Monday, 29 February 2016

HOSPITALI YA WILAYA YA KISHAPU YAWA MSAADA KWA WAKAZI WA WILAYA YA KISHAPU NA MAENEO YA JIRANI

Add caption


Kuanza kufanya kazi kwa Hospitali ya Wilaya ya Kishapu kumeelezwa kuwa ni msaada mkubwa kwa wadau wa huduma ya Afya hususani wagonjwa kutoka ndani ya Wilaya ya Kishapu

Hayo yamethibitishwa na baadhi ya wagonjwa wanaoenda kupata huduma katika Hospitali hiyo ambayo ipo jirani kabisa na eneo la Halmashauri ya Wilaya.

Hospitali hiyo ambayo ni ya Serikali imekuwa msaada mkubwa na wagonjwa wamekuwa wakimiminika kwa wingi kutokana na baadhi ya makundi ya wagonjwa kupatiwa huduma bila malipo kutokana na sera ya Serikali katika kutoa Huduma ya Afya. Makundi hayo ni pamoja na wazee kuanzia umri wa miaka 60, akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Mmoja wa wagonjwa aliyehojiwa na mwandishi wa makala hii alidai yeye anatokea kijiji ya Mwakipoya alidai yeye amekuja Hospitalini hapo kwa kuwa amesikia habari kutoka kwa baadhi ya watu waliowahi kutibiwa hapo kuwa wagonjwa wamekuwa wakipata huduma zote hususani Vipimo na Madawa.
Wagonjwa kutoka vijiji vya Wilaya za jirani za Maswa na Meatu pia wamekuwa wakifika Hospitalini hapo kujipatia huduma.

Mbali na makundi hayo yanayopata huduma bila malipo lakini pia makundi mengine yamekuwa yakijipatia huduma kwa gharama za kawaida ikiwemo familia zinazochangia mchango wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii(CHF) pamoja na wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)

Wakielezea mapungufu wanayoyaona mara wanapoenda kutibiwa Hospitalini hapo, baadhi ya wagonjwa wamedai Hospitali bado inaonekana kuwa na Watumishi wachache kwani muda mwingine wamekuwa wakishuhudia Muuguzi mmoja au wawili wakilazimika kuhudumia Wodi zote za Wanaume, Wanawake, Wazazi na hata sehemu ya Huduma ya Wagonjwa wa nje(OPD). Hivyo wagonjwa wameomba jambo hilo lifanyiwe kazi na mamlaka husika kwani wao(wagonjwa) wamefurahi kufunguliwa kwa Hospitali hiyo maana imekuwa ni msaada kwao na imewaepusha gharama za usafiri kwa wakaazi waliokuwa wakienda kupata Huduma katika Kituo cha Afya Kishapu kilichokuwa kikitumika zamani kwa wakaazi wote. Kituo hicho cha Afya kilichokuwa kikitumika zamani kipo umbali wa zaidi ya Kilometa 8 kutoka mji wa Mhunze.

Hospitali ya Wilaya ya Kishapu ilianza kufanya kazi katikati ya mwezi Novemba 2015 na ina majengo na vifaa vyote vya Huduma ya Wagonjwa wa Nje(OPD), Huduma za kulaza Wagonjwa(IPD), Wodi ya Wazazi(Maternity Ward), Jengo la Upasuaji na Mochwari.
Jina linalotumika kwa Hospitali ni Dr. Jakaya Mrisho Kikwete District Hospital

Sunday, 28 February 2016

TABIA MBAYA 10 ZINAZOFANYA USHINDWE KUWA NA AKIBA "SAVINGS"....HATIMAYE UNAKOSA MTAJI WA KUFANYA MAMBO YAKO..




1.Unanunua nguo bila mpangilio..

Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2.Unanunua Viatu bila mpango.

Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.

3.Unatoa ofa bar bila mpango.

Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4.Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au wasaap Huo ni ujinga. Badilika.tumia internet kujifunza tumia internet kwa mambo ya kukupa biashara yako.

5.Unakopa hela benki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6.Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.

7.Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa Tu na marafiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.

Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!

8.Una michepuko inayokutegemea wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu huzinduki. Badilika.

9.Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.

10.Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au handbag au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.

Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa kufanya vitu vikubwa endelevu.

Saturday, 27 February 2016

Zijue fursa 150 za biashara Ulimwenguni


Zijue Fursa 150 za biashara na miradi mbalimbali nchini Tanzania

1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51. Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo

Friday, 26 February 2016

SABABU ZINAZOPELEKEA BIASHARA YAKO KUFA HATA KAMA NI YA MTAJI MKUBWA AU MDOGO



Mara nyingi wengi wanaoingia kwenye biashara kwa mara kwanza huamini sana mtaji ndio kila kitu. Kwa imani hiyo, hujikuta mara baada ya kuingia kwenye biashara wanakuwa hawaweki nguvu nyingi katika maeneo mengine muhimu ili kuboresha biashara zao. Na matokeo yake hupelekea biashara hizo kuanza kufa huku zikiwa zina mtaji mkubwa kabisa.

