefu (bila kupaka mafuta)
-Kuwa na msongo wa mawazo
-Kubadili joto la mwili yaani kusafiri kutoka  kwenye eneo la joto kwenda eneo lenye baridi au kinyume chake
-Kuvaa mavazi yasiyo ya pamba (cotton)
-Uvutaji wa sigara
-Kukaa kwenye vumbi
-Kukaa kwenye mchanga
-Matumizi ya mafuta ya mwili yanayosababisha mzio wa mwili
-Matumizi ya sabuni zinazosababisha mzio wa mwili
-Ulaji wa chakula kinachosabisha mzio wa mwili, mfano wale wenye mzio wa vyakula vinavyopatikana kwenye maji au baharini.

SABABU ZA PUMU YA NGOZI
Wataalamu wanasema kwamba maradhi haya mtu huzaliwa nayo na kuwa huwa yanarithiwa. Athari za maradhi haya huzidi kutokana na sababu nyingine za ndani au nje ya mwili.
Vitu kama manyoya ya wanyama au mbegu za mimea huweza kusababisha mzio ambao huweza kuleta madhara makubwa  zaidi kutokea kwenye ngozi.

Mtu mwenye dalili au tatizo hili ni vyema awahi kuanza matibabu au anaweza kuwasiliana na sisi kwa namba 0767925000 au whatsapp 0622925000 tutampatia dawa za vidonge atakazozitumia kwa miezi mitatu na tatizo hilo litaisha. Dawa hizi huanza kwa kuondoa chanzo cha tatizo na kuiacha ngozi yako ibaki kuwa nzuri.

Saturday, 15 August 2015

SABABU ZINAZOSABABISHA MWANAMKE ASIPATE MIMBA



Zipo sifa ambazo mwanamke au mwanaume anatakiwa kuwa nazo ili aweze kushika au kumpatia ujauzito mwenzi wake. Kuna wanaume ambao wamekuwa wakiishi maisha ya kutafuta watoto kwa kuwa na uhusiano na wanawake lukuki ndani ya muda mfupi pasipo kutambua kuwa hata wao wana uwezekano mkubwa tu wa kuwa na tatizo la kutozalisha au kutungisha mimba, Wanaume wengi huamini kuwa wanapokuwa na uwezo wa kufanya ngono ndio kigezo cha wao kuweza kuzalisha. DHANA HIYO SIYO KWELI.

Leo tutaziona baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha mwanamke ashindwe kubeba ujauzito. Kwa kawaida mwanamke ili aweze kushika mimba ni lazima aweze kuonekana au kuwa na sifa kama za mwanamke na pia mwanaume ili aweze kumpa mwanamke ujauzito ni lazima awe na sifa kama mwanaume. Hivyo katika sula hili la kutafuta mtoto ni lazima mwanamke na mwanaume washirikiane kwani mwanaume unaweza kujiona kuwa uko fiti kumbe ukija kupima mbegu zako utajikuta una tatizo kubwa.

MATATIZO KWA MWANAMKE
Mwanamke mwenye matatizo ya kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo yafuatayo:
1. Atakuwa amekaa na mwanaume au ameishi katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume kwa zaidi ya mwaka mzima lakini hakuna mafanikio.
2. Hulalamika maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara.
3. Maumivu ya hedhi.
4. Kuvurugika mzunguko wa hedhi.
5. Kutoona ute wa uzazi
6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa na kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa
7. Kuwa na historia ya kutumia njia za uzazi wa mpango au kuharibika/kutoa mimba.
USHAURI: Endapo una muda wa zaidi ya mwaka hujapata ujauzito na unapata baadhi ya dalili nilizozitaja hapo juu, ni vyema uonane na daktari wa magonjwa ya uzazi ambaye hupatikana katika kila Hospitali za Mikoa, Hapo utafanyiwa uchunguzi zaidi hasa katika vichocheo au homoni za uzazi, vipimo vya mirija ya uzazi na vingine ambavyo daktari atakushauri. Uchunguzi huu mara nyingi huchukua muda mrefu hivyo ni vyema kuwa mvumilivu kwani mara nyingine mvurugiko wa homoni, matatizo ndani ya kizazi yanaweza kuwa yamesababishwa na uvimbe au maambukizi.

