Friday, 31 July 2015

TAMBUA MUDA SAHIHI WA KULA MATUNDA



Watu wengi hula matunda kipindi wanapojisikia wao pasipo kutambua kuwa inatupasa kula matunda kipindi maalumu na pia hilo tunda inabidi liwe na sifa maalumu, siyo kula tunda tu mradi ni tunda.

Kama nilivyosema hapo awali kuwa watu wengi hupenda kula tunda kwa muda wanaoutaka wao au wanakula kwa kujikuta tu wanakula matunda pasipo kupanga au wengi wamekariri kula matunda baada ya mlo. Hii siyo sahihi.

Basi leo ndugu zangu napenda kuwaelezea somo hili kuhusu ulaji sahihi wa matunda. Kwanza inabidi tuzitambue faida za matunda katika miili yetu. Matunda yana faida nyingi sana kwa Afya ya binadamu, hivyo yatupasa kuyapa kipaumbele mkubwa katika milo yetu ya kila siku. Matunda ni chanzo kikubwa cha Vitamin mwilini, hulinda  mwili kwa kuongeza kinga ya mwili, hupunguza uzito wa mwili kwa watu wanene, hulainisha ngozi, huondoa sumu mwilini, hufanya mishipa ya damu kusafirisha damu vizuri, huongeza na kuimarisha nguvu ya mwili/nguvu za kiume n.k.

JINSI YA KULA MATUNDA ILI UFAIDIKE

1. KULA TUNDA KIPINDI UKIWA NA NJAA
Unapokula tunda wakati tumbo likiwa wazi/njaa, matunda husagika kwa urahisi. Baada ya saa moja au zaidi unaweza kula sasa mlo wako mwingine wa kawaida.

2. USILE MATUNDA BAADA YA MLO
Imezoeleka watu wengi kula matunda baada ya mlo kamili. Hata kwenye Hafla na Taafrija, matunda huliwa mwishoni baada ya chakula, HII SIYO SAHIHI KABISA na hayo ni miongoni mwa makosa mengi yanayofanyika kwa sababu ya mazoea tu. Inaelezwa kuwa ulaji wa matunda baada ya mlo siyo sahihi kwa sababu matunda huyeyuka haraka kuliko chakula cha kawaida . Tunda linapokuwa tayari kutoka tumboni kuelekea kwenye utumbo mwembamba huzuiliwa na chakula. Baada ya muda tunda huchanganyikana na chakula na kuoza na hatimaye huzalisha asidi ambayo humfanya mtu kuumwa tumbo baada ya kula matunda, lakini pia virutubisho vyake hupotea.

Ili kuepukana na hali hiyo ya msongamano kwenye tumbo, kula matunda saa moja kabla ya mlo au angalau masaa mawili baada ya mlo. UKIZINGATIA UTARATIBU HUO UTAKUWA UMETOA NAFASI YA CHAKULA KUSAGIKA NA BILA KUZUIA UYEYUKAJI WA MATUNDA

3. ZINGATIA KIWANGO CHA SUKARI KWA BAADHI YA MATUNDA
Baadhi ya matunda kama vile papai, ndizi mbivu yana kiasi kingi cha sukari, japo karibu kila matunda yana sukari lakini baadhi yana kiasi kingi zaidi. Hivyo inashauriwa kula matunda kwa kiwango cha wastani kila siku bila kuzidisha kiwango cha sukari cha gramu 25 kinachohitajika kwa siku.
Aidha unapokula tunda hakikisha unakula kwa ukamilifu wake ili kupata virutubisho vyake. Kwa mfano unapokula chungwa hakikisha unakula pamoja na nyama zake ili kupata virutubisho vyote muhimu vilivyomo. Pia ulapo tango jitahidi baada ya kuliosha ule pamoja na maganda yake.

Jiwekee tabia ya kula matunda ya aina mbalimbali kwa nyakati tofauti ili kupata Vitamin na Madini tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mwili. Hii ni kwa kuwa matunda ndiyo yanayojenga na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi na kamwe hutasumbuliwa na magonjwa mara kwa mara.

Mpendwa msomaji wa makala zetu endelea kufuatilia masomo mbalimbali ndani ya Blog hii. Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000.

Thursday, 30 July 2015

JE, KIPODOZI UKITUMIACHO HAKINA SUMU? SOMA HAPA UPATE KUJUA

Serikali ya Tanzania kupitia mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imevipiga marufuku baadhi ya vipodozi kuuzwa na kutumika kwa matumizi ya binadamu hususani ngozi/urembo kwani imebainika kuwa vina madhara makubwa kwa watumiaji.
Madhara hayo yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni madhara yanayotokea baaada ya muda mfupi na yale yanayotokea baada ya muda mrefu.
Madhara yanayojitokeza kwa muda mfupi ni pamoja na kubabuka ngozi na
ngozi kuwa nyekundu au mabaka meusi.
Madhara yanayojitojeza baada ya muda mrefu ni Kansa ya ngozi, kuharibika kwa figo, zinaangamiza mfumo wa fahamu hasa ubongo na kusababisha matatizo ya kusahau na msongo wa mawazo, magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama vile Asthma/Pumu ya ukubwani, kuharibika kwa mfumo wa homoni kwa akinadada na kusababisha matatizo katika via vya uzazi kama vile maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi, kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa, uvimbe kwenye kizazi, mama mjamzito ni rahisi kujifungua mtoto mwenye matatizo ya akili/taahira n.k

Tangu kuanza kwa udhibiti wa vipodozi nchini, aina 250 za vipodozi vimegundulika kuwa na viambata sumu na hivyo kupigwa marufuku kutumika nchini. Japo idadi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku imeongezeka lakini watumiaji ambao wengi ni akinadada na akinamama wamekuwa wagumu kuacha kiasi kwamba vipodozi hivi vimekuwa vikiuzwa kwa siri na wauzaji hivyo kufanya zoezi la uzuiaji wa vipodozi hivi kuwa gumu. Wanawake wengi wametawaliwa kuwa wakiwa weupe basi ndipo watapendeza au watapendwa zaidi na wanaume.

