HATUA SABA ZA KUONDOA WEUSI NDANI YA MAPAJA NA SEHEMU ZINGINE NYUMBANI KWAKO.
By Masha Masanja
Nimekuwa nikipokea maswali mengi sana kwa wadada wengi wakihitaji msaada wa hili wakitaka kujua hasa nini kisababishi baada ya kutumia vipodozi vingi vya kujichua na kuchubua bila mafanikio.
Napenda niseme kwamba hakuna kitu kinachosumbua kisaikolojia na kihisia kama kuwa na weusi katika ndani ya mapaja, kwapa na sehemu zingine, kwani hali hiyo inakunyima uhuru wa mavazi na kujiachia unapokuwa na mwenza wako. Ndio maaana wanawake wengi wamekuwa wakijaribu njia nyingi sana bila mafanikio hasa unapofikia hadi kutumia kemikali kali ambazo zinakuongezea tatizo kuwa sugu zaidi.
Basi usiwaze na huna haja ya kukosa uhuru tena katika maisha yako kwa tatizo hilo kama unajua kufanya utekelezaji wa kitu ulichofundishwa.
Kabla ya yote tuangalie visababishi vya tatizo hili kuanzia vitu vidogo vidogo hadi vitu vikubwa.
VISABABISHI VYA KUWA NA WEUSI KATIKA SEHEMU ZA MAPAJA ,KWAPA NA SEHEMU ZINGINE.
1. Msuguano kati ya sehemu mbili kwa muda mrefu.
Hii ni hali ambayo inawatokea sana watu ambao unakuta viungo vyao vimekaribiana sana hasa mapaja na husuguana na wengine hupelekea kupata maumivu makali sana na kuwapelekea kutumia nguo ndefu za ndani kupunguza msuguano huo.
2. Unene kupita kiasi
Pia hii ni hali ambayo huwatokea watu wa namna hii baadhi, kwa sababu ya uzito kuongezeka bila sababu na kupelekea sehemu hizo kuwa na msuguano mkali sana.
3. Matumizi mabaya ya deodorant spray
Watu wengi wanaotumia deodorant spray hasa zenye aluminium salt zinaziba vitundu vya ngozi na hatimaye ngozi yako kutopumua vizuri na hatimaye kuidhuru ngozi yako. Weusi wa namna hii unapatikana sana ktk kwapa.
4. Matumizi ya vipodozi vikali
Watu wamekuwa wakisumbuka kwa hali na mali kuondoa hiyo hali na wamekuwa wakijitahidi kwa namna yoyote kuondoa hiyo hali.
Lakini sasa matumizi ya vipodozi vikali vinaweza kuharibu sana na kuongeza tatizo kwa kuangamiza [melanocytes] ambazo ndizo seli zinazotengeneza melanin kiini kinachoipa ngozi rangi yake kiuhalisia
5. Vichocheo kuvurugika
Watu wengi wenye vichocheo vilivyovurugika unaweza ukamtambua kuwa ana hormone imbalance kwa dalili hii. Na wengi wapo katika kundi hili, unakuta ana ndevu,kwapa nyeusi na mapaja meusi na hadi kupelekea shingo nyeusi sana. Kumbuka hormon imbalance inatokea kwa wote mwanaume hata mwanamke.
Hivyo ukitaka kumsaidia tatizo hili ,hakikisha unarekebisha vichocheo vyake.
6. Ugonjwa wa polycystic ovarian syndrome [PCOS]
Huu ni ugonjwa unaoathiri ovary za mwanamke. Utakutana na mwanamke analalamika mzunguko mbovu, maumivu makali wakati wa hedhi na wengine watakwambia kuwa anajaribu kutafuta mtoto bila mafanikio.
Wagonjwa wengi wenye PCOS ni wahanga wa tatizo hili, hivyo unapotaka kumsaidia huyu angalia chanzo cha tatizo kisha tibu.
7. Ugonjwa wa kisukari.
Kuna watu maelfu ambao tayari wamegundulika na kisukari aina ya pili tayari tunawaita ni DIABETIC lakini pia kuna wale ambao bado wapo ktk safari ya kuangukia ktk kundi hilo endapo wasipojihadhari na kulinda afya [PRE DIABETIC]
Tofauti kati ya Diabetic na Pre diabetic ni kwamba mtu ambaye ni diabetic sukari huwa ipo juu na insulin pia huwa ipo juu ambapo pre-diabetes wao sukari huwa ipo kawaida kabisa lakini ukipima insulin ipo juu, na wana dalili zingine tunaziita kwa pamoja metabolic syndromes km hizo ecanthosis nigricans[weusi sugu sehemu nyingi] belly fats[ Nyama uzembe] ndio maana ni vigumu sana kumbaini mtu mwenye pre-diabetes kwa kutumia Glucometer[kipimo cha sukari] hadi pale utakapo tumia Insulin Sensitivity test [kipimo cha kuangalia wingi wa insulin]
Kiwango kingi cha insulin kwenye damu kwa muda mrefu kinachotolewa na kongosho kuja kusawazisha kiwango cha sukari kinasababisha seli za melanocytes kufanya kazi kupita kiwango stahiki na hatimaye kusababisha hyperpigmentation [Weusi].
ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO UNAWEZA KUTUMIA KUONDOA TATIZO
1. Pata ushauri kwa mtaalamu wa afya.
Hii itakusaidia kubaini nini hasa chanzo chake na ataanza kukutibu kulingana na tatizo lako baada ya kujua hasa kisababishi ni nini mpendwa.
2. Badili mwenendo Maisha yako katika lishe na mazoezi.
Hakikisha lishe yako unapunguza wanga nzito hasa nafaka, wali n.k pia punguza vyakula vyenye sukari na vionjo vya kemikali km soda.
Pia punguza kula gluten nyingi km vyakula vingi vya ngano iliyokobolewa.
Jitahidi kula sana matunda yenye vitamin C kwa wingi, A kwa wingi E kwa wingi, mboga za majani nk.
3. Majani ya Aloevera.
Chukua utomvu wa jani la Aloevera pale pale unapokata.
Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu/moto
Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka.
Utafurahia jinsi gani mmea huu ulivyo na maajabu katika ngozi yako kwani ngozi mpya itatengenezwa haraka sana na jinsi gani ilivyo mashuhuri km strong natural antibiotics kwenye ngozi yako.
4. Yogurt
Kuna maajabu makubwa sana na yogurt kwani imekuwa ikitumika km natural bleaching agent kutokana na kiini chake [ingredient] lactic acidi pamoja na zinc yenye uwezo mkubwa wa kuzuia kuharibika kwa ngozi kutokana na jasho jingi sehemu za mapaja,shingoni na kwapa.
-Chukua yogurt paka sehemu husika kisha fanya massage [sugua] halafu acha kwa dk 10-15 na baada ya hapo osha na maji ya uvugu vugu.
Pia unaweza kuchukua yogurt kijiko kimoja cha chai ukachanganya na kipande cha limao kisha paka na sugua sehemu husika rudia mara 3 - 4 kwa wiki.
5. LIMAO
Limao ina uasili wa ASIDI ambao unafanya itumike kama Natural bleaching agent cha ngozi yako ambayo imeharibika.
Pia limao ina kiwango kingi cha vitamin C kinachosaidia seli za ngozi yako kuzalishwa upya na kasi ya ajabu.
Chukua pamba na chovya kwenye juisi ya limao kisha paka sehemu husika kisha acha kwa dakika 20 baada ya hapo osha na maji masafi.
Rudia zoezi hili mara 3 hadi 4 kwa wiki moja.
Note: Epuka kutumia juisi ya limao endapo ni muda mfupi umemaliza kunyoa na umejikata sehemu nyeti.
6. TANGO
Hii pia imekuwa ikishika nafasi kubwa kama ni natural bleaching agent ya ngozi.
Inauwezo mkubwa wa kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kurudisha mpya haraka sana. Na hatimaye kufanya mapaja yako kuwa meupe na sehemu zingine.
Chukua kipande cha tango au juisi yake sugua sehemu husika kwa dk 10 hadi 15. Kisha acha angalau dk 10 tena baada ya hapo osha kwa maji ya uvuguvugu.
Pia unaweza kuchukua juisi ya tango, changanya na binzari [unga wake uliosaga] na limao kisha fanya hivyo hivyo.
Fanya zoezi hili mara mbili kwa siku.
7. Mafuta ya Nazi
Haya ni mafuta ambayo yamekuwa na umaarufu mkubwa wa kulainisha ngozi na kuifanya yenye kupendeza. Pia inaondoa sumu zote kwenye ngozi na kuwezesha ngozi kurudisha seli zilizokufa haraka sana.
-Changanya vijiko 5 vya mafuta ya nazi na vijiko
2 vya juisi ya limao
-Pakaa huu mchanganyiko kila siku kwa kusugua kwa dk 10 hadi 15 kisha osha na maji ya moto.
Najua umejifunza namna gani unaweza kuondoa woga wako juu ya tatizo hilo.
Please bofya like ukurasa wangu huu facebook unaitwa Masha Health Products.
Call: 0767925000
Whatsapp: 0622925000
STOP USING CHEMICAL BLEACHING AGENTS, WE HAVE MILLIONS OF NATURAL BLEACHING AGENTS!