MATATIZO YA UZAZI KWA MWANAUME
Uchunguzi kwa mwanaume ni kuangalia mbegu za uzazi na kupima korodani, Mwanaume unaweza kujifahamu kama una tatizo endapo utakuwa na dalili zifuatazo:
1. Kuishi na mwanamke au mpenzi kwa zaidi ya mwaka lakini hakuna mimba kwa mwanamke
2. Upungufu wa nguvu za kiume
3. Kutoa manii au shahawa nyepesi sana na zenye harufu mbaya.
4. Maumivu ya muda mrefu ya korodani
5. Maumivu ya kiuno kwa muda mrefu
6. Maambukizi katika njia ya mkojo mara kwa mara
7. Uvutaji wa sigara kwa muda mrefu
8. Unywaji wa pombe kali, matumizi ya dawa za kulevya mfano bangi na mirungi.
USHAURI: Matatizo haya pia hutibika kwa kumuona daktari wa magonjwa ya uzazi. Vipimo vya mbegu na korodani hufanyika. Vipimo vingine hutegemea uwepo wa matatizo mengine kama kuwahi kumaliza tendo la ndoa, upungufu wa nguvu za kiume, uchovu mkali baada ya tendo la ndoa na maumivu katika njia ya mkojo.

Ni vyema kuwahi Hospitali mapema mara tu unapojigundua kuwa una baadhi ya hizo dalili.

Kwa ushauri na tiba za magonjwa yote hususani ya uzazi tafadhali waweza wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000, tunazo dawa zinazotibu matatizo yote hayo, zimetengenezwa kwa mimea na matunda na ziko katika mfumo wa vidonge.


Sunday, 9 August 2015

Vyakula vinavyoimarisha Afya ya Ngozi



Ni matumaini yetu kuwa hamjambo na mnaendekea na shughuli za uzalishaji ili kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Karibuni tena wasomaji wa makala zetu za Afya. Leo tutaangalia aina ya vyakula vinavyoweza kuimarisha Afya ya Ngozi.

Bila shaka kula vyakula vyenye virutubisho ni jukumu la lazima kwa kila binadamu kama anahitaji kuwa na Afya njema. Dunia ina vyakula vya Asili ambavyo ndani yake kuna virutubisho muhimu vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa na pia kuimarisha Afya.
Vyakula hivyo si vingine bali ni vile vya kijani ambavyo vina uwezo mkubwa zaidi katika kuponya maradhi na kusaidia pia kukarabati, kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Ngozi ni sehemu muhimu ya mwili ambayo ina jukumu kubwa la kuukinga na kuufunika mwili na viungo mbalimbali na Afya yake ni jambo la kuzingatiwa.

Aina ya vyakula tunavyopendelea kula vinaweza kuchangia katika mwonekano wa ngozi zetu na kusaidia kupambana na matatizo ya ngozi, kupunguza mikunjo ya uso na suala zima la Afya na muonekano wa ngozi. Inawezekana kabisa kila mmoja anapenda kuonekana na ngozi nzuri isiyoonekana kuzeeka mapema lakini tatizo kubwa ni kutojua nini cha kufanya ili kudumisha Afya ya ngozi zetu na matokeo yake tunajikuta tunajiletea madhara yasiyoweza kutibika kirahisi kwa kupenda urembo wa njia mkato (vipodozi vyenye sumu kali). Pia inawezekana tukatumia pesa na muda mwingi katika kuhakikisha ngozi inakuwa nyororo, nzuri na ya kuvutia, lakini pengine ukawa hufahamu kuwa kuna aina za vyakula vinavyosaidia katika kutunza ngozi na tena bila gharama kubwa. Kwa kawaida kila aina ya chakula tunachokula huenda moja kwa moja kuwa sehemu ya mwili na pia matatizo mengi ya ngozi kama chunusi ya Eczema yanahusiana kwa kiasi kikubwa na Lishe. Kwa hiyo tunashauliwa kula vyakula ambavyo vina virutubisho vyote vya muhimu kwa kufuata kanuni za Afya ili kuufanya mwili uwe na Afya nzuri kwa kula chakula bora, kufanya mazoezi mara kwa mara, kupumzika kwa muda mrefu. Vivyo hivyo ngozi nayo inatakiwa kutunzwa vyema kupitia lishe.

Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kuimarisha Afya ya ngozi:
1. ASALI=> Asali ambayo hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia ni chakula muhimu kwa ajili ya ngozi na pia Afya ya binadamu. Husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu  kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambavyo huzuia vijidudu wanaozaliana kwenye ngozi. Tunashauriwa kuwa ili tuweze kulinda ngozi, paka asali wakati wa kuoga, acha muda kiasi kisha ioshe. Kufanya hivyo husaidia sana kuimarisha na kunawirisha ngozi.

2. VYAKULA VYA BAHARINI=> Vyakula hivi huwa vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu sana kwa ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi. Zinc husaidia chunusi na harara katika ngozi kwa kuyeyusha homoni za testosterone. Pia husaidia kuzalishwa seli au chembe zilizokufa huku ikiifanya ngozi ing'ae na kuwa na mvuto.