Cream na Lotion zilizopigwa marufuku zenye kiambato cha HYDROQUINONE ni Mekako Cream, Rico complexion cream, princess cream, extra clear cream, miki cream, viva super lemon cream, ultra skin tone cream, fade out cream, palmer's skin success(pack), fair & white active whitening cream, fair & white strong bleaching treatment cream, fair &white body clearing milk, maxi - tone fade cream, nadinola fade cream, clear essence medicated fade cream, peau claire body lotion, reine clair rico super body lotion, tura lotion, miki beauty cream, extra clair lightening body lotion, clear essence skin beautifying milk, tura skin toning cream, madonna medicated beauty cream, kiss medicated beauty cream, princess patra luxury complexion cream, envi skin toner, zarina medicated skin lightening clere lemon cream, binti jambo cream, malaika medicated beauty ceam, Dear Heart with Hydroquinone Cream, Nish Medicated Cream, Care plus fairness cream, Top clear cream, A3 Skin Lightening Cream, Clear Touch Cream, Rico skin tone, Ultimate skin lightening cream, Immediate Claire Lightening Body Cream, Skin Lightening Lotions containing Hydroquinone, Jaribu skin lightening lotions, Princes Lotion, Clear touch lotion, Super max tone lotion, No Mark Cream.

Pia zimo lotion kama G & G Dynamiclair lotion, G & G Teint Uniforme, G & G Cream Lightening Beauty Cream, Dawmy - lightening body lotion, Maxi White Cream, Bio Claire Lightening body lotion. Kundi lingine ni CREAMS za Amira cream, Jaribu Cream, Peau Claire Cream, Skin balance lemon cream, Skin Success Cream, Miss Caroline Cream, Lemonvate Cream, Movate Cream, Mediven Cream, Diproson Cream, Dermovate Cream, Top Lemon Plus, Lemon cream, Beta Lemon Cream na Unic Clear Super Cream. Kwa ujumla ni vipodozi vingi vilivyopigwa marufuku ambavyo vina viambata vya HYDROQUINONE, MERCURY, ALUMINIUM ZIRCONIUM COMPOUND, PHYTOLACEA, TIN OXIDE, MALIC ACID, APPOCYNUM CANNABIUM ROOT EXTRACT, TUSSILAGO FARFARA, BLUE CAP na STEROIDS.Tambua kuwa viambata hivyo ni sumu. Hivyo uonapo kipodozi chenye mojawapo ya hicyo viambata basi tambua hakifai kwa matumizi ya binadamu. Ushauri uliotolewa ni kutumia vipodozi ambavyo havina viambata hivyo au unaweza kutumia baadhi ya vipodozi vinavyotengenezwa kiasili.

Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000, Tunatoa huduma za Tiba kwa kutumia dawa zisizo na kemikali, dawa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda na ziko katika mfumo wa vidonge.

Thursday, 23 July 2015

MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO

PUNYETO ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi. Kwa hiyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yote yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya tendo la ndoa kwani yenyewe haimshirikishi mtu mwingine.

Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbalimbali za kujitomasa na kujipapasa ya kujistarehesha.

Hakuna mtu anayezaliwa akijua mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi, Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama. Na kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyingine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe.

Unaweza kufikia kilele cha starehe yako kwa kuutomasatomasa uume wako au kisimi kwa wanawake, lakini kutakupa hamu kubwa ya ashiki na kufikia kutoshelezwa vya kutosha kama utapapasa pia sehemu nyinginezo za mwili wako.


KWANINI PUNYETO HUONEKANA KUWA MAKOSA?
Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa na jambo lisilokubalika kabisa. Lakini wanasayansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu ni imani binafsi na chaguo la mtu. Wanaume na Wanawake wengi tu hupiga punyeto maishani mwao kwani huwafanya kujisikia vizuri na kuondoa mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwingine.

SASA TUONE MADHARA YA PUNYETO
1. Mtu anapodumu katika kufanya tendo hili, ngozi ya uume wake huwa ngumu na kusababisha kudhoofika kwa nguvu au hisia zake. Hali hii husababisha manii yake kutoka bila ya kuchanganyikana na ute wa prostate ambao una mchango mkubwa katika kutuliza kiamshi-shahawa.
2. Kuna kipindi mpiga punyeto kutokana na sababu hiyo ya kwanza anaweza kumwaga damu badala ya manii. 
3. Hawezi kuridhika kwa kufanya mapenzi na mwanamke maana amezoea kutumia mikono ambayo siyo laini kama uke wa mwanamke. Tukumbuke kuwa mpiga punyeto hawezi kujitosheleza hadi afanye kumleta au kumuwaza mwanamke fulani kisha anakuwa kama vile anafanya nae mapenzi, hapo ndipo ataweza kumaliza haja zake.
4. Madhara mengine ni maumivu ya kichwa, mgongo, kupoteza nguvu za mwili na uwezo wa macho kuona hupungua.
5. Madhara makubwa kabisa hasa kwa wanaume/vijana wanaofanya sana hili tendo ni kupoteza uwezo wa kuzalisha au kumpa mimba mwanamke. Hili linatokana na kukosekana kwa mbegu komavu za kiume zinazotakiwa kwenda kwenye mfuko wa uzazi.
6. Kujichua au kupiga punyeto kupita kiasi huweza kusababisha uume kupoteza hisia halisi ya tendo la ndoa.