Kinaweza kuonekana ni kitu cha kushangaza lakini huo ndio ukweli. Unajua ni kwa nini ? Ni kwa sababu waliaminishwa toka siku nyingi kwamba ukiwa na mtaji mkubwa basi, kila kitu kimekwisha. Lakini, leo katika makala yetu tutaangalia sababu zinazoweza kupelekea biashara yako ikafa, hata kama ina mtaji mkubwa.

Kwa kupitia makala haya itakuonyesha na kukupa ukweli wa wazi  kwamba, mtaji mkubwa peke yake sio ‘gerentii’ ya kukufanya wewe ukafanikiwa kibiashara.  Yapo mambo mengine ya ziada ambayo unatakiwa kuyazingatia na kuyatilia mkazo kila siku, ili biashara yako iweze kukupa yale matunda unayoyataka.

Kumbuka haijalishi biashara yako ina mtaji kiasi gani, lakini elewa ukweli huu inaweza ikafa usipozingatia mambo haya ya msingi. Sasa nataka twende pamoja kujifunza na kujua mambo au sababu zinazoweza kupelekea biashara yako ikafa, hata kama ina mtaji mkubwa vipi.  Karibu sana tujifunze pamoja.

1. Kukosa usimamizi imara.
Kama unaona unataka kuanzisha biashara yako, halafu ukagundua huna usimamizi imara ni bora ukaachana na hiyo biashara. Na kama ungekuja kwangu leo na kunieleza hali hiyo ilivyo,  ningekushauri hivi ‘ Chukua pesa hizo kisha nenda mjini, katafute sehemu wanakochoma nyama nzuri kula pesa yote usibakize hata  Shilingi mia moja.’

Sikutanii. Kwa nini nakwambia hivyo, kufanya biashara yako huku ukiwa huna usimamizi wa kutosha ni sawa na kupoteza pesa hizo. Tena unazipoteza bila kufaidi hata tone. Hapa unaona hata kama ungekuwa na mtaji mkubwa vipi, kama huna usimamizi ni lazima biashara hiyo itakufa tu, hakuna ubishi.

2. Kukosa elimu ya biashara.
Najua umeshawahi kusikia sana fulani alipata mkopo wa  benki milioni sitini, lakini biashara zake zimekufa. Unajua chanzo chake kimojawapo ni nini? Ni kukosa elimu ya biashara. Wengi wanapokosa elimu hii huwekeza kiholela sana matokeo yake kupoteza pesa nyingi bila sababu ikiwa pamoja na mtaji.

Kwa hiyo ili kufanikiwa kibiashara ni lazima wewe kuwa na elimu ya kutosha kibiashara. Pengine unataka kujiuliza nitaipata wapi sasa? Sikiliza huhitaji gharama kubwa sana kuipata. Unaweza kujifunza kupitia semina, huwezi hilo unaweza kujifunza kupitia mitandao ya kuhamasisha au ukanunua vitabu vinavyohusu biashara ukajifunza polepole. Lakini kikubwa usiikose elimu hii, vinginevyo utapoteza mengi ikiwa pamoja na biashara yako.

3. Matumizi mabaya pesa.
Sio kwa sababu biashara yako ina mtaji mkubwa na inaingiza pesa nyingi kwa siku, basi na matumizi yako yanakuwa yako juu bila sababu. Kama unafanya hivyo kwenye biashara yako nikupe tu uhakika huu, huwezi kufika mbali. Ni lazima uwe na mpangilio mzuri wa matumizi yako ya pesa ili kuifanya biashara yako ikazidi kuendelea.

Acha kujidanganya kwa kuendelea kutumia pesa vibaya, utazipoteza zote mpaka utashanga. Kikubwa unajua jinsi huo mtaji ulivyoupata. Kama ni hivyo kwa nini uutumie hovyo? Kuwa makini na pesa zako. Tofauti na hapo biashara yako itakufa tu hata kama sio leo, lakini lazima itakufa.

4. Kukosa ubunifu.
Ili uweze kukabiliana na ushindani, ubunifu ni muhimu sana katika biashara yako. Bila kuwa mbunifu huwezi kufanikiwa katika hiyo biashara kutokana na mazingira ya ushindani mkubwa tulionao kwa sasa. Kwa hiyo ni lazima kuwa mbunifu na kuifanya biashara yako ikaonekana ya tofauti na kukupa wateja wa kutosha.

Wengi wanaoshindwa kwenye biashara ni wale walioingia kwa kiburi cha mtaji mkubwa na kusahau ubunifu. Haijalishi unafanya biashara ndogo au kubwa weka ubunifu. Kila wakati tafuta ni kitu gani biashara yako inakosa, kisha kiboreshe zaidi. Jitahidi sana kuweka ubunifu ili kuifanya biashara yako iwe hai siku zote, vinginevyo utaiua.