3. MAYAI=> Kiini cha yai kina Vitamini A na B huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo ni muhimu sana kwa ngozi. Vitamini A husaidia kuondoa chunusi na mikunjo ya ngozi. Vitamini B pamoja na Protini ni muhimu kwa Afya ya ngozi/kucha na huifanya ngozi iwe nyororo na yenye kung'aa. Husaidia pia kuilinda ngozi na mionzi ya jua.


Mpenzi msomaji, matunda yenye vitamini C ambayo ni Machungwa, Malimao na mengineyo ni muhimu pia katika afya ya ngozi kwa sababu husaidia kutengeneza Collagen ambayo ni aina ya Protini unayotengeneza ngozi. Vitamini C inasaidia kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema.

Hivyo ni baadhi tu ya vyakula ambavyo ni muhimu kwa Afya ya ngozi. Pia tunatoa huduma za tiba kwa dawa ambazo hazina kemikali, dawa zetu zipo katika mfumo wa vidonge. Zinatibu magonjwa tabia yote (yasiyo ya kuambukizwa) kama vile Kisukari, Presha, Matatizo ya moyo, Vidonda vya tumbo, kukosa choo, matatizo ya hedhi, mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa, upungufu wa nguvu za kiume n.k.
Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000. Tunatoa huduma popote Tanzania kupitia kwa Mawakala wetu.
KARIBUNI SANA

Saturday, 1 August 2015

ZITAMBUE DALILI ZA MIMBA CHANGA


Habari za leo mpenzi msomaji wa makala zetu, leo tunapenda kugusia kwa kiasi kidogo kuhusu dalili za mimba changa. Hili somo tumeamua kulileta baada ya wasomaji wetu wengi kuendelea kutuuliza maswali kuhusu namna mwanamke anavyoweza kugundua kuwa ni mjamzito hasa kwa akinadada ambao ndiyo mara yao ya kwanza kuwa katika hali hiyo.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili ya mimba changa:
KWANZA. Mabadiliko katika siku zako(spotting). Unaweza kupata mimba na ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza katika kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa katika ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo ambazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango cha siku za damu hubadilika.

PILI. Kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa(chuchu). Hii inasababishwa na kuongezeka kwa homoni za estrogen pale unakuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.

TATU. Kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapotoka kulala. Na hii ni kwa sababu ya homoni za progesteron ambazo husababisha kupungua nguvu kwa msuli wa mrija wa chakula au koromeo.

NNE. Uchovu na usingizi usiokuwa wa kawaida na bila sababu. Hali hii husababishwa na ongezeko la  homoni ya progesteron na mama utajikuta unapata usingizi kila mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba.

TANO. Kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hii hutokea hasa unapopata mimba ya kwanza utachukia harufu ya baadhi ya vyakula na vinywaji mbalimbali. Wakati mwingine hata harufu za baadhi ya watu zinaweza kukukera. Hapa kidogo panachekesha kwani baadhi ya akinamama huchukia hata harufu ya wapenzi au waume zao.

SITA. Kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinakufanya kujisikia tumbo kujaa.

SABA. Kukojoa mara kwa mara. Hii hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa lishe ya kutosha kwa mama na kiumbe kilichomo tumboni. Kikemia ukiwa na damu nyingi  mwilini utakojoa sana. Pili utajisikia kwenda sana haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.

NANE. Kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa akinamama ambao hupima joto lao kwa njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfululizo.

TISA. Kutoona siku zako za hedhi kabisa. Kwa akinamama ambao siku zao hazibadiliki au huenda vizuri yawezekana wakagundua pale wanapokosea siku na pengine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa wale ambao siku zao hubadilika sana wataona ni kawaida ila kama ameshika mimba ataona mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu, kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.

KUMI. Kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. Pharmacy nyingi huuza vipimo ambavyo ukivichovya kwenye mkojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo. Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani au hata kazini. Kipimo hiki ukikichovya kwenye mkojo kama karatasi inavyoelekea utaona mistari baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini, ikitokea mistari miwili basi utakuwa una mimba na ukitokea mmoja itakuwa hauna mimba. Lakini kipimo hiki huwa kina changamoto zake kwa baadhi ya akinamama ambao kulingana na matatizo ya kiwango cha homoni mwilini hakitaweza kuonyesha majibu mpaka wapitishe wiki moja bila kuona siku zao.

Pamoja na dalili hizo hapo juu, ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu zaidi kutoka kwa daktari aliyepo karibu na wewe.
Kama una tatizo lolote la kiafya, mwanaume au mwanamke waweza wasiliana nasi kupitia namba zetu 0767925000 au whatsapp 0622925000 tutakuhudumia popote ulipo Tanzania. Dawa zetu zote zimetengenezwa kutokana na mimea na ziko katika mfumo wa vidonge.