Nadhani baada ya kuona madhara ya punyeto sasa ni rahisi kuacha tendo hilo, cha muhimu ni kuhamishia hisia kwa mpenzi wako uliyenaye au ni bora kabisa kijana ukaoa ili uishi na mpenzi wako daima.

Je, tayari umeshaathirika na tatizo la upigaji punyeto kutokana makali hii ulivyoisoma na unataka kuacha kisha urudishe heshima ya tendo la ndoa kwa mpenzi wako? 
Wasiliana nasi ili tukupatie vidonge vyetu vilivyotengenezwa kwa mimea ya 'butea superba na cordyceps'. Mimea hii hutibu kabisa tatizo hili kwa muda wa mwezi mmoja tu na itarudisha heshima vizuri tu kwa mpenzi wako. Inaimarisha misuli na kusambaza damu vyema katika uume na kukufanya kufurahia tendo la ndoa kadri utakavyo bila kuchoka.
Mawasiliano yetu ni 0767925000 au whatsapp 0622925000. Utapata huduma yetu popote ulipo Tanzania.

Saturday, 18 July 2015

MWANAMKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa au kukosa nyege huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, lakini wanaume hukerwa zaidi kuliko wanawake, ifahamike kuwa mwanaume akikosa hamu ya tendo la ndoa mwanamke au mke wake atajua tu, ila mwanamke akikosa hamu ya tendo la ndoa siyo rahisi mwanaume kujua kama hatamwambia au hatakuwa muwazi. Tatizo hili linaathiri asilimia 20 ya wanaume wakati wanawake ni mara mbili ya wanaume.

Hali ya kujisikia kufanya mapenzi kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalimbali yanayomtokea katika maisha yake. 

MATUKIO YANAYOATHIRI MWANAMKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
-Kuisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanaume
-Kuwa na matatizo/ugomvi wa mara kwa mara katika mapenzi/mahusiano
-Kupata ujauzito
-Kuwa na magonjwa mbalimbali
-Kuwa na mawazo au stress hasa kwa wanawake waliokosa kushika mimba kwa muda mrefu


JINSI YA KUTAMBUA KAMA UNA TATIZO HILI
Kwanza ifahamike kuwa tatizo hili halitokei ghafla tu kama kuugua mafua, huanza taratibu sana na pengine mwanamke anaweza asigundue. Sanasana pima mwenendo wako wa masuala ya mapenzi kwa mwaka uliopita na miezi ya hivi karibuni. Tatizo hili halitokei kwa kutofanya mapenzi kwa muda mrefu au kuhesabu kuwa umeshafanya mapenzi mara ngapi. Mawazo yako kuhusu tendo la ndoa ndiyo ya muhimu katika kujipima.


Viashiria vingine ni vyaweza kuwa kila mara uwapo chumbani na mpenzi wako na anakutomasa sehemu mbalimbali zenye kuleta hisia lakini kwa muda mrefu husikii chochote au hupati nyege basi tambua tayari una tatizo hilo.



MWANAUME KUWAHI KUMALIZA ANAPOFANYA TENDO LA NDOA

Kutoka mbegu za kiume muda mfupi baada ya kumwingilia mwanamke huitwa premature ejaculation. Huu ni udhaifu wa kawaida kwa wanaume walio wengi ikiwa ni pamoja na vijana wenyewe. 


Mtaalamu Ira Sharlip anasema katika utafiti wake kuwa, ni kiasi cha asilimia 20 hadi 30 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili la kumaliza mapema pindi wafanyapo ngono na wenza au wapenzi wao.

Njia za kitabibu za kuweza kumtambua mtu mwenye udhaifu huu huitwa Intravaginal Ejaculation Latency Time (IELT). Hata hivyo mtaalamu Ira Sharlip anaongeza kuwa utaratibu huu haumsaidii sana muathirika wa tatizo hili. Kuna wanaume ambao wanamaliza katika dakika moja tu baada ya kuingiza uume wake ndani ya uke wa mwanamke, wanaume hawa wengi wao hudai kuwa hawana matatizo japo huo ndo mwanzo wa tatizo hilo.
Na kwa upande mwingine kuna wanaume ambao wanaweza kuchukua dakika 20 au zaidi bila kutoa mbegu wakati wa kufanya mapenzi, hilo linawezekana tu endapo mwanaume hana tatizo la premature ejaculation na anaweza kuhimili na kuzitawala hisia zake hasa shahawa zinapokaribia kutoka. Kwa kawaida kipimo sahihi cha kuwahi kumaliza ni chini ya dakika tano, hapa ina maana kwamba mwanaume yeyote anayemaliza kabla ya dakika tano basi atambue kuwa ana tatizo hili la premature ejaculation.

Zipo baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia tatizo hili ikiwa ni pamoja na mwanaume kuwa na mawazo mengi, upigaji wa punyeto, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi.

Kuna dawa ambazo muathirika wa tatizo hili akipewa anaweza kurefusha muda wa kumaliza kama vile za kupooza msongo wa mawazo, kula chakula bora chenye mboga za majani na matunda,  Kufanya mazoezi ya kutosha ambayo humjenga mlengwa namna ya kukabiliana na tendo la ndoa. Pia njia nyingine ni kujizoeza kuacha kulifikiria tendo lenyewe wakati unapohisi unakaribia kumaliza kwa kufanya polepole zaidi au kufikiria mambo mengine ya nje kama vile kuwaza mpira wa Yanga na Simba au Barcelona na Real Madrid! Jenga mazoea ya kufanya hivyo ili kukufanya  uzoee. 