5. Kukosa nidhamu.
Kama unaendesha biashara yako na ukakosa nidhamu ya kuiendesha biashara hiyo, elewa kabisa utakuwa na mchango mkubwa sana wa kuiua. Nidhamu ni msingi mkubwa sana wa mafanikio yoyote na sio biashara tu peke yake. Jaribu kuangalia watu wote wenye nidhamu ya kazi mafanikio yao yakoje? Bila shaka ni makubwa.

Biashara nyingi sana zinazokufa huku zikiwa na mtaji mkubwa mara nyingi hukosa nidhamu. Tuchukulie una duka la reja reja, huwezi kufanikiwa ikiwa unafungua na kufunga unavyotaka. Ni lazima uwe una nidhamu ya muda, nidhamu ya kuwajali wateja au nidhamu ya kauli nzuri. Kwa kukosa nidhamu hizi biashara itakufa tu hata iwe kubwa vipi.

6. Kukosa wateja.
Kati ya kiungo muhimu sana kwenye biashara yako ni wateja. Bila wateja hakuna biashara inayoweza kufanyika. Sasa kama utakuwa huna wateja hiyo inamaanisha biashara yako kwa vyovyote vile itaenda kufa hata ufanye nini. Maana hao ndio wawezeshaji wakubwa kwenye biashara yako kuendelea.
Sasa huwa zipo sababu zinazopelekea biashara hii ikakosa wateja na nyingine ikawa na watej wengi. Hivyo ni vyema ukazijua sababu hizo ili zikusaidie kuweza kujenga biashara ya uhakika na yenye mafanikio makubwa.

7. Kukosa vipaumbele.
Biashara yoyote iwe inanza au inaendelea ni lazima iwe na vipaumbele vya msingi ambavyo vinatakiwa vifuatwe kila siku. Kama kipaumbele chako kimojawapo ni kutaka kukuza mtaji ni vyema ukawa makini kuhakikisha hilo linatimia na kutekelezeka kwa haraka sana.

Lakini kama pia vipaumbele vyako ni kuhakikisha unadumisha mahusianao mazuri na wateja wako, pia ni bora ukatekeleza. Unapokosa vipaumbele hata vile unavyoviona ni vidogo ni rahisi sana kwa biashara yako kuweza kufa na kushindwa kuendelea hata kama ina mtaji wa kutosha. Kwa sababu hapa tunasema biashara inakuwa inakosa dira maalumu.

8. Kukosa mgawanyo wa majukumu.
Pia biashara inaweza ikafa hata kama ina mtaji wake mkubwa, ikiwa itakosa mgawanyo wa majukumu.  Ni lazima biashara iwe na mgawanyo wa majukumu ili iweze kusonga mbele. Kama unaona unafanya biashara huku kila kitu umeshikilia wewe na hakuna wa kukusidia elewa upo kwenye hali mbaya.

Ni lazima utafute watu wa kukusaidia hata kama pale haupo mambo yaweze kwenda sawa kabisa. Siri mojawapo kubwa ya kufikiwa mafanikio makubwa kwenye biashara yako ni kutengeneza mgawanyo mzuri wa majukumu kwa wasaidizi wako. Kushindwa kufanya hivyo ni lazima utaua biashara yako.

Hivyo kabla hujafanya chochote unapotaka kuanzisha biashara hakikisha hayo mambo utayahimili.

Kwa ushauri na mafunzo zaidi ya biashara wasiliana nami:
0767925000
0622925000 - whatsapp
Email: mashamasanja@gmail.com

Monday, 22 February 2016

BIASHARA UNAYOWEZA KUIFANYA MUDA WAKO WA ZIADA

NETWORK MARKETING ni Industry inayokuwa kwa kasi duniani na ni industry inayopunguza kiwango kikubwa cha watu ambao hawajaajiriwa, ni industry inayosaidia wengi kupata mtaji wa kufanya mambo makubwa duniani.
Wengi hatujui inavyofanya kazi na maajabu yake.
Katika hili suala kuna umuhimu wa kila mtu kujifunza namna inavyoweza kufanya kazi, siyo rahisi kuifahamu biashara hii kama hautafundishwa na mtu anayeifanya, haihitaji Elimu bali ni kutuliza akili na kukubali kufundishwa. Katika hili tunasema "EMPTY YOUR CUP", Endapo kikombe chako kimejaa si rahisi kuendelea kukijaza maji mengine maana yatamwagika tu.
Biashara hii ina unafuu mkubwa sana kuanzia kutokuwa na gharama za malipo ya kodi ya pango la jengo, kodi ya serikali maana kampuni husika hulipia yote hayo, hutumii muda mwingi na hasa unatumia simu yako tena ukiwa nyumbani kwako umetulia.
Njoo ujifunze sector hii inavyofanya kazi na maajabu yake huhitaji pesa unahitaji kutumia akili.
Tutaendelea kuwajuza zaidi kupitia ukurasa huu wa blog yetu.
Kujiunga nasi kujifunza industry hii wasiliana nami kupitia:
Call: 0767925000
Whatsapp: 0622925000
Masha Masanja