Pia ni vizuri ukapata dawa yetu iliyotengenezwa kwa mimea ya butea superba kwani inawezekana pengine misuli ya uume imedhoofika na hata mbegu zimepungua hivyo uume unakuwa hauko imara.
Dawa hii imesaidia wengi sana, ina vidonge vinne tu kwa dozi nzima na utatumia kidonge kimoja tu kwa siku.

KWA MAELEZO ZAIDI JINSI YA KUIPATA DAWA HIYO WASILIANA NASI KWA 0767925000 AU WHATSAPP 0622925000 AU LIKE PAGE YETU FACEBOOK "Masha Nutrition Health Care"ili ujifunze mengi kuhusu Afya yako.

Friday, 17 July 2015

UFAHAMU UGONJWA WA ASTHMA (PUMU)

 Ugonjwa wa Pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa  katika mapafu. Mtu akipata ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu na kuvimba. Maumivu katika njia za hewa huzifanya njia hizo kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda katika mapafu. Hali hii hufanya muathirika kutoa mlio kama filimbi au mluzi wakati wa kupumua.

VYANZO VYA PUMU
Baadhi ya allergy au vizio vifuatavyo huweza kusababisha Pumu:
-Vumbi
-Mende
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k
-Moshi wa sigara
-Harufu kali kutoka kwenye rangi au chakula
-Msongo wa mawazo
-Uchafuzi wa hewa

Vingine ni kama:
-Dawa kama Aspirin
-Ugonjwa wa kucheua
-Kuwashwa mwili au vizio vitokanavyo na kemikali
-Magonjwa ya njia za hewa

DALILI ZA PUMU
Ugonjwa wa Pumu unaweza kuendana na dalili zifuatazo;
-Kikohozi kikali hasa nyakati za usiku na alfajiri, hali hii humfanya mgonjwa kutolala
-Kutoa mlio kama vile mtu anapiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua
-Kifua kubana. Mgonjwa husikia kama vile kuna kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine kujisikia kama vile kuna mtu amemkalia kifuani.
-Uwezo wa kupumua kupungua au mgonjwa anapumua kwa shida. Hali huu husababishwa na kukosekana kwa hewa inayoingia na kutoka kwenye mapafu.
-Kupumua haraka haraka.


Ikumbukwe kuwa si watu wote wanaokuwa na dalili hizo kuwa watakuwa na Asthma, japo hali hiyo yote huashiria uwepo wa matatizo katika njia za upumuaji. Ni vyema kutembelea kituo cha huduma za Afya kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Pumu ni ugonjwa sugu, hivyo matibabu yake ni ya muda mrefu. Vipimo mbalimbali vinaweza kufanyika vikiwemo X-ray ya kifua, Skin allergy test, kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oxygen kilichopo kwenye damu ya mgonjwa (oximetry) n.k.

Matibabu ya Pumu ni pamoja na kuepuka vyanzo vya ugonjwa huo. Wanaopata ugonjwa huu kutokana na msongo wa mawazo hupewa ushauri maalumu. Kuna matibabu ya aina mbalimbali ya ugonjwa huu yakiwemo ya kawaida na yale ya dharura endapo mgonjwa kapatwa na shambulio la ghafla (asthmatic attack). Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na zile za expectorants, bronchodilators, drip ya cortisone au nebulizer, antihistamine, steroids drugs, intravenous muscles relaxants n.k.

Pamoja na hayo, tiba hizo mara nyingi hutuliza dalili tu au muonekano wa namna ambavyo mgonjwa anajisikia kwa muda huo. Tunazo dawa zilizotengenezwa kwa mimea ya militaris, biloba na uyoga mwekundu ambazo zina jumla ya vidonge 60 kila moja, mgonjwa atazitumia kwa muda wa miezi mitatu na atapona kabisa.
Kazi ya uyoga mwekundu katika mwili ni kuongeza uwezo wa mwili kupambana na magonjwa, huufanya mwili uwe imara, kwa kushirikiana na militaris na biloba hutibu kabisa matatizo yote ya mfumo wa upumuaji na kuondoa matatizo yote yanayohusiana na upumuaji. Dawa zote hizo zipo katika mfumo wa vidonge.
NB: MGONJWA ATUMIE DAWA HIZI KWA MIEZI MITATU PASIPO KUKATIZA DOZI 

WASILIANA NASI KWA NAMBA 0767925000 AU WHATSAPP  0622925000 KWA MAELEZO ZAIDI. PIA like page yetu ya facebook 'Masha Health Products" UTAJIFUNZA MENGI KWA AFYA YAKO

Thursday, 16 July 2015

ZIJUE DALILI NA VISABABISHI VYA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER)

 Ugonjwa wa Kansa ya shingo ya kizazi ni ugonjwa unaoshambulia kizazi cha mwanamke. Tukumbuke kuwa sehemu hii ipo chini ya mji wa mimba ambayo huunganisha uke na mji wa mimba. Urefu wake ni karibu inchi mbili hivi.

DALILI ZAKE NI:
1. Kutokwa na uchafu sehemu za siri.
2. Kutokwa damu nyingi kuliko kawaida siku za hedhi
3. Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
4. Kupata siku za hedhi bila mpangilio (siku za hedhi kubadilikabadilika kila mwezi)
5. Maumivu makali chini ya kitovu

VIHATARISHI/VISABABISHI VYA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI
1. Magonjwa ya zinaa
2. Akinamama wanaojifungua mapacha kila mara
3. Mwanamke kuwa na wapenzi wengi
4. Mwanamke kuanza kuzaa akiwa na umri mdogo
5. Uvutaji wa sigara
6. Utumiaji wa vidonge vya uzazi wa mpango/Vitanzi
7. Ulaji mbovu wa vyakula hasa vyenye mafuta mengi
8. Upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI)

AINA ZA KANSA YA SHINGO YA KIZAZI
1. SQUMOUS CELL CANCER.
    Hii hushambulia kwa nje ya kizazi.
2. ADENOR CARCINOMAR CELL CANCER.
    Hii hushambulia ndani ya ngozi ya kizazi.

HABARI NJEMA KWA TIBA YA UGONJWA HUU
Wataalamu wa utafiti wa dawa kwa kutumia mimea kutoka Thailand na China wamegundua na kutengeneza dawa katika mfumo wa vidonge ambavyo vimetokana kwa mimea ya nyanya, maharage ya soya, uyoga mwekundu na ginsen. 
Dawa hizi zitumike kwa muda wa miezi mitatu na mgonjwa atapona kabisa.

Kama una mgonjwa ana tatizo au dalili hizo waweza wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 ili umchukulie dawa hizo popote ulipo Tanzania.
















Sunday, 12 July 2015

FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)


Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea endapo kidonda cha ukubwa wa angalau nusu sentimeta kitatokea kwenye sehemu yoyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili husababisha maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu makali ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa karibu 70% - 90% ya vidonda vya tumbo husababishwa na vimelea vya bakteria wajulikanao kama HELICOBACTER PYLOR. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-Inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenac huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo. Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoathiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama Duodenum.

AINA YA VIDONDA VYA TUMBO.
1. Vidonda vinavyotokea katika mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo. Vidonda hivi hujulikana kama Gastric Ulcers.
2. Vidonda vinavyotokea katika sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo. Vidonda hivi hujulikana kwa kitaalamu kama Duodenal Ulcers.
3. Vidonda vinavyotokea katika koo (Oesophageal Ulcers)
4. Vidonda aina ya Merckel's Diverticulum Ulcers. Vidonda vya aina hii huweza kusababisha matatizo makubwa ya utumbo (intestinal obstructions)

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
1. Maambukizi ya Bakteria aina ya Helicobacter pylor. Imeonekana kuwa zaidi ya 50% ya watu Duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao huwa hawaonyeshi dalili yoyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
2. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs. Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikanavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa utengenezaji vichocheo hivi yaani Prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.
3. Vyakula au viungo vya vyakula vyenye uchachu. Kinyume na ilivyozoeleka kwa wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.
4. Uvutaji wa sigara. Uvutaji wa sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylor huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike kuwa uvutaji wa sigara pekee hautoshi kusababisha vidonda vya tumbo isipokuwa kwa kushirikiana na bakteria wa Helicobacter pylor.
5. Watu walio katika kundi la damu la O. Imeonekana pia kwamba kundi la damu la BLOOD GROUP O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo.
6. Unywaji wa pombe. Unywaji wa pombe kwa kushirikiana na bakteria wa Helicobacter pylor huongeza madhara ya vidonda vya tumbo.
Vitu vingine vinavyohusishwa na uongezaji wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni pamoja na Upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeris), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo na kubadilishiwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
-Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastric pains).
-Maumivu makali kipindi cha kula au baada ya kula.
-Maumivu makali wakati unapokuwa na njaa.
-Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii yaweza kuendana pamoja na kubeua au kujamba mara kwa mara.
-Kucheua au kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumbomi baada ya kucheua.
-Kichefuchefu na kutapika.
-Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.
-Kutapika damu.
-Kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha kuwa mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali.
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia  dawa za kupunguza maumivu NSAIDs kwa muda mrefu bila kufuata ushauri wa Daktari ni ishara moja ya kumfanya mgonjwa kumuona Daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Mara nyingi mchanganyiko wa dawa za Antibiotics mbili hasa Amoxyllin + Metronidazole sambamba na dawa yoyote ya jamii ya PPI kama Pantoprazole au Omeprazole. Hiyo ni kwa mgonjwa wa vidonda ambavyo siyo sugu.
Vidonda sugu inampasa mgonjwa kutumia dawa za antibiotics za aina tatu kama Amoxyllin + Clarithromycin + Metronidazole ambazo hutumika sambamba na dawa yoyote moja kutoka kundi la PPI kama Omeprazole na Pantoprazole pamoja na Bismuth Compound.

Iwapo hakuna ushahidi wa kuwepo kwa uambukizi wa bakteria, dawa yoyote moja ya jamii ya PPI yaweza kutumika kwa muda mrefu bila kuchanganya na antibiotic yoyote.
Hata hivyo inawezekana kabisa ugonjwa huu kujirudia, hivyo ni vyema kuhakikisha unapata matibabu sahihi na uhakikishe unamaliza dozi kwa muda sahihi. Kumekuwa na watu wengi kuanza matibabu vizuri lakini huishia njiani na kutomaliza dozi. Huu siyo ugonjwa mdogo kwamba utumie dawa kwa siku tatu au wiki moja kisha unapona, huu ni ugonjwa sugu hivyo matibabu yake pia ni ya muda mrefu kidogo kutegemeana na aina ya dawa unazotumia.
Dawa iliyotengenezwa kwa mmea wa Mwalovera imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wote wa vidonda vya tumbo. Hutibu kabisa vidonda vya tumbo kwa kuwaangamiza kabisa bakteria wote wasiofaa katika tumbo. Dozi tatu za dawa hii kwa muda wa miezi mitatu humaliza kabisa ugonjwa huu.

=>Kuipata dawa hii wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 utaweza kuipata mahali popote ulipo.

MAUMIVU MAKALI YA KIFUA (ANGINA PECTORIS)

 Huu ni ugonjwa wa Moyo unaohusisha mgonjwa kupata maumivu makali upande wa kushoto wa kifua na maumivu hayo huenda mpaka shavuni, shingoni, mkono wa kushoto na hata mpaka mgongoni. Kwa hiyo mtu aliye na dalili hizo basi tambua ana tatizo la moyo na ugonjwa huo huitwa Angina Pectoris.
  Ugonjwa huo husababishwa hasa na kupungua kwa ujazo wa mishipa ya moyo na hivyo kuufanya moyo wenyewe usiweze kupata damu ya kutosha na kusababisha hewa ya Oxygen kupungua katika minofu ya moyo(myocard).
 Tatizo hili la mishipa hutokana na kula mafuta mengi hasa ya wanyama kama kitimoto, mafuta ya pamba, kula vyakula vya wanga kwa wingi na unywaji wa bia. Hivyo vyote vikiingia mwilini huendelea kuhifadhiwa kama mafuta. Vyanzo vingine vya tatizo hili ni uvutaji wa sigara, kutofanya mazoezi, kuwa na wasiwasi/mawazo kila mara na ugonjwa wa shinikizo la damu(B.P).
 Ugonjwa huu wa Angina Pectoris umegawanyika katika sehemu tatu(3);
1. Maumivu ayapatayo mtu wakati akifanya kazi ngumu au anatembea zaidi ya mita 100. Maumivu hayo hutokana na moyo kuongezeka kufanya kazi lakini damu ya Oxygen inakuwa haitoshi.
2. Maumivu yatokeayo wakati mtu akitembea chini ya mita 100 au kufanya kazi kidogo tu au kupanda ngazi ya ghorofa.
3. Maumivu ayapatayo mtu wakati amekaa au amepumzika tu.
NB: kama ukiwa na maumivu ya aina hizo tatu, tafadhali acha shughuli zote utakazokuwa unazifanya muda huo kisha hakikisha unafungua madirisha ya nyumba ili upate hewa ya kutosha.
Wagonjwa wa tatizo hili hushauriwa mara zote kutembea na vidonge vya Nitroglycerin kwa ajili ya kuondoa maumivu hayo pindi tu yanapowapata. Lakini vidonge hivyo huishia kuondoa maumivu tu na siyo kutibu tatizo.
Ugonjwa huu huweza kutibika kwa kiasi fulani kwa kubadili tabia zetu mfano kuacha kabisa kunywa pombe kali, kutokula mafuta mengi, kula chakula kwa wakati unaotakiwa, kuacha kuvuta sigara, kufanya mazoezi japo kwa kutembea kwa kasi hata kwa muda wa nusu saa au saa moja tu mara tatu kwa wiki na kutibu shinikizo la damu.
Pia kuna dawa iliyotengenezwa kwa majani ya *biloba*. Majani hayo yanapatikana nchini China na Thailand pekee. Dawa hii imeboreshwa na kuweza kutengenezwa katika mfumo wa vidonge na hivyo kuwa rahisi kupatikana sehemu zote hata hapa Tanzania.
 Endapo una ndugu au mtu wako wa karibu mwenye tatizo hilo tafadhali wasiliana nasi kwa 0767925000 au Whatsapp 0622925000 ili ujipatie dawa hiyo popote ulipo.

Saturday, 11 July 2015

MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO(URINARY TRACT INFECTIONS)

Maambukizi katika njia ya mkojo hujulikana zaidi kwa jina la UTI, kirefu chake ni Urinary Tract Infections.
Maambukizi haya tunaweza kuyaweka katika makundi makuu mawili:
(1) Maambukizi ya chini katika njia ya mkojo(lower urinary tract infections).
   Hii inahusisha mrija wa mkojo(urethra) na kibofu cha mkojo.
(2) Maambukizi ya juu katika njia ya mkojo(upper urinary tract infections.
  Haya ni maambukizi ambayo hupanda na kusababisha maambukizi kwenye figo.

Pia tunaweza kuchanganua ugonjwa huu katika namna kuu mbili.
(1) Acute UTI.
  Hii ni UTI ya kawaida tu. Haya ni maambukizi yanayoambatana na dalili zinzosababishwa na usumbufu wa maradhi kwenye njia ya mkojo. Kwa mfano kuumia wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara n.k.
(2) Chronic UTI.
  Hii mara nyingi huwa tunaiita UTI sugu. Katika hali hii huambatana na dalili za hatari kama kukojoa damu inayoweza kuonekana kwa macho tu bila msaada wa Microscope au kukojoa mkojo wenye chembechembe za damu nyekundu ambazo haziwezi kuonekana kwa macho. Sasa ukiona dalili hizo unaweza kujua kama una UTI sugu. Na unapofikia hali hii mara nyingi tunaamini kuwa tayari figo imeshambuliwa(pyelonephritis). Hapa ni kitendo cha kushambuliwa kwa kuta za nje za njia ya mkojo. Hapa mgonjwa anakuwa anasikia maumivu makali sana kwenye pingili za chini ya mgongo zikiambatana na dalili za tumbo kuuma chini ya kitovu na kukojoa mkojo wenye damu.

KWANINI WATU WENGI KILA KONA NI UTI?
Hii ni kwa sababu watu hawafuati utaratibu au kanuni za kuchukua vipimo maabara. Mfano kipimo cha UTI kwa Maabara tunapima kipimo cha mwanzo kwa kutumia mkojo wa katikati yaani MID STREAM URINE. Tatizo wengi wetu tukienda Hospitali tunaambiwa KAKOJOE HUMU ULETE MKOJO!
Mkojo wa mwanzo ni lazima upitie normal flora(bacteria rafiki/wasio na madhara), na kipimo cha mkojo huwa hakibagui, hapo ni lazima kitasoma una bacteria wengi kumbe wala siyo bacteria wenye madhara. Hapo inatakiwa ukojoe mkojo wa mwanzo umwagike kwanza ndipo uje uchukue mkojo unaofuata(wa katikati au mid stream urine catch).

WATU AMBAO WAPO HATARINI KUPATA UTI
=>Watoto wadogo wanaotumia Nepi maana wao hujikojolea humohumo. Hivyo mtoto mdogo kama humbadilishii Nepi mara kwa mara, huzinyooshi ili ziwe safi ana hatari ya kuugua UTI.
=>Wanaume wa umri mkubwa ambao hawajafanyiwa tohara.
=>Mwanamke yeyote yupo hatarini kupata UTI kwa sababu njia ya haja kubwa ipo karibu sana na njia ya uzazi. Na hivyo wengi wa wanawake wanapokuwa katika zoezi la kujisafisha hujisafisha kwa kupeleka uchafu mbele badala ya kusukuma huo uchafu kwa nyuma. Pia wanawake njia yao ya mkojo(urethra) ni fupi ukilinganisha na ya mwanaume. Kwa wanaume ni nadra sana bacteria kufika kwenye kibofu. Maambukizi ya kibofu huitwa CYSTIS.
=>Watu wenye wapenzi wengi yaani michepuko mingi na hawatumii kinga wakati wa kufanya mapenzi.
=>Wanawake wanaotumia nguo wakati wa kujihifadhi hedhi bila kuzikausha vizuri na kuzinyoosha. Kuna wanawake wengi hufua nguo na kuanika ndani nguo wanazotumia wakati wa hedhi.
=>Wanawake wanaotumia ped za madukani ambazo hazina viwango na kuchelewa kubadilisha ped.
=>Matumizi mabaya ya Antibiotics husababisha walinzi wa sehemu za siri kufa na kufanya bacteria nyemelezi kuvamia na kuanza kuharibu mazingira. Hivyo antibiotics ni nzuri lakini zitumiwe kwa misingi maalumu maana normal flora wakifa basi utashambuliwa na kila bacteria au fangasi ambao ni nyemelezi.

JE, VYOO VICHAFU NI CHANZO CHA UTI?
Watu wengi tumekuwa na visingizio kuwa bacteria wa chooni huwezi kuruka na kuingia katika via vya uzazi na kusababisha ugonjwa wa UTI. Ukweli ni kwamba hao bacteria hawana mabawa ya kuwafanya waruke ila sisi watu ndio huwa tunakiuka taratibu za kujisafisha tuwapo chooni. Kwa maana hiyo utaweza kuambukizwa UTI kupitia hivyo vyoo vichafu hasa vya jumuia endapo tu hautatumia Tishu zenye Antibiotics kujifutia.

SASA TUANGALIE TIBA YA UGONJWA HUU KWA KUTUMIA PED ZENYE ANIONS CHIP ZISIZO NA MADHARA.
Anions hizi zimewekwa katikati ya ped kwa kutumia pamba nyepesi. Hali hii huifanya sehemu husika ikilowa maji au damu, inafyonza damu yote na kuruhusu hewa kupenya na kusafisha joto lote kukausha unyevunyevu wote. Hewa inapopita inaondoa joto lote na kuondoa mazingira ya bacteria waharibifu kuweza kuota au kuishi maeneo hayo. Pia inasafisha na kukausha unyevunyevu wote ambao ukiachwa wadudu kama bacteria au fangasi huweza kuchekelea na kuzaliana kwa fujo. Hivyo kwa staili hiyo mwanamke au msichana unakuwa mkavu na hakuna joto kabisa kama vile kuna AC kwa jinsi utakavyojisikia mwenye amani.

SASA TUONE KAZI NA FAIDA YA HIZO ANION CHIP
=>Tujue kuwa hizo anions chip ni negative charged, yaani anions inapokuwa inatolewa inakuwa inatengeneza oxygen ambayo hii huzuia bacteria wote wanaoweza kustawi bila kuhitaji oxygen yaani Anaerobic Bacteria. Mfano mzuri ni mtu anayekuwa na kidonda cha anaerobes huwa kinanuka sana . Hivyohivyo harufu mbaya sehemu za siri kwa wanawake husababishwa na kuoteana kwa bacteria hawa. Hivyo kwa kutumia ped hizo hii hali huondoka kabisa.
=>Huzuia kansa ya shingo ya kizazi.
=>Hutibu kabisa UTI ya aina yoyote
=>Huzibua mirija ya uzazi kwa watu wenye matatizo ya uzazi
=>Huzuia harufu mbaya sehemu za siri
=>Inazuia maambukizi yote ya kizazi hasa unapokuwa katika mazingira hatarishi kama mabwawa ya kuogelea
=>Zinarekebisha tatizo la uwiano wa vichocheo au hormonal imbalances
=>Hurekebisha siku za hedhi kwa wanawake ambao siku zao za hedhi hubadilikabadilika.
=>Huondoa tatizo la kuumwa kichwa na tumbo wakati wa hedhi.
Ped hizo zinapatikana sehemu nyingi hapa nchini. Piga simu namba 0767925000 au whatsapp 0622925000 utazipata popote utakapokuwa. Pia zinapatikana kwa bei ya jumla na rejareja.

Friday, 3 July 2015

TAMBUA MWILI UNAVYOPATA SUMU NA NAMNA YA KUZIONDOA

Sumu ni kitu chochote ambacho huhatarisha utendaji kazi wa mfumo katika mwili.
Sumu huleta madhara ya aina mbili katika mwili
1. Madhara yasiyoweza kurekebishika (irreversible effects).
Madhara haya ni kama vile makovu, upofu, matatizo ya akili, matatizo ya damu, ukiziwi, kulemaa au kupooza n.k
2. Madhara yanayoweza kurekebishika.
Madhara haya ni kama vile uvimbe, kuwashwa kwa ngozi, ngozi kuwa kavu, kutokwa majipu, mwili kubadilika ngozi n.k
VYANZO VYA SUMU KATIKA MIILI YETU
Mwili hupata sumu kupitia njia tofauti kama tatu hivi:
i/ kupitia vitu ambavyo vipo nje ya mwili.
Hivi ni vitu ambavyo binadamu huvitumia na hatimaye humuathiri. Mtu huvitumia kwa kujua au kutojua. Mfano matumizi ya kemikali aina ya Zebaki (Mercury). Hii huathiri sana mapafu na moyo. Pia utumiaji mbovu wa dawa, ulaji mbovu wa vyakula, unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya n.k
ii/ Miili yetu yenyewe huzalisha sumu kupitia mifumo take mbambali ya kazi. Mfano mifumo ya mmeng'enyo wa chakula, mfumo wa hewa n.k. Katika mifumo hiyo baadhi ya sumu huzalishwa na kemikali(free radicals) ambazo hazitakiwi mwilini.
JNSI YA KUZIONDOA SUMU
Zoezi la kuondoa sumu mwilini hutegemea na aina ya sumu yenyewe. Kuna dawa ya kuvunja sumu(antidote). Hapa ni baada ya uchunguzi kufanyika na kugundulika aina ya sumu na kisha kupewa dawa za kuivunja sumu hiyo.
Chakula bora pia ni njia mojawapo ya kuondoa sumu mwilini. Hapa tunakuwa tunamaanisha vyakula vya asili ambavyo ni "antioxidants", hulinda mwili na kemikali hatarishi. Vyakula vya Vitamini A, C na E hupatikana zaidi katika mboga na matunda.
Vyakula vinavyopatikana katika makundi hayo mchicha, spinach, karoti, nanasi, maembe, machenza, mafuta ya alizeti n.k
Swali la kujiuliza katika mboga za majani, je zina ubora unaotakiwa? Maana zinalimwa na zinakuzwa kwa dawa za kuua wadudu. Dawa hizo pamoja na mbolea zake ni kemikali balaa.
Zipo dawa zilizotengenezwa kwa mimea ya aloe vera na militaris zinaondoa sumu mwilini bila madhara yoyote. Mimea hii huota na kustawishwa Barani Afrika na Asia. Dawa hizi zipo katika mfumo wa kawaida kabisa wa vidonge na utavitumia kwa muda wa mwezi mzima.
Wasiliana nasi kwa 0767925000 au whatsapp 0622925000 ili uweze kujipatia dawa hizo au ushauri wowote kuhusu matatizo ya Kiafya.

Thursday, 2 July 2015

AKINAMAMA: KUTOKWA NA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI(MENORRHAGIA)

Hili ni tatizo linalosumbua akinadada/mama. Hiki ni kitendo cha mwanamke kutumia siku nyingi akiwa hedhi au damu kutoka kwa wiki kuliko kawaida.
CHANZO CHA TATIZO
1. FIBROIDS - Hizi ni vimbe katika kizazi na zinaweza kuwa ndani ya kizazi au nje
2. ENDOMETRIASIS - Hii ni hali ambayo seli za ukuta wa kizazi huenda kujiotesha sehemu nyingine. Automatically mwanamke akiwa na hali hii anaweza kupata hedhi hata mara mbili kwa mwezi au mara moja lakini akatumia siku nyingi kuliko kawaida.
3. Hormones imbalances. Ni kipindi ambacho kiwango cha vichocheo kinapokuwa hakiko katika usawa wake, hasa estrogen homoni.
4. Maambukizi katika mfuko wa kizazi
5. Kansa ya mfuko wa kizazi
DALILI ZA TATIZO
=>Kupata hedhi kwa zaidi ya siku saba
=>Kubadili ped zaidi ya moja ndani ya saa moja
=>Damu inayotoka kuonekana kuwa na dalili ya kuganda
=>Kuonyesha dalili za kuishiwa damu kipindi ukiwa kwenye hedhi
Tatizo hili kwa sasa linaathiri mwanamke mmoja kati ya wanawake watano.
USHAURI NA TIBA
Unapoona dalili hizo tafadhali jitahidi umuone daktari kwa matibabu maana siyo hali ya kawaida. Usitumie vidonge vya maumivu au vyovyote vya kemikali maana utakuwa unaongeza kama mbolea tu mwili hivyo tatizo la vichocheo(hormone imbalance) kuwa kubwa zaidi na zaidi. Akinamama wengi wanaumia na tatizo hili kwa kutokujua madhara ya vidonge wanavyovitumia pindi wakiwa kwenye hedhi.
Tumia matibabu ya mmea,  Tunayo dawa ya mmea ambayo iko katika mfumo wa vidonge utakayoitumia kwa mwezi mmoja. Inamaliza kabisa tatizo hilo.
Kama una tatizo hili au una ndugu yako ana shida hiyo basi usisite kuwasiliana nasi kwa namba 0767925000 au whatsapp 0622925000